Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2021 Westlands Mock Exams

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  •  Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka shehemu nne zilizobaki, yaani Riwaya, Hadithi fupi, ushairi na Fasihi Simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

SEHEMU A : TAMTHILIA
Pauline Kea : Kigogo

  1. LAZIMA
    1. Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 5)
      Yaani kusema kwamba mapenzi hayatiwi nyunguni na kutokoswa kama mahindi na maharagwe ni tusi tena? Ana nini kwani ambacho sina? Jamani mimi wa kulinganishwa na Samson Myahudi ama shujaa Lyongo wa waswahili. Nafikiri alikuzungusha ndonga. Mwambie uume si kuvaa suruali tu, hata wanawake wanazivaa.
    2. ... hata wanawake wanazivaa. usemi huu unaafiki wahusika katika tamthilia, Jadili. (alama 5)
    3. Msemaji wa maneno haya ni kigogo. Thibitisha (alama 10)

SEHEMU B : RIWAYA, A. Matei : Chozi la Heri
Jibu swali la 2 au la 3.

  1.                
    1. ….. suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Usalama ni mmojawapo ya mahitaji ya kibinadamu.
      Thibitisha ukweli wa kauli hii. (alama 10)
    2. Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika kujenga ploti. (alama 10)
  2.  ‘Mimi sitakufa maskini’
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2.  Eleza toni ya dondoo hili (alama 2)
    3. Hiari ya maamuzi ya wahusika mbalimbali yamewaletea madhila anuwai. Jadili.(alama 14)
      (alama 14)

SEHEMU C: TUMBO LISILO SHIBA NA HADITHI NYINGINE.
Wahariri: Alifa Chokocho na Damu Kayanda
Jibu swali la 4 au la 5.

  1. Mohammed Khelef Ghassany “Mame Bakari”
    “……… Bwana na Bibi hawawezi kukuvunja,”
    1.  Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 3)
    2. Fafanua jinsi wazazi wa msemewa hawakumvunja. (alama 7)
    3. Jadili ‘mitihani’ katika hadithi ya ‘Mtihani wa maisha’ (alama 10)
  2.  Mtoto wa kiume amesawiriwa kupitia changamoto si haba katika jamii ya sasa.Tetea kauli hii ukirejelea hadithi ya Ndoto ya Mashaka , Mapenzi kifaurongo na Masharti ya kisasa. (alama 20)

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7.

  1. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu masuali
    1.  Mkata ni mkatika, harithi hatorithiwa
      Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
      Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
      Mrithi nini wanangu?

    2. Sina ngo’ombe sina mbuzi,sina kondesi na buwa
      Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
      Sinamazurimakuzi, jinsi nilivyoachiwa
      Mrithi nini wanangu?

    3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa
      Sina chembe ya majazi, mno ni kukamuliwa
      Nakwa’cheni upagazi, mgumu kwenu ku’tuwa
      Mrithi nini wanangu?

    4. Sina sikuacha jina, mkatahatasifiwa
      Hata nifanye la mana, mno ni kulaumiwa
      Poleni wanangu sana, sina kwenu cha kutowa
      Mrithi nini wanangu?

    5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwa liwa
      Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
      Sina wanangu mi sana, la kwacha nakuraduwa
      Mrithi nini wanangu?

    6. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa
      Nyuma yangu ilidhiki, na mbele imekaliwa
      N’na wana na mikiki, hadi n’tapofukiwa
      Mrithi nini wanangu?

    7. Sinai la kesho kwenu,wenyewe kuiongowa
      Muwane kwanyingi,mbinu Mwende pasi kupuwa
      Leo siyo, keshoyenu,kama mutaji kamuwa
      Mrithi nini wanangu?
      (Kina cha maisha A.S.Mohammed)

      MASWALI
      1. Eleza hali ya mzungumzaji katika shairi hili ( alama 4)
      2. Eleza dhamira kuu ya mshairi kulitunga shairi hili (alama 2)
      3. Ni nani anayezungumziwa na nafsi neni katika shairi hili? (alama 2)
      4. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
      5. Fafanua mbinu tatu za lugha zilizo tumiwa katika shairi hili (alama 3)
      6. ambua bahari ya shairi hili ukizingatia. (alama 4)
        1. Mizani
        2. Vina
      7. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya tutumbi (alama 3)

  2. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu masuali

    Jama, Jama, Jamani
    Mbona twabebeshwa mateso hivi
    Mizigo mikubwa ya dhiki kama
    Kwamba hatuna haki ya kusema
    Kukataa ndoa za lazima
    Kukataa kuozwa wazee
    Kukataa kukatishwa masomo
    Kukataa tohara ya lazima

    Jama, Jama Jamani
    Iweje tuteswe mateso haya
    Na watu wasio kuwa hata na haya kama
    Kwamba hatuna haki ya kulalamika
    Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya
    Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
    Kulalamikia kutolindwa na sheria

    Jama, Jama, Jamani
    Sasa hii ni awamu nyingine
    Na macho tumeyafungua kabisa
    Tumekataa kudhalilishwa kabisa
    Tumekataa kuteswa kama watumwa
    Tumekataa tohara ya lazima
    Tumekataa kuozwa....... Tumekataa! Tumekataa
    Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’

    Maswali
    1. Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
    2. Taja na ueleze mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi (Alama 3)
    3. Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
    4. Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kufanikisha shairi lake (Alama 4)
    5. Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine? (Alama 3)
    6. Eleza matumizi ya mishata katika shairi hili (alama 2)
    7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama 3)
      1. awamu
      2. kudhalilishwa
      3. Dhiki

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1.      
    1. Wewe ni mwigizaji wa michezo ya jukwaani. Eleza mambo sita ambayo utazingatia ili kufanikisha uigizaji wako. (alama 6)
    2. Mbinu ya uigaji sauti ina umuhimu gani katika fasihi simulizi: (alama 4)
    3. Soma utungo ufuatayo kisha ujibu maswali. (alama 10)

      Mwananguuu , ni wewe kweli !
      ndimi niliyekupa uhai mwana unoringia,
      Anokufanya upite ukinitemea mate,
      Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,
      Miungu na waone uchungu wangu,
      Radhi zao wasiwahi kukupa
      Laana wakumiminie,
      Uje kuzaliwa mara mia na wanao,
      Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,
      Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,
      Wakazamwanao wasikuuguze katika utu uzimawake
      (kutoka – Fani ya Fasihi Simulizi)

      Maswali
      1. Tambua kipera hiki cha Fasihi simulizi (alama 1)
      2. Eleza sifa zozote nne za kipera hiki cha Fasihi Simulizi (alama 4)
      3. Eleza kwa kutoa ithibati jinsia ya nafsineni? (alama 1)
      4. Fafanua umuhimu wa kipera ulichokitaja hapo juu katika jamii.(alama 4)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1.      
    1. Maswali ya Balagha - …….. ni tusi tena?
      Kejeli - uume si kuvaa suruali tu.
      Litifati – …na Samson myahudi
      Nahau – Kumzungusha ndonga
      Tashbihi – wa kulinganishwa na Samson
      (Zozote 5 x 1=5)
    2. Tunu – ni kiongozi pamoja na sudi katika kupigania ufunguzi wa soko la chapakazi.
      • Anaongoza wanasagamoyo katika maandamano ya kupigania haki zao.
      • Tunu kumkabili majoka na kumweleza wazi uovu katika uongozi wake.
      • Kupanga mikutano – Tunu anapanga mkutano siku moja na majoka – watu wanahudhuria mkutano wa Tunu na kupuuza mkutano wa Majoka
      • Kuangazia uovu wa unywaji wa pombe haramu – yeye na Sudi kule mangweni
      • Majoka kupanga kumwangamiza Tunu ili amuondoe kama mpinzani kwa kupinga uongozi wake.
      • Ashua – Anashughulika kukidhi mahitaji ya familia yake anaenda hata kwa Majoka kuwaombea watoto wake chakula
      • Siti kuwachukua watoto wa sudi na kuwapa chakula.
      • Bi Hashima anapomwonya pia kuwahimiza Siti na Tunu kuwa kama Siafu wakiwa wengi si rahisi kuwamaliza
        (Zozote 5 x 1=5)
    3. Msemaji ni Majoka .
      Majoka ni Kigogo.
      • Anaamrisha kusherekea sikukuu ya Uhuru kwa mwezi mzima pasipo kuwazia athari yazo kwa wanasagmoyo.
      • Anafunga soko la chapakazi.
      • Ananyakua ardhi ya soko la chapakazi kujenga.
      • Anatumia madaraka yake kutumia fedha za ufadhili kwa mradi isiyo muhimu kv uchongaji wa kinyago – cha marara.
      • Anatumia Mamlaka kuwatawanya waandamaji.
      • Kudhibiti vyombo vya habari na kukubali kutuo kimoja tu cha habari ,sauti ya mashujaa.
      • Kuwaua, kuwaangamiza wapinzani wake kama Jabali
      • Kuwafuta kazi wasiomuunga mkono – mfano – Kingi.
      • Kumpa Asiya ,mama Pima kibali cha kuuza pombe haramu.
      • Kuruhusu ukataji wa miti.
      • Kuongeza mishahara na kupandisha kodi.
      • Kuruhusu uwepo wa kiwanda cha kutengeneza sumu ya nyoka – watoto wa shule kuwa makabeji.
      • Kuamrisha kushikwa kwa Ashua bila hatia ili kumshurutisha sudi kumuunga mkono.
        (Zozote 10x 1=10)
  2.      
    1. Chozi – Umuhimu wa kuwa na usalama.
      • Vifo – Ridha kuipoteza familia yake – Terry mkewe, bintiye na mjukuu.Kutokana na ukosefu wa usalama, kuna vifo vinavyotokea, kutoka kwa vita vya baada ya uchaguzi, na maandamano – kuchomewa kwa nyumba ya Ridhaa.
      • Vita vya kikabila – vinasuka kutokana na uchaguzi na kutokubali matokeo ya kumtawaza kiongozi mwanamke Mwekevu.
      • Ubakaji – mabinti na mkewe wa kaisari kutendewa ubahaimu kwa kumpigia kura mwekevu.
      • Ukimbizi/wakimbizi – familia ya Ridhaa na kaizari kuhamia msitu wa mamba na kukaa kule kwa sababu ya ukosefu wa chakula.
      • Ukosefu wa chakula – katika msitu wa mamba, kuna ukosefu wa chakula na Ridhaa daktari mzima anaonekana kula mizizi hadi wanopoletewa msaada wa chakula na mashirika ya kidini.
      • Ukosefu wa makazi bora – Inawabidi kukaa katika kambi kwani hawakuwa na makazi bora.
      • Ukosefu wa misala – Hili unasababisha mkurupuko wa magonjwa kwa kutumia sadarusi kule katika mabanda ya sombera.
      • Usalama wa watoto - Umu, Dick na Mwaliko wanauzwa na Sauna aliyeaminiwa na mwajiri wake kuwatunza
      • Kuvunjika kwa ndoa – Subira
      • Uharibifu wa mali – kuvunja maduka, nyumba ya Ridhaa. Magari kuchomwa.
      • Upweke/ukiwa – Kufiwa na familia – kama Ridhaa anapoipoteza familia yake yote.
      • Kujeruhiwa – Subira kukatwa kwa sime
        (Zozote 10 x 1=10)
    2. Umuhimu wa mzungumzaji katika kujenga Ploti
      Mzungumzaji ni Rachel Apondi kupitia kwake tunapata kujua
      • Kukutana kwao – walivyokutana Mwangeka na Apondi
      • Kilichosababisha ujane wake
      • Alivyompanga umu
      • Ndoa yao na Mwangeka – Hatima ya ujane wa Mwangeka.
      • Tanaangaziwa uhusiano wa M. Dhababu na Apondi na alivyompanga.
      • Kupitia kwake na mwangeka Umu, Dick na Mwaliko wanakutana tena – Hatima ya utengano uliosababishwa na Sauna alipowaiba Dick/Mwaliko.
      • Mwangeka anaanza maisha mapya ya ndoa baada ya mkewe kufa kwa mkasa wa moto
      • Anaonyesha hatima ya msongo wa mawazo aliyokuwa nao. Ridhaa kuhusu mwanaye mwangeka kutokuwa na mke.
      • Anaonyesha hatima ya migogoro kati ya koo mbalimbali – anakubaliwa na Ridhaa baada ya kumzaa Ridhaa – licha ya koo zao kubaidika kama ardhi na mbingu.
      • Anaonyesha hatima ya donge chungu alilokuwa nalo UmulKheri tangu kuondoka kwa mama yake na akaanza kupona kutokana na pendo la Apondi na Mawangeka.
  3.           
    1. Maneno ya Songoa (alama 4)
      • Alijisemea – alisikika akisema.
      • Akiwa n’gambo
      • Kiriri anawazia akiwarai wanawe kurudi nyumbani na kumsaidia kuziendesha baadhi ya biashara.
    2. Toni ya kutamauka/kukata tamaa Songoa amekata tamaa na nchi yake kuwa haina kazi zozote. (alama 2)
    3. Hiari ya maamuzi ya wahusika mbalimbali na jinsi, maamuzi hayo yalivyowatetea madhila anuwai. (alama 14)
      • Majoka analifunga soko la chapakazi hali inayowachochea raia kuandmana na kumngatua mamlakani.
      • Ngao Junior anatumia mihadarati hatimaye inamuua kwenye uwanja wa ndege.
      • Majoka anamuua jabali kupitia ajali, Tunu anamtaka kuwaleta wachunguzi wa nje ili kuchunguza ajali hiyo, hali inayomtia wasiwasi.
      • Majoka ana kampuni kubwa zaidi inayozalisha dawa za kulevya ambazo zinakuja kumuua mwanawe Ngao Junior.
      • Kitendo cha Husda kutokuwa na mapenzi ya dhati kwa mumewe Majoka kinamfanya kuaibishwa na majoka hadharani anapomwambia hadharani kwamba hampendi.
      • Chopi anakubabli kutumiwa na majoka kuwaua wapinzake wake kama Tunu lakini naye anapokosa kumuua Tunu alivyoagizwa majoka anaanza kupanga mauaji yale.
      • Ngurumo anamuunga mkono uongozi wa Majoka lakini uongozi huo unakuja kumuua hatimaye, anauliwa na kundi la watu analotumia Majoka kuwaua wapinzani wake.
      • Boza anamruhusu Ngurumo kuuza pombe na mkewe mama pima, hatimaye Ngurumo anajihusisha naye kimapenzi.
      • Kombe anaunga mkono mrengo wa Majoka unaowadhulumu raia badala ya kuupinga Majoka kupitia kwa wafuasi wake anaanza kusambaza vijikaratasi vinavyoutaka kabila lake kombe kuhama Sagamoyo kwa madai si kwao.
      • Majoka anawaruhusu wanafunzi katika majoka na majoka academy kutumia sumu ya nyoka dawa za kulevya, hivyo kuwasababisha wote kuwa makabeji.
      • Hali ya mumewe Bi Hashima kutokuwa na bima karibu na inafanya familia yake ikose fidia kutoka kwa majoka alipokufa akifanya kazi katika kampuni yake.
      • Majoka anafungua biashara ya kukata miti hali inayotishia mvua kutonyesha jimbo ni hivyo kuathiri maisha ya raia.
      • Majoka kuwaua wengi, hali hii inasababisha kujiona akiwa amefungwa mikono kwa minyororo ndani ya ziwa la dawa anapozirai.
      • Majoka anampa mama pima kibali cha kuuza pombe haramu ambayo hatimaye inawaua na kuwapofisha raia.
        (Zozote 14 x 1 = 14 )
  4.         
    1. Aliyosema maneno haya ni Sarina
      • Akimwambia Sara
      • Walikuwa wanatafuta suluhisho kwa ujauzito wa Sara. (alama 3)
    2. Wazazi wa Sarah walienda hospitali na kumsubiri kuona daktari.
      • Waliweza kugharamia matibabu ya Sara.
      • Walimzungumzia kwa upole kule hospitali
      • Hawakumuonyesha kughadhabika kwao hata baada ya kujua kuwa aliwaficha
      • Wanamnyamazisha anapolia katika chumba cha daktari.
      • Walifahamu juu ya uzito wake kutoka kwa rafikiyo Sara na lakini hawakumgombeza.
      • Walimpa mtoto jina Mame Bakari.
      • Walimwandalia sherehe kumkaribisha mtoto nyumbani kwa kuchinja mbuzi na hata kuwaalika majirani.
        (alama 7 x 1=7)
    3. ‘Mitihani’
      • Mtihani halisi alioufanya shule ya upili na kufeli .
      • Samueli kueleza matokeo kwa wazazi, inabidi adanganye kwamba hajakamilisha kulipa karo.
      • Mtihani kwa Samueli kubaini aliyokuwa akiwaza nira.
      • Samueli kuwaeleza wenzake kuhusu matokeo yake ya mtihani.
      • Kutoweza kukabiliana na maisha baada ya kufeli mtihani na kutaka kujitoa uhai. Kujitosa maishani.
      • Babake Samueli anafeli mtihani wa kuonyesha mapenzi kwa mwanaye baada ya kufeli mtihani shuleni. Anampa kamba ili atoe uhai wake.
      • Mamake anafaulu katika mtihani kwa kuwa mlezi bora kwa kumnasua alipotaka kujitosa.
      • Wanakijiji wanashughulika kumwokoa Samueli alipotaka kujitosa majini.
      • Mwalimu mkuu anafeli mtihani wa maisha kwa kumwona Samueli kama mtu asiyefaa. Anamtupia matokeo.
      • Wazazi wa Samueli walikuwa na mtihani wa kukubali kuwa pesa zao za karo zilipotea bure.
        (Zozote 10 x 1=10)
  5. Mtoto wa kiume amesawiriwa kupitia changamoto si haba katika jamii ya sasa.Tetea kauli hii ukirejelea hadithi ya Ndoto ya mashaka ,Mapenzi Kifaurongo na Masharti ya kisasa
    • NDOTO YA MASHAKA
      • Kutojichagulia mke -Mtoto wa kiume hana hiari ya kujichagulia mchumba ,Mashaka analazimishiwa Waridi kama mke wake akiwa hana chochote. Waliowavamia chumbani mwake ni MzeeRubeya baba yake Waridi,Sheikh Mwinyimvua,kaka yake Waridi Mansuri na Rafiki ya keIdi.
      • Mstahimilivu -Mtoto wa kiume anastahili kustahimili madhila na hana pa kutorokea kukiwa na shida .Waridi anapokabiliwa na shida katika ndoa hujitorokea na kumwacha mume wake Mashaka akiwa pweke
      • Upweke – Mtoto wa kiume kushindwa kustahimili anapokumbana na upweke .Babake Mashaka upweke ulimshinda akafariki na wakazikwa Pamoja na mke wake.
      • Majukumu – Mtoto wa kiume anaachiwa majukumu ya ulezi Biti Kidebe alikuwa haishi kulala mikia miguu yake iliyomuuma.Hivyo,licha ya yeye kumlea Mashaka, naye Mashaka akamlea huyu bibi.Alitafuta kila aina ya vijikazi alivyoviweza tangu akiwa mtoto.Alipomaliza shule tu Biti Kidebe akafariki na kumwa mpweke.
      • Kubaguliwa kwa Mtoto wa kiume-Aibu ni madhila mengine yanayomkumba Mtoto wa kiume . Ndoa ya Mashaka na waridi ilimtia Rubeya aibu kwa kuwa binti yake ameolewa na fukara.Mzee Rubeya na familia yake wakaamua kurudi kwaoYemeni.
      • Kuachwa kwa sababu ya umaskini-Mashaka alikuwa na kazi duni yenye mshahara wa mkia wa mbuzi–alikuwa mlinzi wa usiku
      • Katika kampuni za Zuia Wizi Security(ZWS).Watoto wake wavulana walilala jikoni kwa jirani Chakupewa.Nafasi ilikuwa duni kabisa.Ilibidi mkewe apikie nje ya chumba chao isipokuwa,nyakati za mvua ambapo jiko huwekwa juu ya kinu kuzuia maji yanayotiririka.Siku moja Mashaka aliporudi kutoka kazini alikuta Waridi ametoroka na Watoto wote.Toka wakati huo hakuwaona tena.Akabaki mnyonge na mpweke zaidi.Utengano huo ulimfanya ajutie ufukara wake na kuuona kuwa ni udhia mkubwa maishani.
      • Msongo wa mawazo wanapopatwa na madhila – Mtoto wa kiume anapatwa na fikra nyingi za kujilaumu kutokana na shida nyingi zinazomuandama,Mashaka alikuwa na mawazo mazito na maswali yasiyo na majibu–kwa nini ‘Jumuiya za kimatiafa zinafumbia macho suala la ufukara?
        Ni ufukara uliomtenganisha yeye na Waridi,yeye na Watoto wake na kumwacha katika lindi la maumivu. Mashaka alijipa moyo kuwa Subira huenda ikamletea heri.Hata hivyo,aliendelea kusubiri
        Akitarajia kuwa mambo yatabadilika.Lakini mambo hayakubadilika.

    • MAPENZI KIFAURONGO
      • Ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu -Mtoto wa kiume anakosa kazi hata baada ya kuhitimu masomoni kwa sababu ya ufisadi katika jamii.Dennis anakosa kazi katika shirika la magazeti kwa kukosa kumjua mtu ilhali Shakil ananatafutiwa kazi na mamake kwa sababu anacheo kikubwa kazini mwake.Ni mkurugenzi mkuu.Dennis anaposaka kazi kwingi na anakosa .Miaka mitatu baada ya kufuzu chuoni na bado alikuwa akifanya‘tarmacking’ yaani kutafuta kazi.
      • Migogoro ya mapenzi –Mtoto wa kiume hana hiari kuachwa katika mahusiano ya kimapenzi. Rafiki wa kiume wa kwanza wa Penina anaachwa na Penina kusingiziwa kutokuwa mwaminifu na vilevile Dennis anaaachwa na Penina kwa misingi ya kuwa maskini
      • Kutamauka kwa masomo- Masomo chuoni kwa Mtoto wa kiume yanakuwa una ugumu kiasi kwamba wanafunzi wanahiari kufanya kazi ya matatu na kukusanya kodi za nyumba zinazomoilikiwa na wazazi wao.Dennis na wanafunzi wengine wanakaliwa na ugumu wamasomo katika chou kikuu.
      • Msongo wa mawazo kwa sababu ya umaskini, -Jambo hili linamtatiza Mtoto wa kiume ,Dennis anasumbuka kiakili kwa sababu ya hali na asili yake ya umaskini,anabaki mara nyingi kutamani kumezea mate magari makubwa yanayoendeshwa na wenye pesa Dennis anakiri kuwa “kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani’..
      • Utabaka katika jamii unaadhiri Mtoto wa kiume kwani anakosa kupendwa kwa sababu hana mali.Hali hii inaanzia chuoni baina ya wanafunzi .Umaskini unaleta matatizo kati ya masomo na mapenzi ya DennisMachora na Penina , Dennis anafinyika kimawazo kuhusu ikiwa kijana maskini anaweza kupendwa na msichana wa tabaka la juu,mwenye nacho anapita juu na mwenzake mchochole anapita chini
      • Kukejeliwa kwa kutoelewa – Mtoto wa kiume anastahali kuwa mtambuzi/mjuzi na kuwa na ufahamu wa mambo ,Dennis anachekwa na wanafunzi wenzake hasa msichana mmoja anayecheka hadi kuanguka kwa sababu ya Dennis kutaka ufafanuzi wa mafumbo ya Daktari Mabonga .Vile vile anaposhindwa kujibu maswali wakati wa mahojiano–anaaibika
      • Kujitegemea na kukimu familia – Dennis hapewi pesa za masurufu na wazazi wake anafaa kujimudu kupata chakula,hata ingawa wazazi wake ni maskini ,Penina anashangaa jinsi anavyokunywa uji,vilevile wanapomaliza chuo Penina anakaa tu nyumbani akimtegemea Dennis kwa kila kit una anapouliza kupewa anamwambia hajachangia chochote .

    • MASHARTI YA KISASA
      • Kutunza familia - Mtoto wa kiume ndiye anayetarajiwa kuikimu familia yake hata kama ana kazi duni na mshahara mdogo Dadi ndiye mchuma riziki yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa yake.pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya mpya na mapambo.
      • Kusaidia katika kazi za nyumba bila hiari -Madhila mengine yanayomkunba Mtoto wa kiume ni kulazimishwa kusaidis kazi nyumbani bila hiari yake .Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu.
      • Kutomwamini mke katika ndoa -Mtoto wa kiume anakumbana na madhila ya kutomwamini mke katika ndoa tunapoona Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja.Kila mara mkewe anapofanya hivyo,anaumia asana.Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume wengine. Dadi anapoamua kuzua nmpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu
      • Kudhibitiwa na mke katika ndoa - Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika Maisha ya ndoa lakini anashinda kumweleza.Licha ya kuwa Dadi aliona ugumu wakuzingatia masharti aliyowekewa na mkewe,hangeyavunja.Angefanya hivyo ndoa yao ingevunjika na huko kungekuwa ni kumvunja yeye pia. Dadi aliogopa kuambiwa kuwa yeye si mwanaume tosha
      • Kufuata amri za mke na anapokiuka na hata kumpeleleza kupata lawama kutoka kwa jamii - Kila mara Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula angeviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha. Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui. Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hatakupiga nguo pasi .Anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaanguka na kuumia vibaya sana jambo linalomshutua sana mkewe Pamoja na mwalimumkuu
      • Anayelazimika kumwitia ambulensi impeleke hospitalini.
      • Kufuata masharti anayowekewa na mke bila kukaidi -Mtoto wa kiume analazimishwa kufuata masharti asiyoyapenda kwa sababu ya kumpenda mke -Kwa kuwa Dadi alimpenda kidawa alikubali masharti ya kisasa bila kuyaelewa kama vile kukosa uamuzi juu ya idadi ya Watoto atakayetaka Anapangiwa masharti ya uzazi.Hana hiari ila kukubali kuwa na mtoto mmoja tu
      • Msongo wa fikra -Madhila ya msongo wa mawazo yanampata Mtoto wa kiume hasa anapowazia uaminifu wa ndoa yao.Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu.Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula. Kidawa kufanya kazi za umetroni kunafanya asimwamini
      • Dhihaka kutoka jamii – Mtoto wa kiume anakejeliwa na kuonekana kama asiyekuwa mume wakutosha mkewe kidawa akionekana anasimama na kunena na wanaume wengine .Mtoto wa kiume kufanya kazi za kike kwa sababu hana kipato kikubwa ikilinganishwa na mwanamke. Ncha nyingi za Maisha zinamfanya Kidawa atembeze bidhaa za uarabuni mitaani Jambo lililozidisha shauku ya Dadi kwa kidawa. Bi Zuhura alimkejeli Dadi kwa kumtaka amparalie samaki .Maneno ya watu yalimfanya Dadi aache kusaidia kazi za nyumbani
      • Kuteuliwa kwa mapenzi na mke bila hiari -Mtoto wa kiume anasuhubiwa na hata kuchaguliwa na mwanamke .Mwanamke ana uhuru wakijiteulia mume ,Kidawa alijiteulia Dadi
      • Hashirikishwi katika maamuzi muhimu-Mtoto wa kiume hashirikishwi katika maamuzi muhimu ya ndoa,anampa Dadi masharti ya kumsaidia,anamwaaamulia idadi ya watoto watakaopata ,masharti atakayofuata katika ile ndoa
      • Heshima - Mtoto wa kiume haheshimiwi kwa kuwa na kiwango cha chini cha elimu na kazi duni anazozifanya. Dadi anaamini kuwa ingawa hakusoma sana shuleni yeye si mjinga hivyo ana uwezo wakutambua mambo mbalimbali ila Kidawa ana kisomocha juu. Dadi anafanya kazi ya uchuuzi wa samaki kwavile hakusoma sana
        Kutuza
        Ndoto ya mashaka zozote 5 x 1=5
        Mapenzi kifaurongo zozote 7 x 1=7
        Masharti ya kisasa zozote 8 x 1=8
        Jumla 20
  6. Ushairi
    1. Hali yamzungumzaji. (al 4)
      • maisha yenye umaskini mkubwa.
      • maisha yasiyo kuwa na matumaini.
      • maisha yaliyo kosa thamani.
      • maisha yenye kusikitisha. (4x 1 = 4)
    2. Dhamira kuu ya mshairi (al 2)
      • kuwahimiza wanawe maishani ili kuhakikisha maisha mema ya baadaye kwa vile hali ya sasa ni ya kimaskini. (2 x 1 = 2)
    3. mzungumziwa – watoto (al 1)
      nafsi neni – mzazi (2 x 1 = 2) (al 1)
    4. toni ya shairi (al 2)
      • masikitiko
      • kutamauka/kukosa matumaini
      • ya kuhuzunisha..Mwanafunzi athibitishe (1x 2= 2)
    5. mbinu tatu za lugha zilizotumika. (al 3)
      • sitiari – mkata ni mkatika
      • Balagha – mrithi nini wanangu?
      • takriri – sina (3 x 1 = 3)
    6. Bahari ya shairi ukizingatia. (al 4)
      • mizani – msuko
      • vina - ukara Mwanafunzi athibitishe(2 x 2 =4 )
    7. Ubeti wa mwisho – lugha ya nathari. (al 3)
      • mshairi ana matumaini kwamba wanawe wataimarisha maisha yao ya baadaye .Anawashauri wafanye bidii, wakabiliane na matatizo bila hofu. (3 x 1 = 3)Tathmini mishororo
  7. SHAIRI
    1. Hili ni Shairi Huru
      • Mambo matatu muhimu yaliyozungumziwa na mshairi na maelezo ya kila moja.
        Kutaja alama 1/2
        Kueleza alama 1/2
        Jumla 1)
    2.      
      1. Mateso
        • Mizigo mikubwa ya dhiki
        • Hakuna haki ya kunena
      2. Ndoa ya lazima
        • Kuozwa kwa wazee
        • Kukatishiwa masomo
      3. Tohara
        • Tohara ya lazima
        • Hawaruhusiwi kusema chochote
      4. Sheria
        • Haiwalindi
        • Kudhalilishwa kinyama
      5. Awamu tofauti
        • Wamekataa kudharauliwa
        • Wamekataa kuteswa
        • Wamekataa tohara za lazima.
    3. Muundo wa shairi
      1. Ni wimbo ambao haufuati muundo wowote wa ushairi
      2. Ni shairi huru
      3. Halina mpangilio wowote wa kiarudhi
      4. Halina mgao wa mishororo
      5. Halina vina wala mizani
      6. Halina kibwagizo
      7. Lina beti 3
      8. Mishororo inatofautiana katika kila ubeti
    4. Mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi. Maelezo ya kila moja
      1. Nyimbo-Amezitumia Kwa njia mwafaka ili anase hisia za wasomaji.
      2. Takriri-Amejaribu pia kusisitiza ili kuwekea uzito yale anayozungumzia.
        Anataka msomaji apate mvuto mzuri kwa lile analolizungumzia. Mfano tumekataa kudhalilishwa, tumekataa kuteswa, tumekataa tohara.
      3. Mdokezo. Mfano Tumekataa kuozwa ...
      4. Tashbihi . mfano ubeti wa pili- Kutumikishwa kama ya
    5. Sababu za mshairi kusema; ‘hii ni awamu nyingine’
      1. Ulikuwa ukurasa mpya wa maisha.
      2. Kuna mabadiliko ya kuondoa ukandamizaji.
      3. Wanawake wamekataa kuozwa kwa lazima.
      4. Wamekataa kudhalilishwa kabisa
    6. Mishata ni mishororo ambayo hupatikana katika shairi huru ambayo maana yake haikamiliki katika mshororo huo bali hukamilika katika mshororo unaofuata
      Imetumiwa kukamilishia ujumbe ili ueleweke na kuwasilisha ujumbe vilivyo
    7. Maana ya maneno
      1. awamu-Kipindi
      2. kudhalilishwa-kukandamizwa/ kudunishwa / kufedheheshwa
      3. dhiki-shida
  8.        
    1. Mambo ya kuzingatia kufanikisha uigizaji.
      • Nitakuwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira ili kuwafanya wapendezwe na miagizo.
      • Nitahakikisha nimeufahamu utamaduni wa jamii.
      • Nitapania kufahamu hadhira yangu pamoja na mahitaji yao.
      • Nitapanua kufahamu hadhira yangu pamoja na mahitaji yao.
      • Nitatumia ufaraguzi – uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga kwenye muundo asilia.
      • Kumbukumbu nzuri – uwezo wa kukumbuk
      • Nitabadilisha kiimbo kulingana na mahitaji
      • Kutumia viziada lugha k.v ishara za uso , ishara za mikono na miondoko mbalimbali.
      • Nitainjenga taharuki kwa mtuo wa kidrama ili kuvuta nadhari ya hadhiri yangu
      • Nitaishirikisha hadhira yangu kwa njia mbali mbali k.v uigizaji wa sehemu fulani nyimbo n.k.
      • Nitaitumia lugha kwa uhodari ili kuipa mvuto.
      • Nitavalia maleba yenye kuonna na nafasi ninayoigiza.
      • Nitajenga miahaka mwema na hadhira yangu.
        (zozote 6 x 1 = 6)
    2. Umuhimu wa uigaji sauti
      • Kuburudisha
      • Kusawiti uhalisia
      • Kumakinisha hadhira
      • Kusisitiza matendo.
    3.      
      1. Tambua kipera hiki cha fasihi simulizi (alama 2)
        1. Maapizo- miungu na wakuone/ laana wakumiminie (1×2= 2)
          Kutaja al 1- kufafanua al
        2. Jinsia ya nafsi neni ni gani? (alama 2)
          Mwanamke/ jinsia ya kike- ndimi nilompa uhai mwana unoringia (1×2= 2)
          Kutaja al 1- kufafanua al 1
        3. Eleza sifa zozote sita za kipera hiki cha fasihi simulizi (alama 6)
          • Maapizo yalitolewa kwa watu ambao walienda kinyume na maagizo ya jamii zao; wabakaji, waliowatusi wazazi wazee na wengineo.
          • Katika baadhi ya jamii za Kiafrika, maapizo yalitolewa kabla ya ulaji wa kiapo.
          • Maapizo yanaweza kutolewa moja kwa moja na yule aliyeathirika.
          • Kidini, Mungu, miungu au mizimu huweza kutoa maapizo kuhusu mustakali wa mtu fulani.
          • Maapizo huaminiwa kuwa yataleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa kuyaepuka kwa kutenda mema.
          • Maapizo hutumia lugha fasaha. Lugha ya ulumbi.
          • Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kujaza woga ili kuonya dhidi ya maovu.
        4. Fafanua umuhimu wa kipera ulichokitaja hapo juu katika jamii (alama 4)
          • Hutumiwa kama nyenzo ya kuwaonya wanajamii dhidi ya matendo hasi.
          • Hutambulisha jamii. Kila jamii ina namna yake ya kuapiza.
          • Hukuza umoja katika jamii. Kuwapo kwa kaida na miiko sawa huwafanya watu kujihisi kuwa kitu kimoja.
          • Huadilisha. Wanajamii hujifunza kutenda mema ili kuepuka laana.
            (4×1= 4)
          • Mtahiniwa afafanue hoja zake ili zilingane na kipera cha maapizo.
        5. Fafanua njia sita jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi (alama 6)
          • Wanafunzi hukariri, hughani na kuimba mashairi katika tamasha za muziki.
          • Mawaidha na vipera vingine vya fasihi simulizi hupitishwa katika sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2021 Westlands Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest