Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha utekeleze maagizo yafuatayo
    Utotoni niliamini kwamba kusoma ndiko ufunguo wa kila kitu ulimwenguni kwa jinsi kunavyoonekana kuwatoa watu katika uzuzu, ukata na ugonjwa: na kuweka kwenye maisha bora ya mwangaza wa kujua kusoma na kuandika, utajiri wa kuweza kuvaa hata suti ya vipande vitatu, na kuwa na afya ya kuonekana kwa kitambi. Hizo ni zamani zile ambapo shule ya vidudu haikuwa sharti la mtoto kukubaliwa katika darasa la kwanza. Mtoto angelisha au kusaidia kwa kazi za nyumbani mpaka kufika umri labda wa miaka kumi kisha, kufumba na kufumbua, afisa wa serikali angeonekana akishauriana na mzazi wa mtoto. Matokeo yangekuwa mtoto huyo kuanza safari ndefu ya kila siku, apate asipate chakula.
    Mimi kwa upande wangu sikujali maisha pata-nenda shule, kosa – bado – nenda – shule. Sikujali kero za baridi kali wala karaha za vua la asubuhi. Kuanzia utotoni niliwahusudu wenzangu waliokuwa wakirauka kiasi cha kufikiriwa kuwa walilala kwa shati na kaptula zao, au kwa blauzi na skati na kaptula zao. Nilipendezwa na yunifomu zao nikatamani  na hata kuapa kwamba siku moja nitavaa kama wao na kutembea kwa maringo kama wao. Zaidi nilitamani kufika walikokuwa wakienda na kufanya walivyokuwa wakifanya huko.
    Penye nia hapakosi njia. Nia yangu ilidhihirika pale nilipojiunga na darasa la kwanza. Darasa la kwanza lilinisoma kisogo baada ya siku mbili tu. Nalo la pili likanipungia mkono baada ya juma moja. Miaka mitano baadaye nilikutana na kiunzi cha kwanza kwenye mtihani wa kitaifa wa chumba cha saba uliokuwa kifungua mlango wa kuingilia kidato cha kwanza.
    Baada ya miaka minne nilikutana na mlango funge mwingine ambapo nilibisha na ukanifungukia kwa kutia fora  katika mtihani wa kiwango cha elimu ya upili. Katika miaka miwili iliyofuatia nilijiunga na shule maarufu ya kitaifa siku hizo.
    Masomo hayakuendelea kuwa mteremko kwangu kwani uchechefu wa karo na masurufu ulimaanisha kuwa siku nyingi nilikuwa nje ya kuta za darasa letu. Hata ivyo nilijifunga  masombo.Hatimaye nilifunguliwa milango ya kuingia ndaki.
    Baada ya kuhitimu kwa shahada ya kimsingi ya uzamili, kisha uzamifu au udaktari falsafa hatimaye, nilifanywa meneja kufikia leo. Hata nikiwa ukubwani bado ninazidi kusoma na kutafiti ili nisiote ukurutu wa akili.
    Cheo na madaraka haya ya umeneja yamaanisha kila siku nivae suti kamili na shati nyeupe pe, ambayo shingoni imeambatanishwa na kipande maalumu cha kitambaa kinacholewalewa kifuani. Nijiangaliapo kiooni hujifananisha na mtu ambaye amejitia kitanzi shingoni.
    Nina kitambi ambacho labda ni taashira ya  utajiri. Hata hivyo ingawa mimi si tajiri mwenye sauti kubwa kiuchumi, ninaweza kujivunia elimu yangu iliyoniwezesha kujimudu kidogo maishani. Sasa nina shamba langu mwenyewe, nyumba yangu mwenyewe ambayo imejaa mali yangu mwenyewe. Nina redio yangu mwenyewe, rununu  yangu mwenyewe na wanyama wangu mwenyewe.
    Lakini mwenzangu ambaye zilimwishia ukingoni katika shule za nasari, hana elimu, pesa wala mahali pa  kuzikiwa wakati mpira utakapomwia mwingi.
    1. Eleza imani ya mwandishi kuhusu elimu. (alama 3)
    2. Taja dhiki zilizomkabili mwandishi alipokuwa shuleni  ( alama 2)
    3. Onyesha uhusiano uliopo kati ya elimu, kazi na ukwasi kwa mujibu wa habari hii. (alama 3)                                                                                                   
    4. Ukirejelea makala haya, fafanua msemo, ‘elimu ni bahari haina kikomo’ (alama 3)
    5. Hatima ya wale ambao hawakupata elimu ni ipi? (alama 2)
    6. Badala ya maneno yafuatayo mwandishi angetumia msamiati gani? (alama 3)
      1. Niliwahusudu
      2. Ndaki
      3. Taashira
  2. UFUPISHO 
    Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya siasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu; kabla ya ukoloni. Kubaguliwa na kudhulumiwa kwa wanawake kisiasa kunaoana na kunyonywa kwake kijamii kunakoshuhudiwa siku nenda miaka rudi.
    Elimu ya jadi ilimwandaa mwanamke kuwa chombo kitiifu cha mwanamume. Mwanamke aliandaliwa katika unyago na katika mfumo mzima wa malezi kuwa chombo cha kutumikia mwanamume-kumstarehesha, kumfariji, kumlisha na kumzalia watoto. Mwanamke tangu jadi hakuruhusiwa kushiriki katika shughuli za kisiasa na utawala wala hakuna mtu aliyeamini kwamba mwanmke angeweza kushikilia wadhifa wowote wa uongozi. 
    Demokrasia ya jadi naihusudu sana; ambapo wazee walikaa chini ya mbuyu na kuamua mambo ya jumuiya. Mahakama ya kijiji ilikuwa aghalabu ni ya wazee na na wanaume peke yao. Hakukuwa na mwanamke aliyeshirikishwa, hata kama alikuwa ajuza. Sifa waliyokuwa nayo wanawake ni ile ya usihiri na uganga. Mwanamke yeyote ailiyezeeka alidhaniwa kuwa bingwa wa uchawi, ulozi na ushirikina. Kwa hivyo, wanawake ndio waliokuwa washirikina wakubwa, maana fursa ya kupata elimu pana zaidi hawakuwa nayo. Si ajabu kuwa mwanamke alipojitokeza na kusema jambo la busara, alipuuzwa na pengine kutukanwa hadharani. 
    Kwa bahati nzuri, kumezuka mwamko uliotuingiza katika enzi mpya. Vita vya wanawake vya kujihami na kujiendeleza katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume vimetapakaa kote katika kila sehemu ya dunia. Wanawake wengi wamekiuka misingi na miziz ya utamanduni na kung’oa asasi za kijamii na itikadi ambazo daima zimeendelea kumyanyasa na kumuumbua utu mwanamke tangu jadi. Watetezi wa haki za wanawake zamani walilaumu suala la serikali za mataifa mwaka hadi mwaka. Huku masuala ya wanawake ya kijamii, utu na utamaduni yakishangiliwa kupitishwa, watetezi wameeleza wasiwasi wao ikiwa kupitishwa kwa maazimio kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wanawake kimataifa au katika nchi moja. Fauka ya hayo, baadhi ya wachunguzi wanaonelea kuwa maazimio mengi hayadokezi hatua za kufikiwa haki za wanawake. 
    Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa wanawake (Unifem) na kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa shughuli nyingine katika mkabala huu. 
    Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za maisha; siasa, uchumi, utawala na kadhalika. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao naya watu wengi. Wadumishaji wa dhuluma za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende. Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya dhidi ya wanwake wanojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja naya wanyonge wengine. Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii. 
    1. Bila kubadilisha maana asilia, fupisha aya tatu za kwanza. (Maneno 45-55) (Alama 6) 
    2. Kwa kurejelea aya tatu za mwisho, pambanua hoja muhimu zinazoguziwa na mwandishi. (Maneno 60-65) (Alama 9) 
  3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40) 
    1. Tofautisha Irabu /u/ na /o/ (Alama 2) 
    2. Tunga sentensi ili kubaini  matumizi ya neno vibaya katika sentensi kama; kielezi na kivumishi (Alama 2) 
      kielezi………………………………………………………………………………………………………kivumishi………………………………………………………………………………………………......
    3. Yakinisha sentensi ifuatayo.
      Nisipomwona sitamlipa pesa zake. (Alama 1)
    4. Tumia kivumishi cha ‘a’ unganifu katika sentensi ukitumia nomino katika ngeli ya A-WA. (Alama 2)
    5. Tunga sentensi ili kutofautisha vitenzi vifuatavyo. 
      1. ni (Alama 1) 
      2. yamekuwa (Alama 1)
    6. Tunga sentensi ili kubaini; (Alama 2)
      kivumishi cha idadi jumla
      kivumishi cha idadi kamili
    7. Toa maana mbili ya sentensi hii
      Nionyeshe vile nitakavyobeba. (Alama 2) 
    8. Kanusha  sentensi ifuatayo kwa njia mbili .
      Wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi. (Alama 2) 
    9. Andika katika usemi wa taarifa.
      “Tutakwenda kanisani kesho kutwa.” Kame alisema. (Alama 2)
    10. Changanua sentensi hii kwa kutumia kielezo jedwali. (Alama 4)
      “Mshale huu mrefu umevunjika mara mbili
    11. Tunga sentensi mbili tofauti ili kudhihirisha matumizi ya ‘mshazari’ (Alama 2)
    12. Unganisha sentensi hii kwa kutumia kirejeshi ‘O’ Kucha zake ni ndefu. Kucha zimekatwa. (Alama 1)
    13. Eleza matumizi ya ‘Ki’ katika sentensi 
      Ukirusha kipira kitapotea (Alama 3)
    14. Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizoonyeshwa. (Alama 2)
      1. La (kutendeshana).
      2. Pa (kutendesha).
    15. Andika neno lenye kiyeyusho. (Alama 2) 
    16. Andika kwa wingi 
      Mtoto yuyu huyu ndiye aliyeiba nguo yangu. (Alama 1) 
    17. Unda sentensi yenye vijenzi vifuatavyo vya kisarufi.
      Kiwakilishi + kivumishi + kitenzi + kielezi (Alama 1)
    18. Akifisha sentensi ifuatayo ;
      Bw. Juma alimwambia bibi yake nitakutuza ukiendelea kutenda mazuri. (Alama 2)
    19. Tunga sentensi mbili ili kuonyesha tofauti kati ya maneno yafuatayo;  (alama 2)
      1. kua   
      2. kuwa 
    20. Tunga sentensi moja yenye virai viuatavyo. (alama 2)
      RN (nomino, kivumishi kielezi), RT (kitenzi, nomino)
    21. Andika katika udogo. Kitabu cha mtu huyo kimeletwa na mwanafunzi wake. (alama 1)
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Ndada, mbona umerara sana na kecho akuna kazi. 
      1. Mzungumzaji ana tatizo gani? (Alama 2) 
      2. Tatizo hili limesababishwa na nini? (Alama 1)
    2. Watu wanapozungumza huenda wakafanya makosa ya sarufi na ya kimatamshi hapa na pale, na hata hutumia msamiati vibaya. 
      Eleza sababu saba za kufanywa makosa haya (Alama 7) 


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.        
    1. kusoma ndiko ufunguo wa kila kitu
      huwatoa watu katika ujinga, uzuzu, umaskini na ugonjwa
      huwaweka watu kwenye maisha bora ya mwangaza
      huwaweka watu kwenye utajiri
      zozote 3
    2. kukosa chakula
      baridi kali
      mvua a asubuhi
      ukosefu wa karo na masurufu mengine
      Hoja 4x½ = 2
    3. Onyesha uhusiano uliopo kati ya elimu, kazi na ukwasi kwa mujibu wa habari hii
    4. elimu na kazi – mtu aliyeelimika aliweza kuajiriwa
      elimu na ukwasi – elimu humwezesha mtu kujimudu maishani ingawa si lazima awe tajri
      Hoja 2x1 = 2
    5. Mwandishi ameelimika sana / amepata shahada mbalimbali na kufanywa meneja lakini anazidi kusoma na kufanya utafiti
      Hoja kamili, alama 3
    6. kutojimudu maishani
      kutojimudu kiakili
    7.    
      1. Niliwahusudu - niliwaonea wivu / niliwapenda / niliwahusudu
      2. Nda - chuo kikuu / zutafindaki
      3. Taashira-dalili/ishaa
  2.      
    1.        
      • Dhuluma kwa kwa mwanamke ni hali ya tangu jadi
      • Elimu ya jadi ilimwandaa Kama chombo cha mume 
      • Taasubi ya kiume 
      • Mwanamke Kama msihiri na mgaga.
      • kupuuzwa na kutukanwa hadharani             
      • Demokrasia ilimfungia nje. Alama 6              
    2.      
      • Matokeo ya elimu ya kisasa 
      • mwanamke wa enzi mpya 
      • mwanake kujiami na kujiendeleza 
      • vipaji katika Nyanja mbalimbali
      • Kikwazo cha itikadi na mila za kiasili
      • wadumishaji wa dhuluma wasalimu amri 
      • mwanamke anayeongoza maisha yake 
      • Hadhi ya mwanamke kukua
        alama 8
        6+8+1 ut-hijai-sarufi-ziada
  3.      
    1. Tofautisha Irabu /u/ na /o/ (Alama 2) 
      /u/  juu
       /o/ wastani
    2. kielezi na kivumishi (Alama 2) 
      kielezi- mfano; Ameandika vibaya.
      kivumishi – mfano;   Viatu vibaya vimetupwa
    3. Nisipomwona sitamlipa pesa zake. (Alama 1)
      Nikimwona nitamlipa pesa zake.
    4. mfano ; Mwalimu wa Kiswahili amewasili. 
    5.      
      1. Yeye ni mwalimu.
      2. Yeye alikuwa mwalimu
    6. kivumishi cha idadi jumla
      mfano;  Watoto wachache/ tele/ wengi waliwasili.
      kivumishi cha idadi kamili
      Watoto wawili/watatu/mmoja/ wanne nk wamewasili.
      lazima apigie mstari
    7. jinsi
      vitu vya kubeba
    8.     
      1. Wachezaji hawakuwa wanafanya mazoezi.
      2. Wachezaji walikuwa hawafanyi mazoezi.
    9. Kame alisema kuwa wangeenda kanisani siku ya pili iliyofuata siku hiyo.
    10. “Mshale huu mrefu umevunjika mara mbili
      S
      KN KT
      N V V T E
      mshale huu mrefu umevunjika Mara mbili
    11.      
      1. yaweza kutumiwa kuonyesha kumbukumbu. KA/45/4M
      2. kuonyesha maneno fulani yana maana sawa. Mwana/ mtoto wa shangazi ni mzuri.
      3. Hutumiwa badala ya au.Bw/Bi/Dkt/Prof   Vitabu/kalamu/chaki ni muhimu.
      4. Hutumika katika tarehe, mwezi na mwaka. 13/2/2013
    12. Kucha zake zilizokuwa ndefu zimekatwa.
    13. Ukirusha _ya masharti
      Kipira   _udogo
      Kitapotea _upatanisho wa ngeli
    14. La _lishana al. 1 (hakiki sentensi. Za mtahiniwa)
      Pa _pasha al. 1 (hakiki sentensi. Za mtahiniwa)
    15. /W/   waya    /Y/    yeye
    16. Mtoto yuyu huyu ndiye aliyeiba nguo yangu. (Alama 1)
      Watoto wawa hawa ndio walioiba nguo zetu 
    17. Kiwakilishi + kivumishi + kitenzi + kielezi (Alama 1)
      mfano;    Mimi mfupi kupita kiasi/ Yule mrefu amekimbia sana
    18. Bw. Juma alimwambia bibi yake,  ‘Nitakutuza ukiendelea kutenda mazuri.‘ (Alama 2)
    19.      
      1. zidi kwa umri- mfano-   Mtoto amekua haraka hadi ameenda shuleni.
      2. hali- Alikuwa mgonjwa.
    20. RN (nomino, kivumishi kielezi), RT (kitenzi, nomino)
      Mfano
      Kaka  mzuri sana amenunua matunda.
    21. Kijitabu cha kijitu hicho kimeletwa na kijanafunzi chake.
  4.       
    1. /d/, /b/, /l/, /sh/’ /h/.     (al. 2)
    2.    
      • Athari za lugha ya kwanza.
      • Ujuzi wa lugha nyingi za mzungumzaji
      • kutofahamu kanuni za sarufi 
      • kutafsiri lugha ya mama katika Kiswahili 
      • upungufu wa viungo vya kutamkia kama meno, ulimi
      • ukosefu wa baadhi ya sauti za Kiswahili katika lugha ya asili
      • kuzungumza kwa haraka 
      • ugonjwa
      • kutoimudu lugha vilivyo
      • kurithishwa lugha isiyo sanifu na matamshi mabaya aidha na mwalimu au wazazi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?