Thursday, 23 March 2023 07:06

Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 1 2023 Set 3

Share via Whatsapp

ALAMA 30
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

Hakimu: Wewe jina lako kamili ni Mboko, sio?
Mboko: Ndiyo, Mheshimiwa
Hakimu: Unakiri mashtaka haya mawili, yaliyoelezwa na kiongozi wa mashtaka?
Mboko: La, sikiri, Mheshimiwa.
Hakimu: Kiongozi wa mashtaka, unaweza kuendelea na maelezo zaidi kuhusu kesi hii.
Kiongozi wa mashtaka: Mheshimiwa, huyu mshtakiwa alikamatwa amekaa ndani ya gari la Bi. Cheupe. Maelezo ya alama ya                                               usoni pa Mboko tuliyopewa na Bi. Cheupe yalitusaidia kumkamata.
Karani wa korti:  Mheshimiwa huyu shahidi ni mfanyi kazi katika kituo cha petroli. Jina lake ni Mwema. Ana alama ya kovu usoni                                 pake.
Hakimu: Unaweza kuionyesha korti huyo uliyemwona akiwacha gari la Benz na kuchukua la Toyota?
Mwema: Ni yule mle kizimbani aliye na pingu Mheshimiwa.
Mboko: Mheshimiwa ningependa kumuuliza Kiongozi wa mashtaka swali moja. Polisi aliyenikamata alinikuta mimi nimeketi kiti                    cha mbele cha dereva au cha abiria?
Kiongozi wa mashtaka:  Mheshimiwa huyu ni mhalifu sana. Tuna ripoti kuwa huyu ni mwizi sugu wa magari.
Hakimu: (Akimwelekea Mashtaka) Una lolote la kusema ili kujitetea?
Mboko: Mimi sina hatia, Mheshimiwa. Mimi nilikuwa abiria tu niliyekuwa nikipelekwa nyumbani. Mwizi wa gari ni huyo aliyekuwa                  ameketi kiti cha dereva.
Hakimu: Mimi nitatoa uamuzi wiki ijayo. Kwa hivyo mshtakiwa atabaki korokoroni na kuletwa tena hapa kortini siku nitakayo toa                     hukumu

  1. Aliyeulizwa jina lake na hakimu ni ___________________
  2. Je, mshtakiwa alikubali mashtaka yake? (Ndio, la) ________________
  3. Ni watu wangapi wametajwa katika mazungumzo haya?
  4. Neno kukiri limetumika katika mazungumzo maana yake ni ____________________
  5. Unafikiria ni nani hakusema ukweli kati ya watu waliotajwa kwenye mazungumzo?

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6-9 

Watu wa Afrika mashariki hutumia ala za muziki ambazo zinafanana sana. Kuna ala za nyuzi kama vile gita, zeze, kinubi na udi. Piano pia ni aina ya ala ya nyuzi ingawa nyuzi zake zimefichika ndani.

Ala nyingine hutoa sauti kwa kupuliziwa upepo. Ala hizi ni kama vile kipenga ambacho pia hutumiwa na refa, yaani mwamuzi katika michezo. Zumari na parapanda vile vile ni miongoni mwa ala za kupulizia upepo. Ala nyingine hutoa sauti kwa kutikiswa. Mfano wa ala hizi ni njuga, kayamba, tari na manyanga.

Kuna ngoma ambazo huchezwa uwanjani na kuangaliwa na watu wote, wake kwa waume. Mfano wa ngoma hizo ni kama zile ngoma za kusherehekea mavuno au sikukuu za taifa au za kutumbuiza wageni.

Ngoma na muziki ni njia ya watu kujipatia ajira. Hoteli nyingi huajiri wanamuziki na wachezaji ngoma za kienyeji ili kuwavutia wateja katika hoteli hizo. Inapasa kuhakikisha kuwa hatuwashirikishi wasichana na wavulana wadogo katika ngoma hizi za kutumbuiza watalii katika hoteli.

  1. Ala za muziki zinazofanana mara nyingi hutumiwa na
  2. Taja aina mbili za ala zinazo chezwa kwa kupulizwa. 
  3. Ni aina ngapi za ala zimetajwa katika kifungu hiki?
  4. Chora na utaje ala moja ya muziki iliyotajwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 - 12

Mfalme alikuwa na jozi kumi na mbili za soksi. Jozi sita zilikuwa nyeusi na sita zilikuwa rangi ya kahawia. Alimtuma mtumishi wake kumchukulia jozi moja ya soksi kabatini. Alipofika kabatini, taa zote za umeme katika chumba zilizima.

  1. Mfalme alikuwa na jumla ya soksi ngapi?
  2. Neno jozi limetumika lina maana ya
  3. Unafikiria mtumishi atapeleka soksi ngapi kwa mfalme ili apate jozi moja?

Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 13 - 15

Ni wajibu wa kila mwanafunzi kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati. Tukumbuke kuwa Wahenga hawakukosea waliposema ajizi ni nyumba ya njaa. Hivyo basi haifai kulaza damu darasani.

Ni sharti tufanye juu chini kuwa na adabu na juhudi. Taifa letu linahitaji watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.

Wakulima nao kwa upande ule mwingine kuzidisha mazao mashambani kwa sababu idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Isitoshe, wanabiashara ni lazima kama ibada wajishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi wa wananchi ni wale ambao wana mawazo kuwa ni sharti kila mtu aajiriwe maishani.
nchi

Hivyo basi ni lazima tujitoe mhanga na kuona kuwa nchi yetu imeimarika kiuchumi. Kila mzalendo anafaa kujikaza kisabuni kuona amefanya jukumu lake ili kuona maendeleo ya yamepatikana.

  1. Kulaza damu ni sawa na kusema kuwa
  2. Unadhani ni kwa nini biashara haijaimarika nchini?
  3. 'Ajizi ni nyumba ya njaa' ni aina gani ya tamathali ya lugha?

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Idadi kubwa ya mashabiki ___16___ mchuano wa soka ___17___ Man City na Man United. Nchi yetu, Kenya, ___18___ kushiriki katika mashindano haya___19_-_ si mwanachama wa kombe la Uropa. ___20___ mashabiki wa Kenya, walitazama mechi hiyo moja kwa moja kwenye runinga zao.

   A  B   C   D 
 16.  yalihudhuria  walihudhuria  ilihudhuria   ilihuthuria
 17.  baina ya  dhidi ya   badala ya   katikati ya 
 18.  haiwezi  inaweza   haiezi   hawawezi 
 19.  endapo  sembuse   almuradi   maadamu 
 20.  Licha ya  Kwa hivyo  Hata hivyo  Minghairi ya

 

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu  lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Binuru ni jibu la maamkuzi gani?
  2. Kanusha:
    Angeniita kwa sauti ningeitika.
  3. Ni nini maana ya nahau 'kupiga deki'?
  4. Tunasema baraza la wazee. Tutasema______________________ya watu.   (umati, halaiki)
  5. Chagua sentensi sahihi.
    1. Hapa ndiko kwenye hospitali itajengwa.
    2. Huku ndiko penye hospitali itajengwa.
    3. Humu ndimo kwenye hospital itajengwa.
    4. Huku ndiko kwenye hospitali itajengwa.

Katika maneno yafuatayo, chagua nomino mbili za dhahania.

 kucheza                 Kenya
 wema                    thureya
 daftari                     nyota
 maji                        utulivu
 ndege                  uzalendo

 

  1.  _________________
  2. __________________
  3. Dereva _________________________ gari barabarani vizuri. (dhibiti, thibiti)
  4. Barua ya kirafiki ina anwani ngapi?
  5. Kinyume cha mtu mwangalifu ni mtu _____________________


MARKING SCHEME

  1. Mboko
  2. La
  3. Watano
  4. Kukubali kosa ulilolifanya
  5. Mboko
  6. Watu wa Afrika Mashariki
  7. Zumari, firimbi, kipenga, paapanda
  8. nne
  9. mchoro sahihi
  10. ishirini na nne
  11. vitu viwili vikiwa pamoja/ vinafanana
  12. soksi nne
  13. mvivu/mzembe/mtepetevu/mkunguni/mlegevu
  14. wengi wanaegemea kuajiriwa
  15. methali
  16. C
  17. B
  18. A
  19. D
  20. C
  21. Alamsiki
  22. Asingeniita kwa sauti nisingeitika
  23. Panguza sakafu kwa kutumia maji
  24. Halaiki
  25. D
  26. wema, utulivu uzalendo
  27. ''  " "
  28. dhibiti
  29. moja
  30. msahaulifu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 1 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students