MAAGIZO
- Karatasi hii ina maswali manne.
- Jibu maswali mawili pekee
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Chagua swali moja kwa yale matatu yaliyobaki.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Ndugu yako ameamua kuasi ukapera. Andika ratiba itakayotumiwa siku ya arusi yake.
- Eleza mikakati ambayo serikali ya Kenya imeweka kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Kigaidi nchini.
- Andika insha kuonyesha busara iliyomo katika methali “Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe”.
- Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya:
……………Nilikumbuka ushauri niliopewa na mama mazazi mara kwa mara. Uchungu usiomithilika ulinichoma moyoni, laiti ningalijua.

MARKING SCHEME
- INSHA
- Mwanafunzi azingatie muundo waratiba
- Anwani/mada
- Saa
- Tukio/shughuli
TANBIHI - Shughuli zifafanuliwe vizuri
- Matukio yafuatane vilivyo
- Mikakati iliyowekwa na serikali kukabiliana na Magaidi nchini:
- Kuhamasisha na kuwataka raia wawe macho.
- Kuanzisha mpango wa nyumba kumi-kila mtu amfahamu jirani yake.
- Kuweka kamera za siri /CCTV katika maeneo muhimu.
- Kuimarisha ukaguzi na ulinzi mipakani
- Kukabiliana na makundi haramu kama vile al-Shabaab – huko Somalia.
n.k
- Mtahiniwa atunge kisa kinachoashiria kujuta kwa ajili ya kukosa kutilia maanani nasaha/wosia/mawaidha.
- Kisa kioane na maneno aliyopewa, la sivyo atuzwe BKO.
Lazima mtahiniwa amalize insha kwa maneno aliyopewa, la sivyo apewe Bk 03
Asipojihusisha amejitungi aswali, kwa hivyo apewe Bk 03
Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 ALLIANCE GIRLS MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME).
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates