Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mang'u Mock 2020 Exam

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA PILI
MUDA: SAA 2

Maagizo

  • Karatasi hii ina maswali manne (Ufahamu, Ufupisho, Lugha na Isimujamít)
  • Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa baada ya kila swali

UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

Historia ya katiba

Katiba ni utaratibu wa sheria unaoweka mpango wa jamii kuendesha mambo:Ni muhimu kila raia ajue katiba ya nchi yake.

Katiba yaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa. Katika jamii za jadi, katiba ilihifadhiwa na kupokezwa kwa mdomo. Mtindo wa kuandika katiba ulianza nchini Marekani mwaka 1787. Ingawa katiba hii imefanyiwa mabadiliko hapa na pale,bado ni ileile, Kenya ilipowekwa chini ya himaya ya Uingereza mwaka 1895, ilianza kutumia katiba ya Uingereza. Baada ya masetla wa kikoloni kujikita, Kenya kuwa koloni. Hii ililazimu pawe katiba nyingine mwaka 1920. Waafrika waliupinga mfumo huu kwa sababu haukuwahusisha kikamilifu kwenye masuala ya uongozi. Utetezi wa wanasiasa uliilazimisha serikali ya Uingereza kuitisha makongamano mbalimbali kama vile lile la Devonshire na mengine ili kurekebisha katiba. Waafrika hawakuridhika. Wakaendelea kudai katiba mwafaka. Harakati hizi zilileta kuitishwa kwa kongamano la katiba la Lancaster. Lengo lilikuwa kuandika katiba itakayotumiwa nchini hadi leo. Kati ya wajumbe walioenda Uingereza kuandika katiba mwaka 1962 ni pamoja na Tom Mboya, Jean Marie Seroney, Julius Kiano, Jomo Kenyatta, Masinde Muliro, Oginga Odinga, Ronald Ngala, Daniel Arap Moi na James Gichuru. Wengine ni Martin Shikuku, Dennis Akumu, Taita Towett, Abdilahi Nassir, Jeremiah Nyaga na John Keen.

Katiba ni kitovu cha taifa. Baina ya mambo inayotekeleza ni kuweka utaratibu na kanuni za utawala, kwa mfano utawala wa kimikoa na serikali za wilaya. Pamoja na haya, katiba hufafanua vyombo vikuu vya serikali ,mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda. Vyombo hivi ni bunge, mahakama, urais, jeshi n.k. Hali kadhalika, katiba hupambanua haki za raia.

Hii hudumisha demokrasia na huwawezesha wananchi kupata uhuru na haki za kimsingi. Katiba hukinga haki za kila raia, hasa kutokana na udhalimu wa wengi au wenye uwezo mkubwa. Zaidi ya yote, katiba huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji.

Katiba huhalalishwa na watawaliwa. Hii hutokea wanaposhirikishwa katika uandishi wake. Kuanzia miaka ya themanini, raia walianza kudai katiba igeuzwe. Mwamko wa kutaka mageuzi ulianza kwa harakati za kubadilisha mfumo wa kisiasa kutoka ule wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi. Haja ya mfumo mpya wa kisiasa ulilenga kuwashirikisha wananchi katika utawala na kuondoa uimla.

Harakati zilitia fora miaka ya tisini. Mamnbo yaliyochochea hali hii ni mengi. Kwanza, katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi. Marekebisho haya yalimpa rais mamlaka mengi juu ya serikali kuu na vyombo tofauti vya serikali. Pili, viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba. Raia walihisi wanadhulumiwa. Walipinga hali ya wachache waliomzunguka rais kunufaika huku umma ukitengwa. Tatu, kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo, wanawake, watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.Hatimaye, pakawa na ongezeko la uharibifu wa mazingira, ufisadi na unyakuzi wa mali ya umma kama vile ardhi.

Waliopigania katiba mpya walikuwa na haja ya katiba ambayo uandikaji:wake ungewahusisha Wakenya wote. Mwanzoni, serikali ilipinga wito wa mabadiliko. Lakini mnamo mwaka 2001 iliunda Tume ya Marekebisho ya Katiba ili kutekeleza mahitaji ya wananchi. Tume hii iliwahamasisha na kuwashawishi raia kutoa maoni. Tume iliandaa vikao katika maeneo ya ubunge 210 ambapo wananchi walitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya katiba waliyotaka.

Katika mapendekezo hayo raia walisisitiza mambo kadhaa. Jambo la kwanza ni utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi na maafisa wa umma. Jambo lingine ni kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu. Raia walidai kanuni za usawa na ulinganifu. Aidha walitilia mkazo mahitaji ya msingi kama chakula, afya nzuri, makao, elimu, usalama, uchumi, na kadhalika.

Msingi wa mapendekezo hayo yote ni kuwepo na amani ya kitaifa, umoja na uadilifu ili kulinda maslahi ya wananchi wote na taifa.

Maswali

  1. Eleza kilichosababisha kongamano la katiba la Lancaster (al. 3)
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba.(al. 3)
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wa taarifa.(al. 3)
  4. Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba.(al. 3)
  5. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa(al. 3):
    1. Kitovu
    2. Harakati
    3. Hamasisha

UFUPISHO (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumzo.

Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza kama vila michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile ilivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amefiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati juao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambae amepatikana na mambo kama huyo hana budi kufahamu zaidi.

Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayo , karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.

Inambidi mwanafunzi asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza . Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.

  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
    Matayarisho
    Jibu
  2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho (Maneno 30) (alama 5 utiririko)
    Matayarisho
    Jibu

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Andika sifa mbilimbili za kutambulisha sauti zifuatazo
    1. /d/ (al. 2)
    2. /th/
  2. Ainisha viambishi kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neno hili.
    Alijipelekea (al. 3)
  3. Tambua matumizi ya 'a' katika sentensi ifuatayo.
    Mwanafunzi acheza uwajani (al. 1)
  4. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi.(al. 4)
    Mlango umevunjwa na fundi aliyeujenga
  5. Tunga sentensi moja ukitumia kitenzi kimoja kilichoundwa kutokana na nomino:
    Zawadi
  6. Tambua matumizi ya 'ji' katika sentensi ifuatayo.
    Jina la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule (al. 2)
  7. Andika sentensi moja ukitumia kihisishi cha bezo. (al. 2)
  8. Akifisha
    aisee yale mawimbi ya tsunami yaliyotokea bahari hindi yaliangamiza biashara nyingi sana alisema bomet. (al. 4)
  9. Panda ni kuatika mbegu ardhini au kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili (al. 2)
  10. Bainisha virai katika sentensi hii.
  11. Juma alikwenda mjini kwa miguu (al. 2)
  12. Unda neno lenye silabi ifuatayo KIKKIKI (al. 1)
  13. Tunga sentensi yenye muundo wa:
    kiima, kiarifa, yambwa tendwa, yambwa tendewa na yambwa ala (al. 4)
  14. Yakinisha huku ukigeuza sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili kwa umoja.
    Nisiposamehewa na mola sitapata amani mchana kutwa.
  15. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi(al. 2)
    1. Ngoma ile inalia vibaya kwa kuwa imepasuka.
    2. Ni mlango upi uliofungwa na wewe nilipoenda maktabani?
  16. Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo vikiwa katika hali ya kufanyiza (al. 3)
    1. La
    2. Nywa
    3. Fa
  17. Eleza tofauti iliyo kati ya tanakali hizi za sauti. Anguka chumbwi na anguka tupwi (al. 2)
  18. Weka nomino hizi katika ngeli zake (al. 2)
    1. Mbalungi
    2. Mturuki

ISIMUJAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza majukumu matatu ya lugha ya taifa (al. 3)
  2. Fafanua mtindo wa lugha uliotumiwa katika taarifa ifuatayo huku ukieleza sababu za matumizi ya vitambulisho maalum vya lugha
    Wananchi, mimi sina mengi. Hapana katika nyinyi asiyenielewa. Sina la kusema, ila ninawakumbusheni kuwa mnahitaji kiongozi atakayeshughulikia maslahi ya taifa zima. Mtu huyo ni mimi na ninajitahidi niwezavyo kujenga masoko, barabara, shule zaidi na mazahanati na maisha yenu yatakuwa ya raha zaidi. (al. 4)
  3. Thibitisha kuwa adabu za lugha hazizingatiwi miongoni mwa wanajamii siku hizi (al. 3)

MAAKIZO

UFAHAMU

Maswali

  1. Eleza kilichosababisha kongomano la katiba la Lancaster
    • Waafrika hawakuwa wamehisishwa katika katiba ya mwaka wa 1920.
    • Waafrika walitaka kuhusika katika maswala ya uongozi. Utetezi wa wanasiasa ulilazimu serikali ya uingereza kuitisha kongomano.
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba
    • Utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi
    • Kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu
    • Kanuni za usawa na ulinganifu 
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wa taarifa
    • Kuweka utaratibu na kanuni za utawala m.f utawala wa kimikoa, tufafanue vyombo vikuu vya serikali, mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda
    • Hupambanua haki za raia
  4. Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba
    • Katiba iliyokuwa imeandikwa ho mengi
    • Viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba
    • kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.
  5. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa
    • Kitovu - chenye maana na muhimu
    • Harakati - Shunguli za kufanya jambo fulani
    • Hamasisha - Kufanya jambo lieleweke na kukubalika

UFUPISHO
Maswali

  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
    Matayarisho
    • Kila jambo tufanyalo katika lugha hustawisha ufahamu wake.
    • Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma.
    • Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.
    • Lugha iliyoandikwa ni ya aina ya mazungumzo.
    • Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.
    • Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.
    • Husaidia kufahamu yaliyoandikwa.
    • Hali ya mwanafunzi kujionea sinema ni ujuzi.
    • Matatizo na shida ambazo wanafunzi hupitia pia ni ujuzi.
  2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho (Maneno 30) (alama 5 utiririko)
    Matayarisho
    • Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni.
    • Lugha zote hazina ustawi mwingi.
    • Nyingine hazina vitabu ama zina vitabu vingi.
    • Mwanafunzi anayesoma anafaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisoma.
      a – 09
      b – 04
      Ut - 02

MATUMIZI YA LUGHA

  1. Andika sifa mbilimbili za kutambulisha sauti zifuatazo.
    1. /d/
      • Kipasuo
      • Hutamkiwa kwenye ufizi
      • Ni sauti ghuna 
    2. /h/ -
      • Ni kikwamizo / kwanizo
      • Hutamkiwa menoni
      • Ni hafifu (sighuna)
  2. Ainisha viambishi kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neno hili
    Alijipelekea
    • A-nafsi ya umoja 
    • li- wakati uliopita 
    • ji mtendwa
    • pelek - mzizi 
    • e-kauli
    • a-kiishio
  3. Tambua matumizi ya 'a' katika sentensi ifuatayo
    Mwanafunzi acheza uwajani
    • Hali isiyodhihirika
  4. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi
    kisp2qa3d
  5. Tunga sentensi moja ukitumia kitenzi kimoja kilichoundwa kutokana na nomino Zawadi - Zawidi
    • Alizawadiwa kwa kupasi mtihani
  6. Tambua matumizi ya 'i' katika sentensi lifuatayo.
    Jino la jitu hilo lililiwezesha kuijlia chakula kingi kuliko mkimbiaji Yule
    • Jino - ngeli ya LI-YA
    • Jitu-ukubwa/ uduni wa latu
    • Kujilia - Kirejeshi -
    • Mkimbiaji - mazoea/ uzoefu
  7. Andika senteni moja ukitumia kihisishi cha bezo
    • Mfano. Po! Nyoo! Mha! Ngoo! Mawe! Ebo! Wapi! Zii! Aka!
  8. Akinisha
    aisee yale mawimbi ya tsunami yaliyotokea bahari hindi yaliangamiza biashara nyingi sana alisema bomet.
    • "Aisee! Yale mawimbi ya Tsunami (yaliyotokea Bahari Hindi) yaliangamiza biashara nyingi sana,"Alisema Bomet.
  9. Panda ni kuatika mbeu ardhini an kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili.
    • Kugawika kwa njia - Ingia katika chombo cha kusafiri
    • Paji la uso Pembe kubwa inayopigwa nchani
    • Manati/ chombo cha kurushia mawe
  10. Bainisha virai katika sentensi hii
    Juma alikwenda mjini kwa miguu
    • RN/KN - Juma
    • RT/KT - alikwenda mjini -
    • RE/ Ke-kwa miguu
  11. Unda neno lenye silabi ifuatayo KIKKIKI
    • Mfano-matwana
  12. Tunga sentensi yenye muundo wa: 
    kiima, kiaria, yambwa tendwa, yambwa tendewa na yambwa ala
    • Mama alipika chakula cha mgonjwa kwa sufuria
  13. Yakinisha ukigeuza sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili kwa umoja.
    • Nisiposamehewa na Mola sitapata amani mchana kutwa
    • Ukisamehewa na Mola utapata amani mchana kutwa.
  14. Andika entensi ziuatazo kwa wingi
    Ngoma ile inalia vibaya kwa kuwa imepasuka
    • Ngome zile zinalia vibaya kwa kuwa zimepasuka
      Ni mlango upi uliofungwa na wewe nilipoenda maktabani?
    • Ni milango ipi iliyofungwa na nyinyi tulipoenda maktabani
  15. Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo vikiwa latika hali ya kufanyiza
    • La-Lisha
    • Nywa - Nywesha/ Nywishe -
    • Fa-Fisha (lazima atunge sentensi sahih)
  16. Eleza tofauti iliyo kati ya tanakali hizi za suti.
    Anguka chumbwi na anguka tupwi
    • Chumbwi - kuanguka majini ama kwenye kitu kiowevu
    • Tupwi-kuanguka matopeni
  17. Weka nomino hizi katika ngeli zake
    • Mbaļungi -U-I
    • Mturuki - A-Wa

ISIMU JAMII

  1. Eleza majukumu matatu ya lugha ya taifa
    • Huunganisha watu
    • Huziba mipaka ya kikabila
    • Hukuza utamaduni
    • Hukuza uzalendo
    • Hutambulisha wtu wa taifa fulani
    • Hufanikisha harakati za uongozi
    • Husawazisha watu kilugha kis hisia zitakuwa sawa.
  2. Fafanua mtindo wa lugha uliotumiwa katika taarifa ifuatayo huku ulieleza sababu za matumizi ya vitambulisho maalum vya lugha
    • Lugha ya mwanasiasa
    • Husema mengi ingawa huwaambia watu kuwa ana machache
    • Hujisifu mwenyewe
  3. Thibitisha kuwa adabu za lugha hazizingatiwi miongoni mwa wanajamii siku hizi
    • Watu hawazingatii usanifu wa lugha tena na kutumia sheng pakubwa katika mazungumzo yao.
    • Watumiaji washeng hawazingatii umri na vyweo vya wanaozungumziwa
    • Tatizo la sheng limekuwa chanzo cha kuzorota kwa kiwango cha lugha katika sauti.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mang'u Mock 2020 Exam.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest