Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 3. Andika insha mbili. Swali la kwanza ni la lazima
 4. Kisha chagua iisha nyingine moja kutoka kwa hizo tatu zilizobakia. 
 5. Kila insha isipungue maneno 400. 
 6. Kila insha ina alama 20.
 7. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Jumla  Upeo  Alama 
 1  20  
   20  
JUMLA  40  


MASWALI

 1. Suala la ufisadi limekuwa tatizo sugu katika jamii ya Kenya. Andika hotuba utakayotoa kama afisa wa Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya kuhusu mbinu za kupambana na ufisadi kwa wanakijiji chenu. (al. 20)
 2. Serikali za ugatuzi zitaboresha maisha ya wananchi. Jadili (al. 20)
 3. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. (al.20)
 4. Andika insha itakayoanza kwa maneno yafuatayo: Nilipowakumbuka wenzangu macho yaliingia kiwi na nikaanza kutiririkwa na machozi... (al. 20)


MAJIBU

1. Suala la ufisadi limekuwa tatizo sugu katika jamii ya Kenya. Andika hotuba utakayotoa kama afisa wa Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya kuhusu mbinu za kupambana na ufisadi kwa wanakijiji chenu.
Mbinu za kupambana na ufisadi

 • Kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ufisadi kupitia kwa redio, magazeti, runinga n.k.
 • Kuwaadhibu wahusika - wapelekwe mahakamani na wafungwa jela.
 • Wananchi waadilike (wawe na maadili mema).
 • Viongozi wawajibike katika kazi zao.
 • Sheria za kupambana na ufisadi zibuniwe na kutekelezwa.
 • Kubuni nafasi zaidi za kazi
 • Kuimarisha elimu
 • Kuongeza mishahara kwa wafanyikazi
 • Tume zaidi za kukabiliana na ufisadi zibuniwe.
 • Watu watangaze mali zao
 • Kutwaliwa kwa mali za wafisadi
 • Kuwafuta kazi wafisadi nk nk
  Mtahini azingatia muundo wa hotuba; Hatibu ajitambulishe mwanzoni na pia atambue hadhira yake. Utangulizi, mwili na tamati

2. Serikali za ugatuzi zitaboresha maisha ya wananchi. Jadili
Mwanafunzi lazima azingatie pande zote mbili. Upande wa kuunga uwe ndio una hoja nyingi. Akiegemea upande mmoja asipite C+ alama 10. Baadhi ya hoja za kuunga

 • Miundo misingi kuboreshwa. 
 • Nafasi za kazi kuongezeka.
 • Maendeleo kusambazwa kote nchini. 
 • Huduma muhimu kuletwa karibu na wananchi.
 • Jinsia zote kuhusishwa uongozini.
 • Uongozi kuletwa mashinani kama vile Magavana, Waakilishi wa wadi nk.
 • Usalama kuimarishwa
 • Rasilmali katika kila gatuzi kutumika ipasavyo kwa manufaa ya kila mmoja.
 • Kupunguza misongamano katika miji mikuu - wengi kurudi mashinani kutafuta kazi.
 • Usawa katika ugavi wa mali ya umma.

Baadhi ya hoja za kupinga.

 • Fedha nyingi kutumika kulipia mishahara ya wananchi wengi watakaoajiriwa katika gatuzi.
 • Ukabila kuenezwa - baadhi ya watu kuamini kuwa kuna watu / kabila fulani linalomiliki gatuzi.
 • Majimbo mengine kusalia nyuma pakiwa na uongozi mbaya.
 • Mianya ya ufisadi kuongezeka.
 • Migongano kuibuka kati ya serikali kuu na magatuzi.
 • Kaunti zisizo na rasilmali nyingi kusalia nyuma kimaendeleo. 
 • Mshikamano wa kitaifa kuyubishwa.
 • Kodi zinazotozwa wananchi kuongezeka.

Kadiria hoja nyingine zozote zilizo sahihi.
3. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
Mwanafunzi atunge kisa kinachojibu mada. Si lazima mtahiniwa aeleze maana ya methali. Kisa chake kifafanue maana
Kisa kionyeshe umoja katika kutekeleza jambo (faida za umoja) na udhaifu au hasara za utengano. Ubunifu wa mtahiniwa uzingatiwe

4. Andika insha itakayoanza kwa maneno
yafuatayo: Nilipowakumbuka wenzangu macho yaliingia kiwi na nikaanza kutiririkwa na machozi...
Kisa kidhihirishe hali ya huzuni na nafsi ya kwanza 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest