Kiswahili P2 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MASWALI

1. UFAHAMU ( Alama 15)
soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
“Yakobo, eti babu yako ndiye mnyama? Siamini na sitaamini maneno hayo.”
“Uliuomba ukweli.”
“Kwa nini hukuniambia mambo haya zamani, Yakobo? Kwa nini mama yako hakunifunulia? Kwa nini aliisoma barua hii akaificha?”
“Yote hayo yalifanywa ili uwe na maisha bora. Ulipata wazazi wema waliokulea na kukutunza. Ulipelekwa shuleni, Chaanasa, mimi sikukanyaga shuleni. Ikiwa ungeachwa kinyongo, huenda hungekuwa na maendeleo uliyo nayo. Labda ungeingilia maisha mabaya na kuwa mtu bure kabisa. Zipo siri zinazowekwa ili kuwalinda watu.”
Lakini, Yakobo, inaniuma sana. Miaka yote hii tumetembea pamoja, tumekuwa tukitembeleana, tumekula meza moja, tumefanya mambo mengi pamoja wala huniambii mimi ni mjomba wako.”
Naomba msamaha, kwa moyo wangu wote, kwa kukosa kueleza mambo hayo mapema. Hata hivyo, ni vizuri kuona mambo kwa njia nyingi, si mtazamo mmoja tu. Tuseme, ningekuambia mambo hayo mapema, je, ungekuwa na furaha zaidi? Huenda jitihada zako za kumtafuta baba yako zingekutia chuki. Pengine hata ungetamani kulipiza kisasi kwa dhiki alizokuletea ukafungwa jela au hata kuhukumiwa kifo. Wakati mwingine, ni salama kutojua. Jambo usilolijua halikunyimi usingizi. Hata hivyo, naomba radhi kwa kutokuambia. Ukweli wa mambo ni kwamba hata Mzee Johari muungwana, yaani, babu yangu, au baba yako, hakujua mambo haya yote. Alikufa bila kujua sura au jina la mtoto wake: Chaanasa.”
Bwana Chaanasa, bila kujua, alilia na kudondokwa na machozi kupukupu. Nikaona aibu kubaki hapo, lakini sikuondoka. Nilitaka kusikia hatima ya mazungumzo hayo.
“Yakobo, mpwa wangu,” Bwana Chaanasa aliita huku akilia. Akanyoosha mikono yake na kumkumbatia Yakobo.
“Nimekusamehe. Nimekusamehe. Lazima nitekeleze ombi la mamangu. Alinisihi nisiwe na chuki na mtu yeyote. Siwezi kukuchukia mpwa wangu. Naahidi sitakuchukia kamwe. Asante kwa kuniambia ukweli wote. Asante pia kwa hekima yako kwani pia ulingoja hadi wakati unaofaa kunifunulia mambo haya. Ungaliyafunua zamani, kama ulivyosema awali, huenda nisingaliitikia jinsi nilivyofanya leo. Huenda mambo yangekuwa mabaya. Labda ningelipuka kwa hasira na kusababisha hasara, pengine hasara isiyolipika. Sasa ninaelewa kwa nini tunalandana sana nawe, na mzee Busara. Sisi ni wa damu moja. Baba yangu angalikuwa hai, ningalienda nikamwone na kujitambulisha kwake. Ningalimwita ‘baba’ na huenda angaliniita ‘mwanangu.’ Ningalimsamehe kwa kumwacha mamangu na kunitelekeza.”
“Bado unaweza kumsamehe.”
“Jinsi gani?” Bwana Chaanasa akauliza.
“Kwa kusahau yaliyopita na kuganga yajayo. Yazike mambo yote hayo katika kaburi la sahau. Acha ya kale yawe ya kale, ya nyuma yawe ya nyuma, ya zamani yawe ya zamani. Kilichotendeka kimekwishatendeka. Yaliyofanyika yamefanyika. Yamemwagika na hayatazoleka kamwe hata kwa kuchimbua ardhi. Lililopita limepita, si uwele tena.
“Naam, Bwana Chaanasa, lipitalo hupishwa.”

 1. Eleza sababu za Chaanasa kufichwa taarifa kuhusu babake. (Alama 2)
 2. Thibitisha kuwa babu yake Yakobo alikuwa mnyama. (Alama 2)
 3. Eleza umuhimu wa maswali balagha katika kifungu hiki. (Alama 2)
 4. Je, ni kweli kuwa kama si kuweka siri mambo yangemharibikia Chaanasa? Tetea jibu lako. (Alama 3)
 5. Ni jambo lipi lililomfanya Chaanasa kumsamehe mpwa wake? (Alama 2)
 6. Kwa mujibu wa kifungu, kusamehe kuna matokeo gani? (Alama 2)
 7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (Alama2)
  1. hayatazoleka
  2. tunalandana

2. UFUPISHO ( Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Maadili ni desturi, utamaduni au hulkaa mbazo hubainisha na kulipa kundi fulani la watu upekee wake. Maadili ni muhimu katika kuonesha imani na kanuni za maisha ambazo kundi Fulani la watu huchukulia kuwa chanya na zile wanazozichukulia kuwa hasi. Maadili ndio mwongozo unaothibiti matendo na hulka za kila mmoja.
Kila jamii huwa na maadili yake ambayo yanamhitaji kila mwanajamii kutenda na kuishi kama jamii inavyotarajia. Pia, yaliweza kulegeza mielekeo au mitazamo yao. Hata leo, maadili hutusaidia kubainisha sisini akina nani, mtazamo wetu maishani, pamojana matarajio yetu.
Katika Katiba ya Kenya, maadili ya jamii ya Wakenyayameangaziwavyema. Kwanza, ni wazi kuwa Kenya ni taifa la wacha Mungu, kwa hivyo, kila Mkenyaanatarajiwa kuabudu na kumheshimu Mwenyezi Mungu. Hili limeshadidiwa hata katika wimbo wetu wa taifa. Pamola na hayo, katika kuimarisha umoja wa kitaifa, tofauti zetuWakenya kirangi, kikabila, kitabakana hata kidini hazipaswi kutugawanya.Maadili yanatuhimiza kuzichukulia hizo kuwa sifa za kipekee na kuzionea fahari. Ule utaifa wetu kama wakenya unapaswa kuwekwa mbele daima ili kuzima juhudi zozote za kututenganisha kwa misingi hiyo.
Kama taifa, tunahitaji kudumisha uzalendo wetu kwa kujitolea kuhakikisha kuwa mahasidi hawaporomoshi maadili ya jamii zetukwa kuiga hulka zao potovu. Uzalendo unatuhumiza kuripoti vitendo vyote vya kuihujumu nci au watu wake kwa asasi za dola. Asasi hizo zitachunguza na kuzima utekelezaji wa uhalifu kabla haujatikea, na iwapo utakuwa umetokea, asasi hizo zitawapa adhabu wahalifu ili waweze kubadili mienendo mibaya na kuwa kielelezo kwa wengine wenye nia mbaya.
Maadili, vilevile, humwongoza mtu kuhusu namna za kutatua mizozo na kudumisha amani. Hatuwezi tukajivunia uhuru pasi na kuwepo amani. Amani ndio msingi wa umoja, ustawi na maendeleo ya taifa lolote. Ukosefu wa amani hudumaza na hata kurudisha nyuma maendeleo kwa kuwahini watu nafasi za kushiriki uzalishaji mali. Ukosefu wa amani vilevile husababisha kuongezeka kwa visa vya uhalifu kama vile mauaji, kulememazwa kwa watu, unajisi, uharibifu wa mali na kusambaratika kwa familia, hali ambayo huchangia mporomoko wa maadili katika jamii.
Uadilifu unakwenda kinyume na methali, amani haiji ila kwa ncha ya upanga. Ukweli ni kwamba, tunaweza kusuluhisha tofauti zetu bila kutumia silaha. Matumizi ya silaha aghalabu huzidisha uhasama na kuchochea haja ya kulipiza kisasi. Njia pekee ya kutatua migogoro ni kuelewa chanzo cha migogoro yenyewe, wahusika kufanya kikao na kuizungumzia kwa uwazi na kwa utulivu. Pande zote husika zinafaa kukubali makosa au madhara yaliyotokana na matendo yao na kuomba msamaha ili kupata maridhiano. Kuomba msamaha kusidhaniwe kuwa kujishusha hadhi, bali ni unyenyekevu katika kutatua tofauti kwa manufaa ya muamala wa vizazi vijavyo. Anayeombwa msamaha naye anapaswa kuwa tayari kutoa shifaa kwa dhati na kusahau kosa alilofanyiwa. Yote haya yakishindikana, mgogoro wapaswa kupelekwa mahakamani. Haki za kila mmoja zimelindwa katika katiba yetu na mahakama zipo ili kutetea haki hizi bila kupendelea upande wowote.
Utiifu wa sheria vilevile ni njia mojawapo ya kukuza maadili ya kijamii. Kwa kuwa sheria hulinda haki za kila mtu; wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo, kila mmoja ana wajibu wa kuheshimu sheria. Hii ni pamoja na kulinda rasilimali zetu kama jambo la wajibu bila ya kutegemea kuwepe wadumisha sheria. Uongozi wa kisheria huwapa watu hakikisho kuwa maisha yao hayatakuwa kama ya mahayawani nyikani bali yatafuata utaratibu Fulani. Hivyo basi, sheria ni hakikisho la jamii inayolinda haki na kuendesha mambo yake kwa uwazi, haki na ushwari.
Bila shaka, tukizingatia na kuimarisha maadili, taifa letu litakuwa jamii bora na kivutio cha kila mtu. Kiu ya Wakenya ya kutaka kuhamia nchi nyingine, hasa zilizostawi, itapungua. Wote watakuwa na ari ya kuliendeleza taifa lao.

MASWALI

 1. Eleza umuhimu wa maadili kwa jamii na taifa kwa ujumla. (maneno 60-70) ( alama 7 , 1 ya utiririko)
  Nakala ya matayarisho
  Nakala safi
 2. Fafanua jinsi mizozo inaweza kutatuliwa kwa uadilifu. (Maneno 75-80) (alama 8, 1 ya utiririko)
  Nakala ya matayarisho
  Nakala safi

3. MATUMIZI YA LUGHA ( Alama 40)

 1.                                  
  1. Kwa kutoa mfano mwafaka, fafanua dhana ya kiambishi. (Alama 2)
  2. Eleza dhima ya viambishi katika neno lifuatalo. (Alama 3)
   lililolilia
 2. Andika neno lenye muundo wa IKKKI. (Alama 1)
 3. Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo.
  1. Mwanagenzi mwenyewe aliimba wimbo vizuri. (Alama 1) 
  2. Vyakula vyetu vina ladha nzuri sana. (Alama 2)
 4. Andika vitamkwa vyenye sifa zifuatazo: (Alama 2)
  1. Kikwamizo cha meno hafifu
  2. Kikwamizo cha kaa kaa gumu
  3. Irabu ya chini kati
  4. Nazali ya kaa kaa laini
 5. Andika sentensi ifuatayo katika hali tegemezi. (Alama 1)
  Watakapokuwa wakicheza kandanda tutakuwa tumelala fo fo fo.
 6. Onyesha ngeli za maneno haya. (Alama 2)
  1. nyavu
  2. wizani
  3. miadi
  4. mwalishi
 7. Mbali na kuorodhesha, onyesha matumizi mengine mawili ya koloni. (Alama 2)
 8. Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi. (Alama 2)
  Wapishi wameandika meza haraka ipasavyo.
 9. Andika sentensi moja ili kuonyesha maana mbili za neno ila. (Alama 2)
 10. Andika sentensi ukitumia vitenzi vitokanavyo na nomino zifuatazo. (Alama 2)
  1. hofu
  2. somo
 11. Andika sentensi yenye kishazi tegemezi vumishi cha wakati ujao. (Alama 2)
 12. Pigia mstari kihusishi na uonyeshe kinaashiria nini? (Alama 2)
  1. Mwalimu amesimama karibu na mlango.
  2. Mzee anapoketi huona mbali kuliko kijana anaposimama.
 13. Changanua sentensi ifuatayo kwa mtindo wa matawi. (Alama 3)
  Mbuzi na kuku walikuwa wakiuzwa sokoni.
 14. Badilisha katika kauli ya ketendua. (Alama 2)
  Tulitundika picha hiyo na kuyabandika maandishi ukutani.
 15. Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi hii. (Alama 2)
  Yeyote atakayefika katika mkutano wa chifu atakaribishwa vizuri.
 16. Andika katika usemi wa taarifa. (Alama 2)
  “Ziara ya Rais wetu itakamilika kesho alasiri.” Msemaji wa ikulu alimwambia mtangazaji.
 17. Andika sentensi moja ukitumia kihisishi cha kuridhia. (Alama 1)
 18. Onyesha tofauti za kimaana za neno zuka na suka katika sentensi moja. (Alama 2)
 19. Geuza katika ukubwa. (Alama 2)
  Ng’ombe walivunjika miguu yao
 20. Tunasema kishazi cha samaki , _____________ wa samaki au ___________________ ya samaki (Alama 1)

4. ISIMUJAMII (Alama 10)

 1. Kwa kutoa mifano mwafaka eleza visababishi vitano vya kuchanganya ndimi. (Alama 5)
 2. Kiswahili ni lingua franka. Thibitisha kwa mifano madhubuti. (Alama 5)

Mwongozo wa kusahihisha

1. Ufahamu

 1.                          
  1. Ili awe na maisha bora. √1
  2. ili kumlinda yeye. √1
 2. Alimwacha mamake na kumtelekeza. √2
 3. Maswali balagha yamejenga hisia (ya kutoamini) √1 na kusisitiza ujumbe (wa unyama wa babake) √1
 4. Naam/ndiyo √1 ; hakutelekezwa katika malezi yake, √1 huenda maisha yake yangekwenda mrama kwa kuwa na chuki na kisasi. Aidha huenda angefungwa. √1
 5. Ili kutekeleza ombi la mamake kuwa asichukie mtu yeyote. √2
 6. Kusahau yote yaliyofanyika √1
  na kuanza kushughulikia yaliyo muhimu katika maisha ya baadaye. .√1
 7.                              
  1. hayatakusanywa (pamoja); hayatachotwa √1
  2. tunafanana .√1
   Adhibu
   Sarufi : hadi nusu ya alama alizopata katika kila kisehemu.
   Hijai: hadi sita x1/2 =3
   Adhibu Mara ya kwanza.

2. Ufupisho

 1. Umuhimu wa maadili
  1. huonesha imani na kanuni za maisha za kundi la watu.
  2. hudhibiti matendo na hulka za watu.
  3. huwezesha watu kujitambua, kubaini mtazamo na matarajio yao.
  4. huwahimiza wakenya kuchukulia tofauti za kikabila,kidini na rangi kuwa sifa za kipekee za kuonea fahari.
  5. humwongoza mtu kuhusu namna za kutatua mizozo na kudumisha amani.
  6. hukuza utiifu wa sheria.
   HOJA 6x1
 2. Jinsi ya kutatua mizozo kwa uadilifu
  1. kuepuka matumizi ya silaha
  2. Silaha huzidisha uhasama na
  3. kuchochea haja ya kulipiza kisasi
  4. kuelewa chanzo cha migogoro
  5. kuwaleta pamoja wanaozozana katika kikao ili waizungumzie migogoro hiyo kwa uwazi na utulivu.
  6. pande husika kukubali makosa au madhara yaliyotokana na matendo yao na kuombana msamaha
  7. pande zote kuwa tayari kusamehe kabisa na kusahau.
  8. kupeleka migogoro mahakamani ili kutetea haki bila mapendeleo.
   utuzaji
   Hoja 7x1
   a ------ 6
   b -------7
   ut ------2
   adhibu – h – 6x½; s- 6x½ ; z – alama 1 kwa maneno kumi ya kwanza. Kisha ½ kwa kila maneno mengine matano

3. Matumizi ya lugha

 1.                                        
  1. sehemu ya neno (mofimu) ambayo hufungamanishwa kwenye shina/mzizi wa neno ili kulipa maana zaidi. √2
  2.                      
   • li- umoja/ ukubwa/ngeli √
   • li- wakati (uliopita)/njeo √
   • lo – kirejeshi ‘o’ cha kati √
   • li- ngeli /kitendwa √
   • l/li – mzizi
   • i – mnyambuliko/ kauli ya kutendea √
   • a kiishio √
    √= ½
  3. ambwa,angwa,embwe,engwa,imbwa,ombwa,umbwa,undwa,ungwa √1
   Tanbihi: neno liwe na maana ya Kiswahili
  4. mwenyewe- pekee √1
   vyetu- milikishi √= ½ ; nzuri – sifa √= ½
  5. itamkwa
   1. /th/ √
   2. /sh/ √
   3. /a/ √
   4. /ng’/ √
    Herufi ndogo na ifungiwe.
    √= ½(e) Wangekuwa wakicheza kandanda tungekuwa tumelala fo fo fo.
  6. nyavu- U-ZI/ZI √
   wizani – I-ZI √
   miadi – I-I √
   mwalishi – A-WA √
   √= ½
  7. matumizi ya koloni
   1. katika ratiba
   2. kuonyesha saa
   3. kuonyesha mafungu ya biblia au msahafu
   4. kuonyesha tarehe
   5. kutenga mada kuu na ndogo
   6. katika mtajo wa barua rasmi
   7. kuandika ufafanuzi.
    Zozote mbili.
  8. meza- shamirisho kipozi √1
   haraka ipasavyo- kielezi namna/jinsi
  9. dosari/kasoro/hitilafu; lakini/hata hivyo/ingawa √1
   Ana ila ila nampenda./ Alininunulia baiskeli ila ina ila. √2
   Tathmini jibu la mwanafunzi
  10. hofia,hofusha √1
   soma,somea,somesha. √1
  11. Mtoto atakayeomba vizuri atasamehewa. √ 2/0
  12. karibu na –mahali
   kuliko – ulinganisho
  13.                                                

   M UJYGYTAFDA
  14. Tuliitundua √ picha hiyo na kuyabandua √ maandishi ukutani.
  15. kiwakilishi cha pekee√
   kihusishi cha mahali √
   kihusishi cha ‘a’ unganifu. √
   kitenzi. √
   √= ½
  16. Msemaji wa ikulu alimwambia mtangazaji ya kuwa/kwamba zaira ya Rais wetu ingekamilika siku iliyofuata alasiri/ alasiri ya siku iliyofuata. √2
  17. hewala; sawa; vyema; alhamdulilahi √1
  18. Mwendawazimu huyo alizuka ghafla na kumzaba makofi msusi aliyekuwa akisuka miyaa. √2/0
  19. Magombe yalivunjika maguu yao. √2
  20. mtungo √ ½ wa samaki; numbi √½ ya samaki .
   Adhibu.
   Kama swali 1 ufahamu.

4. Isimujamii

 1. Sababu za kuchanganya ndimi
  1. kuonyesha hisia k.v furaha
  2. kubagua/kushirikisha wengine katika mazungumzo
  3. kujinasibisha na hadhi ya lugha
  4. kuonyesha umahiri wa lugha moja na zaidi
  5. kujitambulisha katika kundi fulani lawatumizi wa lugha
  6. kufidia upungufu wa msamiati wakati wa kujieleza.
  7. malezi au mazingira
  8. Kuficha ujumbe uliokuisudiwa
  9. kusisitiza jambo
  10. tabaka
  11.  miko na tamaduni
   Zozote 5x1=5
 2. Kiswahili kama lingua franka.
  • Kinatumika katika eneo pana lenye makabila mengi
  • Kimekiuka mipaka ya kiutamaduni
  • Kinatumuwa na watu ambao lugha za kwanza ni tofauti
  • Kinatumiwa na watu wa asili mbalimbali
  • Kinapanua mawasiliano baina ya watu wa maeneo mbalimbali na kuleta maelewano na mahusiano
   Hoja 5x1 =5
   Adhabu
   Sarufi 4x ½ =2
   Hijai 4x ½ =2

Download Kiswahili P2 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest