MAAGIZO
- Andika insha mbili.
- Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Chagua insha nyingine moja kati ya tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha sharti iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Andika wasifu wa ndugu yako ambaye anakaribia kuustaafu hivi karibuni.
- Andika insha kuhusu umuhimu wa vijana katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
- Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
Chombo cha kuzama hakina usukani. - Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
Tulijifunga kibwebwe kuwaopoa wahasiriwa waliokuwa wamefunikiwa na vifusi vya
maporomoko ya jengo hilo lakini juhudi zetu ziliambulia patupu.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- WASIFU
Mtahiniwa azingatie muundo wa wasifu.
Mambo chanya yatakayowasilishwa mfano.
- Mwaka wa kuzaliwa mhusika.
- Alikozaliwa mhusika.
- Wazazi wake ni akina nani na pia aila yake.
- Alikosomea/elimu yake.
- Vikwazo alivyoweza kukabiliana navyo katika elimu yake.
- Ufanisi wake katika elimu.
- Kazi na vyeo alivyopata.
- Hii ni insha ambayo inamhitaji mtahiniwa kufafanua/kujadili mawazo yake au mwelekeleo wake kuhusu nafasi ya vijana katika utangamano wa kijamii.
Baadhi ya hoja.
- Vijana ndio wengi.
- Vijana wanathaminiana na kuaminiana hivyo ni rahisi kuwasihi wenzao kutangamana.
- Ikiwa vijana wataweza kufunzwa maarifa au pengine mbinu ishi za kukabiliana na matatizo wataweza kuwasilisha mbinu hizi kwa wenzao.
- Ni muhimu vijana kuepukana kutumiwa na viongozi.
- Kundi la vijana laweza kutumia nishati kuleta shughuli zinazoleta utangamano kama vile michezo.
- Vijana wanaweza kujisajili katika vyuo mbalimbali nchini na kuleta utangamano.
- Vijana wanaweza kutumia lugha yao kama Sheng’ na kuleta utangamano.
- Vijana wanaweza kutumia himizo kukomesha ukabila na kuleta utangamano.
- Kushiriki katika shughuli za kiusomi kama vile kongamano za vijana huwezesha vijana kuja pamoja.
- Mshikamano unaweza kudumishwa kupitia ndoa za mseto.
Na mengineyo yakadiriwe pia
Tanbihi. - Mtahiniwa anaweza kuchukua mwelekeo wa kuonyesha mambo ambayo vijana wanaweza kufanya ili kuleta mshikamano wa kitaifa.
- Mtahiniwa anaweza kuonyesha hatua ambazo vijana wamechukua kuleta mshikamano wa kitaifa.
- Mtahiniwa anaweza kuandika na kuchanganya mielekeo yote miwili akataja hoja na kuitolea ufafanuzi kwa kuonyesha hatua ambazo vijana tayari wamechukua kuhusiana na swala hili.
- Ni insha ya methali
Chombo ambacho kimepangiwa kuzama/ama ambacho kina kasoro na kinaweza kuzama hata kikiendeshwa na nahodha wa aina gani, kitazama tu.
Jambo la kuharibika hata ukajaribu kulirekebisha haitawezekana.
Ruwaza zifuatazo za mawazo zaweza kujitokeza
- Mtahiniwa amsawiri msimulizi/mhusika ambaye anapuuza jambo hadi pale linapoharibika kisha akaanza kulirekebisha.
- Mtahiniwa abainishe hali ambapo licha ya juhudi za mhusika kurekebisha jambo hafanikiwi.
- Mtahiniwa anaweza kuandika kisa kinacholenga kuonyesha umuhimu wa kuyarekebisha mambo kabla kuharibika.
Tanbihi - Masharti ya usahihishaji wa insha za methali yazingatiwe – mtahiniwa lazima aelezee pande zote mbili za methali ili zijitoze wazi wala si kutaja upande wa pili akimalizia.
- Kisa kioane na kimalizio
- pengine mtahiniwa aweze kuandika kuhusu maporomoko ya jengo kubwa lililokuwa linaendelea kujengwa kisha likaporomoka, au mashambulio ya ugaidi.
- Aeleze chanzo cha mapomoroka hayo na kama baada ya juhudi zao na wahusika wengine zilipoambulia patupu walipata msaada.
- Shughuli za baadaye zilikuwaje, kulikuwa na maafa au ni majeruhi.
Tanbihi - Kazi ya mtahiniwa isahihishwe/na kukadiriwa kulingana na viwango vya usahihishaji
wa insha. - Insha yoyote ni alama 20.
- Alama za makosa ya sarufi na hijai ziondolewe.
- Mwanafunzi yeyote yule apewe haki yake kulingana na kazi aliyoiwakilisha.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kangundo Subcounty Pre Mock Exams 2021/2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students