KCSE 2019 Kiswahili Paper 3 Questions With Marking Scheme

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemunne zilizobaki; yaani, Tamthilia, Hadithi Fupi, Ushairi na Fasihi Simulizi
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja

SEHEMU A: RIWAYA

A. Matei: Chozi la Heri

  1. Lazima
    1. "Sasa haya ameyapa kisogo ... kufunguliwa kwa kituo hiki ni kama mana iliyomdondokea kinywani kutoka mbinguni."
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Bainisha tamathali mbili za usemi ambazo zimetumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
      3. Fafanua umuhimu wa mhusika anayerejelewa katika dondoo hili katika kuijenga riwaya hii. (alama 6)
    2. Jadili mikakati mwafaka ambayo vijana wanatumia kukabiliana na hali yao ya maisha Jadilim kwa kuwarejelea wahusika wafuatao:
      1. Chandachema (alama 4)
      2. Dick (alama 4)

SEHEMU B: TAMTHILIA

P. Kea: Kigogo

Jibu swali la 2 au la 3

  1.  
    1. Jadili mbinu kumi ambazo Wanasagamoyo wanatumia kupigana na utawala dhalimu. (alama 10)
    2. Eleza jinsi mbinu rejeshi ilivyotumiwa kukuza vipengele vifuatavyo katika tamthilia hii.
      1. Maudhui (alama 5)
      2. Wahusika (alama 5)
  2.  
    1. "Ushahidi utatoka wapi kama kipanga ndiye hakimu kwenye kesi ya kuku?"
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Fafanua dhima ya vipengele viwili vya kimtindo vinavyobainika katika dondoo hili. (alama 4)
    2.  
      1. Kwa kurejelea tamthilia jadili sifa sita za msemaji. (alama 6)
      2. Eleza umuhimu wa mandhari katika tamthilia hii. (alama 6)

SEHEMU C: HADITHI FUPI

Jibu swali la 4 au la 5

A. Chokocho na D. Kayanda (Wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

K. Walibora: "Nizikeni Papa Hapa"

  1.  
    1. "Isije ikawa hapa habari ya kufuata asali ukafa mzingani." "... Pana hasara gani nzi kufia kidondani?"
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5) 
      2. Andika mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
    2. Hadithi, Nizikeni Papa Hapa inahimiza uwajibikaji. Jadili. (alama 6)
    3. Eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza katika hadithi, Mapenzi ya Kifaurongo." (alama 7)

A. Chokocho: "Shogake Dada ana Ndevu"

  1.  
    1. Onyesha jinsi unafiki unavyoshughulikiwa katika hadithi, “Shogake Dada ana Ndevu." (alama 8)
    2. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: (alama 12)

      "Bi. Hamida alitunga donge kifuani mwake. Na donge likaja juu. Likampanda na kumsakama kooni. Kweli? Uongo? Kweli au uongo yale maneno ya binti yake? Labda kweli anamfikiria mambo mabaya binti yake tu. Labda kweli dhana yake ni mbovu. Bi. Hamida alichanganyikiwa na mambo. Alivutwa huku na huku na nafsi yake yenye chagizo. Upande mmoja sauti yake ya ndani ilikuwa inamtetea Safia, na upande wa pili wa nafsi yake ilikuwa ikimshuku Safia; na sauti zake zote mbili hizo zimo ndani ya kiwiliwili chake zinamvuta yeye mtu mmoja, Bi. Hamida. Hatimaye hakutambua afanye nini."

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7.

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Lilipo lile banda, lile pale,
    Kuna mja kakonda, kwa uwele,
    Wala siye kupenda, hiyo ndwele,
    Ndwele ya kutwishwa!

    Ni ndwele ya kutengwa, penye haki,
    Uwele wa kusutwa, pasi haki,
    Ugonjwa kupuuzwa, na miliki,
    Ndwele ya kutwishwa!

    Mwiliwe kawa sugu, viwandani,
    Uso una kunyugu, ziso fani,
    Ujira wake ndugu, ni mapeni,
    Ndwele ya kutwishwa!

    Na homa akipatwa, maishani,
    Kwa tiba apuuzwa, kama nyani,
    Hajulikani kuwa, yeye nani,
    Ndwele ya kutwishwa!

    Ana chawa nyweleni, ona dhiki,
    Na kunguni nguoni, ahiliki,
    Funza na miguuni, wamesaki,
    Ndwele ya kutwishwa!

    Bado yuasubiri, kisimati,
    Dhiki yake kutiri, 'we tamati
    Ndipo iwe sururi, ya kidhati
    Nyota yake ni nyota ya huzuni.

    (K.Wamitila)

    1. Fafanua kwa kutoa hoja sita kutoka kwenye shairi, jinsi nyota ya anayerejelewa ni ya huzuni. (alama 6)
    2. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
    3. Bainisha aina zifuatazo za uhuru wa kishairi katika shairi: (alama 2)
      1. inkisari
      2. kujifanyanga sarufi
    4. Eleza tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 3)
    5. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
    6. Eleza sifa mbili za anayelengwa katika shairi hili kwa kurejelea ubeti wa mwisho. (alama 2)
    7. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 2)

  2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Kama akili si mali, maskini na tajiri
    Wangalimoja sampuli, asikuwepo fakiri
    Na hangekuwa na mali, mwinyi bila kufikiri
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Ukeshapo kwa fikara, ni kwa wingi wa akili
    Kuwaza kigaragara, una mengi si kalili
    Na kuwa una tambara, metajirika
    kwa hili Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Alokijenga kitanda, ana wingi wa akili
    Hata asiwe na bunda, hamithili kwa akili
    Hata naye paka nunda, pasipo akili hali
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Akili kweli ni mali, kwa kuteua vya mwozo
    Singetumia akili, ungevila vya angamizo
    Afya ikawa thakili, na kuhiliki mawazo
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Vipi gonjwa kikuganda, wawazia spitali?
    Huachi ukawa ng'onda, ukanyauka muwili
    Ugangani unakwenda kutafuta afadhali,
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Kama akili si mali, kusingekuwa na jela,
    Kuwatenga kuwa mbali, wenye hiana na hila,
    Kwa mbavu na ufidhuli, pamwe mbinu tolatola,
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Tajiri na maskini wote wanayo akili,
    Ni kuwa hayafanani, waliyonayo makali
    Kabisa hawashibani, liwe lile au hili,
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    Kama akili si mali, 'singekuwa na hazina
    Ya kudadisi mithali, na kupinga yako mana
    Gani inadumu mali, kuliko huko kusana?
    Kama akili si mali, usingeweza fikiri.

    (T. Arege)

    1. "Ufanisi wa binadamu hutegemea akili." Fafanua kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye shairi hili. (alama 6)
    2. Andika mifano ya vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili: (alama 4)
      1. sitiari
      2. tanakuzi
      3. swali la balagha
      4. kinaya
    3. Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4)
    4. Andika aina mbili za urudiaji zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 2)
    5. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 4)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

    Shangazi anambila
    umewadia muda
    wa kukiacha kiambo
    cha Baba
    Nende kujinasibisha
    na ajinabi tusohusiana
    kwa ngeu wala usaha
    nache niwapendao
    nache aila nache matamanio
    ya elimu kufuatiya.

    Anambile shangazi
    Hino ni neema
    ela moyo wanirai
    "Wajitia shemere", nami nauambia,
    "Najua si utashi wangu"
    ila hiari sina

    kwani hii ni faradhi
    mitamba mepokelewa
    na ami kwa furaha
    kilobaki ni kuvuka
    kizingiti hiki."
    Kwaheri Mama, kwaheri wanuna.
    1. Ainisha wimbo huu kwa kuzingatia kipengele cha maudhui. (alama 2)
    2. Andika sifa mbili za jamii inayosawiriwa na wimbo huu. (alama 2)
    3. Eleza mikakati sita ambayo mwimbaji angetumia kufanikisha uwasilishaji wa wimbo huu. (alama 6)
    4. Unanuia kutumia mahojiano kukusanya habari kuhusu nyimbo za aina hii.
      1. Eleza manufaa matano ya kutumia mbinu hii. (alama 5)
      2. Eleza changamoto tano za kutumia mbinu hii. (alama 5)


MAJIBU

  1.  
    1.  
      1.  
        • Haya ni maneno ya msimulizi/mwandishi
        • Yanamhusu Selume
        • Yumo kwenye kituo cha Afya cha Mwanzo Mpya
        • Anawazia changamoto alizopata alipokuwa akifanya kazi kwenye hospitali ya umma. Kwa mfano, ukosefu wa vifaa vya kimsingi kama vile glavu.
        • Hali imekuwa afadhali baada ya kuajiriwa katika kituo cha Mwanzo Mpya. 4x 1 = (alama 4)

          Tanbihi: Dondoo limetolewa uk. 140
      2.  
        • Nahau/Misemo - ameyapa kisogo
        • Tashbihi - kama mana iliyomdondokea kinywani
        • Jazanda istiari - mana
          2x1 = (alama 2)
      3.  
        • Anaonyesha athari za tofauti za kisiasa. Anafarakana na mume wake kwa sababu alimuunga mkono Mwekevu uk. 30.
        • Mwandishi amemtumia kuendeleza maudhui ya ukabila. Mume wake anaoa msichana wa kikwao (uk. 35) baada ya kufarakana.
        • Ametumiwa kuonyesha tabia za wahusika wengine. Kupitia kwake tunaona utu wa Ridhaa. Ridhaa anamtuliza na kumtafutia kazi (uk. 35)
        • Ni kielelezo cha udugu wa wanyonge. Yeye na wenzake wanamsaidia Ridhaa kukabiliana na hali ya ukiwa iliyosababishwa na kufiwa ng familia yake.
        • Anachimuza changamoto/uovu uliopo katika taasisi za umna Analalamikia ukosefu wa vifaa vya kimsingi kama vile glavu. Analalamikia ukosefu wa huduma muhimu kama vile umeme, kuuzwa kwa dawa zilizotengewa wanyonge....(uk. 140)
        • Kupitia kwake tunaona jinsi kuzingatia tamaduni bila tahadhari kunaweza kuleta maangamizi. Anamwelekeza Tuama na washauri wenzake dhidi ya kupashwa tohara/kufuata mila bila tahadhari (uk. 143)
        • Anaendeleza ploti. Ndiye anaye hadithia kisa cha Kipanga ambaye alianza kutumia pombe vibaya kwa kukataliwa na aliyemdhania kuwa babake (uk. 143)
        • Kupitia kwake mwandishi anaonyesha umuhimu wa mshikamano wa kifamilia katika maadili ya wana. Kukataliwa na baba kunamfanya Kipanga kuwa mraibu wa pombe. 
    2.  
      1. Chandachema
        • Kumwaga dukuduku-kuwasimulia wenzake kisa chake ili kupunguza mwemeo wa matatizo yake. Anawasimulia Umulkheri, Zohali, Mwanaheri na Kairu kisa chake (uk. 102) Bi Tamasha
        • Kujitenga na mazingira-Anaondoka kwa jirani baada ya Satua-mke wa jirani kuanza kumwona kama mzigo (uk. 103)
        • Kuwasaka walezi/kutaka kurudiana na walezi/ukoo. Chandachema anatafuta asili ya mama yake Rehema. Anapopata ameolewa anahiari kutoendelea kumtafuta, (Uk. 104)
        • Kufanya maamuzi/kuchukua msimamo imara wa kujitegemea. Chandachema anasema kwamba hataenda kwa shangazi yake kulelewa huko; haihalisi kumwongezea mzigo (uk. 104) kwani ndiye aliyekuwa akigharamia masomo yake tangu hapo.
        • Kujiendeleza kielimu/ kuamua kutumia uwezo wao katika elimu kujiendeleza. Anaamua kuenda katika shamba la shirika la chai la Tengenea kwani alijua pana shule hapo; ataweza kujiendeleza kielimu (uk. 105).
        • Anasema atajitahidi masomoni (uk, 108) na kutafuta ajira Chandachema anapoona hawezi kuishi kujiendeleza kiuchumi katika mazingira ya nyumbani mwa Bwana Tenge, alianza kuchuma majani chai kwa malipo kidogo akiwa darasa la tano. (uk. 106)
        • Kuweka siri/kutosema kuhusu maamuzi yao ili yasivurugike. Chandachema hawaambii walimu wake kwamba amehama kwa Bwana Tenge hadi anapofanya mtihani wake. (Uk. 107) porota 4x1 = (alama 4)
      2. Dick
        • Anaingilia ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kuhofia adhabu ya mwajiri wake.
        • Kutaka kukidhi mahitaji ya kimsingi kulimsukuma kuingilia ulanguzi wa dawa (uk. 122)
        • Kuuona/kuichukulia hatua kuuchukulia uamuzi anaotoa kuhusu kuingilia uovu kama majaliwa hivyo kupunguza uzito wake. Anasema ulanguzi ndio hali aliyoandikiwa na Mungu (uk. 122-123)
        • Anatathmini matendo yake na kuwazia athari za matendo hayo. Anaamua kuacha ulanguzi wa dawa. (uk. 134)
        • Kujiendeleza kitaaluma. Anasomea Teknolojia ya mwasiliano baada ya kupokea nasaha kutoka kwa Mwangeka, kwa njia hii anakinga dhidi ya kurudia mazoea yake ya awali. (uk. 174)
        • Ujasiriamali: Anaanzisha biashara ya vifaa vya mawasiliano ambayo inamwezesha kujitegemea na kuwaajiri wenzake, (uk. 174) zozote 4x1 = (alama 4)
  2.  
    1.  
      • Tunu na Sudi kujitolea kuwa na mfumo wa kuongoza harakati za ukombozi/kupiga vita udhalimu. Kwa mfano walikuwa watetezi wa haki hata wakiwa wanafunzi Chuoni/Kula Kiapo
      • Sudi kukataa ushawishi wa viongozi dhalimu. "Onakataa, kuchonga kinyago cha Majoka hata baada ya kushawishiwa na Kenga (uk. 11-12)
      • Sudi kuwatia hofu viongozi dhalimu kwamba matendo yao yahamulikwa na washikadau kama vile Jumuiya ya Kimataifa (uk. 12)
      • Kuwazindua wanyonge kuhusu hila za viongozi. Sudi anadhamiria kuwazindua Kombe na Boza. (uk. 14)
      • Kuchunguza mienendo ya viongozi dhalimu. Ashua na l'unu wanatambua kwamba kuna mkutano wa Kenga na kutaka kujua wanachopanga. (uk. 15)
      • Kuwaita/kuwakusanya na kuwaongoza watu wasikilize na kukabili viongozi dhalimu. (uk. 15)
      • Migomo ya wauguzi na walimu kudai haki zao (uk. 16)
      • Kuwakabili viongozi dhalimu moja kwa moja na kuwaambia makosa yao. Ashua anamkumbusha Majoka kuwa hakuna mchuuzi asiyelipa kodi na kuwa hela hizo zingesafisha soko (uk. 25)
      • Maandamano - Tunu pamoja na wanaharakati wanaongoza maandamano kwa madhumuni ya kutetea haki za Wanasagamoyo na kupinga utawala dhalimu (uk. 32)
      • Mikutano ya hadhara na ya wachache kwa mfano, hotuba ya Tunu kwa wanahabari iliyoangazia ukiukaji wa haki za Wanasagamoyo (uk. 32)
      • Kuamua kuunga mkono uongozi ufaao bila kuzingatia tabaka, jinsia au umri. Raia wanamteua/wanamuunga mkono Tunu, Sudi kukataa kuchonga kinyago cha Majoka
    2.  
      1. Maudhui
        • Ukatili - kumbukumbu kuhusu mauaji ya Jabali (uk. 34)
        • Utetezi wa haki - Sudi na Tunu walipoanza brakati za utetezi wa haki walipokuwa chuoni (uk. 18) 
        • Propaganda kumbukizi kuhusu mashujaa kupitia tangazo kwenye redio (uk. 4).
        • Mapenzi - Ashua na Majoka walivyopendana kabla y Ashua kuolewa na Sudi (uk. 19, 23,49)
        • Elimu - Kumbukizi kuhusu Ashua alipofuzu na kukataa ajira katika Majoka and Majoka Academy 
      2. Wahusika
        • Kutokata tamaa kwa Asiya na Ngurumo wanapomwandama Billusda hadi akawapa kandarasi
        • Ukatili wa Majoka tunapoelezwa na Siti kuwa amewaua vijana wengine watano
        • Msimamo mkali wa Tunu na Sudi katika kutetea haki za wanasagamoyo kiasi cha kula kiapo. (uk. 18)
        • Tabia ya Majoka ya kuling'anga'ania/kulishikilia jambo (uk. 20) kwa mfano, anapomkanya Ashua asimwite mzee (uk. 20)
        • Tamaa ya Majoka maelezo ya mzee Kenga kupitia kwa sauti yake inayompitikia Majoka mawazoni (uk. 29)
        • Ashua ni Msomi kupitia kwa maneno ya Majoka anapomkumbusha kuwa ana shahada ya ualimu. (uk. 25)
        • Tabia ya Majoka ya dharau-kumbukizi za Majoka kuhusu kisomo cha Tuny (uk 32) (rin) Knoresha wogli wanaoka anaishi na mie


  3.  
    1.  
      1.  
        • Msemaji ni Ashua
        • Anamwambia Majoka
        • Wamo ofisini mwa Majoka
        • Majoka anakana kwamba kuna ushahidi wa wanafunzi kugeuka kuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka/dawa za kulevya ndipo Ashua anasema haya.(alama 4)(Dondoo limetolewa uk. 26)
      2.  
        • Sitiari - kipanga - kuku
          Imetumiwa kuonyesha uwezo wa mwenye mamlaka juu ya mnyonge
        • Swali la balagha
          Ushahidi utatoka wapi kama kipanga ndiye hakimu kwenye kesi ya kuku? Imetumiwa kumsulą mwenye mamlaka
        • Uhaishaji Tashihisi Uhuishi
          Kipanga kupewa uwezo wa kuwa mtaalam wa sheria hakimu. Kuonyesha upendeleo wa wenye ngivu dhidi ya wanyonge (alama 4)
    2.  
      1.  
        • Mkarimu - anawaletea akina Sudi, Kombe na Boza chai na mahamri (uk. 2)
        • Jasiri - Anamkabili Majoka na kumwambia udhaifu wa shule yake (uk. 25-26)
        • Mwenye kujitunya - Anaiheshimu ndoa yake ndiposa anakataa ushawishi wa Majoka. Anamwambia, "Mimi ni mke wa mtu..."
        • Mwenye hasira - Anamkanya Majoka kwa ukali anapomsimanga mumewe (uk.24) (v) Mwenye matumaini - Ana Imani kuwa maisha yatabadilika na kuwa bora soko likifunguliwa (uk. 25)
        • Mdadisi Anamhoji Majoka kuhusu sababu ya soko kufungwa milele
        • Mwenye mdomo mchafu/mpyaro. Anamwambia Sudi kuwa amechoka kupendwa kimaskini (uk. 47)
        • Kigeugeu - kuomba pesa kwa Majoka na hali anakashifu shule na kampuni yake. kumgeuka mumewe na kumshtumu kwa kutopata matunzo kwake. Hoja 6 x 1 (alama 6) 
      2.  
        • Kuelewa wakati wa kutukia kwa matendo kama vile maelezo kuhusu matukio nyumbani kwa kina Tunu saa mbili asubuhi.(uk. 51)
        • Mandhari hutabulisha/hubainisha wahusika katika onyesho (uk. 88) Tunatambulishwa kwa walinzi wa Majoka. 
        • Mandhari yanadokeza/huonyesha hali ya mchezo kama vile mgogoro (uk. 88)
        • Kulinganua hali za matabaka kwa mfano Majoka na mkewe Husda wanaishi kifahari ilhali Sudi na wenzake wanafanya kazi kwenye mazingira chafu.
        • Kuonyesha kueleza mahali pa tukio mchezoni.
        • Kujenga kuibua taharuki hivyo kuendeleza msuko.
        • Kubainisha kuonyesha maudhui kama vile uozo sokoni (uk. 1)
          Tanbihi
          Mtahiniwa akikita hoja zake kwenye mandhari moja tu kama vile afisini mwa Majoka atuzwe mradi ametosheleza hoja. (alama 6)
  4.  
    1.  
      1.  
        • Kauli ya kwanza ni ya rafiki ya Otii
        • Kauli ya pili ni ya Otii.
        • Otii anayakumbuka mazungumzo haya. Rafiki yake alikuwa akimwonya dhidi ya wasichana Mombasa
        • Anayakumbuka haya akiwa mgonjwa baada ya jamaa kuamua kuchangisha pesa za kumzikia, japo hajafa bado.
        • Yumo kibandani mwake 
          Hoja 5x1= (alama 5)
          Dondoo limetolewa uk. 100
      2.  
        • Kinaya-Kufuata asali ukala mzingani z ira
        • Sitiari-kulia mzingani, Nzi kufia kidondani
          kumaanisha kudhurika na jambo ambalo pia lina faida
        • Swali la balagha - pana hasara gani nzi kufia kidondani? (alama 2)
    2.  
      • Jamaa wamgona Otii ni mgonjwa mahututi. Wanaanza kuchangisha pesa za mazishi
      • Rafiki ya Otii anamwonya dhidi ya mahusiano ya kiholela na wasichana
      • Otii kutoyawajibikia maisha yake, anasema ni kufa kidondani si hasara
      • Rehema kuondoka bila kumuza Otii
      • Jamua kutozingatia ombi la Otii kuwa wamzike papo hapo, wanaishia kuaga kwenye ajali.
      • Jamaa wanamsema Otii akiwa papo hapo bila kujali kuwa wanamuumiza kisaikolojia
      • Jamaa kushikilia mila kiasi cha kujutia baada ya ajali. 
      • Mchezaji mwenzake Otii anamuumiza mchezoni kwa uchezaji hatari
      • Maafisa wa michezo wanamtelekez Otii baada ya kuumia
      • Otii anapopata nafuu baada ya kuumia harudi uwanjani anaanza kufanya kazi duni bandarini ambayo ametosheka kwayo.
      • Kauli ya waziri wa michezo kwamba pengo aliloacha Otii halingeweza kuzibika laonyesha ukosefu wa uwajibikaji kwani hakuna aliyemjali hata pale alipoumia akiwa michezoni. (Alama 6)

        Tanbihi 
        Mtahiniwa anaweza kuonyesha uwajibikaji au kutowajibika 
    3.   
      • Dennis anasoma kwa taabu
      • Wazazi wa Dennis kudharauliwa na kila mtu kwa umaskini
      • Wazazi wa Dennis kufanya kazi duni - vibarua vya kuwalimia matajiri mashamba
      • Kutojitosheleza kwa chakula. Dennis kunywa yu chuoni kwa kukosa 
      • Malazi duni. Shuka za Dennis zimechanika
      • Dennis hana pesa wala hana wa kumwazima
      • Dennis hana pesa za kununulia mahitaji madogo madogo (Uk 17) 
      • Umaskini - Dennis anakosa mahitaji ya kimsingi kama vile chakula na mavazi. Hali hii inamfanya kuogopa kutangamana na wenzake chuoni. Anapoishiwa anaogopa kuufungua mlango.
      • Dennis anaogopa kuhusiana kimapenzi na Penina kwa habu ya maskini uliomwandama.
      • Penina anamkandamiza anului anamdharau Dennis kwa sababu ya umaskini
      • Chumba cha Dennis ni kikavu hakina chochote cha kutamaniwa
      • Dennis hawezi kuzichapisha hadithi zake kwa sababu ya kukosa hela
      • Dennis anafukuzwa na Penina kwa sababu hawezi kujikimu wa kumkimu yeye
      • Dennis ni mtegemezi wa wazazi wa Penina ndio wanaowakimu kwa yote
      • Anapofukuzwa anabeba chole anachomiliki kwa begi moja tu
      • Umaskini unamfanya Dennis kujutia masomo yake ambayo hayamwezeshi kujinyanyua kiuchumi.  (alama 7)
  5.  
    1. Unafiki
      • Safia anaaminiwa na wakazi wake ilihali anawahadaa kupitia kwa matendo yake
      • Safia alimleta Kimwana wazazi wake wakijua kuwa ni msichana ilihali alikuwa mwanamume
      • Anamleta rafiki yake akisingizia kuwa ya wanasoma ilihali walishiriki mapenzi
      • Safia hujifunika gubiguhi akiwa mbele ya wazazi wake ilihali alifanya kinyume akiwa faraghani
      • Alipoulizwa na mamake kuhusu hali yake alisingiria kuwa ni malacia
      • Kimwana huwaamkua wazazi wa Safia kwa heshima ilihali ni mbovu wa maadili anashiriki mapenzi na Safia
      • Kimwana alijifunika surali asionekane na wazazi wa Safia waliodhani ni msichana ilihali alikuwa mwanamume.
      • Wazazi wa Salia walisawiriwa kama wacha Mungu ilihali waliwasimanga watoto wa wengine.
      • Salia anajitetea na kusema kuwa mamake alimfikiria vibaya na kuwa yeye anajilinda (alama 8)
    2.  
      • Matumizi ya nahau/msemo - alitunga donge kifuani mwake kuonyesha uchungu moyoni
      • Tashhisi - donge likaja juu likampanda - kuonyesha athari za hisia/kupandwa na uchungu Sant Un munte
      • Taswira(uoni) - donge likaja juu
      • Swali la balagha - kweli? Uongo?
        Kuonyehsa mgogoro/ukinzani wa nafsi Urudinii-kweli uongo/kweli/uongo - takriri na kuonyehsa mvutano ukilini mwake.
      • Usambamba- labda kweli anjifikiria mambo mabaya binti yake; labda kweli dhana yake..
      • Ulinganuzi wa ukinzani wa mawazo - kumtetea kumshuku 
      • Tanakuzi - kweli uongo; Kutetea - kushuku. 
      • Chuku - sauti kumtetea - haiwezekani (alama 12)
  6.  
    1.  
      • Amedhoofika amekanda kwa ugonjwa na kuteswa
      • Kudhulumiwa haki kutengwa penye haki
      • Kulaumiwa bila sababu
      • Kutofaidika kwa rasilimali kupuuzwa na miliki kutothaminiwa.
      • Kufanya kazi ngumu viwandani na kupokea ujira mdogo
      • Kutopewa huduma za afya 
      • Kutelekezwa katika hali duni ya maisha : chawa, kunguni; funza(alama 6)
    2.  
      • Mishororo minne katika kila ubeti
      • Vipande viwili katika kila mshororo isipokuwamshororo wa mwisho
      • Kipande cha kwanza cha mshororo kina mizani nyingi kuliko cha pili (7.4)
      • Mstari wa mwisho una mizani chache (ni mfupi) isipokuwa katika ubeti wa mwisho una (mizani 11)
      • Kila ubeti unajitegemea kivina, vina vya ndani ni tofauti kutoka ubeti mmoja hadi mwingine vina vya mwisho pia ni tofauti kutoka ubeti mmoja hadi mwingine (alama 4)
    3.  
      1. inkisari
        • kawa - ukawa
        • mwiliwe - mwili wake
        • ziso - zisizo
        • we - iwe (alama 1)
      2.  Kufinyanga sarufi
        • Na homa akipatwa - akipatwa na homa
        • Kwa tiba apuuzwa - apuuzwa kwa tiba
        • Funza na miguuni - na funza miguuni 
          (alama 1)
    4.  
      • Tashbihi - kama nyani
      • Kinaya -kufanya kazi ngumu kwa malipo duni
      • Sitiari - ndwele -matatizo -Nyota -bahati mustakabali (alama 3)
    5. Mtetezi wa haki/mzindushi (alama 1)
    6.  
      • mwenye tumaini - bado yuasubiri
      • Ana bahati mbaya - Nyota yake ni nyota ya huzuni (alama 2)
    7. Anapopatwa na homa/anapokuwa mgonjwa, yeye hupuuzwa kama nyani Hakuna anayemtambua hayo ni matatizo ya kusababishiwa/ni ugonjwa wa kusababishiwa.(alama 2)
  7.  
    1.  
      • Kama watu wasingekuwa na akili watu wote wangekuwa sawa matajiri na maskiniAkili humwezesha mtu kuwa tajiri/mwinyi.
      • Akili humwezesha mtu kuwazia hali yake.
      • Humwezesha kuunda vifaa vya kuyarahisisha maisha-kuunda kitanda
      • Humwezesha kupata chakula-bila akili hata nunda hapati chakula.
      • Akili humwezesha mtu kubagua vilivyo vibaya; hadhuriki, hivyo kusetiri afya yake.
      • Humwezesha mtu kupata matibabu kwa ndwele: anawazia spitali (vii) Akili huwezesha kutenga wahalifu na wasio wahalifu.
      • Humwezesha binadamu kuweka akib humwezesha kulinda mali(alama 6)
    2.  
      • Sitiari
        • akili si mali
        • akili ni mali
        • uhawa ng'onda 
      • Tanakuzi - maskini na tajiri
      • Swali la balagha-vipi gonjwa kikuganda wawazia spitali?
      • Kinaya-kuwa na matambara na kuambiwa umetajirika kwa hili.  (alama 4)
    3.  
      • Inkisari 
        • kigaragara - ukigaragara 
        • metajirika - umetajirik
        • alokijenga - aliyekijenga
          (kutosheleza idadi ya mizani) 
      • Mazida
        • muwili-mwili
          kutosheleza idadi ya miwani)
      • Udondoshaji wa maneno -
        • Pamwe mbinu - pamwe na mbinu
          (Kutosheleza idadi ya mizani).
      • Kufinyanga sarufi
        • gani inadumu mali-Mali gani inadumu
          (Kuleta urari wa vina) 
          (alama 4) 
    4.  
      • Urudiaji wa virai kama akili si mali
      • Urudiaji wa silabi sauti - silabi li nari katika ubeti wa kwanza
      • Urudiaji wa mshororo usambamba kama akili si mali  (alama 2)
    5.  
      • Mishororo minne katika kila ubeti.
      • Vipande viwili katika kila mshororo.
      • Vina vya ndani ya vya nje vinabadilika kutoka ubeti hadi mwingine.
      • Shairi lina kibwagizo kama akilisi mali, usingewera fikiri
      • Kila mshororo una mizani 16 (8,8)  (alama 4) 
  8.  
    1. Wimbo wa harusi - nache aila 
      kutaja 1
      mfano 1
    2.  
      • Kuozwa mapema nassineni inasema itaacha elimu
      • Ulipaji mahari -mitamba imepokelewa 
      • Shangazi na ami kuwa na nafasi katika ndoa.
      • Wanaooana hawana uhusiano wa kinasaba (alama 2)
    3.  
      • Kushusha na kupandisha kidalykulingana na hali anayotaka kuibua.
      • Kuvaa malebaya bibi harusi.
      • Kuigiza baadhi ya vitendo.
      • Kuihusisha hadhira pengine kwa uimbajikuimba pamoja.
      • Kuimba kwa kasi, wastani ili hadhira ipate taathira ifaayo.
      • Kutumia ishara miondoko ili kuonda ukinaifu.
      • Kutumia ala zinazaoafikiana na ujumbe wa wimbo.  (alama 6) 
    4.  
      1. Manufaa ya mahojiano
        • Ni rahisi kupata habari za kutegemewa kwa vile anakabiliana na kwa ana na mhojiwa 
        • Anaweza kurti anayehojiwa baadhi ya maswali.
        • Anaweza kuona vila/ishara ya uso za wawasilishaji hivyo kukua uelewa.
        • Majibu yanaweza kunakiliwa au kunaswa moja kwa moja yanapotolewa, hivyo kuhifadhika.
        • Anaweza kubadilisha mtindo wa kuhoji kulingana na kitembo cha elimu/uelewa wa anayehojiwa
        • Anaweza kung'amua wakati anapopewa habari zisizo za kweli hivyo kutozinakili.
        • Kwa vile anakabiliana na mhojiwa si rahisi kwa mhojiwa kukataa kujibu maswali
        • Mahojiano yanaweza kutolewa kupitia kwenye simu hivyo kupunguza gharama (alama 5)
      2. Changamoto
        • Tatizo la kimawasiliano huenda likaathiri utoaji wa habari
        • Huenda mhoji/mhojiwa asiwe na muda wa kutosha wa mahojiano/home
        • Mhojiwa kumshuku mhoji, hivyo kutotoa habari za kutegemewa.
        • Mhoji kuwajaza wahojiwa hofu kutokana pengine na kiwango chake cha elimu.
        • Kwa vile wahojiwa wanakabiliana na mhoji moja kwa moja, huenda wakampa habari za uongo ili kumfurahisha.
        • Ikiwa matini ya mahojiano imeandikwa kwa lugha tofauti, huenda pukawa na tatizo la kutafsiri
        • Ni njia ghali kwani kwa kawaida mtafiti sharti usatiri kukutana na mhojiwa.
        • Anayehoji akishindwa kuibua maelewano baina yake na mhojiwa mwanzoni, huenda mawasiliano yakatizwe, hivyo kuathiri vibaya utoaji wa habari(alama 5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2019 Kiswahili Paper 3 Questions With Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest