Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Meru Central Cluster Exam 2020

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA PILI
FASIHI

MUDA: SAA 2 ½

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja

 

  1. FASIHI SIMULIZI: SWALI LA LAZIMA

      1. Miviga ni nini? Al.2
      2. Eleza sifa tano za miviga. Al.5
      3.  Fafanua hasara tatu za miviga. Al.3
      4. Eleza changamoto tano ambazo mtafiti hukabiliana nazo anapokusanya data ya fasihi simulizi. Al.5
      5. Eleza majukumu ya wimbo katika hadithi. Al.5

  2. TAMTHLIA: KIGOGO
    1. "....Tulipoanza safari hii matangazo yalikuwa bayana, dhahiri shahiri babu!..."
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Al.4
      2. Tambua mbinu za uandishi zilizotumika katika kifungu hiki. Al.4
      3. Eleza matatizo yanayokumba safari inayorejelewa. Al.12
    2. Tamthlia ya kigogo inazungumza kuhusu hali halisi katika mataifa mengi ya kiafrika. Jadili. Al.20

  3. RIWAYA: CHOZI LA HERI
    1. “Alikumbuka jinsi rafiki yake……..alivyofishwa kwa njia hii. Akili yake ilimtambia kisa chenyewe kana kwamba inataka kumwonya (uk.120)
      1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. Al.4
      2. Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. Al.4
      3. Tathmini nafasi ya anayelengwa na kauli hii katika kuijenga riwaya hii. Al.12
    2.      
      1. Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. Al.10
      2. Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri. Al.10

  4. HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
    1.      
      1. Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10
      2. Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha. Al.10
    2. Mame Bakari
      “Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Uaogopa nini?
      1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. Al.4
      2. Eleza sifa za mrejelewa. Al.6
      3. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. Al.2
      4. Eleza umuhimu wa msemaji. Al.4
      5. Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. Al.1
      6. Fafanua maudhui katika swali la (e) kwa kurejelea hadithi nzima. Al.3
  5. USHAIRI   
    1. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali

      Alikwamba wako mama, kajifanya hupliiki,
      Kakuasa kila jema, ukawa ng’oo!Hutaki
      Sasa yamekusakama, popote hapashikiki,
      Uliyataka mwenyewe!

      Babayo lipokuonya, ukamwona ana chuki,
      Mambo ukaboronganya, kujifanya hushindiki,
      Sasa yamekunganya, kwa yeyote hupendeki,
      Uliyataka mwenyewe!

      Mazuri uliodhania, yamekuletea dhiki,
      Mishikeli miania, kwako ona haitoki
      Mwanzo ungekumbukia, ngekuwa huaziriki,
      Uliyataka mwenyewe!

      Dunia nayo h adaa, kwa fukara na maliki,
      Ulimwenguni shujaa, hilo kama hukumbuki,
      Ya nini kuyashangaa? Elewa hayafutiki,
      Uliyataka mwenyewe!

      Mwenyewe umelichimba, la kukuzika handaki,
      Ulijidhania samba, hutishiki na fataki,
      Manchangu yamekukumba, hata neno hutamki,
      Uliyataka mwenyewe!

      Kwa mno ulijivuna, kwa mambo ukadiriki,
      Na tena ukajiona, kwamba we mstahiki,
      Ndugu umepatikana, mikanganyo huepuki,
      Uliyataka mwenyewe!

      MASWALI
      1. Eleza dhamira ya shairi hili. Al.2
      2. Tambua njia mbili anazotumia mtunzi wa shairi hili kusisitiza ujumbe wake.Al.2
      3. Taja na utoe mifano ya aina zozote mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi. Al.4
      4. Andika ubeti wa tatu katika lugha tutumbi. Al.4
      5. Bainisha toni ya shairi hili. Al.2
      6. Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina mbili za idhini ya kishairi katika shairi hili. Al.4
      7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. Al.2
        1. Mstahiki
        2. Hupuliki

MAAKIZO

  1. FASIHI SIMULIZI: SWALI LA LAZIMA

      1. Miviga ni nini? Al.2
        • Ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi Fulani/maalum cha mwaka.
      2. Eleza sifa tano za miviga. Al.5
        1. Huandamana na matendo yanayofuata utaratibu maalum
        2. Huongozwa na watu mahususi
        3. Kuna utoaji wa mawaidha
        4. Maleba maalum huvaliwa na wahusika
        5. Hufanyika mahali maalum panapofanyiwa sherehe hizi
        6. Huambatana na utamaduni wa jamii husika.
      3.  Fafanua hasara tatu za miviga. Al.3
        1. Baadhi ya miviga imepitwa na wakati kama tohara ya wasichana
        2. Baadhi ya miviga inakinzana na malengo ya taifa
        3. Hujaza watu hofu inapohusisha kafara za binadamu
        4. Ushiriki na unaweza ksababisha uhasama unapohusishwa
        5. Baadhi hughalimu kiasi kikubwa cha pesa
      4. Eleza changamoto tano ambazo mtafiti hukabiliana nazo anapokusanya data ya fasihi simulizi. Al.
        1. Huenda gharama ya utafiti ikawa kubwa.
        2. Mtazamo hasi wa wanajamii, kuhusu ujazaji wa hojaji
        3. Wanajamii kushuku kwamba mtafit anawapeleleza
        4. Mbinu kama hojajo huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika
        5. Wahojiwa hukataa kuhojiwa iwapo wanahisi baadhi ya matendo yanaenda kinyume na imani ya dini yao.
        6. Mtafiti huenda asiwe na wakati wa kutosha kuwahoji watu wengi.
        7. Huenda mtafiti akakosa usalama na hivyo kuvamiwa.
      5. Eleza majukumu ya wimbo katika hadithi. Al.
        1. Kuondoa uchavu/ukinaifu
        2. Ni njia ya kushirikisha hadhira
        3. Husukuma visa mbele – kipengele cha msuko/ploti
        4. Kukamilisha ujumbe au kuutilia mkazo
        5. Kudhihirisha sifa za mhusika Fulani
        6.  Huipa hadithi mnato/mvuto wa kipekee
        7. Kufanya hadithi kukumbukika.

  2. TAMTHLIA: KIGOGO
    1. "....Tulipoanza safari hii matangazo yalikuwa bayana, dhahiri shahiri babu!..."
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Al.4
        1. Msemaji ni majoka
        2. Alikuwa anamwambia babu katika ndoto
        3. Walikuwa katika chumba cha wagonjwa
        4. Hii ni baada ya majoka kupata habari ya kifo cha mwanawe Ngao Junior. (4x1)
      2. Tambua mbinu za uandishi zilizotumika katika kifungu hiki. Al.4
        1. Jazanda – safari kurejelea uongozi
        2. Msemo – Dhahiri shahiri
        3. Nidaa – Dhahiri shahiri babu! ( 2 x2 = 4)
      3. Eleza matatizo yanayokumba safari inayorejelewa. Al.12
        1. Mauaji ya jabali na uongozi
        2. Kufungwa kwa soko la chapakazi
        3. Nja
        4. Urisadi
        5. Kufungwa jela kiholelea
        6.  Kuchapwa na askari
        7. Uchafuzi wa mazingira
        8. Migomo
        9. Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya
        10. Kutowajibika kwa viongozi
        11. Ubadhirifu wa mali ya umma
        12. Kudhirifu wa mali ya umma
        13. Kudhibiti vyombo vya habari
        14.  Utabaka
        15. Ulipizaji kisasi
        16. Usaliti
          (12 x 1 = 12)

    2. Tamthlia ya kigogo inazungumza kuhusu hali halisi katika mataifa mengi ya kiafrika. Jadili. Al.20
      1. Uongozi mbaya unaoendelezwa na majoka
      2. Unyakuzi wa ardhi majoka kipande cha ardhi palipokuwa soko la chapa kazi na kujenga hoteli ya kifahari majoka and majoka Resort.
      3. Mauaji – vijana waoandama wanauawa. Mpinzani k.m Jabali
      4. Vitisho wanasagamoyo wanaishi kwa hofu. Tunu kuvunjwa mguu.
      5. Matumizi ya vyombo vya dola. Askari wanatawanya waandamanaji pasi kupata haki zao.
      6. Maandamano na migomo wafanyikazi wanagoma kutetea haki zao. Walimu na wauguzi.
      7. Uongozi wa kinasaba/ukoo familia ya Ngao inatawala Ngao bin Marara, Majoka bin marara aliyekusudia kumrithisha mwanawe Ngao Junior.
      8. Ufisadi wanasagamoyo wanatozwa kodi ya juu
      9. Ubadhirifu wa mali ya umma. Pesa za mkopo zinatumika kufadhili mradi wa uchongaji vinyago.
      10. Umaskini Ashua anaenda kuomba msaada kwa majoka
      11. Ukoloni mamboloea
      12. Juhudi za mapinduzi
      13. Ubaguzi wa wa kinjisia hasa kwa wanawake – Tunu alikejeliwa kuwa angereuliwa kama kiongozi wa sagamoyo.
      14. Matumizi mabaya ya vyombo vya habari. 10x2 = 20
        Hoja ( al.1)
        Mfano mwafaka al.1

  3. RIWAYA: CHOZI LA HERI
    1. “Alikumbuka jinsi rafiki yake……..alivyofishwa kwa njia hii. Akili yake ilimtambia kisa chenyewe kana kwamba inataka kumwonya (uk.120)
      1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. Al.4
        • Haya ni maneno ya msimulizi
        • Yanamhusu Dick akikumbuka rafiki yake lemi ambaye aliuawa na umati
        • Anakumbuka kisa hiki anapoitshwa kuwa angetupwa nje na mwajiri wake, Buda, kisha asingiziwe wizi na kuchomwa moto.
        • Hofu hii ndiyo iliyomchochea kuingilia ulanguzi wa dawa za kulevya.

      2. Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. Al.4
        1. Tashihisi - Akili ya Dick ilimtambia kisa chenyewe kama kwamba inataka kumuonya.
        2. Chuku - Akili ilimtambia kisa

      3. Tathmini nafasi ya anayelengwa na kauli hii katika kuijenga riwaya hii. Al.12
        1. Ametumiwa kuonyesha nafasi ya familia katika malezi. Kuondoka kwa mama yake kunaisambaratisha familia yake;Dick na mwalike wanaibwa na sauna.
        2. Ametumiwa kukashifu ufisadi. Anasema kwamba maafisa wa usalama wanaingia kwa Buda kwa tabasamu na kutoka kwa vicheko.
        3. Anaendeleza swala la matumizi mabaya ya dawa. Anatumia dawa na kuzilangua.
        4. Anachimu za maudhui ya mabadiliko. Anaamua kuacha ulanguzi wa dawa, kujielimisha na kuanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu.
        5. Anaonyesha nafasi ya vijana katika kuboresha maisha ya jamii zao. Anawaajiri vijana wenzake. Ni kielelezo cha vijana wanaotambua makosa yao na kujirekebisha.
        6. Ametumiwa kujenga tabia za wahusika.
          • utu wa mwangeka. Anamchukua kama mwanawe na kumwelekeza.
          • Ukakamavu wa Umu – umu anamwambia Dick kuwa yeye, umu, atawalea yeye Dick pamoja na mwaliko kwa viganja vyake japo umu ni mchanga wakati huo.
        7. anaendeleza ploti kukutana kwake na umu kunabadilisha mkondo wa hadithi. Anaelekezwa na umu kwa mwangeka ambaye anamsaidia kuyatengeneza maisha yake zaidi.
          6 x 2 = 12
          Hoja (al.1)
          Mfano ( al.1)


    2.      
      1. Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. Al.10
        1. Ridhaa – Kukubali ama kutosheka. Mhusika Ridhaa anakubali na kutosheka na makuruhu aliyofanyiwa ya kuteketezewa mali na familia yake.
        2. Bwana Tenge – Tenge ina maana ya fujo. Bwana Tenge anamfanyia mkewe fujo na vitimbi anamwendea kinyume mke wake, Bi. Kimai. Bwana Tenge anashiriki mapenzi na wanawake wengine.
        3. Mzee Kedi – Neno kedi lina maana ya mambo yasiyopendeza, mambo ya hila pia ni kiburi. Mzee Kedi anamfanyia ridhaa hila kwa kuhusika katika kuiangamiza familia yake.
        4. Bwana Mkubwa – Mkubwa ni neno lenye maana ya cheo au hadhi kubwa. Bwana mkubwa ana cheo kikubwa serikalini.
        5. Tetei – ina maana ya kutetea. Bi. Tetei ni mwanaharakati anayetetea haki za wanaume.
        6. Mwalimu Dhahabu ni madini yenye thamani. Mwalimu dhahabu ni mwalimu anayekuwa wa msaada kwa Umulkheri
        7. Hazina – Hazina ina maana mali iliyohifadhiwa. Mhusika Hazina anakuja kuwa kama hazina kwa Umukheri kwani anamfaa Umu jinsi alivyomfaa kwa kimpa noti ya shilingi mia mbili.
        8. Zohali – Neno hili lina maana ya ajizi. Mhusika Zohali anapachikwa mimba akiwa kidato cha pili ni dalili ya uzembe na kutomakinika masomoni.
        9. Chandachema – Chandachema ni jina lililoundwa kutokana na Chanda kidole) chema ambacho huvikwa pete. Mhusika huyu ingawa anapitia changmoto tele maishani anaishia kupewa ufadhili wa masomo(kuvishwa pete) na shirika la kidini.
        10. Bwana Mabavu – Mabavu ni nguvu. Bwana Mabavu anatumia nguvu kumpoka babake Shamsi ardhi yake.
        11. Mzee Maarifa- anatumia maarifa na hekima kuanzisha kituo cha kupigania hakiza kibinadamu
        12. Neema ni mkewe Mwangemi. Neema ina maana ya Baraka. Mhusika huyu anakuwa Baraka kwa mume na pia kwa mwaliko.
        13. Bwana Kimbaumbau ni mtu kigeugeu. Bwana Kimbaumbau anamsaliti Naomi kwa kutaka kufanya mapenzi naye.

      2. Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri. Al.10
        1. vijana ni wasomi mf. Umu, tila.
        2. Ni walanguzi wa dawa za kulevya mf. Dick.
        3. Vijana wengine wa kike wakubali kukeketwa na wengine wanaaga dunia na kulazwa hospitalini mf. Tauma.
        4.  Vijana ni wapenda fujo.
        5. Vijana hutumiwa na wanasiasa kutekeleza uovu na mauaji.
        6. Ni dhihirisho kama wasio na huruma. K.m kuua wenzao bila huruma.
        7. Wasio na msimamo dhabiti. Wanapotoshwa na wanasiasa bila kuwazia madhara waliosababisha.
        8. Vijana ni wenye bidii katika kazi zao mf. Dick.
          (Tanbihi: kadilia hoja za wanafunzi.)
          10 x 1 = 10

  4. HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA
    1.      
      1. Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10
        1. Kifaurongo ni mmea wenye sifa ya kujifisha mara unapoguswa. Mwandishi akejeli mahusiano yaliyojengwa katika msingi wa unafiki.
        2. Penina anajifanya kumjali Dennis katika hali yake ya kunywa uji na kuonyesha huzuni. Anamtia Dennis mshawasha wa mapenzi ila si mapenzi kamili.
        3. Msimulizi anadai wavulana wengi wameangamia katika utandabui wa mapenzi baada ya kufanyiwa makuruhu na wasichana wenye tabia ya kifaurongo.
        4. Penina anadai atakuwa na Dennis kwa mazuri na mabaya lakini alimwacha alipokosa ajira.
        5. Penina asema kuwa hafanyi mzaha na kuwa hawezi kumchagua mpenzi kwa msingi wowote kama si mapenzi. Mwishowe alivunja ndoa yake kwa sababu Dennis alikuwa fukara. Hii ni tabia ya kifaurongo.
        6. Penina hataki kuitwa mpenzi wa Dennis na amtaka atafute msichana wa kufu yake akidai mgomba changaraweni haupandwi ukamea.
        7.  Penina amfukuza Dennis nyumbani alipolosa kazi ilhali alikuwa ameapa hangemsaliti kwa vyovyote vile.
          Hoja 5 x 2 = 10

      2. Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha. Al.10
        1. Wanafunzi wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne ili kubaini hatima yao. Samueli awaza kuwa matokeao ya mthihani yangekuwa daraja ya ufanisi.
        2. Elimu ina daraja/viwango – Samueli anatarajia kuingia chuo kikuu anapokamilisha kidato cha nne.
        3. Katika masomo kuna kufeli.
        4. Wanafunzi wanahofia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne k.m Samueli.
        5. Wanafunzi wanaojiamini kupindukia huathiriwa kisaikolojia wanapofeli.
        6. Wanakunzi lazima watimize matakwa Fulani kabla ya kupatiwa matokeo yao.
        7. Wanafunzi wengine wanaonea aibu matokeo yao.
        8. Jinsia ya kike inapiku jinsia ya kiume masomoni k.m Dada zake Samueli.
        9. Jinsia ya kike inabaguliwa masomoni. Babake Samueli ameweka matumaini yake kwa Samueli.
        10. Watoto wanatarajiwa kupita mtihani wanusuru familia zao.
        11. Wanafunzi wanaichukulia elimul na masomo kwa mzaha na kejeli.
        12. Samueli aliona shule kama jela.
          10 x 1 = 10

    2. Mame Bakari
      “Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Uaogopa nini?
      1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. Al.4
        1. Msemaji ni babake Sara. Akimwambia Sara. Wakiwa hospitalini kwenye chumba cha daktari. Sara alikuwa ameenda kufanyiwa vipimo vya ujauzito na Beluwa alipowakuta wazaziwe wakisubiri katika chumba hicho.
      2. Eleza sifa za mrejelewa. Al.6
        1. mpenda masomo
        2. ni mwoga
        3. mwenye busara
        4. mwenye mapenzi ya dhat
        5. mwenye utu hakutaka kuavya mimba
        6. ni msiri
        7. mwenye maadili
        8. mwenye majuto
        9. ni mvumilivu.
          (kila sifa itolewe maelezo. Mwanafunzi akitaja sifa tu asituzwe)
          Hoja Zozote 6 (6x 1 = 6)

      3. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. Al.2
        1. Swali la balagha; una nini?
        2. Takriri; unaogopa, unaogopa

      4. Eleza umuhimu wa msemaji. Al.4
        1. Kupitia kwake tunapata habari ya ukali kupita kiasi kwa wazazi kwa wanao.
        2. Ni kielelezo cha wazazi ambao hawako tayari kubadili msimamo wao mkali kwa watoto wao.
        3. Anaonyesha umuhimu wa wazazi kushirikiana katika malezi.
        4. Anaonyesha umuhimu wa kuweka siri katika masuala tata ya familia.
        5. Ni kielelezo cha wazazi wanaouenzi utamaduni wa jamii yao.

      5. Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. Al.1
        1. Malezi
        2. mapenzi

      6. Fafanua maudhui katika swali la (e) kwa kurejelea hadithi nzima. Al.3
        1. Babake Sara anakuwa mkali kwa sara. Babake Sara anadalika na kumwonyesha mapenzi.
          Mapenzi
          1. Kuna mapenzi ya dhati kati ya sarana salime.
          2. Salime anamsaidia sara anapokuwa mjamzito.
          3. Salime aidha anamsaidia sara kuweka siri ya ujauzito.
  5. USHAIRI   
    1. MASWALI
      1. Eleza dhamira ya shairi hili. Al.2
        1. Kueleza madhara ya kutofuata mawaidha/ushauri wa baba na mama.
        2. Kuonyesha hasar/shida zinazowapata watu walio na kiburi, majivuno, tama.
          2 x 1 = 2

      2. Tambua njia mbili anazotumia mtunzi wa shairi hili kusisitiza ujumbe wake.Al.2
        1. Matumizi ya kibwagizo.
        2. Kurejelea methali k.m maajuto ni mjukuu huja kinyume.

      3. Taja na utoe mifano ya aina zozote mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi. Al.4
        1. Swali la balagha – ya nini kushangaaa?
        2. Jazanda - Ulijidhania Samba. 2x 2 = 4

      4. Andika ubeti wa tatu katika lugha tutumbi. Al.4
        1. Yale uliyoyaona kuwa bora ndiyo sasa yamekuletea shida. Mamia ya matatizo hayaishi kwako/ wapo ungetambua hapo awali basi hungekuwa ukitatizika wewe mwenyewe ndiwe chanzo cha haya.. (4 x 1 = Al.4)

      5. Bainisha toni ya shairi hili. Al.2
        1. Inkisari – alikuamba badala ya alikwambia
        2. Kuboronga sarufi – alikwambia wako mama badala ya mama wako alikwambia
        3. Lahaja – huanziriki/hupuliki 2x 2 = 4

      6. Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina mbili za idhini ya kishairi katika shairi hili. Al.4
        1. Toni ya majuto – anashangaa mambo yanvyomendea
        2. Toni ya kusikitika – anasikitika mishikeli haitoki kwake (matatizo yameganda)

      7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. Al.2
        1. Mstahiki -mheshimiwa
        2. Hupuliki - Husikii/Husikizi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Meru Central Cluster Exam 2020.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest