Print this page

KISWAHILI KARATASI YA 2-Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE 2016)

Rate this item
(0 votes)
Download PDF for future reference Install our android app for easier access

Click the link below to download the full 2016 KCSE Past Paper with Marking Scheme pdf document, with all the topics.

https://downloads.easyelimu.com/details/77-2016_KCSE_Past_Paper_with_Marking_Scheme

 1. UFAHAMU (Alama 15)

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 

  Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku.

  Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika tatizo hili.

  Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu, ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi.

  Mataifa yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi husika.

  Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya.

  1. Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.(alama 2)
  2. Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea? (alama 4)
  3. Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika kutatua tatizo la ufukara?(alama 4)
  4. Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2)
  5. Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama 3)
   • Turathi za kikoloni
   • Kuatika
   • Kuyaburai

 2. MUHTASARI (Alama 15)

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

  Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha.

  Nchi moja huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yote hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa.

  Uzalendo ndio mhimili mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake, matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake. Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake maangamizo kwa vyovyote vile.

  Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema. Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake. Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi kuhasirika mradi taifa lake linufaike. 

  Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.

  1. Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.(alama 6, 1 ya mtiririko)
  2. Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70) (alama 9, 1 ya mtiririko)

 3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

  1. Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi. (alama 1)
  2.  
   1. Nini maana ya silabi (alama 2)
   2. Tunga neno lenye muundo huu wa silabi:
    Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu
  3. Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake) (alama 2)
  4. Tambua kiambishi awaii na tamati kati neno: Alalaye (alama 2)
  5. Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi. (alama 4)
  6. Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii) (alama 2)
  7. "Shughuli yetu itakamilika kesho", mama alimwambia mwanaye Juma. (Andika katika usemi wa taarifa). (alama 2)
  8. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. Mpira ulichezwa tulipokuwa tukipika.(alama 3)
  9. Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi "ona" kikinyambuliwa katika kirai hiki "ona ndoto". (alama 3)
  10. Eleza matumizi ya hali za "ka" na "hu" katika sentensi zifuatazo:
   1. Balozi huja hapa kila mara. (alama 1)
   2. Mpishi alipika, akapakuwa na akagawa chakula. (alama 1)
  11. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi: Tuiiitwa na baba.
  12. Akifisha: Shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupcleke kwenu jioni mtoto aliuliza kwetu wapi?(alama 4)
  13. Eleza matumizi mawili ya kiambishi -ji-.(alama 2)
  14. Tunga sentensi hii upya kwa kutumia visawe vya maneno yaliopigwa mstari. Kiambaza kilimuumiza ghulamu alipokuwa akipanda. (alama 3)
  15. Tumia kitenzi "Fa" katika sentensi kuonyesha mazoea. (alama 2)
  16. Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo: Babu alifika mapema kuliko wote halafu akaondoka.(alama 2)
  17. Tumia kitenzi "tafakari" kama nomino katika sentensi. (alama 1)
  18. Andika upya sentensi ifuatayo kwa kutumia viwakilishi badala ya nomino zilizopigwa mstari. Mwanamziki ataembelea mji. (alama 1)

 4. ISIMU JAMII (Alama 10)

  Kwa kutoa mifano maridhawa, eleza kaida zozote tano ambazo matumizi ya lugha hutegemea katika jamii.
Read 508 times Last modified on Wednesday, 27 March 2019 07:54
Print PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates

Related items