Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2020

Share via Whatsapp

 

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:

  1. Andika jina lako, nambari ya mtihani na tarehe katika karatasi ya majibu.
  2. Karatasi hii ina maswali manne.
  3. Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
  4. Swali la kwanza ni la lazima.
  5. Chagua swali jingine lolote kutoka kwa matatu yaliyosalia.
  6. Majibu yote yaandikwe katika karatasi ya majibu uliyopewa.
  7. Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.

 

  1. Wewe ni mwanahabari wa runinga tajika nchini. Matatizo ya kilimo katika
    Nchi yako yameshamiri kwa kiwango cha juu mno. Andika mahojiano baina
    Yako na afisa wakilimo nchini, mkiangazia njia mwafaka za kutahia
    Vizingiti hivyo.
  2. Vijana ndio viongozi wa kesho kama wakinasihiwa kwa njia mwafaka; kwa muda wa miaka kumi vijana wamekumbwa na matatizo chungu nzima. Onyesha matatizo haya na jinsi yananvyoweza kutatuliwa.
  3. Thibitisha ukweli wa methali‘ Mchumia juani hulia kivulini.’ Kwa kusimulia kisa cha kusisimua.
  4. Tunga kisa cha kusisimua na kimalizike kwa … nahapo ndipo nilipong’amua kuwa maisha yangu yalikuwa hatarini.



MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

  1.    
    1. Ni sharti insha hii iwe na kichwa.
    2. Utangulizi ni sharti uwepo.
    3. Mahokiano huwa na hitimisho.

      Hoja za kuangaziwa. (matatizo)
      1. Wakulima kununua mbegu duni.
      2. Uchechefu wa fedha za kuendelea kilimo.
      3. Ukosefu wa elimu tosha ili kuendeleza kilimo cha kisasa.
      4. kupata mbegu na mbolea kwa wakati usiofaa. (kama zimechelewa)
      5. Magonjwa ya mifugo na mimea.
      6. Kiangazi.
      7. Njia mbovu za kusafirishia mazao ya wakulima.
      8. Ukosefu wa wawekezaji nchini.
      9. Ukosefu wa soko mwafaka.
      10. Wezi wa mifugo.

        Suluhu.
        1. Serikali kuhakikisha mbegu na mbolea ni za kiwango cha juu.
        2. Serikali kuwapa wakulima mikopo.
        3. Maafisa waelekezi kutolewa na serikali za gatuzi tofauti.
        4. Maafisa wa kuwatibu mifugo kuajiriwa na serikali za gatuzi tofauti.
        5. Serikali kuona kwamba wakulima wamepata maji kwa wingi.
        6. Serikali kurekebisha barabara ili magari ya kusafirisa mazao kufika vijijini.
        7. Serikali kuwapa wakulima ulinzi na kurai wawekezaji.

          Matatizo.
          1. Ukosefu wa kazi.
          2. Matumizi ya dawa za kulevya.
          3. Uigaji wa hulka za kigoni mitandaoni.
          4. Kuna utepetevu miongoni mwa washika dau kazini.
          5. Ukosefu wa vielelezo wema.
          6. Malezi mabaya
          7. Shinikizo la rika
          8. Kuzorota kwa maadili.
          9. Ubaguni kazini. (uhaba wa tajriba)

            Suluhu
            1. Ni sharti serikali ibuni nafasi za kazi.
            2. Sheria kali kuwekwa.
            3. Vijana kupewa mawaidha mara kwa mara, na kuelimishwa.
            4. Washika dau kukumbushwa majukumu yao, ili wawe vielelezo wema.
            5. Kutokana na malezi mabaya vijana waelimishwe upya.
            6. Vijana wapewe nafasi kazini waache kuanguliwa kwa sababu ya uhaba wa tajriba.
            7. Matatizo katika nambari 8 na 9 vijana wanahitaji kufunzwa upya.
  2. Maana ya methali ni sharti iwekwe bayana.
    Ni lazima mtahiniwa aangazie pandi mbili za methali
    Kuchumia juani, changamoto alizozipata alipokuwa akifanya kazi.
    Kulia juani; ufanisi uangaziwe kwa kina.
    Methali ione na kisa kitachosimuliwa.
  3. Ni sharti kisa kione na kipengele mtahiniwa apewa.
    Kisa kiwe cha kusisimua msomaji.
    Kisa chenyewe kitamatike kwa kipengele kilichotolewa.
    Mtahiniwa asipokitumia kipengele hicho atuzwe.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2020.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest