Kiswahili P1 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika insha mbili
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Kisha chagua insha nyingine moja kutoka kwa hizo tatu zilizo bakia.
  4. Kila insha isipungue maneno 400. 


MASWALI

  1. Wewe ni afisa anayeshughulikia maswala ya kijamii. Andika mazungumzo kati yako na mwanahabari kuhusu kuzorota kwa maadili katika jamii.
  2. Eleza chanzo cha kukithiri kwa mauaji katika jamii.
  3. Kuinamako ndiko kuinukako.
  4. Andika kisa kinachomalizika kwa maneno yafuatayo.
    ………………. Tangu siku hiyo niliapa sitasalimiana na dawa hizo za kulevya tena.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Swali la kwanza
    1. Insha iwe na mtindo wa tamthilia. Majina ya wahusika huandikwa upande wa kushoto wa karatasi.
    2. Insha iwe na kichwa kinachoeleza mazungumzo ni baina ya nani na mada husika.
    3. Maelezo mafupi huwekwa kwenye mabano.
    4. Yaliyomo au ujumbe ukuzwe kwa hoja maalum.
    5. Insha hii lazima iwe na sura ya tamthilia.
  2.                  
    1. Insha iwe na kichwa
    2. Aya ya kwanza iwe utangulizi wa kile kinachoelezewa.
    3. Maelezo yatolewe kwa mpangilio wenye mantiki
    4. Hoja kadhaa zijadiliwe kwa aya tofauti tofauti.
    5. Mtahiniwa anaweza toa mapendekezo yake ya kusuluhisha mauaji katika jamii.
    6. Ahitimishe kwa kujadili maoni yake kuhusu yale ambayo ameelezea.
  3.                          
    1. Mtahiniwa aandike kisa.
    2. Kichwa huwa methali aliyopewa.
    3. Mwili wa insha uwe na sehemu mbili
      1. Kuinamako
      2. Kuinukako
  4.                      
    1. Insha iwe na kichwa mwafaka
    2. Kisa kinachooana na hitimisho na kufafanuliwa
    3. Kisa kisimuliwe kwa nafsi ya kwanza umoja.
    4. Insha lazima imalizike kwa maneno aliyopewa.

MWONGOZO WA JUMLA KWA INSHA ZOTE
Karatasi hii hutahini uwezo wa kuwasiliana kwa Kiswahili kwa kuandika.
Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi, zenye utiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi, na hati nadhifu, Kutegemea raaagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.
Mtahiniwa lazima aisome insha ill aweze kuikadiria akizingatla viwango mbambali vilivyopendekezwa yaani A,B,C na D kotegemea mahaii popote pale pafaapo.
KIWANGO CHAD MAKI 01-05

  1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote vile, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha m hafifu sana, hivi kwamba miahini lazima afikirie kite anachojaribu kuandika. h
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maaeno ya Kiswahili kwa njia inayofaa. /f
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai, na insha ina makosa ya kiia aina ya kisarufi, kimaendelezo, kimundo, n.k.

VIWANGO TOFAUTI VYA D
IV (KIWANGO CHA CHINI)MAKI 01 - 02

  1. Insha haina mpangilio maalum, na haieleweki kwa vyovyote vile. Kwa mfano, kunakili swali au kujitungia swali tofauti na kutijibu.
  2. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili.
  3. Insha za aina hii zifanyiwe uamuzi na kiongozi wa kikundi
  4. Yule anayenakiii kichwa kutoka karatasi ya maswali lakini hakushughulikia mada inayokusudiwa atakuwa amejitungia swali

D (WASTANI) MAKI 03

  1. L Utiririko wa mawazo haupo,
  2. Insha haieleweki
  3. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
  4. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui
  5. Hakuzingatia urefu.
  6. Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 04-05)

  1. Insha hii ina makosa mengi ya kila aina. Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kusema.
  2. Insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili na haina mpangilio.
  3. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka kikamilifu
  4. Hana uhakika wa matumzi ya lugha na hupotoka hapa na pale.
  5. Mpangilio wa kazi ni hafifu na mtahiniwa hujirudia rudia
  6. Mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza k.m papa, badala ya baba, karamu badala ya kalamu,n.k.

KIWANGO CHA C MAKI 06-10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo.

  1. Mada haikukuzwa na kuendelezwa.
  2. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia.
  3. Hana ubunifu wa kutosha.
  4. Anaakifisha sentensi vibaya.
  5. Hana msamiati wa kuvutia wala msamiati mwafaka.
  6. Kuna makosa mengi ya sarufi, msamiati na hijai (tahajia)

VIWANGO TOFAUTI VYA C
C- (KTWANGO CHA CHINI) MAKI 06 - 07

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasiiisha mawazo yake.
  2. Hana msamiati wa kutosha wala muundo wa sentensi ufaao.
  3. Mada haijakuzwa m kuendelezwa kwa njia ifaayo.
  4. Ana makosa mengi ya sarufi, tahajia na msamiati.

C(WASTANI) MAKI 08

  1. Anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Hana ubunifu wa kutosha na dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.
  3. Uakifishaji wa sentensi zake si mzuri.
  4. Amejaribu kushughulikia mada altyopewa,
  5. Ana makosa ya hijai, sarufi na msamiati.

C+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 09-10

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo na mvuto,
  2. Dhana tofauti tofauti zimeanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna utiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lu
  4. Misemo, methali na tanakali za sauti zimetumiwa kwa njia hafifu.
  5. Anashughulikia mada aiiyopewa kwa utiririko mzuri.
  6. Kuna makosa ya sarufi, msamiati na hijai lakini bado insha inaeleweka,

KIWANGO CHA B MAKI II-15

  1. Mtahiniwa anaonyesha kuimundu lugha vilivyo.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
  3. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
  4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha mkubwa kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti na zikaleta maana sawa.
  5. Mada imekuzwa na kuendefezwa kikamilifu.

V1WANGO TOFAUTI VYA B
B- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 11 -12

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti akizingatia mada.
  2. Ana utiririko mzuri wa mawazo.
  3. Ana uwezo wa kutumia mitindo tofauti tofami ya sentensi.
  4. Makosa ni ya hapa na pale.

B (WASTANI) MAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha haii ya kuimudu lugha.
  2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo yanayodhihirka akizingatia mada.
  3. Matumizi ya lugha ya mnato yamejitokeza.
  4. Anatumia mifano michache ya msamiati teule /mwafaka.
  5. Matumizi ya tamathali za usemi yanaanza kudhthtrika.
  6. Makosa yanaweza kutokeahapa na pate.

B+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 14 -15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika - yanajitokeza waziwazi
  2. Anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia huku akizingatia mada.
  3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri.
  4. Sarafi yake ni azari vilevae uakifishaji wake.
  5. Mateayaiiaw^atooteal^fiinaiiak-

KIWANGO CHA A MAKI 16-20

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
    Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na taittririka ,
  2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora
  3. Ufrfjuji wake unadMrisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hah ya kumvutia msomaji wake.
  4. Kazi ya mtahiniwa ni nadhifu na hati ni nzuri.
  5. Insha hii imezingatia urefu unaotakikana

VIWANGO TOFAUTI VYA
A- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 16-17

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
  2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada.
  3.  Anaparnba lugha kwa kutumia tamathali za usemi.
  4. Anazingatia matumizi ya msamiati na sarufi
  5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi.
  6. Makosa machache yasiyokasadiwa.

A (WASTANI) MAKI 18

  1. Mawazo yanadhihirika zaidi na anashughulikia mada aiiyopewa.
  2. Anatumia lugha ya mnato.
  3. Anatumia msamiati wa hah ya juu na unaovutia,
  4. Sarufi yake ni nzuri zaidi.
  5. Anatumia miuado tofauti tofauti ya sentensi IdidimdL
  6. Anajieleza kikamilifu na makosa ni nadra kupatikana.

A+ (KIWANGO CHA JUU ) MAKI 19-20

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kulingana na mada.
  2. Anadhihirisha mawazo yake vizuri zaidi.
  3. Anatoa hoja zilizokomaa.
  4. Msamiati wake ni wa hali ya juu,
  5. Jumla ya makosa yote yaisizidi matano.

JINSI YA KUTUNZA INSHA MBALIMBALI

  1. Mtahiniwa asipozingatia sura ya insha aondolewe maki nne (4) baada ya kutuzwa (4 sura)
  2. Insha isiyotoshele idadi ya maneno itaondelewa maki mbili (2) baada ya kutuzwa.(2u)

SARUFI
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea.
Makosa ya sarufi huwa katika:-

  1. Kuakifisha vibaya. Kwa mfano, vikomo, vituo, alama ya kuulizia , n.k
  2. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
  3. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
  4. Kuacha an kuongeza neno katika sentensi, kwa mfano, "kwa kwa"
  5. Matumizi ya herufi:
    1. Mwanzo wa sentensi
    2. Majina ya pekee-
      1. Majina ya mahali, miji, nchi
      2. Siku za juma,miezi, n.k
      3. Mashirika, masomo,vitabu aiJk
      4. Mashariki, masomo, vitabu, n.k
      5. Majina ya kutambulisha k.m majina ya mbwa k.v Tom, Jim, Peter

MAKOSA YA HIJAI / TAHAJIA.
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukiyaonyesha yanapotokea. Makosa ya tahajia huwa katika:-

  1. Kutenganisha neno kama vile ' aliye kuwa’
  2. Kuanganisha neno kama vile kwasababu
  3. Kukata silabi vibaya kama vile 'ngano'
  4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘mahari badala ya ‘mahali’
  5. Kuacha herufi katika neno kama vile aliekuja' badala ya aliyekuja.
  6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama vile 'piya* badala ya pia'
  7. Kuacha alama mayotarajiwa kawepo katika herufi k.m.j,i
  8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno afikiapo pambizo au mwisho au kukiandika mahali si pake.
  9. Kuacha ritifaa au kuiweka pasipofaa. K.m Ngombe, ngom'be, n'gombe.
  10. Kuandika maneno kwa kifupi Kwa mfano,kan n.k,v.v,k.v

MTINDO
Mambo yamyochmigtizwa:

  1. Mpangilio wa kazi katika aya.
  2. Utiririko wa mawazo
  3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.
  4. Namna anavyotumia tamathali za usemi k.m methali misemo, jazanda n.k
  5. Kuandika herufi vizuri k.rn Jj, pp, Uv,n.k
  6. Sura ya insha.
  7. Kuorodhesha.

MSAMIATI
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kichopendekezwa.
MAUDHUI MA MSAMIATI.
Baada ya kusoma mtungo utafikiria maudfaui na msamiati uliomo kwa jumla.
ALAMA ZA KUSAHIHISHA
Hupigwa chini ya sehemu arnbayo kosa la sarufi limetokeza kwa mara ya kwanza tu.
Hupigwa chini ya sehemu au neno ambako kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu,
Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno,
Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa .Alama hii hutiwa juu ya neon lenyewe Maelezo mafupi kuhusu tuzo la mtahini yanahitajika
Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati kuonyesha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo.

MANENO

  • Maneno 8 Ukurasa 1 ¾
  • Maneno 7 Ukurasa 2
  • Maneno 6 Ukurasa 2 ¼
  • Maneno 5 Ukurasa 2 ¾
  • Mansoe 4 Ukurasa 2 ¾
  • Maneno 3
  • Ukurasa 4 ½

MANENO

  • 101-174 - Nusu
  • 175 - 274 - Nusu
  • 275 - 374 -Robo tatu
  • 375-400 -Kamiii
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest