Kiswahili Paper 1 Questions and Answers -Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali mawili
  • Swali la kwanza ni la
  • Kila swali lina alama
  • Kila insha isipungue maneno
  • Karatasi hii ina kurasa mbili zilizopigwa
  • Watahiniwa ni lazima waangalie kuwa kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa, na kuwa maswali yoyote yamo
  1. Umealikwa kuhudhuria mahijiano ya kazi ya udaktari katika Hospitali ya Afya Nzuri. Andika tawasifu utakayowasilisha katika mahojiano hayo
  2. Fafanua umuhimun wa maabara katika shule za sekondari
  3. Andika kisa kinachoafikiana na maana ya methali: Ukuni juu ya uchaga hucheka ulio motoni
  4. Tunga kisa kinachomalizika kwa maneno yafuatayo:
    …Mzalendo halisi lazima ajitoe mhanga katika kupangia na kuunga mkono mikakati ya kuijenga nchi yake.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

  1. Hii ni insha ya kiuamilifu
    Vipengele vya utungo wa aina hii vizingatiwe, yaani muundo na maudhui.
    1. Muundo
      1. Anwani ( kutokana na mada)
      2. Maelezo ya kibinafsi
      3. Maelezo ya kitaaluma
      4. Tajriba au uzoefu
      5. Maandishi/ uchapisho
      6. Uanachama
      7. Tuzo
      8. Uraibu
      9. Wadhamini
    2. Maudhui
      Hoja za mwanafunzi zilenge taaluma ya utabibu.
  2. Mwanafunzi afafanue umuhimu wa maabara katika shule za sekondari
    Baadhi ya hoja
    1. Huwezesha wanafunzi kukumbuka maswala waliofunzwa darasani wanapofanya uchunguzi maabarani
    2. Huwapa wanafunzi nafasi ya kushuhudia maswala ya kisayansi moja kwa moja
    3. Husaidia wanafunzi kuelewa kwa mapana mada zinazofunzwa darasani
    4. Hukuza mbinu za udadisi,uchunguzi na uwasilishaji wa matokeo ya uchunguzi
    5. Wanafunzi hudhihirisha nadharia za kisayansi kutokana na matokeo baada ya uchunguzi
    6. Hukuza uwezo wa wanafunzi kutatua matatizo mbalimbali na kufanya maamuzi mwafaka
    7. Wanafunzi hupata fursa ya kuelewa uhalisia wa sayansi
    8. Hukuza hamu ya wanafunzi kutaka kujua/ kufahamu zaidi kuhusu mada husika
    9. Kupata maarifa au stadi za kufanya utafiti katika taaluma nyingine
    10. Hurekebisha mawazo potovu kuhusu suala fulani
  3. Hii ni insha ya methali
    1. Kutoa maana na matumizi ya methali
    2. Kisa au visa vinavyowiana/ kinachowiana na maelezo ya methali
    3. Mtahiniwa aonyeshe namna mtu anapopitia hali fulani mwingine awetayari kupitia hali sawa
  4. Hii ni insha ya mdokezo
    Mtahiniwa atamatishe insha yake kwa maneno yayohayo. Asipotamatisha kwayo atakuwa amepungukiwa kimtindo tu, akadiriwe vilivyo.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers -Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest