KISWAHILI PAPER 2 - 2019 LANJET JOINT MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

SEHEMU A: UFAHAMU (ALAMA 15)

Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali uliyopewa.

Kwa miaka mingi, maafisa wa afya ya jamii wamekuwa wakitahadharisha umma kuhusu athari za moshi wa sigara. Sasa kwa mara ya kwanza, watafiti wanasema wamethibitisha moshi wa sigara ni hatari kwa wasiovuta sigara.

Aidha wanasayansi hao wanasema moshi wa sigara husababisha mabadiliko makubwa katika mapafu ya mtu asiyevuta sigara. ‘Tumesikia kwa muda mrefu kwamba moshi wa sigara ni hatari kwa afya ya watu wasiovuta sigara lakini sasa tumepata thibitisho. Kwa mara ya kwanza, tumefanikiwa kutazama uharibifu wa moshi wa sigara kwa mapafu ya wahusika,’’ watafiti hao walisema katika ripoti yao iliyochapishwa mnamo mei 20 katika jarida moja la kisayansi.

Katika utafiti wao, watafiti hao walifanyia uchunguzi mapafu ya watu ambao hawakuwa wakivuta sigara japo walikuwa wakiishi na jamaa au marafiki waliokuwa wakivuta sigara. Aidha, watafiti hao waligundua kwamba mapafu ya thuluthi moja ya watu hao waliofanyiwa utafiti yalikuwa yameharibiwa vibaya sana kutokana na moshi wa sigara.
Ilithibitishwa kuwa mapafu ya watu hao ambao hawakuwa wakivuta sigara yalikuwa sawa naya wale ambao walikuwa wakivuta sigara. Kwa hivyo, mtu yeyote anayevuta sigara anapaswa kujua anaathiri yule aliye karibu na yeye. Watu ambao hawavuti sigara na ambao wanakaa karibu na wale wanaovuta sigara wamo katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa mbalimbali yanayohusiana na moshi wa sigara. Kwa mujibu wa maafisa wa afya, moshiwa sigara unawezakusababisha magonjwa ya pumu, masikio na nimonia miongoni mwa watu wasiovuta sigara. Moshi wa sigara kadhalika unaweza kusababisha vifo miongoni mwa watoto wachanga.

Isitoshe, moshi wa sigara ni hatari kwa watu wazima wasiovuta sigara kwa sababu unaweza kuwaweka katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa hatari ya kansa ya mapafu, moyo na damu na mshutuko wa moyo. Watu ambao hawavuti sigara wanashauriwa dhidi ya kukaa karibu na watu wanaovuta sigara au kuwakubali watu kuvuta sigara ndani ya nyumba zao. Mtu anayekaa karibu na mtu anayevuta sigara hata dakika 8 hadi 20 yumo katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa ya moyo na shida mbalimbali za kupumua.
Kadhalika, wanawake wajawazito wanaokaa karibu na wavutaji sigara au wanaoishi na wavutaji sigara wamo hatarini ya kuzaa watoto walio na uzito wa chini mno. Kadhalika ni rahisi kwa mimba yao kuharibika.

Watoto wachanga ndio wamo hatarini kubwa ya kukumbwa na magonjwa hayo kwa sababu mapafu yao bado ni machanga mno kuweza kuhimili athari za moshi wa sigara

Maswali:

 1. Andika kichwa mwafaka cha kifungu ulichosoma. (alama 2)
 2. Taja vikundi viwili vinavyoathiriwa na sigara. (alama 2)
 3. Ni magonjwa yapi yanayoweza kusababishwa na moshi wa sigara? (alama 5)
 4. Eleza matokeo ya utafiti uliofanyika. (alama 2)
 5. Ni nini maoni ya mwandishi? (alama 2)
 6. Taja vikundi viwili vinavyoathirika sana na uvutaji sigara. (alama 2)

SEHEMU B: MUHTASARI

Uhuru wa Sudan Kusini.

Imewachukua wananchi wa sudan kusini muda wa miaka 56 kujitawala. Vita vya kupigania uhuru vilianza mnamo mwaka wa 1953. Kuna sababu kadhaa zilizosababisha wananchi wa Sudan kusini kupigana. Miongoni mwake ni rasilimali ya mafuta ambayo hupatikana upande wa Kusini japo haikuwa inawanufaisha kwa lolote. Mafuta haya yakiuzwa pesa zilizopatikana zilikuwa zinaendeleza upande wa Kaskazini pekee. Pia kulikuwa na ubaguzi wa rangi ambapo watu weusi wa upande wa Kaskazini,Watu wa Kusini walilazimika kujifunza lugha ya Kaskazini ambayo ni Kiarabu. Pasi na kuijua lugha hii, raia wa Kusini hawangepata kazi kule kaskazini.

Isitoshe,hakuna maendeleo yoyote upande wa Kusini.Miundomsingi ni mibaya na hakuna shule wala chochote kinachodhihirisha maendeleo. Upande wa juu uliongozwa na sheria za Uislamu, maarufu kama Sharia. Upande wa Kusini una Ukristo,jambo ambalo lilizua uhasama mkubwa wa kidini. Watu wa Kusini walihisi wamebaguliwa sana kwa msingi ya kidini.

Shujaa John Garang ni miongoni mwa Wasudani wa Kusini ambao walileta kugawanywa kwa nchi ya Sudan ili watu weusi wajitenge na waarabu. Alipofariki mnamo mwaka 2006,alikuwa ameiongoza Sudan ya Kusini kuweka mkataba na Sudan ya Kaskazini kuhususiana na nchi kushiriki katika kura ya maamuzi.

Japo kabla ya hii kura kupigwa,wananchi wa Sudan wanamheshimu sana kwa mchango wake kwenye mkutano uliokuwa Naivasha na ambao uliwapa wananchi wa Sudan Kusini kuamua iwapo walitaka kujitawala au la. Kura hii ilipigwa mnamo mwezi wa Disemba 2010. Sasa taifa hili ni huru.

Rais wa sasa wa Sudan Kusini,Bw.Salva Kiir anatarajiwa kuongoza taifa hili changa ili kufikia maendeleo makubwa. Hana budi kushirikiana na mataifa ya ulimwengu ili yamsaidie katika kuyatimiza malengo yake.

Sisi kama wakenya tutanufaika si haba. Tayari benki za hapa nchini kama Equity na KCB zina matawi yake huko.Isitoshe, tayari wafanyabiashara wetu wamepenya mpaka huko na biashara ya kuuza nafaka na bidhaa nyingine imenoga sana. Japo safari ya kutoka Nairobi mpaka Juba ni ndefu na yenye hatari,malipo yake ni mazuri. Isitoshe katika juhudi za kulijenga taifa hili changa, pana uwezekano kuwa Wakenya watapata nafasi za kazi. Hivyo wale amabo wamesoma wananufaika si haba. Pia hazina yao kubwa ya mafuta itatufaidi kwa maana tunaweza kununua kutoka kwao kuliko kuyaagiza kutoka nchi za Uarabuni.

Kadhalika,wakimbizi kutoka humo sasa wamerudi kwao na hivyo mzigo mkubwa wa wakimbizi umepungua kidogo. Wakiipata amani,nasi pia tutaipata na hatutakuwa na vita tena mipakani. Utangamano pia utakuwepo hasa kwenye miji ya mipakani. Licha ya manufaa haya yote,hivi karibuni mwaka wa 2013, Disemba; Sudan Kusini imerudi tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Riek Machar. Hali hii imeleta wasiwasi duniani kuhusu hatima ya taifa changa la Sudani Kusini. Hata hivyo,bado kuna matumaini ya kurudia amani kwani juhudi za upatanishi zinafanywa na Umoja wa Africa(AU).

MASWALI

 1. Kwa nini wananchi wa sudan kusini walipigania uhuru wao?(maneno 30-35)   (alama 6,1 ya mtiririko)
 2. Sisi kama wakenya tutafaidika vipi taifa hili la Sudan Kusini litakapojitawala?(maneno 50)alama 9;2 mtiririko matayarisho nakala chafu)

MATUMIZI YA LUGHA(ALAMA 40)

 1. Tunga sentensi zenye viambishi awali vifuatavyo
  1. Kukanusha wakati                                                 (alama 2)
  2. Kirejeshi
 2. Tumia kiambishi –ki-katika sentensi kuonyesha (alama 1)
  1. Waktai ujao hali ya kuendeleza
  2. Hali timilifu katika wakati wa kuendelea.
 3. Huku ukitumia viambishi u na ji unda nomino kutokana na vitenzi hivi. (alama 1)
  1. Zungumza
  2. Kwea
 4. Kanusha sentensi hizi                                     (alama 2)
  1. Kuliko na vita ni kule kulichochewa na wanasiasa
  2. Kanusha sentensihii kwa kuzingatia sehemu iliyopigiwa mstari.
   Utakapokuwa mkubwa utayaelewa mambo haya.
 5. Yape maneno haya ngeli zao (alama 2)
  1. Ghubari-
  2. Gulio-
 6. Vifungie sentensi viunganishi hivi (alama 1)
  1. Mingairi ya
  2. Fakaifa
 7. Ikamilishe methali hii kisha uitolee maana na matumizi (alama 3)
  Mlenga jiwe kundini…………………………
 8. Tunga sentensi kudhihirisha maana ya maneno haya (alama 1)
  1. Nyange
  2. Kulungu
 9. Unda jina kutokana na neno hili.             (alama 1)
  1. Husudu
  2. Ashiki
 10. Tumia’vua’kama. (alama 2)
  1. Kishazi huru
  2. Kishazi tegemezi
 11. Taja sifa mbili bainifu za sauti/d/ (alama 2)
 12. Eleza matumizi ya ‘kwa’katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
  1. Vijana kwa wazee walikusanyika ukumbini
  2. Kakake alifanya kazi hiyokwa ufasaha.
 13. Onkwani:mama!ulinipata wapi mimi?
  Mama:nilikuzaa,onkwani.
  Andika upya katika usemi wa taarifa ambapo mama Onkwani anamweleza baba Onkwani kuhusu mazungumzo haya.                                                                                  (alama 4)
 14. Tofautisha matumizi ya ‘po’ katika sentensi ifuatayo;-
  Talanta alipokuwa safarini kwenda Mombasa aliona palipoanguka gari lililokuwa limebeba mahindi.                                                                                                         (alama4)
 15. Unganisha sentensi hii kwa kutumia kirejeshi cha kati (alama 2)
  Wavu umekatika. Wavu ni wao.
 16. Andikja wingi wa sentensi hii katika hali ya ukubwa (alama 2)
  Kigoma chake kilipigwa hadikikapasuka
 17. Twasema; (alama 2)
  Kiatu cha mwanafunzi kimepotea.
  Toa kiatu na badala yake tumia kaniki
 18. Tofautisha sentensi hizi (alama 2)
  Ningalimwona jana ningalifurahi.
  Ningemwona jana ningefurahi
 19. Onyesha aina za shamirisho katika sentensi hizi (alama 3)
  1. Mama alipika wali
  2. Moishi alikatakata nyama kwa kisu.
  3. Kasisi aliwahubiria waumini kanisani
 20. Tunga sentensi kuonyesha viwakilishi hivi (alama 1)
  1. A-unganifu,ngeli ya LI-YA umoja
  2. Viwakilishi vya sifa,ngeli ya U-I wingi.

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

“Toa zote mpaka senti ya mwisho!Unanisikia,chapuchapu au nikuset.

 1. Hii ni sajili gani? Toa sababu. (alama 2)
 2. Eleza sifa tatu za sajili hii (alama 3)
 3. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama unavyotumiwa katika isimu jamii.(alama 10)
  1. Lahaja
  2. Ujozi lugha
  3. Wingi lugha
  4. Krioli
  5. pijini


MARKING SCHEME

SEHEMU A

Maswali:

 1. Andika kichwa mwafaka cha kifungu ulichosoma. (alama 2)
  • hatari ya sigara kwa watu wasiovuta (1x2)
   Tanbihi: kichwa kisizidi maneno sita.
 2. Taja vikundi viwili vinavyoathiriwa na sigara.(alama 2)
  • Watu wanavuta sigara.
  • Watu ambao hawavutia sigara lakini wanakaa karibu na wale wanaovuta sigara.
   Tanbihi:mwanafunzi aelezee aya tatu kwenye kifingu.
 3. Ni magonjwa yapi yanayoweza kusababishwa na moshi wa sigara? (alama 5)
  • Ugonjwa wa pumu.
  • Ugonjwa wa masikio.
  • Ugonjwa wa nimonia.
  • Saratani ya mapafu.
  • Mshtuko wa moyo.
   Tanbihi; mwanafunzi aorodheshe magonjwa kwa kurejelea aya ya nne kwenye kifung.
 4. Eleza matokeo ya utafiti uliofanyika. (aalam 2)
  • Mapafu ya ambao hawakuwa wakivuta sigara lakini walikuwa wanakaa kribu na watu wanaovuta sigara alikuwa sawa na wale ambao walikuwa wakivuta sigara.
 5. Ni nini maoni ya mwandishi? (alama 2)
  • Mtu yeyote anayevuta sigara anapaswa kujua anaathiri mtu aliye karibu naye.
 6. Taja vikundi viwili vinavyoathirika sana na uvutaji sigara. (alama 2)
  • Wanawake wasiovuta.
  • Watoto wachanga.

SEHEMU B

 1. Kwa nini wananchi wa sudan kusini walipigania uhuru wao?(maneno 30-35)   (alm 6,1 ya mtiririko)
  Matayarisho/nakala chafu
  Jibu/nakala safi
  • Kunyimwa faida ya raslimali yao.
  • Kubaguliwa kwa misingi ya kidini na kirangi.
  • Kunyimwa nafasi za kazi.
  • Kulazimishwa kujifunza lugha ya kiarabu.
  • Kunyimwa maendeleo. 95x1=5+1(mtiririko)=6
   Tanbihi: andika hoja zote muhimu kwa lugha ya nathari katika aya moja. Zingatia maendeleo ya maneno, uakifishaji na upatanisho wa kisarufi.

 2. Sisi kamma wakenya tutafaidika vipi taifa hili la sudan kusini litakapojitawala?(maneno 50)alama 9;2 mtiririko matayarisho nakala chafu)
  Jibu/nakala safi
  • Makampuni kama equity na KCB yana matawi yake hukohuko.
  • Wanabiashara wamepenya huko na wana mapato mazuri.
  • Kutakuwa na nafasi za kazi kwa wakenya hasa wale waliosoma.
  • Hazina yao ya mafuta hatufaidi.
  • Kutakuwa na amani mpakani.
  • Mzigo wa wakimbizi utapungua.
  • Kutakuwa na utangamano hasa kwenye miji ya mipakani.
   Hoja 7x1=7+2(mtiririko)=9
   Tanbihi: hoja zote muhimu ziandikwe kwenye aya majo kwa lugha nathari. Mwanafunzi azingatie uasifishaji na upatanisho wa kisarufi.

MATUMIZI YA LUGHA

 1. Tunga sentensi zenye viambishi awali vifuatavyo
  1. Kukanusha wakati (alama 2)
   Jibu:hakuenda/ hajaenda
  2. Kirejeshi
   Jibu: aliyeenda
   kilichovunjika
 2. Tumia kiambishi –ki-katika sentensi kuonyesha
  1. Waktai ujao hali ya kuendeleza(alama 1)
   Tutakuwa tukila ugali
  2. Hali timilifu katika wakati wa kuendelea.
   Amekuwa akisali.
 3. Huku ukitumia viambishi u na ji unda nomino kutokana na vitenzi hivi
  1. Zungumza
   Uzungumzi/uzungumaji
  2. Kwea
   Ukweaji
 4. Kanusha sentensihizi(alama 2)
  1. Kuliko na vita ni kule kulichochewa na wanasiasa
   Kuliko na vita si kule kulichochewa
   Kuliko na vita ni kule kusikochochewa.
  2. Kanusha sentensihii kwa kuzingatia sehemu iliyopigwa mistari.
   Utakapokuwa mkubwa utayaelewa mambo haya.     
   Usipokuwa mkubwa hutayaelewa mambo haya.
 5. Yape maneno haya ngeli zao(alama 2)
  1. Ghubari- LI-YA
  2. Gulio-   LI-YA
 6. Vitunge sentensi viunganishi hivi(alama 1)
  1. Mingairi ya- pasi ya
   Mf: ameenda mighairi ya ruhusa ya mwalimu.
   (mwalimu ahakiki kazi ya mwanafunzi.)
  2. Fakaifa- mambo mawili- la kwanza liwe zito kuliko la pili mf: iwapo nilimenya na ndovu, fakaifa sungura.
   (mwalimu ahauiki kazi ya mwanafunzi.)
 7. Ikamilishe methali hii kasha uitolee maana na matumizi(alama 3)
  Mlenga jiwe kundini----hajui limpataye.
  Usifanye jambo la kuumiza wengi
 8. Tunga sentensi kudhihirisha maana ya maneno haya
  1. Nyange
   Kelele,rabsha,fuso au mpumbavu,juha,zuzu, jura.
  2. Kulungu
   Mnyama wa porini anayefanya na papa.
   (mwalimu ahakuki sentensi ya mwanafunzi.)
 9. Unda jina kutokana na neno hili
  1. Husudu
   Husuda,hasada,hasidi.
  2. Ashiki
   Mshiki
 10. Tumia’vua’kama
  1. Kishazi huru
   Mvuvi alivua samaki wengi.
  2. Kishazi tegemezi
   Mvuvi aliyevua samaki wengi aliuaawa.
   (mwalimu ahakiki sentensi ya mwanafunzi kikamilifu.)
 11. Taja sifa mili bainifu za sauti/d/(alama 2)
  1. ….. kipasuo
  2. ……hutamkiwa kwa ulimi na ufizi
  3. …….mghumo
 12. Eleza matumizi ya ‘kwa’katika sentensi zifuatazo
  1. Vijana kwa wazee walikusanyika ukumbini
                           Kwa ya jumla
  2. Kakake alifanya kazi hiyokwa ufasa.
                           Kwa ya namna
 13. Onkwani:mama!ulinipata wapi mimi?
  Mama:nilikuzaa,onkwani.
  Andika upya katika usemi wa taarifa ambapo mama onkwani anamweleza baba onkwani juu ya mazungumzo haya.(alama 4)
  Mama Onkwani alimweleza baba Onkwani kuwa Onkwani alitaka kujua/ alishangaa alikokuwa amempata naye akamweleza kuwa alikuwa ameanzaa.
 14. Tofautisha matumizi ya ‘po’ katika sentensi ifuatayo;-
  Talanta alipokua safarini ya kwenda mombasaa aliona   palipoanguka gari nlililokuwa limebeba mahindi.(alama4)
  • Ya kwanza-wakati
  • Ya pili- mahali
 15. Unganisha sentensi hii kwa kutumia kirejeshi cha kati (alama )
  1. Wavu umekatika.wavu ni wao
   Wavu uliokatika ni wao.
   (mwalimu ahakiki sentensi ya mwanafunzi.)
 16. Andikja wingi wa sentensi hii katika hali ya ukubwa(alama 2)
  Kigoma chake kilipigwa hadikikapasuka
  Magoma yao yalipigwa hadi yakapasika.
  (mwalimu ahakiki kazi yamwanafunzi.)
 17. Twasema;
  Kiatu cha mwanafunzi kimepotea.
  Toa kiatu na badala yake tumia kaniaki
  • Kaniki ya mwanafunzi imepotea.
  • Upatanisho wa kisarufi kulingana na ngeli husika (Ki-Vi), moja na I-ZI, umoja) ufuliwe maanani.
 18. Tofautisha sentensi hizi
  1. Ningalimwona jana ningalifurahi.
   Hakuna matamaini au uwezekano wa kumwana na kufurahi, wakati wa kitendo umepita.
  2. Ningemwona jana ningefurahi
   Kuna matumaini au uwezekano wa kumwona na kufurahi.
   Wakati wa kitendo haujapita.
   Tanbihi: elewa matumizi tofauti ya ‘nge’ na ‘ngali’ katika sentensi
   ‘nge’- bado kuna nafasi.
   ‘ngali’- hakuna nafasi tena.
   ‘nge’ na ‘ngali’- hutegemeana na hubeba vitenzi viwili.
 19. Onyesha aina za shamirisho katika sentensi hizi(alama 3)
  1. Mama alipika wali
   Wali-kipozo/yambwa tendwa
  2. Mpishi alikatakata nyama kwa kisu.
   Kisu-ala/kitumizi
   Kasisi aliwahubiria waumini kanisani
   Nyama-kipozi/kitendwa
   Tanbihi: mwanafunzi atambue aina mbalimbali za shamirisho ambazo ni kipozi au yambuwa tendwwa, kitondo au yambwa tendwa na ala au kitumizi.
 20. Tunga sentensi kuonyesha viwakilishi hivi(alama 1)
  1. A-unganifu,ngeli ya LI-YA umoja
   Mf; la mwashi limechongwa
  2. Viwakilishi vya sifa,ngeli ya U-I wingi.
   Mf; mirefu itakatwa
   Tanbihi; viwakilishi mbalambali vinatahiniwa hapa na vilevile utunjgaji wa sentensi. Sheria za uakifishaji zikumbukwe mfano sentensi kwanza kwa herufi kubwa na kuisha kwa kitone,

Download KISWAHILI PAPER 2 - 2019 LANJET JOINT MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest