Print this page

KISWAHILI KARATASI YA 3-Kenya Certificate of Secondary Education(KCSE 2016)

Rate this item
(0 votes)
Download PDF for future reference Install our android app for easier access

Click the link below to download the full 2016 KCSE Past Paper with Marking Scheme pdf document, with all the topics.

https://downloads.easyelimu.com/details/77-2016_KCSE_Past_Paper_with_Marking_Scheme

SEHEMU A: HADITHI FUPI

K. Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine

 1. Lazima
  Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa “Kanda la Usufi”, “Shaka ya Mambo” na “Tazama na Mauti”. (Alama 20)

SEHEMU B: RIWAYA

K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

Jibu swali la 2 aula 3

 1. Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Alama 20)

 2. “Wasemao husema, atafutaye hachoki.”
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  2. Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (Alama 2)
  3. Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Alama 14)

SEHEMU C: TAMTHILIA

T. Arege: Mstahiki Meya

Jibu swali la 4 au la 5

 1. “Anwani Mstahiki Meya ni kinaya.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia. (Alama 20)
 2. “.. .dawa ya adui ni kummegea unachokula.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  2. Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo. (Alama 16)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 aula 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Kilio cha Lugha

  Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
  Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
  Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
  Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia,

  Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanvasa
  Hamna nami imani, wala kupanga siasa.
  Mwasema sayansini. siku ningalitosa.
  Mwanambia nikotosa. kuiva sijafika.

  Ela muelewe sana. Maamuma na Imamu.
  Mulipokuwa vijana. kwenu nilikmva timamu.
  Sasa mumesoma sana. mwaniona ni haramu.
  Mujue kuwa dawamu. utumwa mwauridhia.

  Mzaliwapo mwalia, ‘maa', maneno ya kwanza.
  Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza.
  Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
  Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

  Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
  Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
  Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
  Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

  Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
  Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
  Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
  Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

  Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
  Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
  Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria,
  Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.

  Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
  Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
  Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
  Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

  Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
  Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
  Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
  Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha.

  Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
  Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
  Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
  Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

  Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
  Kukua imeridhia, msamiati kufana,
  Wengine wataijulia, kwa rnarefu na mapana,
  Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
  1. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)
  2. Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha. (Alama 4)
  3. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
  4. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
  5. Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (Alama 3)
  6. Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2)
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3)
   1. nasongwa
   2. kuriaria
   3. adinasi

 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  T. Arege: Barabara

  Barabara bado ni ndefu
  Nami tayari nimechoka tiki
  Natamani kuketi
  Ninyooshe misuli
  Nituliza akili.

  Lakini

  Azma yanisukuma
  Mbele ikinihimiza kuendelea
  Baada ya miinuko na kuruba
  Sasa naona unyoofu wake
  Unyoofu ambao unatisha zaidi.

  Punde natumbukia katika shimo
  Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
  Ghafla nakumbuka ilivyosema
  Ile sauti zamani kidogo
  "Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

  Ingawa nimechoka
  Jambo moja li dhahiri
  Lazima nifuate barabara
  Ingawa machweo yaingia
  Nizame na kuibuka Nipande na kushuka.

  Jambo moja nakukumbukia: Mungu
  Je. nimwombe tena? Hadi lini?
  Labda amechoshwa na ombaomba zangu
  Nashangaa tena!

  Kitu kimoja nakiamini
  Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
  Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
  Nikinaswa na kujinasua
  Yumkini nitafika mwisho wake
  Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
  1. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
  2. Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2)
  3. Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” wa tatu? katika ubeti (Alama 2)
  4. Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (Alama 10)
  5. Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2)
  6. Eleza maana ya: (Alama 2)
   1. kuruba
   2. barabara yenye ukungu

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1.  Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii. (Alama 10)
  2. Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Alama 10)

 

Read 857 times Last modified on Wednesday, 27 March 2019 08:03
Print PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates

Related items