KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Questions Set 2

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali manne pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki..
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.       

SEHEMU YA A: RIWAYA

Assumpata K. Matei: Chozi la Heri

LAZIMA

  1. “Haiwezekani! Hili haliwekazi! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.        (alama 4)
    2. Eleza kwa kifupi yaliyowapata wahafidhina baada ya usemi huu.         (alama.4)
    3. Riwaya ya chozi la heri inaonyesha maovu yanayotamalaki katika jamii.Thibitisha. (alama 12)

 SEHEMU B: TAMTHILIA

Kigogo.Pauline Kea.

Jibu swali la 2 au la 3

  1. Tatizo la uongozi katika bara la Afrika ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Kwa kurejelea matukio kwenye tamthilia ya kigogo, jadili ukweli wa kauli hii    (alama 20)

AU

  1.    “Mtalipa kila tone la damu mlilomwaga sagamoyo ;wewe na watu wako.”
    1. Eleza muktadha wa maneno haya  (alama 4)
    2. Eleza sifa za mzungumzaji   (alama 4)
    3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma.   (alama 12)                

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI

  1. Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo, onyesha jinsi jamii imegawanyika kitabaka  kuegemea.
    1. Kielimu
    2. Kikazi
    3. Kiuchumi  (alama 20)                                                                                                                            

SEHEMU D: USHAIRI

  1. WASIA
    Huno wakati mufti, vijana nawausia
    Msije juta laiti, mkamba sikuwambia
    Si hayati si mamati, vijana hino dunia
    Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula

    Japo aula kushufu, na machoni vyavutia
    Dunia watu dhaifu, yaugua nasikia
    Vijana nawasarifu, falau mkisikia
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria
    Msije andama baa, makaa kujipalia
    Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria
    Uonapo yyang’aria, tahadhari vitakula.

    Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia
    Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia
    Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia
    Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

    Wawapi leo madume, anasa walopapia?
    Wamepita ja umeme, leo yao sitoria
    Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula

    Nambie faida gani, nambie ipi fidia
    Upatayo hatimani, waja wakikufukua
    Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia
    Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula.

    Vyatiririka tariri, vina vyanikubalia
    Alo bora mshairi, pa tamu humalizia
    Nahitimisha shairi, dua ninawapigia
    Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

    Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia
    Wakingie wanarika, na anasa za dunia
    Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    MASWALI:
    1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?.   (alama 4)
    2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili.    (alama 2)
    3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.   (alama 2)
      1. idadi ya vipande katika mshororo
      2. mpangilio wa vina katika beti.    
    4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili.   (alama 2)
    5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
    6. Eleza toni ya shairi hili.   (alama 1)
    7. Tambua:    alama 2)
      1. Nafsi neni
      2. Nafsi nenewa
    8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
    9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’       (alama 1)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Eleza maana ya miviga. (alama.2)
    2. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
    3. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
    4. Fafanua umuhimu wa ngomezi katika jamii. (alama.6)
    5. Eleza vizingiti viwili vinavyokumba ngomezi. (alama.4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Questions Set 2.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest