Kiswahili P3 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee katika karatasi hii
  • Kila swali lina alama ishirini
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
  • Hati yako iwe ya kuonekana vyema
  • Dumisha usafi katika karatasi hii

Kwa matumizi ya mtahini pekee

SWALI   (SEHEMU)

ALAMA

        TUZO

 

 

20

 

 

 

 

20

 

 

 

20

 

 

 

20

 

 

 

 80

 

 



MASWALI

SEHEMU A: USHAIRI (ALAMA 20)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Swali 1. LAZIMA
1. Mkatanimkatika, harithihatorithiwa
Sinaninalolishika, walaninalochukuwa
Mlimwengukanipoka, hata tone la muruwa!
Mrithininiwanangu?

2. Sinango’ombesinambuzi,sinakondesinabuwa
Sinahatamakaazi, mupasayokuyajuwa
Sinamazurimakuzi, jinsinilivyoachiwa
Mrithininiwanangu?

3. Sinakazisinabazi, ilawingiwashakawa
Sinachembeyamajazi, mnonikukamuliwa
Nakwa’cheniupagazi, mgumukwenuku’tuwa
Mrithininiwanangu?

4. Sinasikuachajina, mkatahatasifiwa
Hatanifanye la mana, mnonikulaumiwa
Poleniwanangusana, sinakwenu cha kutowa
Mrithininiwanangu?

5. Sinaleosinajana, sinakeshokutwaliwa
Sinazizisinashina, walatawikuchipuwa
Sinawanangu mi sana, la kwacha nakuraduwa
Mrithininiwanangu?

6. Sina utu sinahaki, milayangumeuliwa
Nyumayanguilidhiki, nambeleimekaliwa
N’nawananamikiki, hadin’tapofukiwa
Mrithininiwanangu?

7. Sinai la keshokwenu,wenyewekuiongowa
Muwanekwanyingi,mbinumwendepasikupuwa
Leo siyo, keshoyenu, kamamutajikamuwa
Mrithininiwanangu?
(Kina cha maishaA.S.Mohammed)

MASWALI

  1. Eleza hali ya mzungumzaji katika shairi hili ( alama 4)
  2. Eleza dhamira kuu ya mshairi kulitunga shair ihili (alama 2)
  3. Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili? (alama 2)
  4. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
  5. Fafanua mbinu tatu za lugha zlizotumiwa katika shairi hili (alama 3)
  6. Tambua bahari ya shairi hili ukizingatia. (alama4)
    1. Mizani
    2. Vina
  7. Andikaubetiwamwishokwalughayanathari/tutumbi. (alama 3)

SEHEMU B: RIWAYA: CHOZI LA HERI - Assumpta K. Matei
Jibuswali la 2 au 3
2. ‘Haya ni matokeo ya ubahimu w abinadamu’

  1. Tia maneno haya kwenye muktadha wake (alama 4)
  2. Eleza sifa sita za msemaji wa kauli hii (alama 6)
  3. Kwa hoja kumi, Jadili ubahimu mwingine unaotendwa na binadamu riwayani(Alama 10)

3. ‘Baba umewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota ;sikwambii kusimama dede?”
Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari katika kauli hapo juu.Tumia hoja ishirini (Alama 20)

SEHEMU C: TAMTHILIA: KIGOGO- Pauline Kea
Jibuswali la 4 au 5
4. “Na hiyo sauti ya Jabali imekuwa adha. Inanikama roho…..”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika dondooni. (Alama 2)
  3. Kwa hoja kumi na nne fafanua matendo mengine yanayomkama roho msemaji (Alama 14)

5. Eleza athari zozote kumi za tamaa na ubinafsi kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (Alama 20)

SEHEMU D: HADITHI FUPI : TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE .
Jibuswali la 6 au 7.
6. Jadili maudhui ya elimu katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba ukizingatia hadithi zifuatazo
(alama 20)

  1. Mapenzi ya kifaurongo
  2. Shogake dada anandevu
  3. Mame Bakari
  4. Mwalimu mstaafu
  5. Mtihani wa maisha
    AU

7. SHIBE INATUMALIZA – Salma Omar Hamad
1. “…madonda ya tumbo obesiti, ni kulatu ! “

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili ( alama 4 )
  2. Taja na ueleze sifa mbili za msemewa ( alama 4)
  3. Taja na utoe mifano miwili ya mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo ( alama 2)
  4. Jadili maudhui matano yanayojitokeza katika hadithi husika. (alama 10)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20)

  1. Eleza maana ya vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama. 8)
    1. Misimu
    2. Ngomezi
    3. Miviga
    4. Maapizo
  2.                    
    1. Fafanua dhima sita za miviga katika jamii yako. (alama. 6)
    2. Tambulisha sifa zozote sita za misimu. (alama. 6)


MWONGOZO – USHAIRI

  1. Hali ya mzungumzaji. (al 4)
    • maisha yenye umaskini mkubwa.
    • maisha yasiyokuwa na matumaini.
    • maisha yaliyokosa thamani.
    • maisha yenye kusikitisha.
  2. Dhamirakuuyamshairi (al 2)
    • kuwahimiza wanawe maisha niilikuhakikisha maisha mema ya baadaye kwa vile hali ya sasa ni ya kimaskini.
  3. mzungumziwa – watoto (al 1)
    nafsineni – mzazi (al 1)
  4. toniyashairi (al 2)
    • masikitiko
    • kutamauka/kukosamatumaini
    • yakuhuzunisha
  5. mbinutatuzalughazilizotumika. (al 3)
    • sitiari – mkatanimkatika
    • Balagha – mrithininiwanangu?
    • takriri – sina
  6. Bahariyashairiukizingatia. (al 4)
    mizani – msuko
    vina - ukara
  7. Ubetiwamwisho – lughayanathari. (al 3)
    mshairi ana matumaini kwamba wanawe wataimarisha maisha yao ya baadaye .Anawashauri wafanye bidii, wakabiliane na matatizo bila hofu.

RIWAYA-CHOZI LA HERI
Jibu swali la 2 au 3
2. ‘Haya ni matokeo ya ubahimu wa binadamu’

  1. Tia maneno haya kwenye muktadha wake (alama 4)
    Haya ni maneno ya Kaizari, alikuwa akijiambia , naongea akiwa kambini baada ya kuona hali na kukumbuka unyama uliotokea pale ambapo walifurushwa kwao.
  2. Eleza sifa sita za msemaji wa kauli hii (alama 6)
    Mvumilivu
    Mwenye busara
    Mwenye mapenzi ya kwa familia yake
    Mtamaushi
    Mwenye kihoro
  3. Kwa hoja kumi, Jadili ubahimu mwingine unaotendwa na binadamu riwayani (Alama 10)
    Ubahimu ni hali ya kuwa na tabia zilizo ovyo/mbovu,tabia mbaya, bila huruma (katili) /unyama
    1. Ubakaji wa watoto wasichana k.v mwanaheri, Lime ni ubahimu
    2. Kujihusisha kwa mapenzi ya wazazi na binti vilevile ni uozo katika katika jamii k.v Mzee Maya kwa Sauna
    3. Mauaji ya watu wa makabila tofauti ni ubahimu k.v familia ya Ridhaa inaangamizwa baada ya vita
    4. Aidha uharibifu wa mali baada ya uchaguzi kutokea ni ubahimu
    5. Uavyaji mimba vilevile ni ishara ya ukatili k.v Pete na Sauna anayejaribu kuavya mimba
    6. Ulanguzi wa watoto k.v Dickson ni ishara ya ukatili
    7. Uporaji wa mali ya watu ni tendo mbaya analotendewa
    8. Kujihusisha kimapenzi ya kiholela na wanawake wengi ni tabia mbovu k.v Nyangumi
    9. Utelekezaji wa watototo bila kuwapa mapenzi kama mzazi ni tabia mbaya k.v Naomi
    10. Utupaji wa watoto baada ya kujifungua ni tendo la ukatili.k.v mtoto aliyeokotwa na Neema

Baba umewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota ;sikwambii kusimama dede?”
Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari katika kauli hapo juu.Tumia hoja ishirini (Alama 20)

  1. Ni kinyume na matarajio yetu kuwa baada ya miaka hamsini ya uhuru bado taifa la Uhafidhina kushikilia kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi bora
  2. Ni kinaya pia kuwa tangu uhuru wa wahafidhina bado Tuama anashikilia mila na tamaduni hasi kuwa ni lazima apashwe tohara ndipo awe mwanamke kamili
  3. Ni kinaya kuwa bado nchi ya wahafidhina inapokea mikopo kutoka mataifa ya kigeni na kuendelea kushabikia mkoloni aliyewatawala
  4. Ni kinyume kuwa bado kuna wakoloni masetla ambayo bado walikuwa wakimiliki mashamba makubwa Uhafidhina huku wenyeji wakikosa ardhi
  5. Ni kinaya kuwa kahawa na bidhaa bora zinazokuzwa na kutengenezwa Uhafidhina zinauzwa ng’ambo huku wao wakipata visio bora
  6. Aidha ni kinaya kuwa miaka hamsini baada ya Uhuru bado wahaidhina hawakuwa wameweza kukabiliana na ukabila mwao…bado kulikuwa na vita baina ya makabila yao
  7. Vilevile ni kinaya kuwa miaka hamsini baadaye bado wanaume wazee hujihusisha kimapenzi na wasichana wadogo bila kujali athari zake k.v Mwalimu Fumba, Mzee Maya n.k
  8. Aidha ni kinaya kuwa wazazi hawajaweza kujua jinsi ya kuwalea watoto wao hivyo basi kuwatelekeza k.v Wazazi wa Chandachema, wa Zohali n.k
  9. Isitoshe, ni kinyume na matarajio yetu kuwa mika hamsini baada ya uhuru, serikali bado haikuwa imeweza kukabiliana na tatizo la umaskini jinsi ilivyoahidi baada ya uhuru
  10. Pia serikali hii inashindwa kuzuia magonjwa mbalimbali yanayowakumba wahafidhina licha ya kuahidi miaka hamsini iliyopita uhuru ulipopatikana.
  11. Aidha uongozi mbaya bado unaendelea Uhafidhina licha ya kumwondoa mkoloni miaka hamsini iliyopita kwani wanachukua usukani bado wanaendeleza ukatili kama vile mkoloni.
  12. Bado serikali haikuwa imweza kupiagana na tatizo la ufisadi linaloathiri ukuaji wa maendeleo yake maiaka hamsini baadaye
  13. Bado suala ya unyakuzi wa ardhi linaendelea licha ya kumwondoa mkolonik.v Shamsi anatueleza jinsi ardhi yao iliyonyakuliwa na mwenye nguvu.
  14. Licha ya mkoloni kuondoka miaka hiyo yote, bado utabaka ulishamiri Uhafidhina na serikali haijaweza kukabiliana nao.
  15. Mbali na hayo, licha ya kuwa Uhafidhina ilikuwa imepata uhuru miaka hamsini, bado demokrasia haikuwa imedumishwa hasa katika uchaguzi uk 19
  16. Ni kinaya kuwa katikamuhafidhina mtu aliye hata na shahada tau hawezi kupata ajira na hivyo huenda mataifa ya kigeni kutafuta ajira miaka hamsini baada ya uhuru
  17. Ni kinaya kuwa viongozi wa uhafidhina wanaona elimu ya kwao kuwa duni badala ya kuikuza miaka hamsini tangu uhuru uk65
  18. Ni kinaya kuwa maiaka hamsini ya uhuru, bado mauaji ya kiholela hasa vijana yanafanywa bila suluhisho ya janga hilo.
  19. Tangu uhuru, bado Uhafidhina haijaweza kudumisha usalama wake kutokana na vita vya wenyewe
  20. Bado hamna mshikamano wa kitaifa tangu uhuru ingawa ni mhafidhina mwenzao anayengoza
    TN: kadiria hoja za mtahiniwa zinazoonyesha kinaya hasa kuhusiana na maendeleo katika taifa la uhafidhina

TAMTHILIA- KIGOGO

  1.  
    1.                    
      1. Msemaji ni majoka
      2. Anamwambia Daktari
      3. Mahali ni ndani ya ambulensi
      4. Kilichotokea hapa ni kuwa Majoka alikuwa amezirai. Anamwambia Daktari maneno haya akiwa anadhani anaongea na babu yake Ngao. 1 x 4 = 4
    2. Mbinu za lugha
      1. Jazanda – Sauti ya Jabali inaashiria mauaji / Adhaa - kero
      2. Uhaishaji – inanikama roho
      3. Mbinu rejeshi / kiseqeve nyuma
    3.                    
      1. Kuendeleza biashara ya dawa za kulevya.
      2. Kuharibu mazingira kwa kuruhusu biashara ya ukataji miti
      3. Kumwendea kinyume mkewe Husda kwa kutaka mapenzi kutoka kwa Ashua.
      4. Kutaka kuharibu ndoa ya Ashua na Sudi.
      5. vijana kuangamia kupitia biashara ya pembe haramu
      6. Majoka anamuua Ngurumo na kukificha kifo chake katika chatu.
      7. Wanajamii wanateseka kwa kitendo chake cha kulifunga soko.
      8. Anakamwa roho na damu ya vijana wanaofia katika kiwanda cha Majoka and Majoka
      9. Anakamwa na damu ya babake Tunu ambaye alifia katika kiwanda cha Majoka bila bima.
      10. Majoka kuwadhulumu wafanyakazi wanaozalisha uchumi.
      11. Anapanga na kumuumiza Tunu
      12. Ukosefu wa chakula katika sokomoko
      13. Mauaji ya waandamanaji
      14. Kutaka kujenga hoteli ya kifari katika ardhi ya umma aliyonyakua.
      15. Anatumia binamu yake Kenga kuendeleza miradi yake ya kihila.
      16. Maandamano ya wanasagamoyo.
  2. Athari zozote kumi za tamaa na ubinafsi katika tamthilia ya kigogo.
    1. Umaskini – Hii inatokana na kunyakuliwa kwa ardhi ya soko la Chapakazi
    2. Ari ya mapinduzi – Tamaa na ubinafsi wa watawala vinakarifisha wazalendo kama Tunu na Sudi na wanaanzisha harakati za kuung’oa mamlakani uongozi wa Majoka.
    3. Uchafuzi wa mazingira – Tamaa ya wanaviwanda inawasukuma kutupa kemikali na taka kwenye mitaro ya maji.
    4. Utabaka – kuna matajiri Sagamoyo kama Majoka kutokana na tamaa ya kuwa na mali nyingi. Kuna maskini kwa mfano walevi.
    5. Matumizi mabaya ya vyombo vya dola- kutokana na tamaa ya kutaka kusalia mamlakani Majoka anatumia vyombo vya dola kama polisi na jela kutekeleza unyama.
    6. Vyombo vya habari
    7. Ukame – ukataji miti ovyo umesababisha maziwa na mito kukauka. Biashara hii imekubaliwa na Majoka.
    8. Kuathirika kisaikolojia – Tamaa na Ubinafsi wa Majoka unamfanya kutekeleza ukatili ambao unaifanya nafsi yake kumuhukumu.
    9. Unyanyasaji – Tamaa ya viongozi inawafanya wadai kodi kubwa ambayo haitumiwi kuimarisha soko la chapakazi.
    10. Tamaa ya kukopa kopa fedha katika mataifa ya nje kunaachia wanajamii mzigo wa kulipa madeni hayo kwa muda mrefu.
    11. Tamaa na ubinafsi wa wafuasi wa Majoka kama vile Boza na Ngurumo vinawafanya kufumbia macho uozo wa kigogo Majoka.
    12. Vifo
    13. Njaa
    14. Utengano katika jamii

HADITHI FUPI
MAUDHUI YA ELIMU
MAPENZI YA KIFAURONGO

  • Elimu ya sekondari inaonyesha utabaka. Wanafunzi wa shule za kitaifa na mikoani wa tabaka la juu.wazazi wao wana uwezo wa kugharamia masomo yao. Wale wa shule za vijijini ni wa tabaka la chini.wana matatizo ya karo kwa sababu ya umaskini.
  • Utabaka pia unadhihirika katika elimu ya chuo kikuu cha Kivukoni, wanafunzi wenye fedha wanadharau wenzao maskini.
  • Elimu ya chuo kikuu inatatiza kwa kutowajibika kwa wahadhiri katika kaziyao. Dkt. Mabonga anakataa kuwajibu wanafunzi wake na kuwatamausha.
  • Mapenzi huathiri matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika chuo kikuu. Dennis alifuzu vyema kwani mwanzoni hakuwa na mpenzi na hivyo alizingatia masomo.
  • Elimu ndio njia pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya kukamilisha masomo.
  • Wazazi wanamatarajio makuu kwa watoto wao kuwa watawafaa baada ya kukamilisha elimu.

SHOGAKE DADA ANA NDEVU

  • Mwandishi anadhihirisha kwamba bila kutia bidi masomoni wanafunzi hawawezi kufaulu masopmoni.
  • Umuhimu wa majadiliano miongoni mwa wanafunzi katika maandalizi ya mtihani. Safia na Kimwana wanasoma pamoja.
  • Hadithi inalenga umuhimu wa wazazi kufuatilia jinsi ambavyo watoto wanavyosoma.
  • Mtoto anayesoma vizuri ni chanzo cha furaha na fahari kwa wazazi. Wazazi wa Safia wanamwonea fahari kutokanana bidi yakemasomoni.
  • Elimu pia inasisitiza kupita mtihani. Safia na Kimwana wanadurusu pamoja kujitayarisha kupita mtihani.

MAME BAKARI

  • Watoto wa kike kubaguliwa na walimu pamojana wanafunzi baada ya kuwa wajawazito. Sara anaogopa kufukuzwa shuleni na mwalimumkuu.
  • Badala ya walimu kuwapa ushauri nasaha wanawapiga vijembe na kuwadhihaki.
  • Umuhimu wa bidi katikamasomo. Sara na rafiki yake Sarina wanasoma masomo ya ziada.
  • Twisheni inayofanyika usiku inahatarisha usalama wa wanafunzi. Hili ndilo linasababisha kubakwa kwa Sara.

MWALIMU MSTAAFU

  • Elimu ni chombo cha ajira. Wanafunzi waliofunzwa na mwalimu Mosi waliishia kuwa madaktari, marubani, wahadisin.k
  • Elimu ina jukumu la kujenga uhusiano mwema baina ya wanajamii. Mosi anajenga uhusiano/ mkabala mwema na wanafunzi wake.
  • Elimu ina dhima ya kukuza vipaji vya wanafunzi. Wanafunzi waliimba na kucheza zeze, violini, marimba, vinubi, kucheza drama na sarakasi siku ya kustaafu kwa mwalimu Mosi.
  • Ina jukumu la kuadilisha wanafunzi. Mfano Jairo anashauri wana Mosi kutoshiriki kunywa pombe.
  • Waliopuuza masomo kama Jairo hawakufua dafu.

MTIHANI WA MAISHA

  • Baadhi ya walimu huwapuuza wanafunzi haswa wanapokosa kufanikiwa kimasomo.  Mwalimu mkuu alimpuuza Samuel kwa sababu ya kuanguka mtihani.
  • Ulipaji karo ni muhimu katika elimu. Babake samueli tayari amelipa karo, kwa hivyo hatarajii samueli kukatazwa matokeo.
  • Mwandishi anaonyesha kuwa wasichana wanafanya vizuri masomoni kuliko wavulana. mf . dada zakesamueli
  • Elimu inasisitiza sana kupita mtihani na mwanafunzi akianguka anaonekana ameanguka maishani. Mf. Samueli anaamua kujitoa uhai.

Swali la pili.( Dondoo.)

  1. Maneno ya Mbura akiwambia sasa .
    Wako katika sherehe za kumea meno kwa mtoto wa Mzee Mambo na wa pili kujiunga na shule ya chekechea. Sherehe inayofanyika nyumbani kwa Mzee Mambo.
    Haya yanatokea baada ya vijana hawa kula kila kitu kisha kuanza kujadiliana ubora wa vyakula walivyovila na madhara yake.
  2. Sifa za msemewa.
    Mlafi..anakula bila kujali
    Mzembe… baada ya kula sahani tatu analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini.
  3. mbinuzalugha
    utohozi… obesity
    nidaa… kulatu !
    jazanda
  4. uongozi mbaya…. Mzee Mambo na DJ wanaongoza umma vibaya kwa kutumia mali ya umma kuandaa sherehe isiyowafaidi wananchi.
    Tamaa na ubinafsi….. DJ ananyakua dawa za wagonjwa na kuziweka kwa duka lake binafsi.
    Ufisadi. Mzee Mambo na DJ wanavuna mabilioni ya pesa za umma kwa sherehe isiyo na manufaa yoyote kwa umma.
    Matumizi mabaya ya vyombo vya dola…. Televisheni ya kitaifa inatumika kupeperusha sherehe ambazo hazi na manufaa yoyote kwa umma.
    Athari ya bidhaa zinazoingizwa inchini kutoka mataifa ya ughaibuni… mchelewa basmati ambao ni plastiki unawasababishia walaji( wanainchimaskini ) magonjwa kama vile saratani na obesiti.Matumizi mabaya ya mamlaka…Mzee Mambo anatumia gari za  serikali kusafirisha vyakula , wageni na ata maji katika sherehe yake binafsi. ( zozote 5 x 2 )

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SWALI LA FASIHI SIMULIZI
Maanaya

  1. Misimu: Ni semi za muda zinazozuka au kubuniwa katika mazingira maalumu na kipindi maalumu cha wakati.( Semi hizi huweza kutoweka pamoja na tukiol ililosababisha kubuni wa kwake au zikanawiri na kuwa misemo.) 1x2=2
  2. Ngomezi: Ni sanaa ya ngoma inayohusisha uchezaji wa ngoma kuwasilisha ujumbe kuhusu mambo kama vile ya vita, kuzaliwa kwa mtoto, janga la moto, uvamizi, msiba au kifo ama harusi kuliko kutumia maneno ya mdomo kwa kutumia mpigo na ishara mbalimbali. 1x2=2
  3.  Miviga: Ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalumu cha mwaka mara nyingi zikifanywa kama njia ya kuvusha mwanajamii kutoka kiwango au kundi moja hadi jingine. 1x2=2
  4. Maapizo: Ni dua au maombi maalumu ya kumtaka Mungu, miungu, au mizimu kumwadhibu mhusika mwovu anayefaa kulaaniwa au kumtakia mabaya na hufanywa na mtu anayehisi kuwa ametendewa uovu au amesalitiwa.1x1=2

b).

  1. Dhima sita za miviga 6x1=6
    • huelimisha wanajamii.Vijana kupitia miviga kama vile jando huweza kufundishwa kuhusu mambo ya utu uzima na namna ya kukabiliana na changamoto za maisha.
    • huonyesha matarajio ya jamii kwa wanajamii kupitia sherehe kama harusi, matarajio kuhusu wake au waume.
    • ni kitambulisho cha jamii kwa kuwa kila jamiii na miviga yake mahususi yenye mpangilio na mtindo wa jamii husika.
    • huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii kwa kuwa hupitishwa kutoka kizazi hadi kingine.
    • hukuza uzalendo kwa kuhimiza wanajamii kuzionea fahari tamaduni za jamii zao wanapojumuika pamoja katika sherehe.
    • huhimiza na kukuza umoja na utangamano miongoni mwa wanajamii wanapojumuika pamoja katika matambiko, harusi au mazishini.
    • huwasaidia wanajamii kukabiliana na hali ngumu za maisha kama vile kifo.
    • ni njia ya kupitisha maadili na thamani za jamii kwani wanajamii kupitia miviga hufunzwa umuhimu wa kazi, unyumba, uzazi na malezi.
    • ni kigezo au mizani ya kuwavusha wanajamii kutoka daraja hadi nyingine kupitia jando kutoka utotoni, harusi kuvusha kutoka useja/ujanena kuingia ndoani.
    • huonyesha imani za kidini za jamii husika kwa kuwa kila miviga huwa na imani zinazoambatana nayo.
  2. Sifa za misimu 6x1=6
    • misimu ni semi zisizokuwa sanifu na hivyo hazitumiki katika miktadha rasmi.
    • misimu huundwa kwa mbinu mbalimbali kama utohozi au kugeuza mpangilio wa maneno kama risto badala ya stori.
    • huzukana kutoweka katika baada ya muda fulani.
    • hutumiwa na watu katika mawasiliano yao katika kipindi maalumu cha wakati.
    • hutumiwa na kundi fulani la watu kufanikisha mawasiliano-kuna misimu ya vijana, wafanyakazi katika vyombo vya usafiri, au ya watoto.
    • baadhi ya misimu isiyopotea hudumu na kubadilika kuwa semi au msamiati sanifu wa lugha husika.
    • misimu hupata maana kutoka kwa watumiaji pamoja na muktadha wa mahali na wakati.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P3 Questions and Answers - Mangu High School Trial Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest