MAAGIZO
- Jibu maswali manne.
- Swali la kwanza ni la lazima
- Chagua maswali mengine matatu kutoka kwa sehemu zilizosalia:
Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Ushairi.
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
SEHEMU YA A
- SWALI LA LAZIMA
-
- Semi nini? (alama 1)
- Fafanua sifa nne za misimu (alama 4)
- Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali
Ewe kilizi
Ulozowea kujificha
Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio
Yanadi ilo juu mbinguni
Jua kesho ni siku ya siku
Siku ya kujua mbivu na mbichi
Kutofautisha jogoo na vipora
Na riba takaposhika, chake kisu
Ndipo utakapojua bayana
Ukoo wetu si wa kunguru
ikiwa hutayari
kisu kukidhihaki
sithubutu kamwe, wanjani kuingia
sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!
Maswali- Huu wimbo huitwaje? (alama 1)
- Eleza majukumu yoyote manne yanayotekelezwa na wimbo huu katika jamii (alama 4)
-
- Mivigha ni nini? (alama 2)
- Eleza sifa tatu za mivigha (alama 3)
- Fafanua matatizo matano ambayo yanaikumba fasihi simulizi duniani (alama 5)
-
SEHEMU YA B
RIWARA: CHOZI LA HERI: ASUMPTA MATEI
- “…haifai kucheza na uwezo wavijana, wao ni kama nanga. Huwezi kuzamisha na kuiongea merikebu.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo (alama 4)
- Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu ya wahafidhina. (alama 12)
- Baada ya dhiki faraja. Onyesha vile ukweli wa methali hii unavyodhihirika kwenye riwaya. (alama 20)
SEHEMU YA C
TAMTHILIA: KIGOGO: PAULINE KEA
- “Sitaki kuaibishwa na mwanamke mimi, siwezi.”
- Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
- Fafanua kwa hoja nane kuwa msemaji wa maneno haya anafaa kuaibishwa (alama 16)
-
- Jadili jinsi kumi ambazo kwazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)
- Eleza mifano mitano ya matumizi ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)
SEHEMU YA D : HADITHI FUPI
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
- Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi fupi zifuatazo.
- Mapenzi ya kifaurongo (alama 5)
- Shogake Dada ana ndevu (alama 5)
- Mame Bakari (alama 10)
- Ndoto ya mashaka: Ali Abdalla Ali
“Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi. Hadi lini haya mashaka ya kutengenezwa? Mashaka ya mashaka!- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika (alama 4)
- Fafanua mambo sita yanayomfanya mrejelewa aradue kufa. (alama 12)
SEHEMU YA E: USHAIRI
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Barabaraba do ni ndefu
Nami tayari nimecho katiki
Natama ni kuketi
Ni’nyooshe misuli
Nitulize akili
Lakini
Azma ya nisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka”.
Ingawa nimechoka
Jambo moja dhahiri
Lazima hufuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipandenakushuka
Jambo moja na kumbuka; Mungu
Je nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja na kiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ikiwa wangu mwisho haitauwahi kabla.
Maswali- Taja naueleze aina ya shairi hili (alama 2)
- Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
- Huku ukitoa mifano mwafaka eleza tamathali tatu za usemi ambazo zinajitokeza katika shairi (alama 3)
- Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano mitatu huku ukitolea mifano. (alama 3)
- Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama 2)
- Andika kifungu cha mwisho katika lugha ya nathari. (alama 4)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi (alama 4)
- Kuruba
- Siha
- Machweo
- Kujinasua
Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Maswali Set 1.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates