Print this page

Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2011) Kiswahili Paper 3

Rate this item
(1 Vote)
Download PDF for future reference Install our android app for easier access

SEHEMU A: TAMTHILIA

KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani
  Swali la lazima

 1. “Alijiona pwagu. Lakini Butangi ina pwaguzi pia.”
  Eleza tofauti baina ya wahusika wanaoejelewa. (alama 20)

  SEHEMU B: RIWAYA
  S.A MOHAMED
  : Utengano
  Jibu swali la 2 au la 3

 2. Eleza mbinu zifuatazo zizlivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Utengano:
  1. Kwelikinzani
  2. Sadfa (alama 20)

 3. “Uhuru alioutaka na ulimwengu alioufahamu Maimuna umemdhuru hatimaye.”
  Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 10)

  SEHEMU C: USHAIRI
  Jibu swali la 4 au la 5

 4. KUJITEGEMEA

  1 Nchi ni ile ambayo, imekuwa ardhini
  Siyo ile iombayo, ghaibu na majirani
  Taratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneni
  Daima kukaa chini, maganja ya upewaji

  2 Chumo lote la mitaji, leo limo maganjani
  Bepari na wanyonyaji, wasalie maguguni
  Shime utekelezaji, vingine havifanani
  Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

  3 Twaishije tujihoji, wanachi humu nchini
  Kila tunachohitaji, kupatakwe ugenini
  Hiyo ni tete haviji, tongo tupungusaneni
  Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

  4 Kuomba wataalamu, ni mwendo haulingani
  Tupate wa humu humu, wajuzi wa kila fani
  Mbele washike hatamu, kwa mapimo na makini
  Daima hukaa chini, maganja ya upewaji

  5 Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imani
  Tushiriki kila kazi, na mambo yaliyomkini
  Mikopo ina kinyezi, si kitu cha tumaini
  Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

  6 Yote huyatimizi, alotimiza ni nani
  Lakini tuwe maizi, tusizurure mijini
  Tukamshabihi cozi, kipanga au kunguni
  Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

  7 Shujaa itakiwavyo, aonekane vitani
  Na sisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani
  ‘Kutegemea’ vilivyo, kondo tujiamueni
  Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

  Boukhet Amana: Malenga wa Mrima
  Mwinyihatibu Mohammed
  Oxford University Press
  1977


  1. Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)

  2. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (alama 2)

  3. Eleza maneno matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili kujitegemea. (alama 3)

  4. Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)

  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)

  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kamaa yalivyotumiwa katika shairi.:
   1. Ghaibu
   2. Tukamshabihi (alama 2)


 5. HAKI

  1. Haki watatuitisha, usikuandame, kwa matendo yetu,
  Watukorofisha, tusikwandame, kila penye kitu,
  Mbona watugwisha, mwiba ituchome, kwenye huu mwitu,
                       Tutokwe na utu!

  2. Hatukukufanya, mwana kwa mvyele, aliyemzaa,
  Haki watunyima , machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
  Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
                     Haki twashangaa!

  3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
  Tukatazamana, kwa kuuliza, kuweza thubutu,
  Na kwenye milima, ilotueka kupandia watu,
                   Usipande katu!

  4. Sio hao mabwana, walioteuliwa, kupata mwangaza,
  Haki wakubana, liliotarajiwa, kwenye hichi kiza,
  Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
                Kambi yatuviza!

  5. Haki huna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
  Tukiifatia, hatufiki mbali, tunaganda,
  Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
               Haki yatuponza!

  6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kisha haribika,
  Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itakavyopatika,
  Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika,
              Kwetu ni mashaka!

  7. Haki hufanyiki, paitapo mambo, na vikubwa visa,
  Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
  Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
                Na ndio ya sasa!

  8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
  Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
  Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
                Haki wauliwa!

  9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
  Hatuna ashiki, kuvuta la haja, haki ituvae,
  Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
                Haki tamati!

                   Suleiman A. Ali:
                    Malenga Wapya


  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)

  2. Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)

  3. Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)

  4. Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili. (alama 6)

  5. Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)

  6. Mshairi ana maana gani kwa kusema:
   1. Kambi yatuviza
   2. Kuweza kutukisi (alama 2)

    SEHEMU D: HADITHI FUPI

    K. W. WAMITILA
    : Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo.

    Jibu swali la 6 au la 7


 6. “Cheche ndogo hufanya moto mkubwa.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

  2. Fafanua maudhui manne yanayohusiana na chanzo cha tukio linalorejelewa katika dondoo hilo. (alama 8)

  3. Eleza matokeo manne ya tukio linalorejelewa katika dondoo. (alama 8)

 7. “Mganga na wateja wake wote wlikosa busara.” Fafanua ukweli wa kauli hii kwa mifano kumi kutoka hadithi ya ‘Siku ya Mganga.’ (alama 20)

  SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1. Eleza maana ya malumbano ya utani. (alama 2)

  2. Bainisha sifa nne za malumbano ya utani. (alama 8)

  3. Fafanua majukumu matano ya malumbano ya utani katika jamii. (alama 10)
Read 1632 times Last modified on Thursday, 18 October 2018 17:26
Print PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates

Related items