Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

 1. Hii karatasi ina kurasa kumi na mbili zilizopigwa chapa. 
 2. Mtahiniwa anapaswa kukagua hili karatasi ili kuthibitisha kuwa kila ukurasa umepigwa chapa na kuwa hakuna swali linalikosekana 
 3. Jibu maswali yote. 
 4. Andika majibu yako kwenye nafasi uliyotengewa baada ya kila swali.
 5. Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili sanifu.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI  UPEO  ALAMA 
 1  15  
 2  15  
 3  40  
 4  10  
 JUMLA  80  


MASWALI

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Idadi ya watu wanaotoka mashambani kwenda mijini kutafuta ajira huzidi kuongezeka kila mwaka. Kile wasichokijua wahamiaji hao ni kuwa kuna njia nyingine za kujipa riziki, mojawapo ikiwa kujiajiri. Hii ndiyo sababu wanafunzi wanashauriwa daima kutumia elimu na maarifa wanayopata shuleni na vyuoni kujitegemea kwa kuanzisha kazi zao za binafsi.

Wengi watasema kuwa ni vigumu mtu kuanza kazi kama hizo bila kuwa na mtaji. Ndiyo mtaji huhitajika katika kustawisha kazi yoyote ile, lakini zipo njia nyingi za kujikwamua na kuwezesha hili kufanyika. Mojawapo ni kujiwekea akiba kidogo kidogo kwa muda hata kutokana na masurufu yako ya shuleni.

Manufaa ya ajira ya mtu binafsi ni kwamba inamwezesha mtu huyo kuendeleza kazi yake bila kuingiliwa na mtu mwingine. Mtu hupata fursa ya kujihusisha na shughuli mbalimbali zinazohusiana na kazi yake kama vile mauzo, masuala ya usimamizi wa kifedha,mipango na hata kuwasimamia wale wanaomfanyia kazi.Bila shaka ni fahari kuu kujisimamia na kufanya kile ambacho anakifurahia mbali na kuwa utapata fursa ya kuwachagua wale ambao ungependa kufanya nao kazi. Aidha,utaweza kuwahudumia wateja wako,na hivyo kukuwezesha kujua vyema mahitaji yao.

Kujisimamia katika kazi yako vilevile kutawezesha kudhibiti maamuzi yote ambayo yanaathiri shughuli zao kikazi.Utakuwa huru kuweka mikakati bora ya kibiashara,taratibu na kuhakikisha ubora wa bidha na huduma zako, bei za bidhaa zako na kadhalika.Pamoja na hiyo, hutaishi kwa hofu ya kuwachishwa kazi kwa kufanya mambo jinsi uonavyo ni mwafaka.Isitoshe,utaweza kupanua tajriba yako kikazi kadiri unavyoweza kujishirikisha na kazi zako, pamoja na kuwa utapata uhuru wa kuamua namna ya kutumia muda wako kufanya kazi na maeneo ya kufanya kazi. Yote yakikuendea vyema, bila shaka utaweza nyingi kuliko kiasi ambacho ungepata kwa kuajiriwa.

Kwa upande mwingine, kuajiriwa kunahitaji kujitolea kwa hali ya juu. Zipo nyakati ambapo unahitajika kutafuta pesa zaidi ili kufidia upungufu fulani na kulipa baadhi ya bili zako. Aidha,zipo wakati ambapo utajinyima baadhi ya mahitaji ama starehe ili kutimiza ndoto zako.Unafaa pia kukumbuka kuwa kwa kila siku utakayokosa kufanya kazi, hakuna kiasi cha pesa utakazopata,kwa hivyo utalazimika kutumia muda wako mwingi ukifanya kazi. Mbali na hayo utakuwa ukijilipia bima kama vile ya matibabu, pamoja na kujiwekea mipango ya kustaafu kumbukwe pia kuwa pamoja na kuwa na uwezo wa kuchagua wateja wako, huna uhuru wa kudhibiti matarajio yao ikiwa umeajiriwa

Kimsingi, ukitaka kujiajiri, lazima uwe tayari kufanya kazi kwa bidii na kwa muda mwingi zaidi. Ni lazima pia uweze kuvumilia hatari na mzongo wa akili na uweze pia kukabiliana na majanga au hata hali ya kufeli kwa jambo.

MASWALI 

 1. Taja sababu za watu kuguria mijini. (alama1)
 2. Eleza njia za kupata chumo. (alama2)
 3. Mojawapo ya njia iliyotajwa ina changamoto. Ifafanue. (alama1)
 4. Tambua manufaa ya kujiajiri. (alama 4)
 5. Bainisha upungufu wa kujiajiri. (alama 4)
 6. Yatolee maana maneno haya kwa kurejelea kifungu.(alama 3)
  1. Mzongo wa akili.
  2. Mtaji...........
  3. Masarufu........

2. UFUPISHO (ALAMA 15)
Sanaa ya jadi ni njia moja ya mawasiliano ambayo ni adhimu, hasa barani Afrika. Mawasiliano kupitia ya jadi ni njia bunifu ya kuwasilisha ujumbe kupitia kwa sanaa tendi kama vile drama, ushairi tendi, nyimbo, ngoma na kadhalika. Njia hii imekuwa ikitumika katika jamii nyingi za Kiafrika toka jadi mkubwa sana, kuwasilisha ujumbe kwa wanajamii, hasa hekima na busara ya wakongwe kwao chipukizi.

Takribani katika jamii zote za Kiafrika, sherehe yoyote ya jadi haikukosa sana tendi. Lazima pana sanaa tendi katika sherehe kama vile tohara, kutakaswa na kutawazwa kwa viongozi, mazishi, ndoa na burudani. Licha ya kuburudisha na kuchangamsha waliohudhuria, sanaa hizi zilitumika kuwasilisha ujumbe. Sanaa hizi hata hivyo hazijapitwa na wakati na bado zinaweza zikatumika sambamba na mawasiliano kama vile redio. Runinga. Magazeti, majarida na wavuti. Matumiza ya sana aya jadi pamoja na njia za kisasa za mawasiliano yana manufaa lukuki. Kwanza haya yataweza kuwashirikisha kikamilifu watu wengi katika mawasiliano, hasa akina yale wanaotoka katika mita aya mabanda ambao huhisi wametengwa na njia za kisasa za mawasiliano, njia za kisasa za mawasiliano huchukuliwa na baadhi ya wanajamii kuwa ni milki ya walioclimika, na hasa wenye ushawishi mkubwa katika kuunda na kutekeleza sera zinazotawala nchi.

Hali kadhalika, mawasiliano huchukuliwa kuwa ni himaya ya watu wanaojiweka mbele kuwa wajuzi. Wao huzitumia njia hizo kuendeleza maslahi yao kwa kutoa maamuzi yanayowaathiri hata bila kuwashirikisha katika maamuzi hayo. Fauja ya haya, njia za kisasa za masiliano hutumia hazizahamiki na wengi. Aghalabu hutumia lugha za kigeni kama vile kiingereza na kifaransa, ndizo lugha za kimataifa na lugha tukufu, ingawa ujumbe unaowasilishwa na lugha hizo huusiwa yenye utata na isiyaeleweka na wengi. Matokeo ya ujumbe huo ni athari kwao pamoja na vizazi vya njia hizi kuwa ghali na pia huchukuana na teknolojia inayokanganya. Hali hizi ndizo huchangia kwa wanajamii na viongozi, na kuwafanya watumiaji baridi na njia hizi za mawasiliano kwa kuwakosea kutoa mwitiko ama michango yao kupitia kwa njia hizi.

Kwa upande mwingine, matumizi ya njia ya sanaa za jadi hushirikisha watu wote - walioelimika. Hii ni kwa kuwa njia hii haitegemei matini yaliyoandikwa. Pili, njia hii haitumii inayokanganya na iliyo ghali. Zaidi ya sanaa za jadi hupasha ujumbe huku kuburudisha, kuteka na kuwaburudisha wengi huku ikidumisha urazini na taharuki zao. Aidha, sanaa nafasi ya kurudia igizo au onyesho na kuwasilisha jumbe anuai kwa muda mfupi sana.

Sanaa y ajadi, kama njia ya mawasiliano, hutoa nafasi sawa kwa watu wote kuelimika na kupata kubagua kwa misingi ya umri au jinsia. Hii ni kwa kuwa wakubwa kwa wadogo, chipukizi kwa waku kwa wanaume na wavulana kwa wasichana wanaweza kashiriki katika maonyesho au maigizo. S kiafrika aidha hutoa nafasi kwa hadhira kushiriki. Njia hii pia ni maarufu katika kuzindua,kusambaza ujumbe kwa watu wengi bilaa kuwachish wala kuwasinya. Licha ya kuwa ina uwezo wa na kumchambua mtu kwa wakati huo huo, ina uwezo pia wa kumfanya mtu asijihisi kusimangwa , kukashifiwa wala kufanyiwa stihizai. Hivyo basi, hakuna kwenda mahakamani kush fidia kama ilivyo katika njia za mawasiliano za kisasa. Sanaa tendi huwa hailengi mtu mahususi inayoshiriki, na kila mmoja huthirika kivyake.

MASWALI

 1. Kwa maneno kati ya 40-50, eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya kwanza na ya pili. (alama 7).
  MATAYARISHO.........................................................
  JIBU .........................................................
 2. Fupisha ujumbe katika aya tatu, nne na tano kwa maneno kati ya 100-110. (alama 10)
  MATAYARISHO.........................................................
  JIBU.........................................................

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

 1. Tofautisha irabu katika neno: Pindu (alama 2)
 2. Eleza uamilifu wa viambishi katika neno: wafiwao. (alama 2)
 3. Ziweke nomino zifuatazo katika ngeli zake:(alama 2)
  1. Baridi ....... 
  2. Undu ........
 4. Eleza matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
  Wazee kwa vijana walivuka barabara kwa makini ila sita kwa kumi ndio waliofika kwa Yohana
 5. Tunga sentensi moja kubainisha matumizi mawili ya kiambishi (31).(alama 2)
 6. Andika katika usemi wa taarifa:
  (alama 3) "Kiwango cha umaskini katika gatuzi hili kinasikitisha sana; itabidi sote wakazi wa hapa tujizatiti ili tutimize malengo ya Milenia, "Seneta mteule alituhimiza.
 7. Eleza maana tatu katika sentensi: Baba alimwanbia mtoto kuwa angeenda shuleni. (alama 3)
 8. Ukizingatia kauli zilizo mabanoni tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi. (alama 2)
  1. pa (tendewa).
  2.  Hubiri (tendeka)
 9. Changanua sentensi hii kwa njia ya jedwali Viwanda vyote vilivyoundwa juzi vitaleta faida kubwa ajabu.(alama 4)
 10. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana za vitate: kura na gura. (alama 2)
 11. Kanusha:(alama1)
  Mama aliingia chumbani kisha akawapikia watoto wali.
 12. Tumia kiwakilishi cha 'a-unganifu katika sentensi kuonyesha: (alama 2)
  1. Aina ya
  2. Umilikaji
 13. Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari.
  Ni jukumu la maskauti kupandisha bendera kila Ijumaa. (alama 2)
 14. Tumia 'o' rejeshi ya mazoea katika sentensi ifuatayo:(alama 2)
  Mti ambao ulikatwa ulipelekwa uwanjani.
 15. Andika katika udogo. (alama 2)
  Ngamia huyo atausafirisha mzigo mzito.
 16. Ainisha sentensi hii kwa kuzingatia dhamira/jukumu.(alama 1)
  Mezeni tembe mbili kwa maji vuguvugu kila baada ya kula.
 17. Tunga sentensi iliyo na: kirai nomino, kirai kihusishi na kirai elezi. (alama 3)
 18. Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi:(alama 3)
  Wanafunzi wataletewa zawadi bora na wazazi wao kesho kutwa.

4. ISIMU JAMII (ALAMA10)

 1. Eleza dhima nne za lugha ya taifa. (alama 4)
 2. Fafanua manufaa matatu yatokanayo na usanifishwaji wa Kiswahili (alama 6)
 3. Onyesha namna kaida zifuatazo zinavodhibiti mawasiliano:(alama 3)
  1. Mada.
  2. Wahusika
  3. Malezi


MAJIBU

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
MASWALI 

 1. Taja sababu za watu kuguria mijini. (alama1)
  Kutafuta ajira/kutafuta kazi (1x1=1)
 2. Eleza njia za kupata chumo.(alama2)
  Kujiajiri
  Kuajiriwa (2x1=2)
 3. Mojawapo ya njia iliyotajwa ina changamoto. Ifafanue. (alama1)
  Kujiajiri. Njia hii ina changamoto kwa kuwa kujiajiri kunahitaji mtaji (1x1-1)
 4. Tambua manufaa ya kujiajiri. (alama4)
  Mtu haingiliwi katika kazi yake
  Mtu hujihusisha na shughuli mbalimbali zinazohusiana na kazi zake.
  Mtu ana uwezo wa kudhibiti maamuzi Kuna uhuru wa kuweka mikakati bora ya kazi/biashara Hakuna hofu ya kuwachishwa kazi na mwajiri. Kuna uwezekano wa kupanua tajriba. (4x1-4)
 5. Thibitisha kuwa kujiajiri kuna kero zake. (alama4)
  Kujiajiri huitaji kujitolea
  Huenda mtu akahitajika kutafuta pesa zaidi kufidia upungufu au kulipa bili
  Mtu kujinyima mahitaji na starehe.
  Mtu akikosa kufanya kazi hatapata malipo
  Hakuna uhuru wa kudhibiti matarajio ya wateja (zozote 4x1=4)
 6. Maana ya maneno haya kwa kurejelea kifungu
  1. Mzongo wa akili Uchovu wa akili kutokana na mawazo meni
  2. Mtaji-Mali au pesa za kuanzisha biashara
  3. Masurufu-Pesa za matumizi ya ziada (3x1=3)

2. UFUPISHO (ALAMA 15)

 1.                        
  1. Sanaa ya jadi kama njia ya mawasiliano
  2. hupasha ujumbe na kuwasilisha hekima ya wakongwe kama njia bunifu na inayoburudisha.
  3. imetumika tangu kale kwa ufanisi
  4. haijapitwa na wakati.
  5. hutumika sherehe zote za kiafrika.
  6. inaweza kutumika sambamba na njia za kisasa za mawasiliano (Hoja-alama 4, mtiritiko-alama 1 = jumla
 2.                            
  1. Sanaa ya jadi ikitumika na njia za kisasa za mawasiliano ina manufaa mengi.
  2. hushirikisha watu wote bila kubagua kinyume na njia za kisasa ambazo zinachukuliwa kuwa za wale wenye nguvu ambao huzitumia kujinufaisha.
  3. Huwatenga walio wengi kwa kuwa ni ghali.
  4. Hutumia lugha ngeni na teknolojia inayokanganya.
  5. Hazitoi nafasi ya mwitiko au kuchangia maoni. 
  6. Njia ya sana aya jadi haitumii teknolojia inayokaganya.
  7. Hutumia lugha inayoeleweka na wote an ambayo si ghali. 
  8. Inapasha ujumbe anuai kwa watu wengi na muda mfupi.
  9. Huburudisha, hunasa an dkudumisha taharuki huku ikihimiza madhira kubadilika bla yeyote kuhisi amekosewa.
   (hoja - alama 8, mtiririko alama 2 - jumla 10)

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40) 

 1. Tofautisha sauti /i/ na /u/. (alama 2)
  /i/ ni irabu ya mbele /u/ ni ya nyuma
  /i/ ni ya midomo tandazwa /u/ ni ya midomo viringwa 
 2. Eleza uamilifu wa viambishi katika neon:
  wafiwao. (alama 2)
  • wa - nafsi ya tatu wingi
  • iw-kauli ya kutendewa
  • a-kiishio kauli tenda
  • 0-kirejeshi tamati
 3. Ziweke nomino zifuatazo katika ngeli zake: (alama 2)
  1. Baridi 1-1
  2. Undu U-ZI d)
 4. Eleza matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
  Wazee kwa vijana walivuka barabara kwa makini ila sita kwa kumi ndio waliofika kwa Yohana
  1. Pamoja na 
  2. Namna/jinsi
  3. Sehemu ya kitu kizima
  4. Mahali kunakomilikiwa. 
 5. Tunga sentensi moja kubainisha matumizi mawili ya kiambishi ji} (alama 2)
  • kuunda nomino - usomaji msomaji
  • kuonyesha ukubwa wa nomino-jitu, jiji
  • kuonyesha urejeshi wa mtenda
  • amejikata (zozote 2x1)
 6. Andika katika usemi wa taarifa: alamaz “Kiwango cha umaskini katika gatuzi hili kinasikitisha sana; itabidi sote wakazi wa hapa tujizatiti ili tutimize Malengo ya Milenia, "Seneta mteule alituhimiza
  Seneta mteule aliwahimiza kuwa kiwango cha umaskinikatika gatuzi hilo kilisikitisha sana, ingebidi wakazi wote wa hapo wajizatiti ili kutimiza Malengo ya Milenia.
 7. Eleza maana tatu katika sentensi:
  Baba alimwanbia mtoto kuwa angeenda shuleni. (alama 3)
  Baba ndiye angeenda shuleni.
  Mtoto ndiye angeenda shuleni.
  Mtu mwingine ndiye angeenda shuleni
 8. Ukizingatia kauli zilizo mabanoni tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi. (alama 2)
  1. pa (tendewa). Walipewa zawadi. 
  2. Hubiri (tendeka). Neno lilihubirika vyema. 
 9. Changanua sentensi hii kwa njia ya jedwali (alama 4)
  Viwanda vyote vilivyoundwa juzi vitaleta faida kubwa ajabu.
  S Changamano
   KN           KT 
  N RN   
  Viwanda vyote vilivyoundwa juzi vitaleta  E
           faida  kubwa  Ajabu
 10. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana za vitate: kura na gura. (alama 2)
  Aliligura sehemu hiyo baada ya kupiga kura.
  Mwalimu akadirie 
 11. Kanusha: (alama1)
  Mama aliingia chumbani kisha akawapikia watoto wali.
  Mama hakuingia chumbani wala kuwapikia watoto wali.
 12. Tumia kiwakilishi cha 'a-unganifu katika sentensi kuonyesha: (alama 2)
  1. Aina ya. Watapewa ya manjano. 
  2. Umilikaji. La Yohana limepotea. 
 13. Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari.
  Ni dhima/shart/faradhi/wajibu la maskauti kupandisha beramu kila Ijumaa. (alama 2)
 14. Tumia 'o' rejeshi ya mazoea katika sentensi ifuatayo:
  (alama 2) Mti ambao ulikatwa ulipelekwa uwanjani. Mti ukatwao ndio upelekwao uwanjani. 
 15. Andika katika udogo. (alama 2) Ngamia huyo atausafirisha mzigo mzito. Kigamia hicho kitakisafirisha kizigo kizito. 
 16. Ainisha sentensi hii kwa kuzingatia dhamira/jukumu. (alama1) Mezeni tembe mbili kwa maji vuguvugu kila baada ya kula. Sentensi agizi
 17. Tunga sentensi iliyo na: kirai nomino, kirai kihusishi na kirai elezi. (alama 3) wutu wote (RN) waliketi kando ya meza (RH) juzi usiku (RE). mwalimu akadirie
 18. Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi: (alama 3) Wanafunzi wataletewa zawadi bora na wazazi wao kesho kutwa.
  Shamirisho kitondo - wanafunzi
  Shamirisho kipozi - zawadi bora
  Chagizo ya wakati - kesho kutwa

4 ISIMU JAMII (ALAMA10)
a) Eleza dhima nne lugha ya taifa. (alama 4)

 1. Hutumiwa kwa mawasiliano ya kawaida kati ya wananchi wa taifa husika.
 2. Huakisi na kuendeleza utamaduni wa taifa husika. 
 3. Ni kitambulisho cha kitaifa kama ilivyo bendera.
 4. Hukuza uzalendo na fahari ya kitaifa.
 5. Hutumiwa kuendeleza shughuli na sherehe muhimu za kitaifa kama za sikukuu.
 6. Hufanikisha shughuli za utawala wa kiserikali.

b) Fafanua manufaa matatu yatokanayo na usanifishwaji wa Kiswahili.(alama 6)

 1. kusawazisha mawasiliano kwa kuondoa utata ulioletwa na lahaja mbalimbali.
 2. Kufanikisha elimu katika mataifa husika, hasa Kenya na Tanzania.
 3. Kutumiwa katika shughuli za kidini.
 4. Kutumiwa katika vyombo vya habari - redio, runinga magazeti kwa nia ya kujuza, kuelimisha na kuburudisha.
 5. Kuchochea uandishi wa vitabu vya kiada na bunilizi. 
 6. Kusaidia shughuli za utawala wa serikali katika mataifa ya Kenya na Tz.

c) Onyesha namna kaida zifuatazo zinavodhibiti mawasiliano. (alama 3) 

 1. Mada.
  Huamua misamiati. huelekeza kuhusu utaratibu wa kujieleza.
 2. Wahusika
  Huongoza kuhusu mada ya mawasiliano. Huamua taratibu za salamu. Huelekeza kuhusutaratibu za kujieleza na mikakati ya heshima. 
 3. Malezi
  Huongoza kuhusu heshima. Huongoza kuhusu uteuzi wa misamiati.

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest