Kiswahili Trial Exams Paper 2 Questions - Alliance Boys High School Mock December 2020

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 1. Jibu maswali yote. 
 2. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
 3. Karatasi hii ina kurasa 12.
 4. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
  SWALI/SEHEMU  ALAMA  ALAMA ZA MWANAFUNZI 
 UFAHAMU 15   
 UFUPISHO 15  
3  MATUMIZI YA LUGHA 40  
5  ISIMU JAMII 10  
   JUMLA 80  
       


MASWALI

UFAHAMU (Alama 15)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali.
Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusisha amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi vidogo kunatokana na sababu mbalimbali.

Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda. Katika msingi huu viwanda vikubwa vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa matatizo sugu. Tofauti na mataifa ya kitasmia (yenye viwanda vingi) mataifa mengi yanayoendelea hayana mifumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.

Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mtaji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa hiyo uwe mdogo ukilinganishwa na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri huwa ni kwa kiwango kidogo.

Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo mzuri wa kimapato nchini. Mweneo huo wa mapato unachangia katika kuboresha uwezo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Upanuzi na ueneaji wa viwanda vidogo vidogo ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.

Maswali

 1. Kwa nini viwanda ni muhimu? (Alama 7)
 2. Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea? (Alama 1)
 3. Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani? Alama 4)
 4. Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu. (Alama 3)
  1. Kujasurisha
  2. Amali
  3. Utashi

UFUPISHO (Alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ufupishe habari kulingana na maswali uliyopewa.
Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa, hasa katika nchi zinazoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi za ulimwengu huu. Kuna idadi kubwa ya watoto wanaoajiriwa katika nyanja mbalimbali za jamii. Zipo sababu nyingi zinazowasukuma watoto kutafuta ajira barani Afrika kwa mfano, familia nyingi huishi maisha ya ufukara hivi kwamba hushindwa mahitaji muhimu hususan kwa watoto. Kupanda kwa gharama ya maisha kunazidisha viwango vya umaskini. Ukosefu wa lishe pia huwafanya watoto kutoroka nyumbani kutafuta ajira. Janga la ukimwi limesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya mayatima wanaoishi kutafuta ajira ili kuyakimu maisha. Ukimwi umezifanya familia nyingi pia kuwaondoa watoto shuleni ili waweze kuajiriwa kwa lengo la kuzalisha pato la familia hizo. Watoto wengine hutoroka makwao kwa sababu ya maonevu. Maonevu haya ni kama vile kupigwa, kutukanwa kila wakati, kunyanyaswa kijinsia na kadhalika. Huko nje hutaabishwa kimwili na kiakili. Hufanyishwa kazi za sulubu zenye malipo duni au wasilipwe kabisa. Hili huwasononesha na kuathiri afya yao.

Wengine hujiingiza katika vitendo vya jinai pale wanapokosa ajira huchukua sheria mikononi mwao, wakaendeleza vitendo vya ukatili kama vile kuwahangaisha watu na kupora mali yao au hata kuwakaba roho. Aidha wengine hujikuta kwenye madanguro ambako huendesha biashara haramu.

Uundaji wa Umoja wa Afrika ni hatua muhimu ya kushughulikia matatizo ya Afrika kama vile ajira ya watoto, kuzorota kwa miundo msingi, magonjwa, njaa, umaskini, ufisadi na ukabila Katika kushughulikia haki za watoto nchi za Afrika hazina budi kuzingatia masharti yaliyowekwa na umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto. Nchi nyingi za Afrika ziliidhinisha mkataba wa masharti hayo, ikiwemo nchi ya Kenya. Nchi hizi basi lazima zishughulikie haki za watoto kupitia sheria za nchi. Watoto ni raslimali muhimu na ndio tumaini la kuwepo kwa kizazi cha binadamu,

Maswali

 1. Eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya kwanza. (maneno 80) (Alama 6, 1 ya mtiririko)
  Matayarisho
  Jibu
 2. Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwisho (maneno 90)
  (Alama 7, 1 ya mtiririko)
  Matayarisho
  Jibu

MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

 1. Taja vikwamizo viwili ambavyo ni konsonanti hafifu (Alama 1)
 2. Tambua aina ya sentensi hizi kwa kuzingatia azma. (Alama 2)
  1. Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya.
  2. Naomba uwaite wanafunzi wale.
 3. Mbali na kuandikia usemi halisi, tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mengine mawili tofauti ya alama za mtajo. (Alama 1)
 4. Andika katika wakati ujao hali timilifu udogo (Alama 2)
  Wanafunzi walifanya mtihani wa mwigo
 5. Zaidi ya kuonyesha kitenzi kishirikishi kipungufu, tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiambishi ndi- (Alama 1)
 6. Tunga sentensi moja yenye fungu tenzi lenye muundo ufuatao (Alama 2)
  t+T+N
 7. Andika kwa usemi wa taarifa (Alama 1)
  Mama watoto aliuliza, "mbona mnajikunyata kama mayatima".
 8. Badilisha vitenzi vifuatavyo viwe katika hali ya kutendeka. (Alama 2)
  1. kwea
  2. dhuru
 9. Bainisha aina za nomino zilizotumika katika sentensi ifuatayo (Alama 1)
  Kikosi cha askari kiliabiri ndege hadi ujerumani
 10. Tumia mzizi -w- katika sentensi kama: (Alama 2)
  kitenzi kisaidizi
  kitenzi kishirikishi
 11. Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya 'na' kama (Alama 1)
  Kihusishi cha 'na' ya mtenda.
 12. Tunga sentensi kwa kutumia kibadala cha kiasi jumla katika ngeli ya A-WA.(Alama 2)
 13. Onyesha muundo wa silabi ya kwanza katika maneno yafuatayo: (Alama 2)
  Nyakua.............................
  Chura.............................
 14. Ainisha mofimu-li-katika tungo hili. (Alama 1)
  Alivyolikimbilia
 15. Viambishi vilivyopigiwa mstari vinawakilisha dhana zipi za kisarufi?(Alama 2)
  Udhaifu
  Walani?
 16. Neno matukio liko katika ngeli gani? (Alama 1)
 17. Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii. (Alama 1)
  Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?
 18. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali. (Alama 4)
  Mlango umevunjwa na fundi aliyeujenga.
 19. Andika katika wingi karibu. (Alama 1)
  Mtu yuyo huyo aliubeba mzigo uo huo licha ya kukanywa.
 20. Weka kirejeshi 'o' tamati kwenye kitenzi chunga katika wingi kisha ukitungie sentensi katika ngeli ya KI-VI. (Alama2)
 21. Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utunge sentensi katika ukubwa - wingi. (Alama 2)
 22. Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi.(Alama 1)
 23. Msomi hakutuzwa siku hiyo.
  Onyesha matumizi ya chagizo ya mfanano katika sentensi. (Alama 2)
 24. Tunga sentensi moja ukitumia kitenzi kimoja kilichoundwa kutokana na nomino zawadi (Alama 1)
 25.  Panda ni kutia mbegu ardhini au kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili (Alama 1)
 26. Tunga sentensi yenye muundo wa: (Alama 1)
  Kiima, kiarifa, yambwa tendwa, yambwa tendewa na yambwa ala.

ISIMUJAMII (Alama 10)
Jadili sifa mbilimbili za sajili zifuatazo

 1. Michezo
 2. Magazetini
 3. Darasa
 4. Mazungumzo ya simu
 5. Biashara
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Trial Exams Paper 2 Questions - Alliance Boys High School Mock December 2020.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest