Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kapsabet Highschool Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Jibu maswali mengine matatu kutoka sehemu zilizosalia yaani Kigogo, TumboLisiloshiba ,Ushairi na FasihiSimulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

SEHEMU A: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo

  1. Lazima
    Soma kifungu ufuatao kisha ujibu maswali.

    1. Utaiondoa karaha,
      Usiwe kama juha,
      Kujipa bure usheha,
      Kutembea kwa madaha,
      Eti waenda kwa staha,
      Ndani kwa ndani kuhaha,
      Domo mbele kama mbweha.
      Dume acha mzaha,
      Shika lako silaha,
      Kujipa mwenyewe raha,
      Iwe yako shabaha.

      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Taja mtindo huu wa uandishi. (alama 1)
      3. Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
      4. Fafanua majukumu ya nafsineni katika tamthilia Kigogo. (alama 4)

    2. Kwa kurejelea wahusika mbalimbali katika tamthilia Kigogo. Eleza jinsi mwandishi alivyofanikiwa kutumia nyimbo kuendeleza maudhui, (alama 10)

SEHEMU B: RIWAYA (CHOZI LA HERI)
Jibu swali la 2 au 3

  1. “Kumbe hata mja akafanikiwa vipi kielimu na kitaaluma, maisha yake huwa ombwe bila mwana, awe wa kuzaa au wa kulea?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Taja tamathali moja iliotumika katika dondoo (alama 1)
    3. Onyesha ukweli wa kauli hii ukirejelea wahusika wowote watano riwayani (alama 5)
    4. Fafanua umuhimu wa elimu katika jamii ukirejelea riwaya nzima. (alama 10)
  2. “Una bahati kupata mfadhili, mimi mzazi wangu wa pekee ni mama ambaye ni muuza samaki na baada ya ule mzozo… biashara imepigwa na mawimbi makali.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
    2. Jadili jinsi mwandishi alivyoshughulikia maudhui ya ufadhili. (alama 6)
    3. Ukirejelea hadithi zozote tano riwayani, onyesha jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya hadithi ndani ya hadithi kujenga maudhui.(alama 10)

SEHEMU C: USHAIRI
Jibu swali 4 au 5

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofauta.

    SIONDOKI
    1. Eti
      Niondoke!
      Nimesaki; licha ya risasi
      Vitisho na mauaji, siondoki.

    2. Mimi
      Siondoki
      Niondoke hapa kwangu!
      Kwa mateke hata na mikuki
      Marungu na bunduki, siondoki.

    3. Hapa
      Siondoki
      Mimi nipahame!
      Niondoke hapa kwangu!
      Fujo na ghasia zikizuka
      Na kani ya waporaji, siondoki.
    4. Haki
      Siondoki
      Kwangu siondoki
      Niondoke hapa kwangu!
      Nawaje; waje wanaokuja
      Mabepari wadhalimu, siondoki.

    5. Kamwe
      Siondoki
      Mimi niondoke hapa
      Niondoke hapa kwangu!
      Ng’oo hapa kwangu!
      Katizame chini mti ule!
      Walizikwa babu zangu, siondoki.

    6. Sendi
      Nende wapi?
      Si’hapa kitovu changu!
      Niondoke hapa kwangu
      Wangawa na vijikaratasi
      Si kwamba hapa si kwangu, siondoki.

    7. Katu
      Siondoki
      Sihitaji karatasi
      Niondoke hapa kwangu
      Yangu mimi ni ardhi hii
      Wala si makaratasi, siondoki.

      MASWALI
      1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 2)
      2. Fafanua sifa mbili za nafsineni (alama 2)
      3. Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
      4. Eleza umuhimu wa kihisishi katika shairi (alama 2)
      5. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia usambamba katika shairi (alama 2)
      6. Ukirejelea shairi, eleza namna mtunzi alivyotumia idhini zifuatazo (alama 3)
        1. Inkisari
        2. Kufinyanga lugha
        3. Udondoshaji wa neno
      7. Taja mbinu tatu za lugha katika shairi (alama 3)
      8. Toa mfano mmoja mmoja wa mishororo ifuatayo (alama 2)
        1. mshororo mshata
        2. mshororo kifu

  2. Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

    SHAIRI LA A

    Falaula ngalijua, singalikuwa kijana,
    Kwa sababu sikujua, kajipata mvulala,
    Mengi mambo nikajua, nikashinda wasichana,
    Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

    Mwili wangu kabadilli, toto hadi utu uzima,
    Sauti yangu kabadili, nikajiola mzima,
    Kakiuka maadili, dunia nikaizima,
    Kweli ujana moshi, ukienda haurudi.

    Masikiongu katonga, herini nikavalia,
    Nywele yangu nikasonga, na mikufu kuvalia,
    Video pia runinga, tazama bila tulia,
    Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

    Malaika kapata, moyo wangu kapambika,
    Jina lake kaloreta, mie wangu malaika,
    Penzi langu kalipata,mambo mengi katendeka,
    Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
    Moyongu kausumbua, nilipomtia mboni,
    Penzi lanisumbua, aingiapo moyoni,
    Sautiye kazindua, yatoa nyoka pangoni,
    Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

    Penzi lake kalionja, kwangu likawa asali,
    Nikawa kionjaonja, kuliwasha kawa kali,
    Vitabungu nikakunja, navyo kavitupa mbali,
    Kweli ujana ni moshi , ukienda haurudi.

    Mzigo kabebesha, ukamwachisha skuli,
    Mashakani kaniingisha, nikawa sasa silali,
    Kulisaka suluhisho, likawa sasa ghali,
    Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

    SHAIRI LA B

    Mhariri nipe fursa, nifichue jambo hili,
    Nipige wengi msasa, nakusihi tafadhali,
    Ukweli wajue sasa, wamakinike ki hali,
    Samaki pale barini,kweli huwa si mmoja.

    Nawajuza mahawara, pale walipo hakika,
    Si ya neni kihasira, ukweli nautamka,
    Wayaepuke madhara, wazidi kumakinika
    Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.

    Dunia imegeuka, waja leo wana shani,
    Wazidi kuhangaika, watatizika moyoni,
    Utesi umeshazuka, mashambani na mijini,
    Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.

    Mahaba yakigeuka, hakika huwa ni dhiki,
    Ugomvi uje kuzuka, uharibu urafiki,
    Wakosane washirika, wapigane kila mwezi,
    Samaki pale barini, kweli si mmoja.

    Lakini sasa tengeni, vigogo niwasaili,
    Iwapo ni hayawani,mpungufu kiakili,
    Unisamehe sabini, kwa kosa moja kwa kweli,
    Samaki pale barini kweli huwa si mmoja.

    Hakika huwa si vyema, kibaya kukimiliki,
    Mchongaji nayasema, natangaza uhakika,
    Mtu mate huyatema, iwapo hayamezeki,
    Samaki pale barini, huwa si mmoja.

    Nafumbua fumbo wazi, mnielewe vizuri,
    Nafasili ya mapenzi, yalokumbwa nazo zari,
    Yalofitinika wazi, hapo ndipo nashauri,
    Samaki pale barini, huwa si mmoja.

    Maswali
    1. Jadili maudhui katika shairi A na shairi B (Alama 6)
    2. Eleza muundo wa shairi la A (Alama 4)
    3. Toa mifano ya uhuru wa utunzi uliotumiwa katika shairi la B. (Alama 2)
    4. Andika ubeti wa nne wa shairi la A katika lugha nathari. (Alama 4)
    5. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi haya. (Alama 4)
      1. Nikajiola
      2. Mzigo kambebesha
      3. Shani
      4. Zari

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI

  1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    1. A: Kumbe mambo yenyewe rahisi hivi?
      B: Rahisi, lakini usije ukabakwa tena
      A: Hapana, safari hii itakuwa zamu yako. (Alimrudishia … huku akichekacheka)
      C: Hapajaharibika mambo mama’ngu. Kwani la ajabu lipi? Sasa miye namsubiri Bakari mpya tu, hichi kikongwe nikipe talaka.(Akitabasamu)
      D: Haachwi mtu hapa. Tutabanana humo humo. Yeye atakuwa mke mdogo na mimi mkubwa.
      1. Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 1)
      2. Toa sababu mbili kuthibitisha jibu lako la (i) hapo juu. (alama 2)
      3. Eleza manufaa saba ambayo jamii hunufaika nayo kwa kushiriki katika kipera hiki. (alama 7)
    2. Soma kifungu ufuatao kisha ujibu maswali.

      Siwezi kuhutubu. Mimi sikuwafundisha ubaguzi. Kwa nini mnabaguana? Kwa nini hamukuwapa watu wa matabaka yote nafasi ya kuzungumza? Kwa nini? Kwa nini mnafanya hali hii ya kuwa kuna watu na nusu watu? Nataka wazungumze wale ambao hawata sifu tu.
      1. Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 2)
      2. Eleza mitindo mitatu katika kifungu hiki. (alama 3)
      3. Eleza majukumu matano ya kipera hiki katika jamii. (alama 5)

SEHEMU E: HADITHI FUPI
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
“Tulipokutana Tena” (Alifa Chokocho)

  1.    
    1. Halikuwa jambo la kawaida maana maji yalikuwa hayapatikani karibu pale kijijini petu. Sharti mtu aende masafa marefu kuyatafuta. Na sabuni? Sabuni ilikuwa kitu cha anasa kwa familia yetu. Wazazi wangu hakuwa na uwezo wa kununua Sabuni. Labda mara moja moja siku za sikukuu.
      1. Eleza muktatha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Eleza majukumu mawili ya takriri katika dondoo hili. (alama2)
      3. Kwa kurejelea hadithiTulipokutana Tena jadili jinsi haki za watoto zinavyokiukwa.(alama 6)
    2. Jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa ukirejelea hadithi zifuatazo: (alama 10)
      1. Masharti ya Kisasa
      2. Ndoto ya Mashaka

Mwongozo wa Kusahihisha

  1.    
    1.       
      1. Muktadha wadondoo
        • Huu ni wimbo unayoimbwa na Asiya
        • Anawaimbia Subina Tunu
        • Anawaimbia wakiwa mangweni
        • Tunu na Sudi wanawalika waliokuwa mangweni kuhudhuria mkutano utakaofanyika mbele ya lango kuu la soko la Chapa kazi siku ya maadhimisho ya uhuru ilikushinikiza kufunguliwa kwa soko. 4×1=4Alama
      2. Mtindo wa uandishi
        • Wimbo
      3. Tamathali ya usemi
        • Tashbihi kwa mfano usiwe kama juha.
      4. Majukumu ya mhusika
        • Ametumiwa kufanikisha maudhui ya ulevi na athari zake- unywaji wa pombe haramu imewafanya watu kuwa vipofu.
        • Ametumiwa kuonyesha udhalimu wa viongozi kwani anapewa kibali cha kuuza pombe haramu na Majoka.
        • Anachimuza changamoto zinazokumba ndoa kama ukware.
    2. Jinsi mwandishi alivyofanikiwa kutumia nyimbo kuendeleza maudhui. (alama 10)
      • wimbo wauzalendo- wimbo unaoimbwa katika kituo cha habari cha uzalendo. Wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake.
      • Wimbo wa Hashima- wimbo unaoashiria kuwa mambo hubadilika, kilasiku wasema heri yalipita jana. Uk 51
      • Wimbowa Ngurumo- Ngurumo anaimba wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwananke anapaswa kuolewa.
      • Wimbo waumati- umati wanaimba wimbo katika lango la soko la chapakazi. Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka.
    3. Wimbo wa Ashua- Ashua anaimba kuwa soko la funguliwa bila Chopi. Kumanisha vikaragosi hawananguvu dhidi ya wanamapinduzi. 5×2=10Alama

SEHEMU B: RIWAYA (CHOZI LA HERI)

  1.       
    1. Muktadha wa dondoo (alama 4)
      • Msemaji ni Mwangeka
      • Anajisemea kimoyomoyo ( uzungumzi nafsi)
      • Yeye na Neema wako katika afisi ya Annastacia katika kituo cha watoto cha Benefactor
      • Wamekwenda kumchukua mwanao wa kupanga (Mwaliko) baada ya kukosa kufanikiwa kuwa wan a mwana wa kuzaliwa. Wanamlea kwa tunu na kumsomesha hadi chuo kikuu.
    2. Tamathali moja (alama 1)
      • Istiara- maisha huwa ombwe
    3. Ukweli wa kauli (alama 5)
      1. Selume – amehitimu kuwa mkunga na kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali kuu ya Tumaini na hatimaye katika kituo cha Afya cha Mwanzo Mpya.
        Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe baada ya kutengana na mumewe ambaye anachukua binti yao Hajui kama atakutana na mwanawe Sara baada ya mumewe kuoa msichna wa kikwao
      2. Ridhaa- amehitimu katika taaluma ya udaktari na kufanikiwa maishani. Ni mkurugenzi, mfanyi biashara mkubwa na anamiliki hospitali ya Mwanzo Mpya
        Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe anapopoteza mwanawe Dede na Tila baada ya jumba lake kuchomwa na mzee Kedi. Anapomkumbuka Tila anatokwa na machozi yanayolovya kifua chake.
      3. Mwangeka- amehitimu katika taaluma ya uhandisi, anajiunga na vikosi vya usalama na kupanda ngazi hadi juu.
        Maisha yake yanakuwa ombwe anapompoteza bintiye Becky katika mkasa wa moto, anabaki katika upweke mkuu. Anajuta kutofuata ushauri wa mkewe Lily. (uk62)
        Apondi anapoamua kumlea Umu, Mwangeka anamwona Umu kama Baraka kutoka kwa Mungu, fidia ya mwanawe aliyekufa. (uk 118)
      4.  Neema na Mwangemi- Neema amehitimu katika taaluma ya uhasibu na ameajiriwa katika Hazina ya Kitaifa kama hasibu mwandamizi na Mwangemi ana shahada ya uzamili katika uuguzi. Miaka mitano katika ndoa bila mtoto inawahuzunisha, wanachekwa kuwa Neema hawezi kulea mimba.
        Maisha yao yanakuwa ombwe wanapompoteza mwanao Bahati kutokana na ugonjwa wa sickle-cell.
        Hatimaye wanaamua kupanga mtoto, wanajaliwa kupata Mwaliko (uk 159-167)
      5. Naomi- anamwacha Lunga na kwenda kutafuta riziki baada ya Lunga kupoteza kazi na mali yake.
        Hatimaye anajuta kuwatelekeza wanawe, anawatafuta kote na anapata habari kuwa Dick na Mwaliko waliibwa na Sauna anahuzunika.
    4. Umuhimu wa elimu (alama 10)
      1. Chombo cha kueneza amani na upendo (uk 11)
        Mamake Ridhaa anamtuliza Ridhaa baada ya kusimangwa na wanafunzi wenzake shuleni na kumshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba.
      2. Nyenzo ya kumfikisha binadamu kwenye kilele cha ufanisi (uk 11)
        Mwangeka, Ridhaa, Mwangemi, Lunga n.k wanafanikiwa maishani kutokana na elimu.
      3. Chanzo cha umilisi na stadi za kujitegemea (uk 21)
        Kijana mmoja wakati wa vurumai baada ya uchaguzi analalamikia uongozi duni unaohimiza elimu duni isiowasaidia vijana. Anasema elimu inafaa kuwafunza ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujitegemea.
      4. Nyenzo ya kuzindua jamii. (uk 38-39)
        Shuleni Tila wanafunzwa kuhusu mabadiliko, uwajibikaji wa mtu usipimwe kutokana na jinsia. Mwekevu anachaguliwa kama kiongozi baada ya jamii kuzinduliwa.
      5. Nyenzo ya kutoa maarifa ya kuendeleza jamii. (uk 67-68)
        Lunga anatumia elimu katika kilimo kuwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo
      6. Nyenzo ya kuleta mabadiliko. (uk 97)
        Mwanaheri anajiunga na shule ya Tangamano kwa lengo la kuandama elimu ili aweze kuleta mabadiliko katika jamii.
      7. Nyenzo ya kuwaokoa vijana kutokana uovu. Uk88
        Hazina anaokolewa kutokana na kinamasi cha uvutaju gundi na matumizi ya mihadarati anapopelekwa shuleni katika mradi wa serikali.
      8. NJia ya kukabiliana na changamoto za maisha (uk 88)
        Hazina anapata kazi katika hoteli , wengi wao (watoto wa mtaani)ni maseremala, waashi na mafundi wa juakali baada ya kuelimishwa.
      9. Nyenzo ya kuondoa mwemeo wa mawazo/huzuni (uk92)
        Wasichana katika shule ya Tangamano wanatumia fursa hiyo kusimulia juu ya maisha yao na kuliwazana. Walimu pia wanawaliza wanafunzi wao na kuwapa matumaini..mf Mtawa Pacha anamliwaza Zohali.
      10. Chanzo cha kuboresha miundo msingi katika jamii
        Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya.
        Serikali inajenga makao ya watoto pamoja na shule ili kufadhili elimu.
      11. Kigezo cha kupima uwajibikaji
        Neema anakiokota kitoto barabarani kwani alielewa haki za watoto.
        Mwangeka anamshauri Dick kuacha ulanguzi wa dawa za kulevya na pia anakubali uamuzi wa Apondi kumlea Umu.
        Mwekevu anaikwamua jamii kwa miradi ya maji kinyume na wagombea wenza
  2.        
    1. Muktadha wa dondoo (alama 4)
      1. Msemaji ni Kairu
        • Anamwambia Umu
        • Bwenini, shule ya Tangamano pamoja na wanafunzi wengine; Zohali, Chandachema na Mwanaheri.
        • Baada ya Umu kusimulia hadithi yake na jinsi alivyopata ufadhili katika makao.
    2. Tamathali (alama 2)
      • Msemo
      • kupigwa na mawimbi makali – changamoto
    3. Maudhui ya ufadhili (alama 6)
      1. Shirika la Makai Bora lilijitolea kuwajengea wakimbizi nyumba bora.
      2. Misikiti na makanisa yalikusanya magunia ya vyakula kuwalisha wakimbizi. (CWA, Woman’s Guild, Mothers Union)
      3. Serikali inajenga makao ya watoto wa mtaani na kufadhili elimu yao. Mf Hazina (uk 88)
      4. Serikali inazindua hazina ya kufadhili masomo ya watoto (Idara ya Watoto). Mf Umu (uk 89)
      5. Kituo cha Wakfu wa Mama Paulina kinawafadhili watoto wa mtaani kama Zohali.
      6. Familia ya Bw. Tenge inamfadhili Chandachema kwa kukubali kuishi naye anapopata nafasi katika shule ya Msingi ya Kilimo (uk105)
      7. Shirika la kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu lilimpeleka Chandachema katika makao ya Jeshi la Wajane (uk 107)
      8. Ridhaa anawasomesha wapwaze Mzee Kedi .
    4. Matumizi ya mbinu ya hadithi ndani ya hadithi kujenga maudhui. (alama 8)
      1. Hadithi ya Billy na Sally (uk 80)
        • mapenzi na ndoa -usaliti -utabaka
      2. Hadithi ya Lemi na Tindi (uk 121)
        • Anasa -ukatili/ mauaji
      3. Hadithi ya Pete (uk 146)
        • Ndoa (migogoro) -malezi duni -utamaduni ( tohara,ndoa za lazima)
        • taasubi ya kime -ajira duni -ukatili/uavyaji mimba
      4. Chandachema (uk 102)
        • elimu -tanzia/mauti -ukiukaji wa haki za watoto( malezi duni, ajira)
        • umaskini -ukware
      5. Hadithi ya Zohali (uk 98)
        • utabaka -elimu -malezi duni/kutowajibika/ ukiukaji wa haki za watoto
        • majuto -changamoto za vijana( mimba za mapema)
      6. Hadithi ya Mwanaheri (uk 93)
        • elimu -ndoa na changamoto zake
        • ukabila -majuto -mauti
      7. Kairu (uk 91)
        • tanzia -utamaduni -ukimbizi
        • umaskini -malezi duni

SEHEMU C: USHAIRI

  1.   
    1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 2)
      1. Kuangazia/ kuonyesha nia ya mabepari/ Viongozi dhalimu kuwahamisha watu katika ardhi
        • Kuwahimiza watu/ wanyonge kupigania haki/ardhi yao
    2. Fafanua sifa mbili za nafsineni (alama 2)
      • Mwenye msimamo dhabiti- siondoki kamwe
      • Mtamaduni- anakataa kuhama kwenye ardhi kwa kuwa babu zake walizikwa hapo
      • Mkakamavu/ jasiri- haogopi lolote, …na waje wanaokuja mabepari wadhalimu siondoki
    3. Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
      • Lina beti saba
      • Mishororo sita katika kila ubeti
      • Idadi ya mizani inabadilika katika kila mshororo
      • Vina vinabadilika
      • Mishororo haijagawika katika vipande isipokuwa mshororo wa mwisho katika kila ubeti.
    4. Eleza umuhimu wa kihisishi katika shairi (alama 2)
      • kuchimuza/ kusisitiza ujumbe kwamba nafsineni haondoki
      • kubainisha hisia za nafsineni
    5. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia usambamba katika shairi (alama 2)
      • Urudiaji wa vishazi -Niondoke hapa kwangu
      • Urudiaji wa neno- siondoki
    6. Ukirejelea shairi, eleza namna mtunzi alivyotumia idhini zifuatazo (alama 3)
      1.  Inkisari
        • Sendi- siendi,
        • nende- niende
      2. Udondoshaji wa neno
        • si’hapa- si ni hapa
        • katiza chini mti ule- katizame chini ya mti ule
      3. Kufinyanga lugha
        • yangu mimi ni ardhi hii- ardhi hii ni yangu mimi
        • kwangu siondoki- siondoki kwangu
    7.  Taja mbinu tatu za lugha katika shairi (alama 3)
      1.  NIdaa- niondoke!
      2. Balagha-nende wapi?
      3. Takriri- Siondoki siondoki siondoki
    8. Toa mfano mmoja mmoja wa mishororo ifuatayo (alama 2)
      1. Mishororo kifu
        • Siondoki
        • Kwangu siondoki
        • sihitaji karatasi
      2. Mishororo mishata
        • Ng’oo hapa kwangu
        • Fujo na ghasia zikizuka
        • Kwa mateke hata na mikuki
  2.                 
    1. linganisha kimaudhui
       Maudhui A  Maudhui B
       Kijana alijiingiza kwenye anasa
      Akapuuza masomo
      Akampachika msichana mimba akaacha shule.
      Kijana sasa anajuta kwa vitendo vyake.
       Marafiki waliobadilika na kuwa masahidi.
      Amekatisha urafiki.
      Walio katika ndoa ambao uhusiano wao umeharibika na kutengana
    2.    
      • Tarbia – Lina mishororo minne katika kila ubeti.
      • Mathnawi – Limegawika katika vipande viwili.
      • Ukaraguni- vina vya kati na vya nje vinabadilikabadilika katika kila ubeti.
      • Kibwagizo – kweli ujana ni moshi, ukienda hauridi.
      • Mizani 16- kwa kila mshororo (Zozote 4x1 = 4)
    3. Uhuru wa utunzi
      1. Shairi A
        • Inksari – ngalijua, sautiye.
        • Kutotaja dhamiri – Kajipata badala nikajipata au kumpa
        • Lahaja – nikajiola – nikajiona.
        • Kubironga sarufi – malaika kumpata – kumpata malaika.
      2. Shairi B
        • Inkisari – nayasema.
        • Kuboronga sarufi – ukweli wajue sasa – wajue ukweli sasa.
          (Tuza zozote 2x1 = 2)
    4. Lugha nathari (Alama 4)
      • Nikampata malaika na akaupamba moyo wangu. Malaika wangu anaitwa karoleta. Alilipata penzi langu na mambo mengi yakatendeka . Ni kweli ujana ni moshi ukienda haurudi.
    5.  
      1. Nikajiola – nikajiona
      2. Mzigo kambebesha – Nikamdunga mimba.
      3. Shani – vituko
      4. Zari – shida , mahangaiko.
  3.        
    1.   
      1. Kipera cha utungo
        • Utani. Alama 1×1=1
      2. Anamtania mwenzake kuwa ni zamu yake ya kubakwa.
        • Anamtania mkewe kuwa atamtaliki. Alama 2×1=2
      3. Manufaa ya kushiriki katika kipera hiki.
        • Hupunguza urasimi miongoni mwawa jamii.
        • Huimarisha urafiki- waliona uhusiano mwema ndio hutaniana.
        • Hukuza utangamano miongoni mwa jinsia/tabaka/kabila wanapotaniana.
        • Hutambulisha Imani/mila/tamaduni ya jamii kwa kutaja sifa zake. Kupeana talaka na kuwa na wake wawili.
        • Kukosoa/ kukashifu tabia hasi katika jamii mfano ubakaji.
        • Huburudisha kutokana na ucheshi katika malumbano ya utani.
        • Utani hutoaa maarifa ya kukabiliana na hali mbalibali katika maisha.
          Alama 7×1=7
    2.  
      1. Kipera cha utungo
        • Mawaidha- Alama 1×2=2
      2. Mitindo mitatu Alama 1x3
        • Balagha- kwa nini mnabaguana?
        • Takriri- kwa nini
        • Taswira- watu na nusu watu
        • Jazanda- tofauti za kitabaka
      3. Majukumu matano ya kipera hiki.
        • Kuelekeza /kutoa mwongozo wa jinsi ya kukabiliana na matatizo/jinsi ya kutenda jambo.
        • Kuwapa wanajamii maarifa kuhusu majukumu yao ya kijamii na matarajio ya jamii kwao.
        • Kujifunza maadili yanayoambatana na itikadi za jamii.
        • Kutambulisha jamii kwani mawaidha hutolewa kulingana na mila,desturi na itikadi za jamii.
        • Kusuta na kukashifu tabia hasi katika jamii kwa mfano ubabuzi. Alama 5×1=5
  4.        
    1.          
      1. Muktatha wa dondoo
        • Maneno haya ni ya Bogoa.
        • Anawambia msimulizi na Kazu.
        • Wako katika club Pogopogo.
        • Bogoa na msimulizi wanakutana baabaya miaka 41 baada ya kutoroka kwasababu ya kuwa mtumwa wa nyumbani kwa Bi. Sinai.
      2. Majukumu mawili ya takriri
        • Imetumika kuchimuza hali ya umasikini kwani hata sabuni hawangeweza kununua.
        • Imetumika kuendeleza maudhui ya umasikini
        • Imetumika kusisitiza wazo. Mfano kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni isipokuwa siku ya sikukuu.
        • Imetumika kuendeleza tamathali nyingine za semi mfano chuku. Kuthamini sabuni sana na hata kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni.
      3. Jinsi haki za watoto zinavyokiukwa.
        • Kutengwa na familia- Bogoa alikuwa na umri mdogo wa miaka mitano na hakuta kakutengwa na baba,mama, ndugu, kaka na dada zake. Uk 114
        • Kuamrishwa kufanya vitu bila hiari ya Bogo uk. 115
        • Bogoa alitwishwa mambo yote ya nyumbani alikuwa mtoto mdogo. Uk 115
        • Watoto masikini hawapaswi kusoma shuleni. Uk 116
        • Bogoa hakuwa na uhuru wakucheza na watoto wa Bi. Sinai.
        • Kutishiwa maisha- Bi. Sinai alimtisha Bogua kuwa angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yake ya ndani.
        • Kuadhibiwa kwa kuchomwa- Bi. Sinai alimchoma viganja Bogoa kwa kosa la kuchoma maandazi.
        • Kutoambiwa ukweli- Bogoa anawalaumu wazazi wake kwa kumdanganya Alama 6×1=6
    2. Changamoto katika ndoa (alama 10)
      • Masharti ya Kisasa
        • Masharti katika ndoa
        • Ukosefu wa uaminifu
        • uhuru
        • Taasubi ya kiume/ utamaduni
        • Wivu
        • Utabaka
        • Ukengeushi
      • Ndoto ya Mashaka
        • Ndoa ya lazima
        • Utabaka
        • Umaskini
        • Upangaji wa uzazi
        • Usaliti
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kapsabet Highschool Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?