Maagizo
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki..
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
- Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
SEHEMU YA A: RIWAYA
Assumpata K. Matei: Chozi la Heri
LAZIMA
- “Haiwezekani! Hili haliwekazi! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza kwa kifupi yaliyowapata wahafidhina baada ya usemi huu. (alama.4)
- Riwaya ya chozi la heri inaonyesha maovu yanayotamalaki katika jamii.Thibitisha. (alama 12)
SEHEMU B: TAMTHILIA
Kigogo.Pauline Kea.
Jibu swali la 2 au la 3
- Tatizo la uongozi katika bara la Afrika ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Kwa kurejelea matukio kwenye tamthilia ya kigogo, jadili ukweli wa kauli hii (alama 20)
AU
- “Mtalipa kila tone la damu mlilomwaga sagamoyo ;wewe na watu wako.”
- Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
- Eleza sifa za mzungumzaji (alama 4)
- Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma. (alama 12)
SEHEMU YA C: HADITHI FUPI
- Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo, onyesha jinsi jamii imegawanyika kitabaka kuegemea.
- Kielimu
- Kikazi
- Kiuchumi (alama 20)
SEHEMU D: USHAIRI
- WASIA
Huno wakati mufti, vijana nawausia
Msije juta laiti, mkamba sikuwambia
Si hayati si mamati, vijana hino dunia
Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula
Japo aula kushufu, na machoni vyavutia
Dunia watu dhaifu, yaugua nasikia
Vijana nawasarifu, falau mkisikia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria
Msije andama baa, makaa kujipalia
Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria
Uonapo yyang’aria, tahadhari vitakula.
Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia
Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia
Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia
Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.
Wawapi leo madume, anasa walopapia?
Wamepita ja umeme, leo yao sitoria
Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula
Nambie faida gani, nambie ipi fidia
Upatayo hatimani, waja wakikufukua
Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia
Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula.
Vyatiririka tariri, vina vyanikubalia
Alo bora mshairi, pa tamu humalizia
Nahitimisha shairi, dua ninawapigia
Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.
Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia
Wakingie wanarika, na anasa za dunia
Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
MASWALI:- Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?. (alama 4)
- Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (alama 2)
- Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 2)
- idadi ya vipande katika mshororo
- mpangilio wa vina katika beti.
- Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
- Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
- Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
- Tambua: alama 2)
- Nafsi neni
- Nafsi nenewa
- Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
- Eleza maana ya msamiati: ‘aula’ (alama 1)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
-
- Eleza maana ya miviga. (alama.2)
- Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
- Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
- Fafanua umuhimu wa ngomezi katika jamii. (alama.6)
- Eleza vizingiti viwili vinavyokumba ngomezi. (alama.4)
Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Questions Set 2.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students