KISWAHILI KARATASI YA 3 Marking Scheme - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
  1.  
    1.  
      1. Shairi huru
      2.  
        • Vina vinabadilika
        • Idadi ya mizani katika kila mshororo ni tofauti
        • Idadi ya vipande si sawa katika kila mshororo
        • Shairi halina kibwagizo
    2.  
      • Kuboronga sarufi mf. Nje na ndani ya nyumba
        watazunguka – watazunguka nje na ndani ya nyumba
      •  Inkisari mf. Kaziyo – kazio yako
    3.  
      • Uhaishaji / tashihisi / uhuishi mf. Jingi jasho likuoshe.
      • Tanakali za sauti – nje na ndani ya nyumba usiku mchana uwasake
      • Taswira mf. Kifo cha mende sharti miguu juu
    4. Hata ukiweka dawa nyingi na nyumba, uiame na ukae nje siku nzima ukisubiri, ukirudi usiku bado        utakuta ni wazima, wamelala kwani mende ni vichwa vigumu hawafi kwa urahisi.
    5. Ukijenga nyumba yako, hutakaa sana bila kuingiliwa na wageni
      • Hata mende wataanza kutalii bila ruhusa na bila woga wakila ulicho nacho wakuachie masalio
      • Hata ukiweka dawa hawafi
      • Haiwezekani mtu kuishi pweke kwenye nyumba
      • Mende wakifa sharti miguu juu.
    6.  
      • Kisha paa uweke na ukande
      • Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni utakaa
    7.  
      1. Mende
      2. Kifo cha mende
      3. Mende nyumbani

Tamthilia

  1.  
    • Ukosefu wa dawa hospitalini
    • Ufisadi
    • Kukosa lishe bora
    • Ukosefu wa ajira
    • Umaskini / njaa
    • Kupanda kwa gharama ya maisha
    • Ahaadi za uongo
    • Mishahara duni
    • Vitisho kwa wananchi
    • Wananchi kupigwa wanapoandamana
    • Maandamano na migomo
    • Ukoloni mambo leo
    • Unafiki
    • Migogoro kutokana na viongozi wasoadilifu
    • Magonjwa
    • Ubadhirifu wa mali ya umma
    • Uchafuzi wa mazingira
    • Dini kutumiwa kama ngazi ya uongozi
    • Wizi – Fimbo ya meya
    • Matumizi ya propaganda
    • Utabaka – madiwani na wananchi
    • Ubinafsi na tamaa
    • Uongozi mbaya
    • Kukosa maendeleo
    • Matumizi mabaya ya vyombo vya dola
    • Utegemezi wa misaada kutoka ng’ambo
    • Tenga tawala
    • Mauaji – wakati wa maandamano
    • Elimu duni Hoja 20 x 1 = 20
  1.  
    1. Haya ni maneno ya Daktari Siki akimwambia Mstahiki Meya.
      Wako nyumbani kwa Mstahiki Meya.
      Hii ni baada ya meya kuuliza Siki ni watu wangapi wanamuunga mkono.
    2.  
      1. Wana Cheneo wana njaa – chakula
      2. Wana kiu ambayo haikuzimwa – uongozi mbaya. 2 x 2 = 4
    3.  

      Meya

      Siki

      Fisadi

      Mnafiki

      Mwenye hamaki / kiburi

      Mwoga

      Msaliti

      Mtetezi wa haki

      Mwadilifu

      Jasiri

      Mwenye busara

    4.  
      • Mgogoro baina ya meya na wafanyikazi wakitaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na mishahara bora Zozote 2 x 2 = 4
      • Mgogoro baina ya meya na Siki. Siki anamshauri Meya kuhusu uongozi wake mbaya lakini Meya anakataa
      • Mgogoro baina ya Meya na Diwani wa tatu (III) kuhusu nyongeza ya mishahara na kutolipa kodi kwa madiwani.
      • Mgogoro baina ya Meya na wanajamii wanaotaka huduma bora za kijamii
      • Mgogoro baina ya meya na askari – Wamechoshwa na hatimaye kumkamata meya. Za kwanza 4 x 1 = 4
  1.  
    1. Mazungumzo haya ni kati ya Fikirini na Fiona. Walikuwa njiani.
      Ni wakati ambapo Fikirini alikuwa ameachwa na basi la chuo.
      Fiona aliyekuwa Mmarekani mweusi amekutana na Fikirini na kutaka kutoka kwa hali hii.
    2.  
      • Kuchanganya ndimi – Ahaa! You guys are brothers.
      • Matumizi ya nidaa mf. Ahaa!
      • Kinaya – Ingawa Fiona anasema watu weusi ni ndugu zao, anamtapeli Fikirini na kumuibia.
      • Chuku – Fikirini anadai kwao wanawaabudu watu weupe.
    3.  
      • Fikirini kuachwa katika kitui cha basi na dereva mweupe.
      • Wahadhiri kutoa alama nyingi kwa wanafunzi weupe na chache kwa weusi.
      • Watu weusi kufuatwa madukani na mlinzi kwa kushukiwa kudokoa vitu
      • Wahudumu na wateja mkahawani kumwangalia Fikirini
      • Fikirini kukamatwa baada ya kuvuka barabara taa zikiwa zimewaka rangi nyeusi bali weupe wenzake hawakukamatwa.
      • Jela marekani zimejengewa watu weusi
      • Waume weusi hawapati shahada vyuoni, wanang’ania kula kalenda tu
      • Fikirini amechoshwa na bezo na dharau za wazungu
      • Fikirini kuulizwa maswali mengi yanayomdunisha. Toa mfano.
      • Fikirini kuitiwa polisi kwa kukosa kufunga zipu ya suruali yake.
      • Bob anamwuliza Fikirini kinachowatoa Afrika kuja kuwasumbua huko marekani
      • Fikirini anakumbuka jinsi Afrika wanavyowaabudu wazungu ambao hawawajali. Zozote 6 x 2 = 12

 

  1.  
    • Kuna matabaka matatu katka jamii. Maskini na matajiri na tabaka la wastani
    • Abu anakumbuka jinsi alivyokuwa maskini wa kupindukia miaka saba iliyopita anasema “Kijiji tulikuwa maskini wakupigiwa mfano”
    • Zama hizo msimulizi alikuwa maskini wa kutupwa, kula na kuvaa kwa taabu lakini alijibidiisha akajijengea kijijumba cha msonge kilichokandikwa kwa udongo.
    • Abu siku ya Arusi ni tajiri ana gari
    • Siku ya arusi gari lake limefuatwa na magari mengine.
    • Eneo walilozuru lilikuwa limezagaa harufu ya mchanganyiko wa manukato na mafusho yaliyokuwa yamefukizwa ndani na nje ya nyumba mandhari ya kitajir
    • Msimulizi alipoamua kupata jiko na kumuendea Amali yeye na mjombake, mama Zena alimkataa sababu ya umaskini
    • Msimulizi alihangaika vibarua kwa mitaa ya walalaheri na walalahoi. Aliishi kukopa na kufanya kazi za ziada
    • Msimulizi alifanikiwa kwenda arabuni na kuwa hamali alibahatika na kutajirika “sasa nikisowerea katika utajiri.”
    • Aliporudi nyumbani alijijengea nyumba ya kifahari, akanunua matatu, akawajengea wazazi wake
    • Anasema (Abu) Hakuwa na shida ya kuandaa harusi ya ndovu kumla mwanawe
    • Alipopeleka posa mara ya pili kwa kina Amali alikubaliwa kwa sababu alikuwa tajiri. Alipata orodha ya vitu avinunue kwa maandalizi ya Arusi. Zozote 10 x 2 = 20
  1.  
    1. haya ni maneno ya mwalimu Majisifu akimwambia Mashaka alipomletea barua ya mwaliko wa   wangwani. Wako nyumbani kwa Majisifu. Hii ni baada ya Mashaka kumwambia hajakuwa           akihudhuria kuwafunza Kiswahili na kumtania kwamba amekuwa mkaguzi wa shule na kujitetea          kwa maneno haya.
    2. Mbinu ya Kinaya – Msemaji ni miongoni mwa wanajamii wanaoirudisha jamii nyuma kielimu kwa        kutohudhuria vipindi vyake. Anamwambia Mashaka kuwa wanahitajika kusoma kukomboa jamii        ilhali yeye haendi kuwafunza. Yeye kama msomi hajafanya lolote kuikomboa jamii yake
    3. Ujinga
      Njaa
      Umaskini 3 x 1 = 3
    4.  
      • Katika jamii ya Majisifu hali ya elimu ni duni wengi hawajasoma kwa sababu tofauti mf. Wanawe Majisifu
      • Mashaka hakukamilisha masomo yake sababu ya wendawazimu
      • Amani anaacha masomo baada ya fitina za uchochezi na kufungwa jela
      •  Ben Bella hajasoma anasumbua jamii kwa vitendo kama uvutaji bangi na ubakaji. Hii ni utumwa wa ujinga.
      • Wanafunzi wa shule ya Nasaba bora hawasomeshwi vizuri. Mf. Majisifu haudhurii vipindi vyake vya Kiswahili
      • Imani anaacha masomo sababu ya ukosefu wa karo hivyo jamii kubaki nyuma kielimu
      • DJ Bob anakosa kusoma kutokana na ufukara wa familia yao. Anasingiziwa wizi na kufungwa jela ya watoto jambo linalomkosesha elimu
      • Hotuba ya kiingereza ya Mtemi Nasaba Bora haieleweki kwa sababu wengi wa wananchi hawajasoma mf Bi Kizee
      • Lowela anachia masomo kidato cha tatu kuponda raha
      • Dadake Fao anaachia masomo baada ya kuringwa na mtoto wa waziri
      • Fao anatamatisha masomo ya mwanafunzi mmoja baada ya kumringa hivyo kudumaza elimu yake
      • Pesa zilizotengewa kusomesha watoto wa familia maskini zatumika kusomesha watoto wa matajiri na kuwapeleka ng’ambo. Mfano Fao na Madhubuti. Watoto wa maskini wanabaki nyuma kielimu Zozote 5 x 2 = 10
  2.  
    • Ngoma ya vijana haikeshi (uk 5)
    • Mla nguruwe huchagua aliyenona (uk 14)
    • Hatafutaye hachoki (uk 17)
    • Lisilo budi hutendwa (uk 22)
    • Pasi na viganja viwili kofi hazilii (uk 41)
    • Kwa mbaya wako mzuri hakosi (uk 42)
    • Penye nia pana njia (uk 51)
    • Usione wembamba wa reli gari moshi hupita. (Uk 51)
    • Mdharau biu hubiuka (uk 51)
    • Safari ni hatua (uk 62)
    • Baada ya dhiki faraja (uk 66)
    • Ukikosa la mama hata la mbwa huamwa (uk 73)
    • Akipenda chongo huita kengeza (uk 79)
    • Damu nzito kuliko maji (uk 91)
    • Ujana ni moshi, ukienda haurudi (uk 92)
    • Achekaye kilema hafi hakijamfika. (uk 101)
    • Mgala muue na haki humpe (uk 104)
    • Mwenda juu kipungu hafiki mbingu (uk 119)
    • Kumbe kuinamako ndiko kuinukako, (uk 155)
    • Atendaye jambo asishe ni kama asiyetenda. (uk 161)
      Mwanafunzi ataje na aeleze aliyesema na maana ya methali   Zozote 10 x 2 = 20
  1.  
    1.  
      1. Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo huambatana na kanuni za jamii husika
      2.  
        • Hufanyiwa mahali maalum
        • Msingi wa matukio fulani katika jamii husika
        • Huongozwa na watu maalu
        • Huandamana na matendo
        • Utoaji wa nasaha / mawaidh
        • Maleba maalum
        • Hulenga kundi maalum
        • Huambatanishwa na nyimbo
        • Vyakula maalum Zozote 5 x 1 = 5
      3. Hasara
        •  Baadhi husababisha vifo mf. Tohar
        • Kusambaza magonjwa mf. Tohara
        • Baadhi hukiuka haki za kibinadamu mf. Ukeketaji
        • Baadhi huitaji rasilimali nyingi
        • Baadhi husisha imani na shirikina zinazosababisha uhasama baina ya wanajamii Zozote 3 x 1 = 3
    2.  
      1. Ngomezi ni matumizi ya ala/ngoma kupitisha ujumbe
      2.  
        • Filimbi
        • Kengeli
        • Milio ya ambulensi
        • mlio wa simu  Zozote 2 x 1 = 2
      3.  
        • Watu kutafuta kazi mijini na kutengana na jamii zao
        • Watu kutangamana na wengine kusasahau ngomezi
        • Ukosefu wa magwiji na kupiga ala / ngoma
        • Ukosefu wa magwiji wa kutengeneza ala / ngoma
        • Kelele nyingi zinazokanganya sauti za ngomezi
        • Elimu na teknolojia ya kisasa Zozote 3 x 2 = 6
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 Marking Scheme - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest