Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Andika jina lako na Nambari yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Weka sahihi yako kisha tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
  3. Jibu maswali yote.
  4. Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Swali

Upeo

Alama

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 

QUESTIONS

  1. UFAHAMU: (Alama 15)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    KUKITHIRI kwa visa vya utoaji wa hongo kwa wapiga kura walioshiriki chaguzi ndogo zilizofanyika Jumatatu katika eneobunge la Malindi na Kaunti ya Kericho ni ithibati tosha kuwa ufisadi ume-kita mizizi nchini.Kadhalika,visa hivyo vilidhihirisha kuwa demokrasia imedidimia na taasisi za kupambana na visa vya ufisadi zimefifia.mwezi uliopita, Wakenya kupitia mitandao ya kijamii walishtumu Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutokana na kile walichotaja kuwa
    matumizi ya mabavu’ kuhifadhi kiti chake baada ya kuwatishia wapinzani wake.

    Watumiaji wa mitandao ya kijamii pia walimkosoa Rais Uhuru Kenyatta kumpongeza wenzake wa Uganda huku wakisema aliunga mkono ukandamizaji wa demokrasia,Lakini, visa vya uhongaji wa wapiga kura vilivyoshuhudiwa katika maeneo ya Malindi na Kericho vikitekelezwa na viongozi wa kisiasa hata Wengine wakiwa wa muungano tawala wa Jubilee, ni dhihirisho tosha kuwa Wakenya hawakuwa na sababu ya kushutumu Rais Museveni.

    Utumiaji wa mabavu au kununua wapiga kura ili kushinda uchaguzi ni hujuma kwa demokrasia. Baadhi ya wanasiasa pia wameripotiwa wa kuwa Wanatumia fedha zao kusafirisha watu kutoka eneo moja hadi jingine ili wajiandikishe kuwa wapiga kura na wawachague katika uchaguzi ujao. Huu pia ni ukiukaji wa misingi ya demokrasia.

    Ununuaji wa wapiga kura unamanisha mabwanyenye ambao wamehusishwa na sakata mbalimbali za ufisadi ndio nyadhifa mbalimbali za uongozi kwa kuwa wao ndio wana mabunda ya fedha za kuhonga wapiga kura.Viongozi wanaochaguliwa baada ya kuwahonga wapiga kura huwatafanya maendeleo yoyote na badala yake, watakuwa wakihusika na wizi wa rasilimali za umma ili kupata fedha za kuwahonga watu katika uchaguzi unaofuatia. Mabwanyenye hawa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wapiga kura wanaendelea kuzama katika lindi la maskini ili waweze kununuliwa kwa urahisi. Sawa na Esau katika Bibilia tuliyeelezwa kwamba aliuza urithi wake wa kuzaliwa kwa Yakobo kwa kubadilishana na chakula,maskini pia wako tayari kuuza haki yao ya kuchagua kiongozi bora kwa Shilingi mia moja.

    Viongozi wanaotoa hongo kwa wapiga kura kwa lengo la kushinda uchaguzi ni ishara kwamba hawana maono wala sera za maendeleo. Badala yake wanang’ang’ania mamlaka ili kujilimbikizia utajiri wala si kusaidia mpiga kura kujiinua kimaisha.
    (Taifa leo. Machi 10,2016)

    MASWALI

    1. Kwa kurejelea kifungu,visa vya kutoa rushwa kwa wapiga kura vinadhihirisha nini? (Alama 3)
    2. Bainisha jinsi nne ambazo viongozi wa kisiasa wanatumia kuendeleza ukiukaji wa misingi ya demokrasia. (Alama 4)
    3. Fafanua athari za uozo unaorejelewa katika taarifa kwa
      1. Viongozi. (alama 2)
      2. Raia (Alamama 2)
    4. Thibitisha kuwa nyani haoni ngokoye katika muktadha wa Makala haya. (Alama.2).
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa (Alama 2)
      1. Mitandao ya kijami
      2. Mabwanyeye
  2. UFUPISHO (ALAMA 15)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Tunapinga na kulaani vikali visa vya ugaidi vinavyoendelea kutetemesha usalama wa wananchi. Hivi ni vitendo vya kinyama vinavyotekelezwa na watu waliokosa ubinadamu na utu kabisa . Inakera mno kwa vitendo vya kigaidi. Inagadhabisha kuona Wakenya wasio na makosa wakiteswa na kuuwawa kinyama bila huruma na watu wasio na utu. Hatuogopi wala hatuna fedheha kwamba magaidi hawa wameelaaniwa na siku zao zimehesabiwa hapa duniani, damu ya mwananchi asiye na makosa katu watailipia. Napinga vikali pale magaidi hawa wanapohusisha vitendo hivi kuwa vita vya kidini, vita hivi si vya kidini kwani hakuna dini yoyote iliyo na Imani ya kumwua kinyama binadamu asiye na makosa.

    Kando na tishio la ugaidi, Wakenya pia wanakabiliwa na hatari za ujambazi,manaji,unajisi,ubakaji na maovu mengine. Katika juhudi za kudumisha usalama, polisi wana jukumu la kutumia kila mbinu kuhakikisha kuwa haki ya kikatiba ya Wakenya kuhusu kulindwa kwa maisha na mali yao. Lakini cha kusikitisha ni kuwa,mbinu ambazo polisi wamekuwa wakitumia hasa ile ya kufanya misako inayoishia kuwanasa mamia ya raia wasio na habari kuhusu kinachoendelea,inawaongezea Wakenya mateso. Hali hii inawaacha kwennye hatari ya kunaswa na majambazi ama polisi.

    Matumizi ya mbinu hii ya misako imeishia kunasa raia wengi wasio na makosa. Wanaponaswa,hurundikwa kwenye seli usiku mzima ama siku kadhaa na hata kama wanaachiliwa huwa tayari wameteseka. Huu ni ukiukaji wa haki za raia. Kadhalika,mbinu hii yanaonekana kama hila ya polisi kutaka kuonyesha wanafanya kazi lakini sio mwafaka kwani wanapokuwa wakiwanasa raia mijini na mitaani,magaidi na majambazi wanaendelea na shughuli zao.

    Badala ya kusaka wakora kwa kubahatisha kwenye umati,polisi wanapaswa kubuni njia ambazo zitawapa mwelekeo mwafaka Zaidi kuhusu wahalifu ili waweze kuwafuatilia. Ushirikiano baina yao na majasusi uwepo. Hii itawezesha polisi kupata habari muhimu kuhusu vitisho vya uhalifu. Maafisa wa usalama pia wanaweza kupata habari muhimu kutoka kwa raia.

    Maswali

    1. Ni nini maoni wa mwandishi kuhusu suala la ugaidi. (alama 7 1 utiririko) maneno 60-70)
      Nakala chafu

      Nakala safi
    2. Kwa kutumia maneno yasiyozidi 50 fupisha aya mbili za mwisho. ( Alama 6, 1 utiririko)
      Nakala safi

      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. Andika sifa zozote mbili za sauti zifuatazo. (alama 2)
      1. /u/
      2. /ch/
    2. Tenga silabi katika maneno yafuatayo kisha uandike muundo wake. (Alama 2)
      1. igwa
      2. Oa
    3. Andika upya sentensi kwa kutumia ‘O’ rejeshi tamati. (alama 2)
      Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia
    4. Unda nomino kutokana na kivumishi kifuatacho; (Alama 1)
      Tepetevu
    5. Badilisha katika usemi halisi (alama 3)
      Afisa wa usalama alisema kuwa wangemsaidia ikiwa angeshirikiana nao
    6. Pambanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha Vishale. (Alama 4)
      Letu lililopaliliwa limetuletea mazao mengi.
    7. Ainisha virai vyovyote vitatu (Alama 3)
      Mwanafunzi yule mtoro hupenda kutembea katikati ya barabara kila wakati.
    8. Tunga sentensi moja kutofautisha vitate vifuatavyo: (Alama 2)
    9.              
      1.  Chaka
      2. Shaka
    10. Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao,hali timilifu (alama.2)
      Mwanafunzi aliandika insha nzuri
    11. Andika sentensi hii katika udogo wingi. (alama.2)
      Mtoto amefunga mlango wa nyumba yao
    12. Onyesha matumizi matatu ya alama ya vifungo katika sentensi. (alama.3)
    13. Eleza maana ya kishazi. (Alama 2)
    14. Nyambua vitenzi vifuatavyo kama ulivyoelekezwa (Alama 2)
      1. Suka (kauli ya kutendata)
      2. Pa (kauli ya kutendeka)
    15. Onyesha yambwa na chagizo katika sentensi ifuatayo.
      Babu alijengewa nyumba kwa mawe na Juma. (Alama 2)
    16. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa
      Mzazi alishangilia matokeo ya mwana. (alama 2)
      (Anza Mwana)
    17. Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
      Mama aliniletea Kanga. (alama.2)
    18. Yakinisha.
      Usiponiita sitaandamana nawe (alama.2)
    19. Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo.
      Mgeni alikuwa amewasili jana. (alama 1)

ISIMU JAMII (Alama 10)

  1. Wewe ni mfanyabiashara katika soko la Chapakazi,eleza sifa tano za lugha utakayotumia kuwasiliana na wateja pamoja na washiriki wengine siku ya soko. (Alama 10)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    1.                  
      1. Ufisadi umekita mizizi nchini√
        Demokrasia imedidimia√/ukandamizaji√ wa demokrasia/hujuma√ kwa demokrasia
        Za kwanza 3x1=3
      2.  
      3. Taasisi za kupambana na visa vya ufisadi zimefifia.√
    2.                    
      1. kutoa hongo kwa wapiga kura/kununua wapigakurua
      2. Matumizi ya mabavu
      3. kuwatishia wapinzani
      4. Kuunga mkono ukandamizaji wa demokrasia
      5. Kusafirisha watu kutoka eneo moja hadi jingine ili wajiandikishe kuwa wapiga kura na wawachague katika uchaguzi
        Za kwanza 4x1=4
    3.              
      1. Viongozi
        - Kushinda uchaguzi/mabwanyenye fisadi wataendelea kushikilia nyadhifa za uongozi
        - Ukosefu wa maono na sera za maendeleo/ukosefu wa maendeleo
        - Kujiinua kimaisha/kujilimbikiza mali (utajiri/wizi wa rasilimali za umma? Zozote 2x1=2
      2. Raia/wapiga kura
        Kuendelea kuzama katika lindi la umaskini
        Kuuza haki yao ya kuchagua viongozi bora 2x1=2
    4. Wakenya walimshutumu Rais Museveni kwa kung’ang’ania mamlaka ilhali visa vya uhongaji wa wapiga kura vilishuhudiwa Malindi na K==ericho vikitekelezwa na viongozi wa kisiasa baadhi wakiwa katika muungano tawala. 2x1=2
    5.                  
      1. Mitandao ya kijamii
        Mifano ya mawasiliano inayounganisha ulimwengu kwa matumizi ya rununu au tarakilishi. 1x1=1
      2. Mabwanyenye
        Matajiri/walonavyo/walalaheri,makabaila,mamwinyi watu wenye mali nyingi. 1x1=1
  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Maswali
    1. Ni nini maoni wa mwandishi kuhusu suala la ugaidi. (alama 7,1 utiririko)
      • ugaidi ni kitendo cha kinyama kinachotekelezwa na watu waliokosa ubinadamu
      • Ugaidi hauna uhusiano na dini yoyote.
      • Polisi wanazembea katika kuzuia matendo ya kigaidi.
      • Polisi wabuni njia mbadala ya kukabiliana na ugaidi badala ya kunasa raia wasio na hatia.
      • Wakenya wasio na makosa huteswa na kuuawa kinyama.
      • Agaidi watalipia matendo yao.
      • Wakenya wana haki ya kulindwa kikatiba.
    2. kwa kutumia maneno yasiyozidi 50 fupisha aya mbili za mwisho. (alama 6, 1 utiririko)
      • Raia wasio na hatia hunaswa
      • Hurundikwa kwenye seli na kuachiliwa huru kama wameteseka.
      • Huu ni ukiukaji wa haki za binadamu.
      • Hii ni hila ya polisi kujionyesa kuwa wanafanya kazi.
      • Magaidi huendeleza shughuli zao.
      • Polisi wanapaswa kubuni njia zitakazowapa mwelekeo mwafaka kuhusu wahalifu.
      • Ushirikiano baina yao na majasusi uwepo.
      • Maafisa wa usalama kupata habari muhimu kutoka kwa raia.
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.                  
      • /u/sauti ya nyuma ½
      • ulimi huwa juu ½
      • midomo huviringwa
      • /ch/ ni kipasuo kwamizo ½
      • ni ya kaakaa gumu ½
      • ni hafifu/sighuna
        Alama 2
    2.                  
      1.  i=gwa ½ I – Kki ½ →IKkI
      2. O-a ½ i- ½ → II
    3. Gari liangukalo si lile ilizungumzialo
      (alama 2
    4. Utepetevu alama 2 kutepetea (kiternzi –jina)
    5. “Tutakusaidia ikiwa utadhirikiana nasi,”
      afis wa usalama akasema.
      6x1/2 =3
    6. S→ KN + KT √½
      KN→W+S √ ½
      W→ Letu√ ½
      S→ lililopaliliwa √½
      KT→ limetuletea √½ (alama 4)
      N→ mazao√ ½
      V→ mengi √½
    7. Yule mtoro – kirai kivumishi
      Katikati ya barabara-kirai kihusishi
      Kila wakati-kirai kielezi
      Mwanafunzi yule mtoro- kirai nomino (yoyote 3x1=3)
    8. Chaka – mwitu/eneo lenye miti mingi.
      Shaka – wasiwasi
      Sentensi moja na maana zidhihirike (Alama 2 x1=2)
    9. Mwanafunzi atakuwa ameandika insha nzuri.
      Alama 2
    10. Vitoto vimefunga vilango vya vijumba vyao
      alama 2
    11. Kufungia maelezo ya ziada/pembeni.
      - Kufungia herufi na nambari.
      - Katika tamthilia kufungia maelekezo
      - Kufungia neno ambalo ni kisawe.
      - Kifungia maelezo ambayo ni ufafanuzi wa jambo lililotaiwa.
      Zozote 3 = alama 2
    12. Fungu la maneno lenye muundo wa kiima na kiarifa. (alama.2x1=2)
    13. I. Sokota
      II. Peka alama 2
    14.          
    15. Shamisho kipozi/yambwa tendwa-nyumba√ ½
      Shamirisho kitondo/yambwa tendewa-Babu √½
      Shamirisho ala – mawe√ ½ (al2.)
      Chagizo – kwa mawe. √½
    16. Mwana alishangiliwa matokeo yake na mzazi.
      - Mwana lishangiliwa matokeo yake na mzazi
      - Mwana alishangiliwa matokeo na mzaziye.
      Alama 2
    17. Kanga – mnyama
      Kanga – aina ya vazi
      Alama 2
    18. Ukiniita – nitaandamana nawe
      alama 2
    19. alikuwa – kitenzi kisaidizi (TS) √½
      amewasili – kitenzi kikuu (T) √½
      (Jumla = Alama 1)
  4. ISIMU JAMII
    1. wewe ni mfanyabiashara ktika soko la chapakazi,eleza sifa za lugha utakayotumia kuwasiliana na wateja pamoja na washiriki wengine siku ya soko. (al.10)
      • Hutumia msamiati wa biashara kama vile fedha,faida,hasara,bei,bidhaa,uchumi. Hii ni kwa sababu kila sajili huwa na msamiati wake.
      • Matumizi ya lugha shawishi na rahisi kueleweka ili kuweza kumshawishi mteja. Hii inatokana na ukweli kwamba muuzaji anataka kununua kwa bei nafuu kwa mudax mfupi uliopo.
      • Ni lugha yenye ucheshi na porojo kwa sababu ya kutaka kuvutia wanunuzi na kupata wateja wengi Zaidi kwa kuwa kuna ushindani mkubwa. Kuna ai kule kupewa Guarantee.
      • Ni lugha changamfu, kwa jinsi inayofurahisha ili kuwavutia wateja.
      • Ina kuchanganya na kubadili msimbo ili kuwavutia wanunuzi aina mbalimbali. Kwa mfano, “Nunua kwa bei nafuu,almos free!”
      • Ni lugha ya kijazanda na yenye taswira na tashbihi tele . Maelezo ambayo hutumika katika kuvutia wateja yamejaaa vifananisho na bidhaa nyingine ambazo ni bora ama duni kwa minajili ya kuhuisha na kuinua sifa za bidhaa inayohusika.
      • Ni lugha ya kupumbaza na kufurahisha,kwa mfano, ‘Utavaa hadi uzeeke!’Wakai mwingine ni lugha ya kulaghai ili kuuza.
      • Ni lugha iliyojaa matumizi ya chuku. Kwa mfano,”Dawa hii itaondoa wadudu wote nyumbani mwako mara moja!” au “Inatoka Ujapani straight!” ili kuwavutia wateja.
      • Lugha hii huchanganywa na nyimbo na hata mashairi wakai mwingine kama njia ya kuvutia wateja, hasa katika mazingia ya masoko wazi. Kwa mfano: “Ni ya leo,ahahaha,ni ya leo…”Inapotumika kwenye mabango na vipeperushi,sajili hii hutumia picha zinazopendeza kwa rangi, sitiari fiche,vifupisho na vidokezi,maana ni sajili yenye mnato.
      • Ni lugha ya mvutano/malumbano. Mteja hukosoa bidhaa ili kumshawishi muuzaji kushusha bei,naye mwenye bidhaa husifu bidhaa zake.
        Ni lugha yenye heshima na unyenyekevu kwa mnunuzi ili kuwasawishi wateja
        (zozote 5x2=10)
        (Hoja √1 ufafanuzi √1=
        (Za kwanza 5x2)=10)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?