KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 BAHATI MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME)

Share via Whatsapp
  1. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la Zindukeni ukitoa maoni kuhusu sekta ya usafiri wa pikipiki.
  1. Fafanua njia mbalimbali za kustawisha michezo nchini. 
  1. Andika insha inayoafikia methali, Ukiona vyaelea vimeundwa. 
  1. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:
    Nilijaribu kuuinua mguu wangu uliojaa maumivu kutokana na jeraha…..


MARKING SCHEME

  1.  
    1. Hii ni insha ya kiuamilifu – Mtahiniwa azingatie vipengele hivi vya kimsingi: -
      1. Sura iwe ya barua rasmi – Anwani mbili.
      2. Mtajo – Kwa mhariri
      3. Kichwa cha barua/mada
      4. Kiwiliwili/Maudhui
      5. Hitimisho
        – Jina kamili la mwandishi liweko
        - Sahihi itangulie
    2. Hoja za kuzingatia.
      Maoni yaweza kuwa faida na / au hasara.
      Faida.
      1. Ajirakwa vijana.
      2. Kupunguza uhalifu.
      3. Usafiri wa haraka.
      4. Usafiri wa kutegemea.
      5. Kupenya maeneo yasiyofika magari.
      6. Kuimarisha uchumi wa jamii.

        Hasara.
      7. Kuongezeka kwa ajali.
      8. Kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na sekta ya usafiri.
      9. Kuzidisha msongamano kwenye hospitali.
      10. Kuongeza gharama ya huduma za hospitali.
      11. Kuchangia ongezeko la uhalifu/wizi wa pikipiki.
      12. Kuzidisha msongamano wa trafiki.
  1. Njoa za kustawisha michezo nchini.
    Vidokezo
    • Wanamichezo waajiriwe na serikali.
    • Waalimu wa michezo wawe wamehitimu.
    • Vipawa vya wanamichezo vitambuliwe mapema.
    • Vyuo maalumu vya michezo vianzishwe nchini.
    • Kufanya somo la michezo kuwa la lazima nchini.
    • Kuondoa siasa michezoni.
    • Wanamichezo wastaafu wapewe heshima.
    • Pawe na bima ya kushughulikia wanaoumia.
    • Vifaa vya michezo visitozwe ushuru.
    • Kuwe na vifaa vya kutosha na vya kufaa.

      Kutuza
    • Insha kamili iwe na hoja zisizopungua tano na zifafanuliwe.
  1. Ukiona vyaelea vimeundwa.
    Hii ni insha ya methali.
    Maana: Ukiona kitu kimenawiri au kizuri jua kuwa kuna juhudi na wakati uliotumika.
    • Mwanafunzi akuze pande zote mbili.
    • Mtahiniwa aonyeshe juhudi za aliyeelezwa zilizozaa matunda.

      Utahini/usahihishaji
    • Mtahiniwa akikuza upande mmoja asipite alama kumi.
    • Azingatie masharti yote ya insha ya methali.
    • Insha hii lazima iwe na kichwa/anwani ambayo ni methali yenyewe.
  1. Kisa kionyeshe alivyopata jeraha ( atumie mbinu rejeshi) na akiendeleze kisa bila kuongeza maneno kwenye kianzio au kuongeza maneno.
    MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA-2019
    UTANGULIZI
    Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa .Mawasiliano haya yanategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asili , ubunifu mwingi na hati nadhifu.Kwa ketegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha,ni lazima kutilia mkazo mtindo ,mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hoja ,msamiati ma mtindo ili aweze kuikadiri kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa.Viwango vyenyewe ni A,B’C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.                                                                                                     
    VIWANGO MBALIMBALI   
    KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05
    • Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wakutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile mtahiniwa anacho jaribu kuwasilisha.
    • Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa
    • Lugha imevurugika ,uakifishaji na insha ina makosa ya kila aina.
    • Kujitungia swali na kulijibu
    • Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa

      NGAZI MBALIMBALI KIWANGO CHA D
      D-(D YA CHINI) MAKI 01-02
    • Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile
    • Kujitungia swali tofauti na kulijibu
    • Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
    • Kunakili swali au maswali na kuyakariri
    • Kunakili swali au kichwa tu

      D WASTANI MAKI 03
    • Mtiririko wa mawazo haupo
    • Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
    • Matumizi ya lugha ni hafifu mno
    • Kuna makosa mengi ya kila aina

      D+ (D YA JUU) MAKI 04-05
    • Insha ya aina hii huwa na makosa mengi ya kila aina .Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha
    • Hoja hazikukuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
    • Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
    • Mtahiniwa hujirudiarudia
    • Insha yenye urefu wa robo ikadiriwe hapa.

      KIWANGO CHA C KWA JIJMLA: MAKI 06-10
    • Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
    • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia /hana ubunifu wa kutosha.
    • Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
    • Mtiririko wa mawazo unaanzakujitokeza japo kwa njia hafifu.
    • Insha inamakosa mengi ya sarufi, ya misamiati na ya tahajia (hijai.)
    • Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

      NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C
      C-(C YA CHINI) MAKI 06-07)
    • Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
    • Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
    • Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi

      C WASTANI MAKI 08
    • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu,
    • Dhana tofautitofauti hazijitokezi wazi.
    • Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
    • Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
    • Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa
    • Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
    • Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

      C+(C YA JUU) MAKI 09-10
    • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
    • Dhana tofautitofauti zinajitokeza japo kwa njia hafifu.
    • Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
    • Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
    • Ana shida ya uakifishaji.
    • Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

      KIWANGO CHA B KWA JUMLA: MAKI11-15
    • Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
    • Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
    • Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
    • Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
    • Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

      NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA B
      B-(B YA CHINI): MAKI 11-12
    • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.
    • Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
    • Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
    • Makosa yanadhihirika/kiasi

      B WASTANI MAKI 13
    • Mtahiniwa anadhihirisha haliya kuimudu lugha
    • Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
    • Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka.
    • Sarufi yake ni nzuri.
    • Makosa ni machache/kunamakosa machache

      B+ (B YA JUU) MAKI 14-15
    • Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
    • Mtahiniwa anawasiliha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
    • Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
    • Sarufi yake ni nzuri.
    • Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
    • Makosa ni machache ya hapa na pale.

      KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20
    • Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
    • Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
    • Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemiilikutoa hisia zake kwa njia bora nakwaurahisi.
    • Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo
    • Insha inaurefu kamili

      NGAZI MBAL1MBALI ZA KIWANGO CHA A
      A-(YA CHINT) MAKI 16-17
    • Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
    • Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anashughulikia mada.
    • Ana mtiririko mzuri wa mawazo
    • Msamiati wake ni mzuri na unaovutia.
    • Sarufi yake ni nzuri.
    • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
    • Makosa ni machache yasiyokusudiwa

      A WASTANI MAKI 18
    • Mtahiniwa anawasilishaujumbe vizuri kulingana na mada.
    • Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato/kunasa.
    • Anatoa hojazilizokomaa.
    • Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
    • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
    • Makosa ni nadra kupatikana

      A+(AYAJUU)MAKI 19 -20
    • Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
    • Anajieleza kikamilifu akitumia Iugha ya mnato.
    • Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
    • Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia zaidi
    • Sura yake ninzuri zaidi/kabisa
    • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentesi kiufundi.
    • Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

      VIWANGO MBALIMABLI KWA MUHTASARI
      USAHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA
      Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati,mtindo, sarufi na hijai

      MADHUI
    • Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa.
    • Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile.
    • Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule

      MSAMIATI
      Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika, Mtahinwa anatarajiwa kutumia msamiatiunaooana na mada teule. Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana namaendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

      MTINDO
      Mtindo unahusu mambo yafuatayo.
    • Mpangilio wa kazi kiaya.
    • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
    • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
    • Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano, methali, misemo, jazanda nakadhalika.
    • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp. Uu, Ww na kadhalika.
    • Sura ya insha
    • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

      SARUFI
      Sarufi ndio msingi wa 1ugha. Ufanisiwa mawasilianohutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yake katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufihuweza kutokea katika:
    • Matumizi yaalama za uakifishaji.
    • Kutumia herufi kubwa au ndogo mahali pasipofaa.
    • Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
    • Mpangilio wa maneno katika sentensi.
    • Mnyambuliko wa vitenzi na majina
    • Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
    • Matumizi ya herufi kubwa:
    • Mwanzo wa sentensi
    • Majina yapekee.
    • Siku za juma,mwezi n.k.
    • Majina ya mahali, mji, nchi, mataifa na kadhalika.
    • Mashirika, masomo, vitabu n.k.
    • makabila, lugha nk.
    • Jina la Mungu.
    • Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa, popi, simba, Tomi na mengineyo
    • majina ya watu (binadamu)

      MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA
      Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosaya tahajia huweza kutokeakatika:
    • Kutenganisha neno kwa mfano‘aliye kuwa’
    • Kuunganisha maneno kwa mfano ‘kwasababu’.
    • Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‘ngan –o’
    • Kuandika herufiisiyofaa kwamfano ‘ongesa’ badala ya ‘ongeza’
    • Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‘aliekuja’ badalaya ‘aliyekuja’.
    • Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‘piya’ badala ya ‘pia’.
    • Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile ji.
    • Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukiandika mahali pasipofaa.
    • Kuacha ritifa au kuiandika mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe,n.k
    • Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v., k.m., .y.v., n.k. na kadhalika.
    • Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

      ALAMA ZA KUSAHIHISHA
    • Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarafi limetokea kwa mara ya kwanza tu .
    • Hupigwa chini ya sehemu au neno ambalo kosa la hijai imetokea kwa mara ya kwanza tu.
    • Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilikia pambizoni kushoto.
    • Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno/maneno.
    • Hutumiwa kuonyesha msamiatibora. Alama hiihutiwa juu ya neno lenyewe.
    • Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
      Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lililotolewa. Kila ukurasa uwe na alama ya katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitiaukurasa huo.

      UREFU
      Mtahiniwa akiandika insha iliyo na maneno yafuatayo atakuwa ametimiza kiwango kilichoonyeshwa:
    • 1-174     -robo-asizidi alama             05/20
    • 175-274 –Nusu-asizidi alama           10/20
    • 275-374   Robo tatu-asizidi alama   15/20
    • Zaidi ya 375-Kamili
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 BAHATI MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest