MTIHANI WA PAMOJA WA SUKELLEMO
KISWAHILI
KARATASI YA 1
INSHA
Muda: Saa 1 ¾
MAAGIZO
- Andika insha mbili. Swali la kwanza ni la lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
- Andika wasifu utakaosoma katika sherehe ya kuadhimishwa kwa siku ya mashujaa katika jimbo lenu kuhusu shujaa unayemuenzi.
- Mchakato wa kisiasa umeleta madhara mengi nchini. Jadili kauli hii.
- Andika kisa kitakacho dhihirisha maana ya methali ifuatayo: Dudu liumalo silipe kidole.
- Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo: ...Nilimtazama kwa muda punde tu aliponikaribia. Nikajisemea kimoyomoyo, Hili haliwezi kukubalika.
MAAKIZO
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Mwanafunzi azingatie muundo wa wasifu;
- Kichwa
- Kitaje wasifu ni wa nani, iandikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
- Mwili
- Maelezo ya kibinafsi kuhusu anayesifiwa mfano majina yake kamili, alikozaliwa, alikosomea, wazazi au familia yake n.k
Mambo mengine kumhusu ,matendo aliyotenda, ushindi wake n.k
- Maelezo ya kibinafsi kuhusu anayesifiwa mfano majina yake kamili, alikozaliwa, alikosomea, wazazi au familia yake n.k
- Hitimisho
- Mwanafunzi ahitimishe kwa kutoa kauli ya mwisho kuhusu umaarufu wa anayeandikiwa wasifu na sababu za kuhitaji utambulisho.
- Maudhui katika mwili wa insha yatiririke kiwakati
- Wasifu uandikwe kwa wakati uliopita kwa sababu yanayosimuliwa huwa yamefanyika tayari.
- Mwanafunzi atumie nafsi yan tatu umoja.
- Wasifu uwe wa kuvutia kwa KUZINGATIA SABABU ZA MHUSIKA KUWA SHUJAA na kutoa mifano ya mambo maarufu yaliyotendwa na mhusika.
- Mambo hasi ambayo yanaweza kumwathiri au kumwaibisha mhusika yaachwe.
- TANBIHI
- Akitumia nafsi ya kwanza amepotoka apewe 03
- Akitumia hotuba kama sura atuzwe maudhui na atolewe maki nne za sura
- Maudhui yake yazingatie kwa nini mhusika ni shujaa
- Kichwa
- Mchakato wa kisiasa umeleta madhara mengi nchini. Jadili kauli hii.
- Kiuchumi - umezorota
- ukabila–mauaji
- ukoloni mamboleo – wale wanaotawala wananyanyasa watu
- ukosefu wa miundomsingi
- utabaka – jamii kugawika
- uchochezi kupitia kwa wafuasi wa viogozi hasa vijana
- ufisadi – umekithiri kwa vile wezi wanafichwa
- uhalifu
- maendeleo kuegemea sehemu fulani za nchi na kusahau wengine
- ubadhinifu wa mali – hela nyingi kutumika kwa siasa badala ya kusaidia wananchi
- sera potovu
- Hii ni insha ya methali; ukiona mahali kuna hatari /jambo linaloweza kukudhuru usikaribie
Insha hii ina sehemu mbili;- Dudu liumalo - hatari ya aina yoyote ile
- Silipe kidole – tahadhari
-
- Kisa kioane na mdokezo uliopewa.
- Kisa kisimuliwe katika nafsi yoyote
- Lazima kisa kisimulie tendo / tukio ambalo msemaji aliliona na halikubaliki katika jamii yake kama vilemitindo ya mavazi, ulevi/dawa za kulevya, mahusiano yasiyokubalikahali ya anayerejelewa n.k.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock 2020/2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates