KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 ALLIANCE GIRLS MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME)

Share via Whatsapp

SEHEMUYA A

 1. SWALI LA LAZIMA
  1.  
   1. Semi nini? (alama 1)
   2. Fafanua sifa nne za misimu (alama4)
  2. Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali
   Ewe kilizi
   Ulozowea kujificha
   Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio
   Yana diilo juu mbinguni
   Jua kesho ni siku ya siku
   Siku ya kujua mbivu na mbichi
   Kutofautisha jogoo na vipora
   Nariba takaposhika, chake kisu
   Ndipo utakapo jua bayana
   Ukoo wetu si wa kunguru
   ikiwa hutayari
   kisu kukidhihaki
   sithubutu kamwe, wanjani kuingia
   sijekuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!

   Maswali
   1. Huuwimbohuitwaje? (alama1)
   2. Elezamajukumuyoyotemanneyanayotekelezwanawimbohuukatikajamii (alama4)
    1. Mivighaninini? (alama2)
    2. Elezasifatatuzamivigha (alama 3)
   3. Fafanuamatatizomatanoambayoyanaikumbwafasihisimuliziduniani (alama5)

SEHEMU YA B
RIWARA: CHOZI LA HERI: ASUMPTA MATEI

 1. “…haifai kucheza na uwezo wa vijana, wao ni kama nanga. Huwezi kuzamishana kuiongea merikebu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo (alama 4)
  3. Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu ya wahafidhina(alama12)
 2. Onyesha vile ukweli wa methali hii unavyodhihirika kwenye riwaya(alama20)

SEHEMU YA C
TAMTHILIA: KIGOGO: PAULINE KEA

 1. “Sitaki kuaibishwa na mwanamke mimi, siwezi.”
  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Fafanua kwa hoja nane kuwa msemaji wa maneno haya anafaa kuaibishwa     (alama16)
 2.  
  1. Jadili jinsi kumi ambazo kwazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika tamthilia ya Kigogo (alama10)
  2. Eleza mifano mitano ya matumizi ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo (alama10)

SEHEMU YA D : HADITHI FUPI
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

 1. Eleza nafasi ya vijana ukirejelea hadithi fupi zifuatazo
  1. Mapenzi ya kifa urongo (alama 5)
  2. Shogake Dada ana Devu (alama 5)
  3. Mame Bakari (alama10)
  4. Ndoto ya mashaka: Ali Abdalla Ali
 2. “Sasa nimechoka mja.Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi.Hadilini haya mashaka ya kutengenezwa? Mashaka ya mashaka!
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika (alama 4)
  3. Fafanua mambo sita yanayo mfanya mrejelewa aradue kufa. (alama12)
 1. SEHEMU YA E: USHAIRI
  Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Barabara bado ni ndefu
  Nami tayari nimechoka tiki
  Natamani kuketi
  Ni’nyooshe misuli
  Nitulize akili

  Lakini

  Azma yanisukuma
  Mbele ikinihimiza kuendelea
  Baada ya miinuko na kuruba
  Sasa naona unyoofu wake
  Unyoofu ambao unatisha zaidi

  Punde natumbukia katika shimo
  Nahitaji siha zaidi ilikupanda tena
  Ghafla nakumbuka ilivyosema
  Ile sauti zamani kidogo
  “Kuwa tayari kupanda na kushuka”.

  Ingawa nimechoka
  Jambo moja dhahiri
  Lazima hufuate barabara
  Ingawa machweo yaingia
  Nizame na kuibuka
  Nipande na kushuka

  Jambo moja nakumbuka; Mungu
  Je nimwombe tena? Hadilini?
  Labda amechoshwa na omba omba zangu
  Nashangaa tena!
  Kitu kimoja na kiamini

  Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
  Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
  Nikinaswa na kujinasua
  Yumkini nitafika mwisho wake
  Ikiwa wangu mwisho haitauwahi kabla.

  Maswali
  1. Taja na ueleze aina ya shairi hili (alama 2)
  2. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
  3. Huku ukitoa mifano mwafaka eleza tamathali tatu za usemi ambazo zinajitokeza katika shairi    (alama 3)
  4. Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano mitatu huku ukitolea mifano. (alama 3)
  5. Fafanua  dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama 2)
  6. Andika kifungu cha mwisho katika lugha ya nathari. (alama 4)
  7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi (alama 4)
   1. Kuruba
   2. Siha
   3. Machweo
   4. Kujinasua


MARKING SCHEME

 1.  
  1.  
   1. Semi ni kauli fupi za kisanaa ambazo hubeba ujumbe au mafunzo yaliyofichika.                                                                                                                   (1x1=1)
   2. Sifa nne za misimu
    • Misimu ni semi ambazo huibuka na kutumiwa na kundi la wanajamii kwa kipindi kifupi kisha hutoweka.
    • Misimu ni semi au msamiati ambao huibuka kisha hutoweka
    • Misimu hutumika na kundi ndogo la wanajamii kuwasiliana
    • Misimu huwa na maana fiche.
    • Baadhi ya misimu huja kukubalika kama msamiati sanifu.
    • Misimu huundwa kwa mbinu mbalimbali kama vile utohozi, au kugeuza mpangilio wa neno.
    • Maana ya misimu hutokana na watumiaji, mahali na wakati.(za kwanza 4x= 4)
  2.  
   1. Nyiso             (1x1= 1)
   2.  
    • Nyiso hutimiza ujasiri na kudharau woga.
    • Nyiso huwaandaa kihisia wanaotahiriwa kwa kuwapa …..ya kukabiliana na kisu.
    • Nyiso huwafahamisha wanaotahiriwa kuhusu majukumu yao mapya katika jamii.
    • Nyiso huhimiza uzalendo wa ufahari wa utamaduni husika.
    • Nyizo huwaburudisha waliohudhuria.
    • Nyiso huongeza furaha ya wavulana kuvuka kutoka utotoni hadi utu uzima.
    • Nyiso hutoa ushaurikwa vijana.             (za kwanza 4x1= 4)
  3.  
   1. Mivigha ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi maalum cha mwaka. (1x2= 2)
   2.  
    • Mivigha hufanywa kwa sababu maalum.
    • Mivigha huongozwa na mtu au watu maalum.
    • Mivigha huandamana na matendo Fulani k.v kupiga magoti. kunyolewa n.k
    • Baadhi ya mivigha huandamana na maleba maalum.
    • Mivigha hufanyiwa mahali maalum.
    • Sherehe za mivigha huandamana na utoaji mawaidha kupitia hotuba, nyimbo au maigizo     (za kwanza 4x1= 4)
  4.  
   1. Fasihi simulizi hukumbwa na ushindani kutoka kwa fasihi andishi.
   2. Fasihi simulizi huathiliwa na ukosefu wa utafiti wa kutosha.
   3. Watu huwa na mielekeo hasi kuhusiana na fasihi simulizi.
   4. Kuna uhaba wa walaalamu wa fasihi simulizi.
   5. Kusahaulika kwa baadhi ya vipera.
   6. Wakati mwingine fasihi simulizi huhusishwa na ushirikina au kutostaarabika.
    (za kwanza 4x1= 4)
 1.  
  1.  
   1. Ni maneno yake mwangeka
   2. Anamwambia Ridhaa
   3. Wamo katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Rubia.
   4. Ni baada ya kuyakumbuka maneno ya Tila kuwa haifai kucheza na uwezo wa vijana katika jamii (4x1=4)
  2.  
   1. Tashibihi – wao ni kama nanga.
   2. Jazanda –merikebu inasimamia taifa la wahafidhina.
   3. Taswira – Picha ya merikebu inayozamishwa.                                                       (2x2=4)
  3.  
   • Jinsi vijana walizamisha merikebu ya wahafidhina
   • Genge la wavulana watano linawabaka lime na mwanaheri kwa kukisia kwamba wazazi wao hawakumpagia kwa mwanzi.
   • Wanazorotesha usalama kwa kumvamia Subira na kumkata kwa sime kwa kumdhania kuwa hakumpigia kura Mwanzi.
   • Vijana wanawavamia abiria barabarani wakiongozwa na kijana aliyekuwa amevaa shati lenye maandishi “Hitman” na kuwachomea ndani ya magari.
   • Wanayachoma magari barabarani.
   • Sauna awaiba watoto wake Lunga-Dick na Mwaliko na kuwatenga na dada yao Umu.
   • Pete anameza vidonge ili kuavya kitoto chake cha pili ila hakufanikiwa.
   • Zohali anajiingiza katika mapenzi na kupata mimba akiwa kidato cha pili.
   • Wanawe Kiriri wanakataa kurundi nyumbani. Kutoka ughaibuni walikoenda kusoma.
   • Vijana wanamdhalilisha Mwekevu baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi. Kipanga anaachia masomo kidato cha pili na kuanza kunywa kangara –ananusurika kifo.
   • Wanafunzi shukeni –anakomesea Ridhaa, wanaendeleza ukabila dhidi ya wanafunzi walowezi.
   • Vijana wanapokea hongo kutoka kwa wanasiasa kama papa iti wawachague, hivyo kuimarisha uongozi mbaya.
   • Vijana wasichana wanajifungua watoto na kuwatupa kwenye majaa ya taka kama Yule aliyeokolewa na Neema.
   • Wanavunja sheria kwa kuandamana huku wamebeba picha za Mwanzi na kumhimiza atawale ingawa alikuwa ameshindwa n.k (6x2=12)
 1. Baada ya dhiki faraja. Onyesha vile ukweli wa methali hii unavyodhihirika kwenye riwaya
  • Ridhaa anapata uchungu baada ya mali yake kuteketezwa, na kuwa mkimbizi. Anarejea hali ya kawaida baadaye anapojenga kituo cha afya cha mwanzo mpya.
  • Ndugu Kaizari anapitia adha mbalimbali na kuishia katika kambi ya wakimbizi. Baadaye anaajiriwa na Ridhaa katika kituo cha afya kama Afiza wa matibabu.
  • Salome anafurushwa kwa mumewe kwa sababu ya ukabila na kuwa mkimbizi. Mwishowe anajiunga na kitui cha afya cha mwanzo mpya kama muuguzi.
  • Zohali anaringwa akiwa kidato cha pili na kusimangwa na wazazi wake. Baadaye anajifungua salama na kurejea shuleni.
  • Mwangeka anasononeka kwa kumpoteza mkewe Lily na mwanaye Becky. Baadaye anamwoa Apondi na kuishi kwa raha.
  • Apondi anaishi kwa woga wa kuhusiana na mwanamume wingine kwa miaka sita lakini baadaye anakutana na mwangeka na kufunga nikaha.
  • Pete anakataliwa na babake, kuozwa kwa lazima, kujaribu kuavya na kujitia kitanzi. Baadaye anawaza jinsi ya kuboresha maisha yake bila kujjidhalilisha.
  • Maisha ya Umu yamejaa mateso-kuachwa na mama, kufa kwa babake na kutoroshwa kwa ndugu zake, Dick na Mwaliko. Baadaye anaishi kwa raha nyumbani mwa Mwangeka, kusoma na muhitimu kama mtaalamu wa Zaraa.
  • Dick anaingizwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya. Hatimaye anaanza biashara yake mwenyewe –kuuza vifaa vya umeme.
  • Mwaliko anaibwa na sauna na kuishia mikononi kwa Bi. Kangara. Baadaye anaokolewa na polisi na kupelekwa kwa kituo cha watoto ambako anapangwa na Mwangemi.
  • Mwangemi na Neema wanaishi bila mtoto baada ya kifo cha Bahati. Hata hivyo wanafaulu kumpanga mtoto mvulana,Mwaliko.
  • Chandachema anaishia kuchuna majani katika shirika la chai la Tengenea baada ya kumpoteza nyanyake. Baadaye anaokolewa na kupelekwa katika makao ya watoto mayatima anakoendeleza masomo. n.k (10x2=20)
 1.  
  1.  
   1. Msemaji ni Majoka
   2. Anamwambia Kingi
   3. Wako mkutanoni nje ya soko la Chapakazi.
   4. Majokamlinzi wake Kingi na mshauri Kenga wameuvamia mkutano uliokuwa ameandaliwa na Tunu ili kuendeleza harakati za kupinga uongozo wa Majoka            (4x1=4)
  2. Fafanua kwa hoja nane kuwa msemaji wa maneno haya anafaa kuaibishwa    
   • Majoka analifunga soko la chapakazi kwa mwezi mmoja kwa madai ya kusherehekea uhuru…ilikuwa tegemeo.
   • Chini ya utawala wake soko linachafuka huku taka na kemikali zikitapakaa kote.
   • Anabinafsisha raslimali za umma na kuwaachia wanasagamoyo masalio-keki ya uhuru inaliwa na wachache.
   • Anakopa mikopo kutoka nje na kuviachia vizazi vya usoni mzigo wa kulipa.
   • Anaingilia ndoa za wanajamii. Anamtaka Ashua kimapenzi japo anajua ni mkewe Sudi.
   • Anatumia raslimali za umma kuwahonga wachonga vinyago vya mashujaa ambao anatambua.
   • Anatumia vyombo vya usalama kuwakandamiza waandamanaji ambao wanajaribu kudai haki zao.
   • Anakiuka haki za wafanyakazi kwa kuwapa mishahara duni huku akiwatoza kodi.
   • Majoka anaruhusu ukataji miti hali inayosababisha ukame na ukosefu wa chakula.
   • Majoka anawatumia vijana vibaya ili kukidhi mahiataji yake ya kisiasa –wanatumika kama wahuni kuwashambulia wapinzani wake.
   • Majoka anaruhusu biashara ya upishi wa pombe haramu licha ya kuwa kinyume cha sheria. nk. (8x2=16)
 2.  
  1. Jadili jinsi kumi ambazo kwazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika tamthilia ya Kigogo
   • Majoka analifunga soko lachapakazi ambalo ni tegemeo la raia wa Sagamoyo.
   • Majoka anawaita viongozi wa vyama pinzani ambao wanaupinga uongozi wake.
   • Majoka anawaua wahuni ili wamshambulie Tunu.
   • Majoka anamweka korokoroni Ashua kwa kuwa alikataa vishawishi vyake vya kimapenzi.
   • Kuruhusu upikaji pombe haramu kwa mamapima pasipokuhofu madhara yake.
   • Kuwaingiza vijana katika matumizi ya mihadarati katika Majoka na Majoka Academy.
   • Kuwatishia kifo wanaokiuka amri na njama zake mbovu k.v Chopi.
   • Kuamrisha waandamanaji wapigwe risasi na askari.
   • Kuwatisha kumfuta kazi Kingi kwa kukosa kutekeliza amri yake.
   • Kukataa kutoa msaada wa chakula kwa watoto wa Ashua.
   • Kujaribu kumshawishi Ashua ashiriki naye mapenzi naye kama kisasi.
   • Kumwinjikia kisasi Sudi alipokataa kuchonga kinyago cha Morara (za kwanza 10x1=10)
  2. Mifano ya matumizi ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo
   • Ni kinaya kwa Majoka kusema anampenda Ashua ilhali anakataa kumsaidia kwa chakula.
   • Ni kinaya kwa Kenga kufika katika karakana na kuwaeleza akina Sudi kuwa alikuwa ametembea kwa manufaa yao.
   • Ni kinaya kwamba Majokaalimwoa Husda bila kumpenda.
   • Majoka hakuhuzunishwa wala kushughulikia mazishi ya Ngurumo ilhali alikuwa rafiki na mafuasi wake Sugu.
   • Kenga anabadilika mwishonina kuanza kumpinga Majoka ulhali hapo awali alikuwa mfuasi wake.
   • Ni kinaya kuwaona askari wakiwapiga waandamanaji badala ya kulinda usalama wao.
   • Ashua anasema kwamba anampenda Sudi lakini anapokuwa korokoroni anasema kuwa ataomba talaka . Kadiria (5x2=10)
 1.  
  1. Mapenzi ya kifaurongo
   • Vijana ni wasomi -Dennis na Penina Chuoni.
   • Vijana ni wategemezi – Penina kwa wazazi /Dennis kwa Penina
   • Vijana ni wabadhirifu –Penina anatumia pesa nyingi kila wiki (5,000/=)
   • Vijana ni wenye mapenzi – Dennis kwa Penina.
   • Vijana ni wenye usasa na anasa – wanachuo wanashiriki raha huku wakitumia vifaa vya kisasa kama Ipad.
   • Vijana ni waathiriwa wakuu wa uhaba wa kazi –Dennis (5x1=5)
  2. Shogake Dada ana Ndevu
   • Vijana ni wasomi –Safia
   • Vijana ni waongo –Safi
   • Vijana ni wanafiki –Safia na kimwana wanajifanya wacha Mungu kwa kujifunika.
   • Vijana ni wazinzi – Safia na Kimwana
   • Vijana ni wajanja – Safia na Kimwana
   • Vijana wamechorwa kama wakatili –Safia anaavya mimba.
   • Vijana wamechorwa kama wasiri-Safia (5x1=5)
  3. Mame Bakari
   • Vijana ni wasomi –Sara anabakwa akitoka masomo ya ziada.
   • Vijana wamesawiriwa kama wenye visasi –Sara anafikiria jinsi angemwadhibu mbakaji wake.
   • Vijana ni wabakaji – Sara anabakwa na janadume.
   • Vijana ni wenye siri –Sara na Sawira wanaficha siri ya ujauzito wa Sara.
   • Vijana ni wafanya kazi –Beluwa ni daktari wa uzazi.
   • Vijana ni wasaliti – Beluwa alivunja ahadi ya kujicha siri ya ujauzito wa Sara. (5x2=10)
 1.  
  1. Muktadha wa dondoo hili
   • Anarejelea hali yake ya maisha ya kimaskini katika mtaa wa Tandale.
   • Maisha yake ni yenye shida kuanzia kuzaliwa, kuelewa, ndoa .
   • Ameachwa na mkewe na amefika mwisho wa subira na kilichobaki ni kufa –hajui mwisho wa mateso yake. (4x1=4)
  2. Mbinu mbili za lugha zilizotumika.
   • Swali la balagha – Hadi lini haya mashaka ya kutengenezwa?
   • Nidaa- hisia za ndani za mashaka zinadhihirika anaposema “Mashaka ya Mashaka!”(2x2=4)
  3. Mambo yanayomfanya mrejelewa ajaribu kufa.
   • Maisha ya Mashaka yametawaliwa na mateso na maonevu.
   • Mashaka anatoroshwa na mkewe waridi kwasababuya umaskini.
   • Anaishi katika kibanda duni – Mtaa wa Tandale.
   • Ameajiriwa na Kampuni ya ulinzi ya ZWS kwa mshahara duni.
   • Mashaka amefikia kiwango cha kujichukia kwa sababu ya nafasi yake katika jamii.
   • Mamake aliaga dunia kabla ya kumtia machoni
   • Anampoteza babake kutokana naukiwa.
   • Anasoma kwa dhiki.
   • Analazimishwa kufunga ndoa na mzee Rubeya bila mpango wowote.
   • Anaishi maisha ya dhiki mikononi B. Kedebe ambapo analazimika kufanya vibaswa.(za kwanza 6x2=12)
 1.  
  1. Ni shairi huru/guni. Hii ni kwasababu halijafuata kanuni za utunzi wa mashairi. (1x2=2)
  2. Toni ni ya matumaini/himizo (1x2=2)
  3.  
   1. Tashihisi/huhuishaji –azma yanisukuma
   2. Kinaya –Unyoofu ambao unatisha zaidi
   3. Mbinu rejeshi –jambo moja nakumbuka, kama niendelee kumwomba Mungu.
   4. Tanakali za sauti – nimechoka tiki.
   5. Nidaa –nashangaa tena! (za kwanza 3x1=3)
  4.  
   1. Inkisari –anasema naona badala ya ninaona/yaingia n.k
   2. Kuboronga sarufi –Ikiwa wangu mwisho badala ya ikiwa mwisho wangu (2x2=4)
  5. Dhamira ya mtunzi ni kuwapa /kuwahimiza wanaopitia matatizo maishani wasife moyo bali waendelee kujikaza na baadaye watafanikiwa. (1x2=2)
  6. Mimi ninaamini kwamba ni lazima niendelee kutia bidii katika kila jambo ninalofanya. Nifanye juhudi kuifuata barabara ingawa ina matatizo mengi. Iwapo nitaingia kwenye shida nitafanya bidii ili nijitoe humo. Nina imani kwamba nitafanikiwa kama sitafariki mapema.(4x1=4)
  7.  
   1. Siha –afya
   2. Machweo –Jioni
    Kujinasua –Kujiondoa/kujitoa (3x1=3)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 ALLIANCE GIRLS MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME).


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest