Kiswahili P2 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

  • Jibu maswali yote.
  • Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  • Karatasi hii ina kurasa nane. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

UPEO

ALAMA

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 



MASWALI

UFAHAMU (Alama 15).
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.

Binadamu heshi kuwa na falsafa zinazojiri akilini mwake. Amejichanjia kijisayari chake na kufikirika mfano wa Mirihi katika falaki yake ya maisha. Ni sayari ndogo ambayo imejitenga na sayari nyingine kama vile kausi.
Mirihi kuna viumbe mauluti vyenye mitindo ya kustaajabisha. Tofauti na Kausi ambayo mabinti huwa na urembo wa kiasilia, wanamirihi ni "warembo" mithili ya walioanguliwa ja vifaranga. Viganja vyao na nyuso zao huwa zimekandwa kwa mafuta ya zebaki zikawa nyororo japo wengi huwa mithili ya suriama. Wasalaminiapo na wanakausi mikwaruzo yao huwachipua ngozi kwa kazi ya sulubu waifanyayo shambani. Fauka ya uchotara huo, wamefungasha kiasi huku wamejisetiri kwa vijisuruali na vijisketi ambavyo vimewabana kana kwamba vimeundwa kwa vitambaa vya mikononi na kutafuta misaada kutoka kwa majirani kuvivua na kuvivaa.

Wanakausi waliovalia nguo zinazowafika kwenye visigino, huchushwa mno na hivi vijiguo vinavyowasetiri hadi kwenye sisemi vilengesambwa, ukipenda magotini, bali kwenye mapaja. Ni kweli kwamba waso haya wana mji wao. Wanapondatia hasa kwenye hafla za maziko au arusi katika sayari ya Kausi Wanakausi hujibana pembeni kujionea malimwengu ulimwenguni. Minong'onezo ndio itajaa hewani "ni yakini Pemba ndiko kwenye nguo na wenda uchi wapo". Katika hafla hizo, wale mabinti wazuri wa Mirihi hubeba vibogoshi ambamo mara kwa mara hutoa vidubwasha vidogo vidogo na kuendelea kujipodoa huku shughuli zinapoendelea. Pengine huenda umesahau kuwa katika mipango na makadirio ya matumizi ya hafla hiyo marejeleo yanayokaririwa huwa "......... wajua watu wa Mirihi hawapendi......"
Mabinti wazuri wa Mirihi kila mmoja huwa amejibebea mwavuli na kujizuia mvua au jua huku amekumbatia maji ya chupa ya kutoka kwenye sayari ya Mirihi.
Wanakausi walalahoi huwa wakikata kiu yao rahisi kutoka kwenye mapipa yaliyojazwa maji au kwenye mifereji waliyobahatika kuwekewa na wizara ya maji, kwa kutumia viganja vya mikono. Mabwana wa Mirihi hawana haja na miavuli, wao huwa watu wenye zao. Huvalia kofia nene zinazoonekana kama somberero. Watembeapo huning'iniza funguo za magari ya kifahari katika mkono wa kushoto na simu ya rununu katika mkono wa kulia.
Hapa na pale watakuwa wakiwasiliana kwa simu zao na pia kupiga gumzo na maghulumu wa Kausi ambao kwa kawaida watakuwa wakiwarai Wanamihiri, "Utaniacha hivyo"
Baada ya hafla, mlo ambao huwa Wanamirihi hupakuliwa huku Mabwanamirihi wakidakia wasichelewe, mabintimirihi wakinyofoa kwa mikono au kung'ofoa kwa midomo yao myekundu na Wanakausi wakichungulia kwa mbali wakisubiri nafasi yao itimie.
Ghafla mawingu yataanza kutanda upande wa mashariki na mambo sasa yatachukua mkondo mpya. Wanamirihi mchakamchaka huengaenga, mbio kwenye magari yao. Lakini kuna wale ambao hawana magari ya kukimbilia. Kawaida yao huwaita Wanamirihi wenzao faraghani "Baba fulani umejaza?".
Wengine ubaki kusema, "Uenda basi letu likaniacha, tutaonana nikija wikendi."
Hali iwapo mwanana, Wanakausi wakakuwa sasa ndio wakati wa kujitambulisha na wengine kuyajaza magari ya Wanamirihi ya kifahari, kwa maembe, avocado, ndizi na makochokocho ya vitu vya shambani. Baada ya miezi kadha,Wanakausi wachache watawazuru Wanamirihi kuwapa shukurani katika kijisayari chao cha Mirihi.
Hapo sasa watafumbua jibu la kitendawili watakapokumbana na Bintimirihi amebeba kijikaratasi cha nailoni kimejazwa embe dodo moja, sukumawiki bila kusahau kisehemu cha nyama alichopimiwa cha shilingi kumi. Kwa kuwa atapata malazi kwake atamshauri, ".....pengine unionyeshe bucheri tununue nyama.... tupitie dukani tununue ....." hapo kwake Malaika atakuwa ameshuka kutoka Kausi hadi Mirihi.
Lakini wengine ni wale ambao pindi tu utakapowasalimia watakukwa na "zamu ya usiku siku hiyo." Wanaovalia somberero watamlaki mwanakausi kwa mlahaka wa kifalme ili akastaajabie vitu kama Majirafu, mazulia, makochi, taja nitaje.
Yule wa awali atalala usiku huo usingizi mnono usio wa bugudha na kwenye kochi huku akihimiria kurauka mapema asikutwe na waliolala nyuma ya pazia. Hisia za Mwanakausi zitamrudisha katika tamthilia ya WoleSoyinka "Masaibu ya ndugu Jero kuwa "vidole vyote havikuumwa sawa." Mirihi ni sayari iliyo sheheni watu na viatu, kumbe Kausi ni shamba la paukwa pakawa la Edeni. Tafakari haya.

Maswali.

  1. Andika anwani mwafaka ya taarifa hii. (alama 2)
    …………………………………………………………………………………………………………………………………….........…………………………………………………………………………
  2. Eleza tofauti kati ya wanawake wa Mirihi na wale wa Kausi. (alama 2)
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………............……………………
  3. "Mabwana wa Mirihi ni watu wenye zao". Thibitisha. (alama 3)
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  4. Ni dhahiri kuwa Mirihi ni Sayari yenye watu na viatu. Nini maana ya viatu. Je, kuna viatu hapa? Thibitisha. (alama 3).
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  5. Mwandishi anamaanisha nini anaposema " utaniacha hivyo?" (alama 2)
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  6. Eleza maana ya: (alama 2).
    1. Jirafu
      ………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………….........……………………………………….
    2. Vibogoshi.
      ……………………………………………………………………….………………………………………………………………………………….........……………………………………………………

UFUPISHO.
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:
Mitihani imetumiwa siku nyingi kama kigezo cha kupima werevu wa mwanafunzi katika kutekeleza majukumu ya kiakili yenye kuhitaji stadi mbalimbali. Hii ni njia ya kuaminika na ni rahisi ambayo imetumiwa miaka mingi na watahini kukadiria uwezo wa mtu. Lakini wale wanaopinga mitihani wanasema kuwa mitihani haipimi kwa njia inayoaminika uwezo wa kiakili wa mwanafunzi, badala yake, mitihani inakadiri tu uwezo wa mwanafunzi wa kukadiria mambo kama kasuku kwa muda mfupi uliojaa vitisho na shinikizo.
Wasioithamini mitihani pia wanadai kuwa mitihani humpa mtahiniwa wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu hadhi na umuhimu wa mitihani imekuzwa sana miongoni mwa watahiniwa na jamii zima kwa jumla. Mitihani ndio kigezo pekee kinachokadiria kufaulu au kutofaulu Kwa mwanafunzi. Mustakabali wa mwanafunzi kuamuliwa na mtihani. Watahini hawajali Sana masuala mengine ambayo yanaweza kuhathiri jinsi mwanafunzi anavyoweza kuufanya mtihani. Kwa mfano, mtahiniwa anaweza, kuwa mgonjwa, au pengine hakulala vizuri siku iliyotangulia mtihani. Haya yote ni masuala yanayoweza kumfanya mtahiniwa kutofanya vizuri katika mtihani.
Elimu nzuri humfundisha mwanafunzi kutumia akili. Lakini mfumo wa elimu unaopendelea mitihani haufanyi hivyo. Mfumo wa aina hiyo husisitiza kufundisha yale yale yanayopatikana katika mwongozo uliotolewa tu. Mwanafunzi hapewi motisha ili kusoma kwa mapana na marefu ili kupanua akili yake. Badala yake mwanafunzi hufungiwa kwenye uwanja finyu ambamo haruhusiwi kutoka. Mwalimu naye kadhalika hana uhuru wa kumfundisha mwanafunzi kile anachofikiria kuwa muhimu katika maisha. Badala yake jukumu kubwa analoachiwa mwalimu huwa ni kumpa mwanafunzi mbinu za kukujibu maswali na kupita mtihani.
Ingawa wanaoitetea mitihani hudai kuwa matokeo ya mitihani ni ya kuaminika kwa sababu husahihishwa na watu wasiowajua watahiniwa, lakini ni vizuri pia kukumbuka kuwa watahini ni binadamu tu. Binadamu huchoka, huhisi njaa na zaidi ya yote anaweza kufanya makosa. Licha ya hayo yote, watahini hutakiwa kusahihisha rundo kubwa la karatasi, kwa muda mfupi. Mjadala uliopo kati ya wanaopendelea mitihani na wale wasiopendelea watukumbusha kuwa kuna haja kubwa ya kuendelea kuboresha mfumo wa mitihani ili uweze kukadiria kwa yakini uwezo wa kiakili wa mtahiniwa.

Maswali.

  1. Fupisha aya ya kwanza na ya pili. (maneno 60) (alama 9)
    Matayarisho.
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………............................………………………………………………
    …………………………………………............................………………………………………………
    …………………………………………............................………………………………………………
    Jibu.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..................................................………………………
  2. Fupisha aya ya tatu na ya nne. (maneno 50) (alama 6)
    Matayarisho.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………….....................................…….………

    Jibu.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    …………………………………………............................………………………………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA. (Alama40)

  1. Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii.
    Kazi hii itaondoa matatizo mengi. (alama 2) ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………............………………..
  2. Andika kwa ukubwa. (alama 2)
    1. Neno hilo halimo katika kitabu (alama 2)
      ……………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………..………………
    2. Pakua ugali katika sahani
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  3. Changanua sentensi hii ukitumia visanduku.
    Twiga hukimbia mbio ingawa ni mrefu. (alama 3)
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  4. Eleza dhima ya kila mofimu katika neno: (alama 3)
    Waliofiana.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  5. Eleza maana ya maneno yaliyopigiwa mstari. (alama 2)
    Vibofu vya vipofu wale ni vibovu kwani vinatoa mkojo wenye vipovu vya rangi
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  6. Bainisha matumizi ya 'ni' katika sentensi . (alama 2)
    Mkamateni Kanini ambaye ni mwanafunzi wangu niliyempeleka shuleni.
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  7. Tambulisha na ueleze aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
    Maua atakuwa akicheza uwanjani.
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  8. Tambulisha aina za yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Mwathe alimsomea Katua barua.
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  9. Unda nomino mbili mbili kutokana na vitenzi vifuatafyo. (alama 2)
    1. Jaribu
      ……………………………………………………………………………………………....................
    2. Jua
      ................................................................................................................................................................
  10. Eleza matumizi ya viambishi vilivyopigiwa kistari (alama 3)
    1. Kaketi chini …………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………….............……….............
    2. Nikisoma kwa bidii nitapita mtihani
      ...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
    3. Mulinge acheza mpira vizuri.
      ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  11. Sauti /e/ na /u/ hutamkwa vipi? (alama 2)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………....……………........……………
  12. Tunga sentensi moja ukitumia -a- ya uhusiano kuonyesha umilikaji (Alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  13. Tunga sentensi ukitumia 'mume' kama kielezi. (alama 2)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  14. Andika katika usemi halisi sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Mshauri aliwasisitizia watoto kuwa kulikuwa na umuhimu kuwatii wazazi wao kwani hili
    linaongeza siku zao duniani.
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  15. Yakinisha sentensi hii katika nafsi ya pili umoja . (alama 2)
    Tusipoelewana na walimu hatutapata amani siku zote shuleni.
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......…………………
  16. Andika kwa wingi. (alama 3)
    Mwenye nguvu achimbe nguzo ya ua.
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………........……………
  17. Andika upya sentensi ifuatayo ukifuata maagizo. (alama 2)
    Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu nyumbani.
    (Anza…….Panya……)
    ………………………………………………………………………………...........................................................................................................................................................................................................
  18. Tumia mzizi -zee katika sentensi kama (alama2)
    1. Nomino…………………………………………………………………...........…………………..
    2. Kivumishi…………………………………………………………………..........…………………….

4. (ISIMUJAMII) (alama 10)

  1. Katika jamii huwa wakati mwingine kuna matumizi ya lugha isiyo ya kistaarabu. Taja mifano
    mitano ya lugha sampuli hiyo (alama 5)
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2. Taja mambo matano yanayoathiri jinsi tunavyoweza kutumia lugha katika jamii. (alama 5)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    ……………………………………………………………………………………………………………………


MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

MAJIBU YA UFAHAMU

  1. Wanamirihi / maisha ya wanamrihi (anwani ioane na maudhui na isizidi maneno matano)
    Hoja 1 x 12 = (alama 2)
  2.  –
    1. Wasichana wa kausi huwa na urembo wa kiasilia lakini wa mrihi huwa urembo wao ni kama walioanguliwa kutokana na kujirembesha kwao.
    2. Viganja vya wasichana wa mhiri huwa vyororo lakini vya wakausi huwa na mikwaruzo kutokana na kazi yao ya sulubu.
    3. Wasichana wa mrihi huvaa nguo fupi zinazowafika hadi magotini lakini wa kausi huvaa nguo zinazowafika hadi kwenye visingino.
      Hoja (3 a 1 = (Alama 3)
      Mwanafunzi arejeree pande zote mbili
    1. Huvalia kofia kubwa zinazoashiria utajiri.
    2. Huninginiza funguo za magari makubwa ya kifahari.
    3. Huwasiliana kwa simu za rununu.
    4. Wana majumba makubwa yenye mazulia, majirafu na makochi ya kifahari.
      Hoja zozote 3 x 1 = (alama 3)
  3. Hawa ni watu wa matabaka ya chini. Hoja 1 x 1 = (Alama 1)
    Ithibati
    1. Wananunua bidhaa duni kama embe moja, kipande cha nyama na sukumawiki.
    2. Vyumba vyao vidogo vimegawa kwa zulia.
    3. Hawana vyumba vikibwa kwani hata wageni wao hulala kwenye viti.
      Hoja zozote 2 x 1 = (alama 2)
  4. Ataondoka bila ikumwachia chochote. (alama 1 a 2 - 2)

  5. Jirafu – jovu / friji/Kifaa cha kuhifadhia vitu view baridi visiharibike.
    Kibogoshi – mkoba mdogo wa ngozi / mfuko mdogo.

JINSI YA KUTUZA

  • Ondoa ½ maki kwa kosa la sarufi likitokea kwa kila kisehemu.
  • Makosa ya sarufi yasizidi nusu ya anachostahili kupata katika sehemu.
  • Ondoa ½ maki kwa kosa la tahajia litokeapo mara ya kwanza hadi kufikia makosa 6.
  • Mwalimu akadireie majibu ya mwanafunzi vilivyo.

Majibu ya ufupisho

  1.  –
    • Mtihani ni kigezo cha kupima werevu wa mwanafunzi.
    • Njia hii imetumiwa miaka mingi kukadiria uwezo wa mtu.
    • Kuna wanaopinga.
    • Wanasema mtihani hupima ukadirifu wa mambo kikasuku.
    • Huwa na vitisho na shinikizo.
    • Mtihani huwapa wanafunzi wasiwasi.
    • Ndicho kigezo cha kukadiria kufaulu au kutofahulu.
    • Mustakabali wa mwanafunzi kuamuliwa na mtihani.
    • Watahini hawajali mengine yanaweza kuathiri matokeo.
  2.  –
    • Elimu nzuri humfundisha mwanafunzi kutumia akili.
    • Mfumo wa kupendelea mitihani haufanyi hivyo.
    • Husisitiza yale yaliyoko kwenye mwongozo au silabasi.
    • Haupatii mwanafunzi motisha.
    • Mwalimu hana uhuru wa kufundisha, anafunza mbinu za kujibu maswali.
    • Watahini ni binamu na uchoka.
    • Mtindo wa kukadiria wanafunzi huendelea na kuboreshwa.

NAMNA YA KUTUZA

  • Mtiririko (alama 2).
  • Ondoa ½ maki kwa kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza hadi makosa 10.
  • Ondoa ½ maki kwa kila kosa la tahajia litokeapo mara ya kwanza hadi makosa 6.
  • Nakala safi inandikwe kiujazo / mfululizo.

MAJIBU YA SWALI LA TATU (matumizi ya lugha)

  1. Hii – mengi.
    Kiashiria – idadi / jumla.
    • Jineno hilo halimo katika kitabu. (alama 1)
    • Pajua jiugali katika jisahani. (alama 1)
  2.  –
     

    S

    ½

    S1.

    U

    S2 ½

    KN

    KT

     

    KN

    KT1/2  ½

    N

    T

    E

       

    T

    V ½

    Twiga

    hukimbia

    mbio

    ingawa

     

    ni

    mrefu ½

    (Alama 3
    Kuchora jedwali yenyewe ni nusu alama.
  3. WA – nafsi.
    Li – wakati.
    O – Kirejeshi.
    F - Mzizi.
    Ian – kauli.
    a – kiishio. (Kila kipengee ½ x 6 = 3)
  4. Mfuko wa mkojo / mipira inayojazwa pumzi na kuchezewa na watoto.
    vipofu – aliyemaa macho.
    vibovu – vibaya.
    vipovu – viputo puto vya hewa / jokofu / jifuo.
    (kila sehemu sahihi alam ½ z 4 = 2 Alama )
  5. Makamateni – wingi, (ni)-kitenzi kishirikishi kipugufu .
    Niliye mpelekea – nafsi, shuleni – mahali ndani ya.
    (kila sehemu alama ½ x 4 = 2)
  6.  Atakuwa – kitenzi kisaidizi, akicheza – kitenzi kikuu.
    (alama 2 x 1 = 2)
  7. Barua – kipozi katua – kitondo. (alama 2 x 1 = 2 )
  8. Jaribu – jaribio, majaribu, mjarabu, kijarabu. (alama 1)
    Jua – ujuzi, njuzi, kujua. ( alama 1)
  9. Kaketi chini – ‘ka’ – kaumrisha. (alama 1)
    Nikisoma- ‘ki’ – masharti. (alama 1)
    Acheza – ‘a’ – wakati usiodhihirika. (alama 1)
  10. - /e/ ulimi ukiwa mbele – midomo imetandazwa. (alama 1)
    /u/ ulimi ukiwa nyuma – miodomo imevirigwa. (alama 1)
  11. Ng’ombe wa jirani amejifungua (1 x 2 = 2) mwalimu ukadirie sentensi ya mwanafunzi.
  12. Yeye ufanya kazi kiume. (alama 2)
  13. “Kuna umuhumu kuwatii wazazi wenu”. Mshauri aliwasisitizia watoto. “Hili litaongeza siku zenu duniani.” (alama 1/5 x 10 = 2)
  14. Ukielewana na mwalimu utapata amani siku zote shulkeni. (alama 2)
  15. Wenye nguvu wachimbe nguzo za nyua. (alama 3)
  16. Panya wote wanaotusumbua hapa kwetu nyumbani nimewaletea paka ili awaue (alama 2).
    1. Mzee Yule amenyolewa. (alama 1)
    2. Paka mzee hunywa maziwa. (alama 1)

KUTUZA
Ondoa ½ maki kwa kosa la kisarufi lakini usiadhibu zaid ya nusu alama katika sehemu.
Ondoa ½ maki kwa kosa la tahajia linapotokea hadi makosa sita (6).

4. Isimu jamii

  1.  –
    • Lugha hutaja sehemu nyeti za mwili wa binadamu kama vile za uzazi.
    • Kutaja mada pale isipofaa mf. Vifo, magonjwa, upimaji wa kinyesi, makamasi nk. Wakati wa kula.
    • Wanataja vilema ua wenye udhaifu wakiwepo k.v zeruzeru, kipofu, kiziwi.
    • Hutumia maneno ya kimatusi k.v mjinga, pumbavu n.k.
    • Hutumia lugha ya kulaani k.v ninakuombea ufe haraka / ufutwe kazi n.k.
      (Hoja zozote 5 x 1 = 5)
  2.  –
    • Hadhira mf. wale anaowazungumzia kama ni watoto akatumia lugha yenye ucheshi.
    • Utungo / matini / muktadha – kama ni mashairi atatumia lugha yenye ukiushi.
    • Tabaka mf. la juu amezoea kiingereza hapendi mf. Kiswahili.
    • Hali – chlokoro wanatumia lugha ya kutisha, mlevi, mgonjwa lugha yake huwa tofauti.
    • Mada – zile ngumu hutumia lugha nzito, zile rahisi hutumia lugha nyepesi.
    • Matilaba mf. Mtu anapotaka wenzake wamuunge mkono atatumia lugha ambayo itawavuta kwake.
    • Umri – kundi la kiumri husababisha vilugha mf. Vijana wana mtindo wao.
      (Hoja 5 x 1 = 5)

Zingatia makosa ya sarufi kutengemea alama alizopata mwanafunzi katika sehemu
Tahajia mkosa 6.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P2 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest