Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali manne pekee. 
  2. Swali la kwanza ni la lazima. 
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: Tamthilia, Ushairi, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi. 
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. 
  5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  6. Karatasi hii ina kurasa 20 zilizopigwa chapa. 
  7. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi zilizoachwa baada ya maswali.
  8. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali  Upeo  Alama 
 1  20  
   20  
   20  
   20  
  JUMLA  


MASWALI

SEHEMU YA A: RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la Heri

1. Swali la lazima
"Uhusiano kati ya marehemu mama yangu na mavyaa yake ulikuwa umeingia ufa."

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Kwa kurejelea hoja kumi na sita kwenye riwaya hii, thibitisha kuwa mahusiano nchini Wahafidhina yameingia nyufa.  (alama 16)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo

Jibu swali la 2 au 3

2. "Ndugu zangu Wanasagamoyo, kuisherehekea miaka sitini ya safari yetu baada ya kujikomboa kutoka kwenye mikatale ya utumwa si jambo dogo." 

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 
  2. Kwa kurejelea hoja kumi na sita katika tamthilia, onyesha kinaya kinachojitokeza katika kauli (alama 16)

3. "Watu wa Sagamoyo mu wajinga sana!" 

  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya katika kuijenga tamthilia ya "Kigogo." (alama 6) 
  3. Kwa kurejelea tamthilia nzima, onyesha jinsi kauli hii inavyowaafiki Wanasagamoyo. (alama 10)

SEHEMU YA C: USHAIRI
Jibu swali la 4 au 5

4.Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Baba Watoto Fufuka

Yanilemea malezi, nateseka na watoto
Yamekuwa kwangu kazi, ngumu yenye na uzito
Nalala sipati njozi, silali kufunga mato
Fufuka baba watoto, nateseka na watoto.
Baba watoto fufuka, fufuka baba watoto
Mwenzio ninateseka, nateseka na watoto
Ni lini huno wahaka, lini utafika mwito?
Fufuka baba watoto, nateseka na watoto.
Una mateso ujane, na udhia na majuto
Zama zile tuchumbane, nili na kiwi ya mato
Kumbe twaja tutengane, nitabike na watoto
Fufuka baba watoto, nateseka na watoto.
Maisha yao nda chungu, ya chungu pia ya moto
Na mashaka na wanangu, wa bado mno watoto
Nimekosani kwa Mungu, nistahili mazito?
Fufuka baba watoto, nateseka na watoto.
Zaidi nina imani, maisha ni kama mto
Namuati manani, mwenye kupea mapato
Yeye yu mwenye hisani, yanapojiri mazito
Fufuka baba watoto, nateseka na watoto.
(Mwalaa Mranga Nyanje) 

  1. Kwa nini nafsineni anamtaka baba watoto kufufuka? (alama)
  2. Eleza umuhimu wa aina tatu za urudiaji katika shairi hili. (alama 6)
  3. Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi.  (alama 4)
  4. Fafanua mbinu saba za kimtindo ambazo zimetumiwa na mshairi katika kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe wake.(alama 7)

5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Vifusi vya Damu

Njiwa waliokuwa juu wakiruka
Na mapaani mwetu kutua
Kotekote wakafurika
Na yao mvumo kukolea
Sasa wameadimika
Wakabaki kuhadithia.

Imebaki saa mikoromo
Ya zao tingatinga
Pamoja na mingurumo
Ya ndege zao zinotanga
Zisizoisha mifumo
Ya uhai kuunyonga.

Vimebaki vifusi
Chini ya mahame haya
Wamezikwa ndugu zetu
Walioachwa kujiozea
Chini ya magofu.

Yamesalia siyo matuta ya mchanga
Tulivyozoea kucheza mwajificho
Bali vichuguu visivyo kikomo
Vilivyochanganyika na damu
Ya jamaa zangu
Ambayo ilishikanisha pamoja
Mchanga uliovijenga vichuguu vipya
Vilivyozaliwa baada ya mngurumo mkubwa kusikika
Ndani mwake mna mifupa; vyuma vya kukiimarisha
Kichuguu hiki ambacho nachelea kukikaribia.

Sasa limebaki kutanda wingu zito jeusi
Nami kompyuta yangu ya mawazo
Hamasisho ipatapo
Machozi hunitoka taratibu
Kama bomba la maji lililotoboka. -

Machozi yasiyoweza kuwarudisha tena
Wale njiwa weupe
Walioimba nyimbo bembelezi.

Machozi haya yazamapo chini machangani
Najua mchanga uliochanganyika na damu
Yanaufikia na kichuguu kukiimarisha
Hadi pale mchwa chini watakapotoka
Na chao kichuguu kukijenga
Kwa yao mate.

Ingawa bado mavumbi yatifuliwa
Kwa yao makombora
Najua siku moja itanyesha
Kubwa mvua
ya kulinyonga vumbi
Ili njiwa wapate kuiona tena njia
Ya kuwarejesha mara nyingine
Hapa Mashariki ya Kati
Ambapo mtoto huyu mchanga
Anaendelea titi kulinyonya
La mamake aliyelala usingizi usio mashaka;
Baada ya kushindwa kucheza mwajificho
Na makombora katika msokotano
Wa hivi vilima vilivyojengwa kwa mifumo.

(T. Arege)

  1. Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha. (alama 3)
  2. Bainisha mifano sita ya mishata katika shairi hili.  (alama 6)
  3. Bainisha toni ya shairi hili. (alama 2)
  4. Changanua muundo wa shairi hili. (alama 5)
  5. Kwa kurejelea mifano mitatu, jadili uhuru wa kishairi katika ubeti wa mwisho. (alama 4)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
Jibu swali la 6 au 7
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda (Wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

6.                               

  1. Tathmini matumizi ya kinaya katika hadithi ya, "Mwalimu Mstaafu." (alama 10) 
  2. Onyesha jinsi matumizi ya unga yalivyozorotesha maisha ya vijana katika taifa la Machafukoge kwa mujibu wa hadithi ya, "Mkubwa." (alama 10)
    Mohammed Khelef Ghasany: Mame Bakari
    "Mapenzi ya Kifaurongo" (Kenna Wasike)

7. "Mgomba haupandwi changaraweni ukamea. Potelea mbali mkata wee!" 

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 
  2. Bainisha sifa sita za anayeambiwa maneno haya. (alama 6) 
  3. Kwa kurejelea hoja kumi, onyesha jinsi maudhui ya elimu yalivyoshughulikiwa katika hadithi ambamo dondoo hili limetolewa. (alama 10)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

8.

  1. Onyesha mfanano uliopo kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi.  (alama 5)
  2. Bainisha vipera vitatu vya sifo. (alama 3)
  3. Fafanua umuhimu wa misimu katika jamii.  (alama 7)
  4. Jadili athari hasi za miviga katika jamii. (alama 5)



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

1. uk. 94

  1. Dondoo 
    1. Haya ni maneno ya Mwanaheri.
    2. Anamwambia Umu, Kairu, Chandachema na Zohali.
    3. Yumo katika shule ya upili ya Tangamano. 
    4. Anawasimulia kuhusu mgogoro uliokuwepo baina ya mamake Subira na mavyaa yake kwa sababu ya kutofautiana kiusuli - Subira anatoka katika jamii ya Bamwezi. 4x1 = 4
  2. Jinsi mahusiano yameingia nyufa: Mtahiniwa aonyeshe hali ya mvutano/hali ya kutoelewana/msambaratiko wa mahusiano baina ya wahusika mbalimbali. Baadhi ya hoja hizi:
    1. Wanafunzi wanamsimanga na kumdhihaki Ridhaa wakiwa shuleni kwa sababu ya tofauti za kiusuli/wanatenga Ridhaa mchezoni/wanamwita Mfuta Mvua n.k.
    2. Vikaratasi vinasambazwa kule Msitu wa Heri vikiwatahadharisha walowezi kuhusu gharika inayotarajiwa kutokea baada ya kutawazwa
      kwa kiongozi mpya. 
    3. Vijana watano wanawabaka Lime na Mwanaheri kwa kuwakisia wazazi wao kutowapigia Mwanzi kura. 
    4. Vijana watano wanamkata Subira kwa sime kwa kumkisia kumtompigia Mwanzi kura, 
    5. Mama Kaizari anamdhulumu Subira kwa sababu ya tofauti zao za kiusuli - anamwita Muki' kwa sababu ya kutoka katika jamii ya Bamwezi. 
    6. Pete anaachana na mumewe Fungo kwa sababu ya kutoyafurahia maisha na Fungo.
    7. Zohali anakosana na wazazi wake kwa kumsimanga na kumdhalilisha kwa kupachikwa mimba akiwa kidato cha pili.
    8. Walinda usalama wanawaua raia machafuko ya baada ya uchaguzi yanapotokea.
    9. Kedi anaichoma familia ya Ridhaa kwa sababu ya kuwa walowezi katika Msitu wa Heri. Kimbaumbau anampiga na kufuta kazi Naomi
      kwa kukataa kuwa mpenziwe.
    10.  Cliendachema anatoroka nyumbani kwa Satua kwa sababu ya Satua kulalamikia mambo kama vile kuisha haraka kwa sababu kwa sababu ya kuwepo kwake huko.
    11. Mama Sauna anamtoroka mumewe Kero kwa sababu ya kufutwa kazi kutokana na ulevi.
    12. Maya anambaka mwanawe wa kambo Sauna. 
    13. Maya anampiga mkewe makonde/anamtisha/anamtusi anapomuuliza swali.
    14. Wanaume wanamtisha na kumtusi Mwekevu kwa kujitosa siasani. 
    15. Wanawake wanawapiga wanaume na kuwasababishia dhiki za kisaikolojia. 
    16. Naomi anamtoroka mumewe Lunga kwa sababu ya kufilisika.
    17. Zohali hataki kumwambia mwanawe Nasibu kwamba ana babu na nyanya kwa sababu ya kumsimanga na kumdhalilisha alipohitaji msaada wao.
    18. Annette anamtoroka mumewe Kiriri kwa kuhamia ughaibuni licha ya Kiriri kumraia abaki Wahafidhina ili wasaidiane kuondoleana upweke. 
    19. Wanawe Kiriri wanakataa kurudi nyumbani licha ya kuraiwa na baba yao Kiriri kurudi ili wamsaidie kuziendesha baadhi ya biashara zake n.k. Za kwanza 16 x 1 = 16.

2. KIGOGO

  1. Dondoo - uk 4
    1. Haya ni mane Haya ni maneno ya Majoka/Yanasomwa na mtangazaji wa habari/mjumbe. 
    2. Yamerekodiwa redioni. 
    3. Sudi, Kombe na Boza wanaisikiliza habari hii kutoka kwenye redio ya rununu ya Sudi/Raia wamo kwenye karakana.
    4. Majoka anawatangazia raia kusherehekea uhuru wa Sagamoyo kwa mwezi mmoja. 4 x 1= 4
  2. Mtahiniwa aonyeshe kwamba Mwafrika bado anatawaliwa kikoloni; aonyeshe udhalimu unaoendelezwa na uongozi wa Majoka jamii ya Sagamoyo. Baadhi ya hoja ni: 
    1. Wanyonge wanalipa kodi hali soko halisafishwi. 
    2. Unyakuzi wa mali ya umma. Sudi anasema kwamba wamepokwa kilicho chao.
    3. Ubaguzi-kandarasi kutolewa kwa vikaragosi. Asiya anapewa kandarasi ya kuoka keki kwa vile Boza ni kikaragosi wa Majoka.
    4. Matumizi ya pesa za umma. Pesa kutumiwa kukichonga kinyago cha Majoka.
    5. Kupigwa - Ashua anapigwa gerezani, Tunu analema zwa.
    6. Mauaji - Jabali anauawa.
    7. Unyanyasaji wa kijinsia - Majoka kumdhalilisha mkewe mbele ya Ashua, anasema mwanamke ni mwanamke.
    8. Matumizi mabaya ya vyombo vya dola - polisi kuwatawanya waandamanaji.
    9. Wafanyakazi katika kampuni ya Majoka kutokuwa na bima.
    10. Soko kufungwa bila kuwazia hali ya maisha ya wanyonge.
    11. Uharibifu wa mazingira - majitaka kuelekezwa wanakofanyia kazi wanyonge. 
    12. Unyonyaji - kupandishwa kwa bei ya bidhaa katika kioski cha kampuni.
    13. Ukosefu wa ajira/kutobuni nafasi za kazi. Sudi na Ashua wanalazimika kufanya kazi za kujidhalilisha na hali wamehitimu shahada. 
    14. Kuwapitisha wanyonge kwenye dhiki ya kisaikolojia. Majoka anamsimanga Ashua anapokwenda kumwomba usaidizi 
    15. Majoka kuwaangamiza wanafunzi kwenye Academy yake - wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana dawa. 
    16. Ukosefu wa uwajibikaji. Majoka kutotimiza majukumu yake ya unyumba. Haonekani nyumbani kwake/kumtamani Ashua. 
    17. Majoka kumwita Ashua ili amfumanishe na mkewe 
    18. Kuwaangamiza wapinzani. Majoka kumfungia Ashua kwa kisingizio cha kuzua vurugu kwenye afisi ya umma. Anataka kumwadhibu Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago chake.
    19. Kuwanyima wanyonge haki ya kuandamana. Wanatangaza kuwa maandamano ni haramu.
    20. Mbinu hasi za utawala, hila, propaganda, hongo... 
    21. Ubaguzi - vituo vya kurekebishia tabia kuwa na seli spesheli kama vile ya mke wa Majoka na Ashua.
    22. Uongozi kutohakikishia raia huduma za kimsingi kama vile maji ilhali kwa viongozi kuna visima. 
    23. Serikali kuidhinisha uuzaji wa pombe haramu. Mamapima anasema amepewa kibali na serikali.
    24. Viongozi wanaendeleza wizi wa mali ya umma. Uongozi kugawia vikaragosi ardhi. Kenga amegawiwa kiwanja. 
    25. Viongozi kuwazamisha vijana zaidi katika matumizi mabaya ya vileo. Wanapitia kwa Mamapima kuwafanikishia ulevi; vijana wanapewa shibe yao.
    26. Badala ya wanyonge kuungana na Sudi na Tunu kupigania haki zao, wanafanikisha njama za kidhalimu za Majoka. Ngurumo anatumwa na Majoka kumpiga Tunu. Anasema kwamba hawezi kumpa mwanamke kura, heri ampe paka.
    27. Kufunga kituo cha Runinga ya Mzalendo. 
    28. Kuongeza mshahara wa walimu na wauguzi na kuwatoza kodi.
    29. Ufunguzi wa ukataji miti ilhali raia hawana maji. 
    30. Viongozi wanatishia kuwafurusha baadhi ya Wanasagamoyo kwa kusambaza vikatarasi na kuwaamba kuwa Sagamoyo si kwao - Kombe/Siti.
    31. Majoka kutaka kurithisha uongozi wake kwa Ngao Junior badala ya raia kumchagua.  

3

  1. Dondoo - uk. 88
    1. Haya ni maneno ya Majoka.
    2. Anawaambia Waandamanaji/raia.
    3. Yumo kwenye lango kuu la soko la Chapakazi.
    4. Ni baada ya waandamanaji kuususia mkutano wake na kukutana nje ya soko la Chapakazi kama njia ya kumlazimisha kuwafungulia soko. (4 x 1 =4)
  2. Umuhimu wa Majoka:
    1. Kielelezo cha viongozi wanaopambana na upinzani wa kuwaangamiza vinara wake anamuua mpinzani wake kisiasa -Jabali ili kupunguza joto la kisiasa. 
    2. Kuendeleza maudhui ya ufisadi -ananyakua ardhi ya umma - ya soko la Chapakazi na kujenga hoteli.
    3. Kiwakilishi cha viongozi wanaoharibu misitu bila kuwazia madhara yake anafungulia biashara ya ukataji miti hali inayotishia kuzuka kwa ukame. 
    4. Kielelezo cha wanaume wenye tamaa ya wanawake - ana mkewe Husda lakini anawatamani wanawake wengine kama Hashima na Ashua.
    5. Ni mfano wa viongozi wanaoendesha biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya - anafungua kampuni zaidi ya uzalishaji wa dawa za kulevya zinazoishia kuwadhuru raja.
    6. Kielelezo cha viongozi wanazipagaza nchi zao madeni kwa kukopa nchi za nje Analipagaza jimbo deni litakalolipwa kwa miaka mia moja baada ya kukopa pesa za kugharimia mchongo wa Ngao.
    7. Ni kielelezo cha viongozi wanaowadhulumu wafanyakazi - anawalipa walimu na wauguzi mshahara duni, hivyo kuwasababisha kuandamana.
    8. Ni kiwakilishi cha viongozi wanaochangia uchafuzi wa mazingira - serikali yake inamwaga taka na kemikali sokoni Chapakazi hivyo kuwasababisha wafanyabiashara kuugua. Zozote 6x1=6 
  3. Mtahiniwa adhihirishe ujinga/upumbavu wa Wanasagamoyo. Baadhi ya hoja ni:
    1. Licha ya Majoka kuwaongoza kiimla, raia kama Ngurumo wanaapa kumpigia kura.
    2. Baada ya soko kufungwa Boza, Kombe na raia wengine wanahamia Magweni kubugia pombe badala ya kuungana na raia wengine kutetea haki yao.
    3. Wanafunzi katika shule ya Majoka and Majoka Academy kutumia kunywa sumu ya nyoka na kuishia kuwa makabeji ilhali walienda shuleni kusoma.
    4. Ingawa Majoka alifunga soko la Chapakazi, kuna wachache waliohudhuria mkutano wake katika uwanja wa ikulu.
    5. Badala ya kushirikiana na raia wengine kuleta mageuzi kuna raia waliopanga kutoroka k.v Hashima.
    6. licha ya kuwa pombe aliyokuwa akiuza Mamapima alikuwa na madhara makubwa kwa Wanasagamoyo, aliendelea kuiuza.
    7. Baadhi ya Wanasagamoyo walikubali kutumiwa vibaya na Majoka kuendeleza udhalimu k.v Ngurumo aliyetumiwa na Majoka kumvamia Tunu.
    8. Tunu alipoitisha mkutano mkubwa nje ya soko, kuna raia wale k.y Ngurumo waliosusia mkutano huo na kuapa kuhudhuria dhifa ya Majoka ilhali mkutano huo ungetumika kumlazimisha Majoka kwuafungulia soko.
    9. Kituo cha Sauti ya Mashujaa hakikuangazia masaibu ya wanasagamoyo kutokana na uongozi mbaya wa Majoka badala yake kinafika katika uwanja wa sherehe kupeperusha habari za Majoka.
    10. Majoka alipuuzilia mbali maandamano ya Wanasagamoyo na kuita Tunu na Sudi vikembe, baadaye maandamano hayo yanamng'oa mamlakani.
    11. Majoka alitangaza kipindi cha mwezi mm cha kusheherekea uhuru, pasi na kujua alikuwa anaufilisi uchumi wa jimbo la Sagamoyo.
    12. Wanasagamoyo waliendelea kuteua viong kutoka kwa familia moja ya Ngao kwa kipindi kirefu hali iliyochangia uongozi hu kuwadhulumu kwa muda mrefu.
    13. Majoka aliharibu kiwango cha elimu katik Majoka na Majoka Academy kwa kuwaruhusu wanafunzi kutumia dawa za kulevya na kuishia kuanguka mtihani. Zozote 10 x 1=1

4. Ushairi

  1. Nafsineni anamtaka baba kufufuka kwa sababu zifuatazo: 
    1. Amelemewa na malezi ya watoto. 
    2. Halali uzingizi vizuri/analala akiwa amefungua macho. 
    3. Yeye pamoja na watoto wanateseka. 
    4. Mateso ya ujane. Zozote 3x1= 3
  2. Umuhimu wa aina tatu za urudiaj
    1. Urudiaji wa silabi - to, zi, ka, ne, ngu, ni Umuhimu - kujenga ridhimu ya shairi/kuleta urari wa vina 
    2. Urudiaji wa neno - watoto, baba - Umuhimu - kusisitiza ujumbe
    3. Urudiaji wa mshororo - Fufuka baba watoto, nateseka na watoto Umuhimu: Kusisitiza ujumbe Kutaja - ; mfano - ; umuhimu - alama 1 
  3. Lugha tutumbi Licha ya hayo ninaamini kuwa maisha ni sawa na mto/Ninamwachia Mungu anayewapa watu riziki (kipato/Yeye (Mungu) hutoa msaada jambo gumu linapotokea/Ninakuomba ufufuke mume wangu kwa maana malezi ya watoto yamenilemea. Zote 4x1-4 
  4. Mbinu za kimtindo 
    1. Ritifaa - Nafsineni kunena na marehemu. 
    2. Tasbihi - maisha ni kama mto 
    3. Chuku
    4. Lahaja - mato/huno/namuatia
    5. Swali la balagha. Ni lini huno wahaka, lini utafika mwito?/Nimekosani kwa Mungu, nistahili mazito?
    6. Kuboronga sarufi - una mateso ujane - ujane una mateso 
    7. Taswira - picha ya mtu aliyelala bila kufunga macho.
    8. Urudiaji-chungu, baba, watoto 
    9. Inkisari - nitabike - nitaabike Za kwanza 7x1=7

5. Ushairi

  1. Aina ya shairi
    Shairi huru
    Ithibati
    • Idadi ya mishororo inatofautina katika kila ubeti
    • Idadi ya mizani inatofautiana katika kila mshororo
    • Kila mshororo una kina tofauti na mwingine n.k.
      Kutaja - alama 1; kufafanua - alama 1
  2. Mishata 
    1. Imebaki sasa mikoromo
    2. Pamoja na mingurumo
    3. Walioachwa kujiozea
    4. Vilivyochanganyika na damu 
    5. Machozi yasiyoweza kwarudisha tena 
    6. Na chao kichuguu kukijenga
    7. Ingawa bado mavumbi yatifuliwa 
    8. Najua siku moja itanyesha 
    9. Ili njiwa wapate kuiona tena njia 
    10. Na makombora katika msokotano
    11. Anaendelea titi kulinyonya Zozote 6 x1=6
  3. Toni
    Toni ya huzuni - nafsineni inahuzunika kwa kuzikwa kwa ndugu zao.
    Toni ya uchungu - nafsineni kutokwa machozi. Toni ya matumaini - Nafsineni ina matumaini kuwa ipo siku mvua kubwa itanyesha ili kulinyonga vumbi, hivyo kumsaidia njia kuiona njia tena. Yoyote 1 x 2=2 
  4. Muundo
    1. Lina beti inane.
    2. Idadi ya mishororo inatofautiana katika kila ubeti. Vina vinabadilika kutoka mshororo mmoja hadi mwingine.
    3. Kiishio kinatofautiana katika kila ubeti. (v). Idadi ya mizani inatofautiana kutoka mshororo mmoja hadi mwingine.
    4. Kila mshororo una kipande kimoja isipokuwa ubeti wan ne, mshororo wa tisa wenye vipande viwili. Zozote 5x1-5
  5. Uhuru wa mshairi
    Kuboronga sarufi
    • kwa yao makombora
    • kubwa mvua
    • anaendelea titi kulinyonya
      Kutaja - alama 1; mifano mitatu - alama 3

6.

  1. Kinaya kat ka "Mwalimu Mstaafu" 
    1. Ni kinaya watu kudhani kuwa kuota mvi kwa Mwalimu Mosi akiwa na miaka thelathini ni ishara ya hekima.
    2. Mwalimu Mosi anataka mwanafunzi wake wa zamani au wa sasa wapewe nafasi ili kumkashifu badala ya kumsifu.
    3. Ni kinaya Jairo kudai kuwa iwapo angeachiliwa kutoka shuleni mapema ili aende kuiba na kuna angekuwa mtu wa maana.
    4. Ni kinaya kuwa Jairo akilewa hujikwaa na kudungwa miiba ila hahisi kitu.
    5. Jairo anadai kuwa maisha ni matamu bila nasaha za mwalimu ilhali wanafunzi wengine walikuwa wamenufaika kutokana na nasaha hizo anazokataa.
    6. Ni kinaya Jairo kudai kwamba alikuwa amefurahi kutokana na kustaafu wa Mwalimu Mosi kwa maana hakuna mtoto mwengine wa mtu ambaye angekatishiwa tamaa na Mwalimu Mosi ilhali wanafunzi wengine walikuwa wamehutubu na kumsifu kwa kuwasababisha kufaulu maishani.
    7. Jairo anapendekeza kuwa wanafunzi wanaoshindwa na masomo wajiendee zzo kuzumbua riziki kwa kutapeli, kuiba, kupora na kuua ilhali haya ni maovu yasiyokubalika katika jamii.
    8. Mwalimu Mosi anawataka watu wampigie makofi Jairo baada ya kumkashifu katika hotuba yake.
    9. Jairo anamkejeli Mwalimu Mosi mbele ya umati uliohudhuria sherehe za kumuaga lakini anapomaliza kuhutubu anamkaribisha katika jukwaa la wageni mashuhuri. Jairo anapewa zawadi na Mwalimu Mosi lakini anamfuata kwake akiteta kuwa kufanya hivyo ni kumuaibisha.
    10. Mwalimu Mosi anatuzwa zawadi kadhaa lakini hachukui hata moja; anampa Jairo zote ilhali sherehe ilikuwa yake.
    11. Ni kinaya Mwalimu Mosi kudai kuwa alimpa Jairo zawadi kwa maana aliipenda hotuba yake ilhali Jairo alimuaibisha katika hotuba hiyo kwa kumlaumu kwa masaibu ya maisha yake,
    12. Ni kinaya Jairo kumpelekea Mwalimu Mosi mke wake na watoto kuwa mali yake kwa sababu ya zawadi alizompa.
    13. Jairo alipomwachia Mwalimu Mosi familia yake aliapa kuwa hangekanyaga kwa Mwalimu huyo lakini alirudi kwake baada ya kusikia habari za Mwalimu Mosi kuishi na bintiye, Sabina mjini.
    14. Sera anamruhusu Mwalimu Mosi ambaye ni mumewe kumchukua mkewe Jairo kuwa mkewe ilhali yeye ndiye mkewe halisi. 10x1=10
  2. Madhara ya unga
    1. Uzembe - Vijana mateja wanasinzia/wanalala mchana badala ya kufanya kazi ili kuimarisha uchumi wa taifa. 
    2. Wizi - Vijana mateja huwaibia watu mali zao. Tunaambiwa kwamba ukisinzia watakuibia.
    3. Kuzorota kwa afya ya vijana - Mihadarati huwasababisha vijana kukosa nguvu za kimwili/Miili yao imejaa matundu kwa sababu ya kujitoga/ wamekonda na kukondeana. 
    4. Fujo - Vijana mateja huzua fujo na kupigana wakitumia kisu na bisibisi.
    5. Kufungwa - Vijana mateja wanafungwa hivyo kulihini taifa ikama inayohitajika katika kuimarisha uchumi wa taifa. 
    6. Hongo - Mkubwa anatoa hongo kwa Ng'weng'we ili Mkumbukwa afunguliwe baada ya kupatikana na dawa za kulevya. 
    7. Kifo - Dawa za kulevya zimewaua vijana mateja.
    8. Sober house - Pesa zinazohitajika kuleta maendeleo zinatumika katika kufungua vituo vya kurekebishia tabia. 
    9. Magonjwa - Dawa za kulevya ziliwasababishia vijana mateja magonjwa kama vile kifua kikuu na Ukimwi kutokana na kujitoga mwilini.
    10. Kuzorotesha kwa maadili - Vijana mateja wanamwita Mkubwa makande na mavi ya bata. 
    11. Vitisho - Mkubwa anapowaangalia vijana wanaotumia dawa za kulevya, mmoja wao anamtisha kuwa angemtoa chango. 
    12. Kudhurika kwa akili za vijana - Kijana mmoja mla unga anamlaumu Mkubwa kwa kumkatishiastimu anapomgusa akiendelea kutumia unga. Anasema alikuwa anakata beda kuelekea kwa baba Obama kabla amtibulie starehe zake na kumlaumu kwa kumvunjia safari yake aliyokuwa karibu kufika 10 x 1 = 10

7. Mapenzi ya Kifaurongo

  1. Dondoo
    1. Haya ni maneno ya Penina. 
    2. Anamwambia Dennis 
    3. Yumo katika mtaa wa New Zealand
    4. Ni baada ya Dennis kutafuta kazi bila mafanikio na Penina kuamua kumfukuza. 4x1=4
  2. Sifa za Dennis 
    1. Mwenye shukrani. Anawashukuru waza wake kwa kujitaabisha kwa ajili yake - apate masomo ya chuo kikuu. 
    2. Mwenye tamaa. Anayamezea mate mag ya kifahari yaliyokuwa yakipita barabara na kusema kuwa angekuja kumiliki mc endapo angefanikiwa maishani.
    3. Mwenye matumaini. Ana matumaini kuv siku moja angefanikiwa angemili mojawapo ya magari aliyokuwa ameyaon yakipita barabarani. Pia, licha y wachapishaji kufumbia macho wasan wanaoinukia, Dennis hakuwa amekat tamaa katika uandishi wake kwa maan: anaamini kuwa siku moja atatajwa kama mwandishi bora. 
    4. Mvumilivu. Anavumilia dhiki anazopitia chuoni kama vile uchechefu wa pesa hadi anamaliza masomo yake na kufuzu.
    5. Mwenye bidii. Licha ya uchechefu wa pesa, amejikaza kisabuni na kukamilisha masomo yake. (Uk. 21)
    6. Mkweli. Penina anapomuuliza sababu ya kunywa uji anamjibu kuwa pesa zake zilikuwa zimekwisha na hakuwa na kwingine pa kuazima. 
    7. Mnyamavu. Penina anasema kuwa huwa anamwona Dennis akiwa mnyamavu darasani,
    8. Mwepesi wa kushawishika. Licha ya kukataa uchumba wa Penina katika hatua za mwanzo mwanzo hatimaye anakubali na kuwa mchumba wake baada ya Penina
      kuendelea kumshawishi
    9. Mwenye mapenzi ya dhati. Alimpenda Penina hadi anapomfukuza kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi anaendelea kumwita mpenzi.
    10. Mwerevu. Tunaambiwa kwamba ilikuwa vigumu kwa shule za vijijini kumwibua  bingwa katika mitihani ya kitaifa lakini yeye anasoma katika shule hizo za vijijini na kufaulu. 
    11. Mtiifu. Yeye anatumia stovu katika mapishi yake k.v. uji kwa sababu chuo kimepiga marufuku matumizi ya umeme katika kupika. Isitoshe, Penina anapomuagiza kufunganya virago vyake na kuondoka alifanya hivyo bila kubishana naye. 
    12. Mchoyo. Penina anapomtembelea katika chumba chake anamkuta amepika uji lakini anakunywa peke yake bila kumpa. 
    13. Mwoga. Alipoenda kutafuta kazi aliulizwa kueleza sababu ya kutafuta kazi katika shirika hilo lakini akashindwa kulijibu swali hilo kwa sababu ya woga. Tunaelezwa kuwa alihangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi. Isitoshe, alianza kutiririkwa jasho kwapani. Za kwanza 6x1=6
  3. Maudhui ya elimu
    1. Masomo yamewalemea wanafunzi. Kwa mfano, Dennis Machora yumo darasani ila haelewi anachofunzwa na mhadhiri Dkt. Mabonga. Isitoshe, wengine wanadai kuwa masomo ya chuo kikuu ni madubwasha yasiyojulikana yalikotoka hadi wengine wanataka kuacha kusoma.
    2. Wanafunzi wanaosoma katika shule za mikoa au za kitaifa huibuka mabingwa katika mitihani wanapolinganishwa na wale wanaosomea katika shule za vijijini.
    3. Elimu ni ghali. Dennis amesoma kwa taabu kutokana na umaskini. Iliwabidi wazazi wake kufanya kibarua cha kuwalimia matajiri mashamba ili wapate karo ya kumlipia shuleni.
    4. Elimu husababisha kiburi. Kutokana na kusoma sana kwa Dkt. Mabonga, yeye hakujua kuwa kuna wengine wasiojua be wala te.
    5. Hali ya mhadhiri Mabonga kuwadhalilisha wanafunzi wake imeonyeshwa kuwa kichocheo cha baadhi ya wanafunzi kutaka kuacha masomo. Kuna mwanafunzi anayetaka kuacha masomo ili kuepuka kutukanwa ovyo na Dkt. Mabonga. (uk.15) 
    6. Elimu humsaidia binadamu kuwa mwandishi E vitabu. Dennis anasema kuwa angetaka kusoma ili awe miongoni mwa waandisha farisi wanaoutawala ulimwengu wa fasihi. Aidha, Dennis ana madaftari ambayo ameandika hadithi akisubiri zichapishwe.
    7. Utajiri wa wazazi umesawiriwa kuwa chanzo cha baadhi ya wanafunzi kutaka kuacha masomo. Kwa mfano, kuna mwanafunzi anayetaka kuacha kusoma ili awe manamba kwa maana baba yake ana matatu na mabasi ya abiria chungu nzima.
    8. Wanafunzi wanaendeleza utabaka/utengano. Pana utengano mkubwa baina ya wanafunzi maskini na matajiri. Wenye uwezo wa kifedha hawatangamani na maskini 
    9. Elimu pia imesawiriwa kama njia ya kujipatia ajira. Baada ya kufuzu masomo ya chuo kikuu cha Kivukoni, Dennis anaandika tawasifu na kuzituma kwingi akiomba ajira.
    10. Elimu hufunza maadili kama vile kujitegemea. Mhadhiri Mabonga anawahimiza wanafunzi kujitegemea na kusuta ubwete.
    11. Ugumu wa masomo ni kisingizio cha wanafunzi kuacha kusoma. Kwa mfano, kuna mwanafunzi mmoja anayetaka kuacha kusoma ili awe manamba katika magari ya baba yake kwa sababu ya kutoelewa kinachofunzwa chuoni. 
    12. Baadhi ya wanafunzi huyaona masomo kama adha/ usumbufu. Tunaambiwa kuwa kuna mwanafunzi msichana aliyetaka kuolewa ili aondokane na adha ya masomo 
    13. Elimu ina jukumu la kumpa binadamu uhuru wa kujipangia mustakabali wake. Dennis anataka asome ili awe daktari au profesa.
    14. Elimu ni ya jinsia zote. Dennis na Penina ni wanafunzi katika chuo kikuu cha Kivukoni. 
    15. Wanafunzi wamekosa umakinifu masomoni. Dennis Machora yumo darasani ila fikra zake zimo katika magari yanayopita barabarani badala ya kusikiliza Dkt. Mabonga. Zozote 10x1=10

8. FASIHI SIMULIZI

  1. Mfanano 
    1. Zote hutumia lugha kupitisha ujumbe kwa wanajamii. 
    2. Zote humlenga binadamu.
    3. Zote hutumia wahusika kuwasilisha ujumbe - wahusika hawa ni kama binadamu, wanyama,
    4. mazimwi, mizuka n,k.
    5. Zote zina majukumu yanayofanana kama vile kuelimisha, kuadilisha, kuburudisha, kuonya n.k. 
    6. Zote zinatumia lugha ya kitamathali kuwasilisha ujumbe. Tamathali hizi ni kama methali, majazi, misemo, taswira n.k. 
    7. Zote huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakati. 
    8. Zote zina utendaji. Zote zinaweza kuigizwa jukwaani. 5xl-5 
  2. Vipera vya sifo
    1. Majigambo 
    2. Tondozi 
    3. Pembezi 3X1=3 
  3. Umuhimu wa misimu katika jamii.
    1. Kuongezea lugha msamiati - misimu inapoimarika kimatumizi na kukubalika kama lugha sanifu.
    2. Kupamba lugha/kuiyafanya mazungumzo kuwa na mvuto. 
    3. kurahisisha mawasiliano baina ya watumiaji. Kwa mfano, kuchemka kwa maana ya kulewa kupindukia.
    4. Kitambulisho cha kikundi fulani cha watu kama vile vijana. 
    5. Kuhifadhi historia ya jamii. Misimu huweza kubuniwa kufuatia matukio muhimu ya kijamii. 
    6. Kuhifadhi siri za kundi fulani. 
    7. Kukuza umoja wa wanaoitumia. 
    8. Huondoa urasmi katika mazungumzo hivyo kuwapa wanajamii uhuru wa kuzungumza bila kuogopa kwamba wanakiuka kanuni za kisarufi. 
    9. Kutasfidi lugha - kwa mfano, boli kwa maana ya mimba. 
    10. Kuburudisha - baadhi ya misimu huburudisha inapotumiwa.
    11. Hukuza uwezo wa kufikiri ili kuelewa maana ya misimu.
    12. Hukuza uhusiano bora miongoni mwa wanaoitumia.
  4. Athari hasi za miviga
    1. Miviga ya kuwatahiri wasichana huwasababisha kuvuja damu na kuaga dunia.
    2. Huwasababishia wanajamii wasiwasi/hofu, kwa mfano, sherehe za matambiko ya kufukuza pepo. 
    3. Mingine huwafukarisha wanajamii kwa maana inagharimu pesa nyingi kama vile sherehe za kumkumbuka marehemu.
    4. Huwarithisha vijana tabia hasi ya wizi. mfano, katika baadhi ya jamii baada ya sherehe za jandoni, wavulana huhitajika kuiba mifugo kutoka jamii jirani ili kuonyesha ujasiri wao, hivyo kuleta uadi baina ya jamii hizo.
    5. Ni chombo cha ukiukaji wa haki za wanyama kwa mfano, katika baadhi ya jamii, baada ya sherehe za jandoni, wavu. huhitajika kuingia porini na kuwawinda wanyama kama vile simba, ndovu, chuin ili kuthibitisha ujasiri wao.
    6. Sherehe za kumsifu mtu fulani aliyeleti ufanisi katika jamii huenda zikasababisi wivu kutoka kwa wale wasiompenda.
    7. Ni chanzo cha vijana kupuuza masomo na kutamani kuolewa/ kuoa kwa sababu katil jamii nyingine, sherehe hizi ni kibali cha kuoa au kuolewa. 5x1=5
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Sukellemo Joint Mock Examinations July 2020.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest