Maagizo
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki..
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
- Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa.
- Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: RIWAYA
Assumpata K. Matei: Chozi la Heri
LAZIMA
- “ ...anajihisi kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Haya ni mazingira mageni kwake na hakuja hapa kwa hiari."
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
- Dondoo hili ni ushahidi tosha wa ufundi mkubwa wa lugha alionao mtunzi. Dhihirisha.(Alama 4)
- Wengi katika riwaya hii ni samaki waliotiwa demani. Fafanua kwa hoja 12. (Alama 12)
SEHEMU B: TAMTHILIA
Kigogo.Pauline Kea.
Jibu swali la 2 au la 3
- “Wamenigeuka...Nilijua nawaponza, nilijua ninawapunja, nilijua ninawadhulumu,”
- Eleza muktadha wa dondoo. (Al 4)
- Tambua mtindo katika dondoo. (Al 2)
- Eleza kwa mifano faafu hulka nne za msemaji katika tamthilia. (Al 4)
- Jadili usaliti unavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (Al 10)
- Jadili matumizi ya mbinu zifuatazo katika tamthilia ya Kigogo.
- Ishara.(Al 10)
- Majazi. (Al 10)
SEHEMU YA C: HADITHI FUPI
Jibu swali la 4 au la 5
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (Wahariri: Alifa Chokocho na Dumu Kayanda)
- “Lo! Vitu vidogo tu hivi vimeshinda yale madude makubwa.”
- Eleza muktadha wa dondoo. (Alama 4)
- Tambua mbinu mbili za kifani kwenye dondoo na udhibitishe. (Alama 4)
- Tambua sifa sita za washindi wanaorejelewa. (Alama 6)
- Eleza hali ya eneo lililokuwa likipiganiwa kabla ya uharibifu uliotokea. (Alama 6)
- “Kila mwamba ngoma huvutia kwake”. Kwa kurejelea hadithi zozote nne, tetea ukweli wa kauli hii. (Alama 20)
SEHEMU D: SHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Nyoosha mkono, uviringe ngumi, unyanyuwe kwa hasira.
Nyoosha mkono, sema hunitumi, ila haki ujira.
Nyoosha mkono, alama ya kukataa.
Alama ya nguvu
Nyoosha mkono, na macho makali, uwaonyeshe kukerwa
Nyoosha mkono , wataka halali , kwamba hutaki kuporwa
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
Nyoosha mkono, umekula njama, uyakatae madhila
Nyoosha mkono, nyanyua kwa hima, watambue hukulala
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
Nyoosha mkono, jiunge umoja, na wateswaji wenzako
Nyoosha mkono, mwonyeshe miuja, yaondoke masumbuko
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
Nyoosha mkono, ivume sauti, inayojaa kitisho
Nyoosha mkono, mumejizatiti kwa mengi maamrisho
Nyoosha mkono,alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
Nyoosha mkono, mumeshikamana, huo ukuta wa chuma
Nyoosha mkono, kitisho hakuna , wao watarudi nyuma
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
Maswali- Bainisha bahari tatu zinazojitokeza katika shairi.(alama 3)
- Andika ujumbe mkuu unaojitokeza katika shairi hili.(alama 4)
- Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
- Onyesha tamathali mbili za lugha zilizotumiwa. (alama 2)
- Bainisha kwa njia tatu ni vipi mtunzi amefanikiwa kutumia uhuru wa kishairi .(alama 3)
- Tambua toni ya shairi hili (alama 1)
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
- Madhila
- Jizatiti
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hukuja hapa kwa vingi,
Vitimbi vya kila namna,
Kanambia nikuruzuku,
Kimwana awe mwenzio,
Hukumtwaa mwananngu,
Kisema mno walavu,
Vipi wamgeuza ngoma,
Mapepo wampigia?
Siwe uloandaa,
Harusi ya kukata na shoka
Masafu ya magari, yakilalama jua kali,
Hadi kanisani kungia, mimbari we kusimama
Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko?
Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu?
Hukunambia we fidhuli
Mwanangu utamtunza?
Taandamana naye daima,
Ja chanda na pete?
Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno?
Midisko wampeleka, kisingizia mapenzi
Vipi wamtezea shere. Mwanangu kumliza?
Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo,
Tachukua lini majukumu
Ya kumlea na vifaranga?
Huachi kulia u waya.
Wanao kitelekeza
Nadhiri zako zako za nitakipu promise,
Zi wapi mwana balaa?
Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli,
Alotwala wengi wapendi,
Kwa jicho la nje kuwangia,
Imeanguka miamba mingapi, nayo ng’ang’ania kufia dondani,
Zinduka mwana zinduka,
Ailaya waangamiza.
Maswali- Hili ni aina gani ya shairi. Fafanua (alama 4)
- Mwandishi anaibua maswala kadhaa ya kijamii. Yaandike. (alama 3)
- Eleza matumizi ya uhuru wa kishairi katika utungo huu. (alama4)
- Eleza mbinu ya fasihi iliyotumika katika utungo huu. (alama 3)
- Bainisha matumizi ya: (alama 4)
- mistari mishata
- mistari kifu
- Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama ilivyotumiwa kwenye kifungu? (alama 2)
- vipaa mwitu
- kufia kidondani
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
- “Walisema walosema
Kitali hakina macho
Huvizia wapendwa
Kikafamia
Kwenye kinywa kisochoka
Kwa mara nyingine hasidi
ametudhalilisha
Amewapukutisha wanetu…”- Tambulisha huu ni wimbo wa aina gani. (alama 2)
- Wimbo wa aina hii hutekeleza majukumu gani katika jamii? (alama 8)
- Eleza faida tano ambazo mtafiti wa aian hizi za nyimbo anaweza kuzipata anapohiari kushiriki katika uimbaji wake. (alama 10)
Download Kiswahili Paper 3 Questions - Kassu Joint Mock Examination 2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates