Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika jina lako na nambari ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Tia sahihi kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Jibu maswali manne pekee.
  4. Swali la kwanza ni la lazima.
  5. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki.
  6. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  7. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  8. Majibu yote sharti yaandikwe kwenye nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  9. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote tano za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Lazima
SEHEMU A: HADITHI FUPI

A. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

  1. “Alipokuwa kiguu na njia akimwinda kama kunguru mwerevu, moyoni mwake alidhani anafuata nyuki apate kula asali.”
    1. Weka dondoo katika muktadha wake. (alama 4)
    2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
    3. Eleza sifa za anayerejelewa kama kunguru mwerevu. (alama 6)
    4. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (alama 8)
      Anamwona baba akilini akifoka kama hayawani aliyejeruhiwa. Hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Familia yao si ya watu mbumbumbu. Dada zake Samueli walipasi mtihani huo huo wa kidato cha nne pasi hatihati kwenye shule hiyo ya Busukalala miaka michache iliyopita. Yule mkubwa, Bilha ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta naye Mwajuma anasomea ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Eregi. Kwa hivyo, shule si sababu wala udhuru. Ingawa baba yao anayaonea fahari mafanikio ya binti zake, aliwaona wanawake tu. Fahari yake ya dhati imo katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Baba alisadiki kwamba pindi walw mabinti wakishaolewa, hana satua tena juu yao na amatumizi yao ya fedha zao. Samueli ndilo tegemeo, nguzo hasa. Alijuzu kuwa tegemeo na nguzo ya familia yake.
      Yaani akiwa mtoto wa pekee wa kiume alitegemewa kuwategemeza na kuwahami wazee wake na kulidumisha jina la ukoo wa babake…Ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa. Lo! Iweje yeye mwanamume kushindwa na dada zake, wanawake..!

      SEHEMU B: TAMTHILIA

      P. Kea: Kigogo
      Jibu swali la 2 au la 3
  2. “La, koma! La, koma! Siwezi mimi, siwezi mimi. Sitaki kuwa gurudumu la akiba… hujayaacha hayo?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Fafanua umuhimu nne wa msemewa. (alama 4)
    3. Bainisha mbinu za kimtindo kwenye dondoo hili. (alama 4)
    4. Wanasagamoyo walifanya nini kujikomboa kutokana na uongozi dhalimu wa Majoka? (alama 8)
  3. “Tuacheni kufumbatia maji kama jiwe. Sagamoyo inahitaji mabadiliko,damu nyepesi ili kuufungua ukurasa mpya.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Tambua sifa sita za msemaji wa dondoo hili. (alama 6)
    3. Kwa hoja kumi, thibitisha kuwa Sagamoyo inahitaji kubadilika. (alama 10)

      SEHEMU C: RIWAYA

      A. Matei: Chozi la Heri

      Jibu swali la 4 au la 5
  4. “Hili ni pigo la tatu kutoka kwa walimwengu. Tofauti ni kwamba hili linauma na kudhalilisha zaidi kwani…”
    1. Weka dondoo kwenye muktadha wake. (alama 4)
    2. Eleza sifa tano za mrejelewa kwenye riwaya hii. (alama 5)
    3. Ni maudhui gani yanayojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 1)
    4. Fafanua pigo lililowapata wahusika wengine kumi wenye jinsia sawa na msemaji. (alama 10)
  5. Hakuna msiba usiokuwa na mwingine. Kwa hoja ishirini thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

    SEHEMU D: USHAIRI

    Jibu swali la 6 au 7
  6. Mfumo wa kibepari, mkwasi atononoke Naye aliye mkata, ufukara atuame
    Nao hao mabwanyenye, walopoka watwonjeshe Utagawiwa mwairo!
    Wizi eti wa kalamu, waziwazi serikali Wizara kila idara, si huduma zinauma Raslimali za umma, wachache wazifaidi
    Utapewa madhila!
    Lengo lao kutuzuga, akili kutuzuzua Kila kona tuwafate, makombo kututupia
    Keki nzima tulooka, makapi tu ndiyo yetu?
    Kila chako kitaporwa!
    Tunotaka ni ajira, kwao waliohitimu Iwafae iwakimu, si mtu kusujudia
    Siasa za peremende, zajenga umaskini Tumebaki fakiri!
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 2)
    2. Taja mambo ambayo nafsi neni analalamikia. (alama 4)
    3. Tambua bahari nne za shairi hili. (alama 4)
    4. Tambua arudhi zilizotumika kwenye shairi hili. (alama 4)
    5. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)
    6. Tambua mbinu mbili za kimtindo kwenye shairi hili. (alama 2)
  7. Soma shairi hili kisha uyajibu maswali yafuatayo:
    Ni sumu, sumu hatari Unahatarisha watoto Kwa ndoto zako leweshi Za kupanda ngazi
    Ndoto motomoto ambazo Zimejenga ukuta
    Baina ya watoto Na maneno laini
    Ya ulimi wa wazazi
    Ni sumu, sumu hasiri Unahasiri watoto
    Kwa pupa yako hangaishi Ya kuwa tajiri mtajika Pupa pumbazi ambayo Imezaa jangwa bahili Badala ya chemichemi
    Ya mazungumzo na maadili Baina ya watoto na mzazi
    Ni sumu, sumu legezi Unalegeza watoto
    Kwa mazoea yako tenganishi Ya daima kunywa ‘moja baridi’
    Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu
    Hadi saa nane usiku
    Huku yakijenga kutofahamiana Baina ya watoto na mzazi
    Ni sumu, sumu jeuri Unajeruhi watoto kwa pesa, Kwa mapenzi yako hatari
    Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
    Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi
    MASWALI :
    1. Andika mifano miwili ya mistari mishata katika shairi hili. (alama 2)
    2. Fafanua maudhui yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
    3. Fafanua umuhimu wa urudiaji katika shairi hili. (alama 4)
    4. Bainisha nafsi neni na nafsi nenewa katika shairi hili. (alama 2)
    5. Yanayozungumziwa yanajenga ukuta kwa njia gani. (alama 4)
    6. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari. (alama 4)

      SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
  8. Tambua vipera vifuatavyo: (alama 3)
    1. Wewe ni mweusi sana hadi ukibeba mtoto, analala akidhani ni usiku.
    2. “Kwa nini mnabaguana? Mimi sikuwafundisha kubaguana…”
    3. …hadi leo jamii hiyo inasadiki kuwa Luanda Magere alikuwa jagina wa kuenziwa.
      1. Tegua vitendawili vifuatavyo: (alama 5)
        1. Popoo mbili zavuka mto.
        2. Pango lenye mawe meupe na mkeka mwekundu.
        3. Naingia ndani ya nyama natoka bila kushiba.
        4. Amenifukuza kote kwa blanketi lake jeusi.
        5. Aliwa yuala, ala aliwa
      2. Eleza umuhimu wa nyimbo katika utambaji wa ngano. (alama 6)
      3. Ukusanyaji data katika fasihi simulizi huwa na changamoto zipi? (alama 6)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SEHEMU A: HADITHI FUPI
A. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

  1. “Alipokuwa kiguu na njia akimwinda kama kunguru mwerevu, moyoni mwake alidhani anafuata nyuki apate kula asali.” (uk 56)
    1. Weka dondoo katika muktadha wake. (alama 4)
      Ni maneno ya msimulizi/mwandishi. Anamrejelea Dadi alipokuwa na msukumo wa kumtaka Kidawa kuwa mpenzi wake. Kidawa alikuwa amemwambaa Dadi. Dadi alikuwa kufa kupona kumtafuta Kidawa.
    2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
      1. Nahau. Alipokuwa kiguu na njia
      2. Sitiari/jazanda. Maneno kunguru na nyuki ni jazanda inayomrejelea Kidawa.
      3. Tashbihi/tashbiba- kama kunguru mwerevu
    3. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (uk 136) (alama 8)
      Anamwona baba akilini akifoka kama hayawani aliyejeruhiwa. Hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Familia yao si ya watu mbumbumbu. Dada zake Samueli walipasi mtihani huo huo wa kidato cha nne pasi hatihati kwenye shule hiyo ya Busukalala miaka michache iliyopita. Yule mkubwa, Bilha ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta naye Mwajuma anasomea ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Eregi. Kwa hivyo, shule si sababu wala udhuru. Ingawa baba yao anayaonea fahari mafanikio ya binti zake, aliwaona wanawake tu. Fahari yake ya dhati imo katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Baba alisadiki kwamba pindi walw mabinti wakishaolewa, hana satua tena juu yao na amatumizi yao ya fedha zao. Samueli ndilo tegemeo, nguzo hasa. Alijuzu kuwa tegemeo na nguzo ya familia yake. Yaani akiwa mtoto wa pekee wa kiume alitegemewa kuwategemeza na kuwahami wazee wake na kulidumisha jina la ukoo wa babake…Ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa. Lo! Iweje yeye mwanamume kushindwa na dada zake, wanawake..!
      1. Taswira –Anamwona baba akilini akifoka
      2. Nahau-kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. …anayaonea fahari
      3. Chuku- baba kuweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima
      4. Takriri/urudiaji- nguzo, tegemeo kuonyesha matumaini makubwa kwa Samueli
      5. Tashihisi. Ilmuradi mawazo yanamwadhibu
      6. Mdokezo- jina la ukoo wa babake…/wanawake..!
      7. Uzungumzinafsia- mawazo haya yatokea mawazoni mwa Samueli
      8. Nidaa-Lo! wanawake...!
      9. Tabaini – familia yao si ya watu mbumbumbu
        Zozote 8x1

        SEHEMU B: TAMTHILIA

        P. Kea: Kigogo
        Jibu swali la 2 au la 3
  2. “La, koma! La, koma! Siwezi mimi, siwezi mimi. Sitaki kuwa gurudumu la akiba… hujayaacha hayo?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Fafanua umuhimu nne wa msemewa. (alama 4)
    3. Bainisha mbinu za kimtindo kwenye dondoo hili. (alama 4)
    4. Wanasagamoyo walifanya nini kujikomboa kutokana na uongozi dhalimu wa Majoka?(alama 8)
      1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
        1. Msemaji ni Majoka
        2. Msemewa ni Ashua
        3. Wako ofisini mwa Majoka
        4. Majoka alikuwa akimwiga Ashua na kujaribu kumshawishi kumkubali kimapenzi.
      2. Umuhimu wa Ashua.
        1. Ametumika kuendeleza ploti. Anafungwa jela ili kumshinikiza Sudi kuchonga kinyago.
        2. Anaendeleza maudhui ya elimu. Amesoma na kuhitimu kama mwalimu.
        3. Ni kielelezo cha watu wenye msimamo thabiti. Anakataa kushiriki mapenzi na Majoka.
        4. Anaonyesha ukatili wa Majoka. Anafungwa bila kosa licha ya kuwa ananyonyesha.
          Kwanza 4x1
      3. Mbinu za kimtindo
        Nidaa – la, koma!
        Takriri – la, koma! La, koma! Swali balagha – hujayaacha hayo?
        Mdokezo – sitaki kuwa gurudumu la akiba… 4x1
        1. mbinu ambazo Wanasagamoyo walitumia kujikomboa
        2. Kula kiapo. Tunu na Sudi wanakula kiapo wakiwa chuo kikuu kuwa watetezi wa haki.
        3. Kukataa ushawishi. Sudi anakataa kuchonga kinyago cha Majoka hata baada ya Kenga kumshawishi.
        4. Kuwatia hofu viongozi. Sudi anamweleza Kenga kuwa wamemulikiwa mbali.
        5. Kuwazindua wanyonge. Sudi na Tunu wanaenda Mangweni kuwazindua walevi kuhusu udhalimu wa uongozi wa Majoka.
        6. Elimu. Tunu anasomea uanasheria ili kupigania haki za Wanasagamoyo.
        7. Kuchunguza mienendo ya viongozi. Ashua na Tunu wanatambua kuwa Kenga anawahutubia wahuni.
        8. Migomo. Wauguzi na walimu wanagoma ili kudai nyongeza ya mshahara.
        9. Kuwakabili viongozi dhalimu moja kwa moja. Ashua na Tunu wanaenda ofisini mwa Majoka kumweleza kuhusu maovu yake.
        10. Maandamano. Tunu na Sudi wanaongoza maandamano ya kutaka soko la Chapakazi kufunguliwa.
        11. Mikutano ya hadhara. Tunu anahutubia baadhi ya Wanasagamoyo katika lango kuu la soko la Chapakazi.
        12. Vyombo vya habari. Runinga ya Mzalendo inapeperusha habari za watetezi wa haki.
        13. Kususia mkutano. Baadhi ya Wanasagamoyo wanakosa kuhudhuria mkutano wa Majoka.
          Zozote 8x1
  3. “Tuacheni kufumbatia maji kama jiwe. Sagamoyo inahitaji mabadiliko,damu nyepesi ili kuufungua ukurasa mpya.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Tambua sifa sita za msemaji wa dondoo hili. (alama 6)
    3. Kwa hoja kumi, thibitisha kuwa Sagamoyo inahitaji kubadilika. (alama 10)
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
        Msemaji ni Sudi. Anawaambia Ngurumo, Boza na walevi wengine. Ni Mangweni kwa Mamapima. Sudi alikuwa akibadilishana maneno na kina Boza na Ngurumo na ndipo Tunu anamkumbusha asisahau ajenda yao waliyokuwa nayo kama sababu ya kufika Mangweni kuwakumbusha vijana kuhusu kukongamana kwao katika lango kuu la soko la Chapakazi.
      2. sifa sita za Sudi. (alama 6)
        1. Ni msomi. Walikuwa na Tunu chuo kimoja wakiwa viongozi wa wanafunzi.
        2. Mwenye mapenzi ya dhati. Anamkumbatia Ashua anapompelekea chai katika soko la chapakazi.
        3. Mwenye msimamo thabiti. Anakataa kabisa mradi wa kuchongea Majoka kinyago.
        4. Ni mwenye hasira. Anamwambia Boza achunge ulimi wake kwa hasira.
        5. Mwenye huruma . Anamwambia mkewe pole baada ya kuona damu kwenye vidole vyake
        6. Ni mkali. Anamwambia kwa ukali Boza wasikoseane heshima baada ya Boza kudai Sudi alizaliwa na meno mdomoni.(uk.64)
        7. Ni mwajibikaji anachonga shujaa halisi wa Sagamoyo ambaye ni mwanamke. Anawajibika kujenga Sagamoyo mpya.
        8. Ni jasiri. Walikula kiapo kutetea haki za wote hata kama ingewagharimu uhai wao/pumzi yao ya mwisho.
        9. Mtetezi wa haki. Anashiriki katika maandamano ya kupinga uongozi dhalimu wa Majoka.
          Mwenye utu. Anawapa wachongaji wenzake chai na mahamri.
          Kwanza 6x1
      3. Sababu za Sagamoyo kuhitaji mabadiliko.
        1. Haki ya kuishi inakiukwa. Mauaji ya kupangwa yanafanyika chini ya uongozi wa Majoka. Ngurumo, Jabali na vijana watano wanauawa.
        2. Haki ya kupewa usalama. Jamii ya Sagamoyo inaishi kwa woga. Watu wananyongwa/kuuliwa na chatu.
        3. Uhuru wa kutangamana haupo. Watu wanapokutana sokoni, wanatawanywa. Kenga anasema watu wa Tunu walifurushwa,ulinzi ni mkali sokoni.
        4. Vyombo vya habari havina uhuru. Majoka anatoa amri Runinga ya Mzalendo kufungwa kwa kupeperusha hafla ya Wanamapinduzi.
        5. Wafanyabiashara wanafungiwa soko. Ashua alikuwa muuzaji wa maembe na soko linapofungwa anadai matumaini yao yamekatishwa.
        6. Elimu bora haipo Sagamoyo kwa kuwa wanafunzi wamekuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka na kukosa kufuzu.
        7. Wanasagamoyo wananyimwa uhuru wa kuzungumza/kujieleza. Majoka anawataka polisi kutomruhusu Tunu kuzungumza sokoni.
        8. Wanasagamoyo hawaheshimiwi na viongozi. Majoka anawaita wajinga.
        9. Maslahi ya wafanyakazi si bora. Walimu na wauguzi wanagoma wakitaka nyongeza ya mishahara. Uongozi unapendekeza waongezwe kwa mkono mmoja na mwingine kuwapandishia kodi.
        10. Viongozi wanakusanya kodi na kitu juu yake lakini hawatoi huduma za kimsingi katika Sagamoyo. Wanasagamoyo hawana maji,kazi,umeme n.k
        11. Wafanyakazi katika kiwanda cha Majoka hawana bima. Babake Tunu anafia kiwandani. Vijana wengine watano pia wanafia kiwandani kule.
        12. Utawala ni wa kinasaba na mapendeleo. Kenga ni binamu yake Majoka. Majoka anapanga kumtambulisha Ngao Junior katika sherehe za uhuru kama mrithi wake.
        13. Mazingira safi ni haki inayokiukwa. Soko lilikuwa chafu, maji machafu ya taka yanasababisha Wanasagamoyo kukumbwa na magonjwa.
        14. Uongozi unapanga kuwafurusha wafadhili na makundi ya kutetea haki yanayounga mkono hatua za kina Tunu.
        15. Huduma muhimu kama matibabu ni ndoto bado. Tunu anasema huduma muhimu ziletwe karibu k.v hospitali, barabara, maji safi, elimu n.k
        16. Majoka hafuati sheria anapomfuta kazi Kingi. Huku ni kukiuka haki ya mfanyakazi
        17. Raia wanauziwa pombe haramu. Huku ni kukiuka haki ya watumiaji bidhaa. Hii inasababisha vifo na kupofuka kwa watu.
        18. Haki za wafungwa zinakiukwa. Watu wanafungwa bila kuwa na kosa. Ashua anafungwa bila hatia. Kwanza 10x1

          SEHEMU C: RIWAYA

          A. Matei: Chozi la Heri
          Jibu swali la 4 au la 5
  4. “Hili ni pigo la tatu kutoka kwa walimwengu. Tofauti ni kwamba hili linauma na kudhalilisha zaidi kwani…”
    1. Weka dondoo kwenye muktadha wake. (alama 4)
    2. Eleza sifa tano za mrejelewa kwenye riwaya hii. (alama 5)
    3. Ni maudhui gani yanayojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 1)
    4. Fafanua pigo lililowapata wahusika wengine kumi wenye jinsia sawa na msemaji. (alama 10)
      1. Ni maneno ya msimulizi/mwandishi anamrejelea Lunga ambaye yuko kwake katika Mlima wa Simba. Ni baada ya kupata ujumbe mfupi katika rununu yake kuhusu kuondoka kwa Naomi. Anahisi kuwa kuondoka kwa Naomi kulimkandamiza Lunga. (uk 81)
      2. Mrejelewa ni Lunga
        1. Mtetezi wa haki – anakataa Wahafidhina kuuizwa mahindi yaliyoharibika.
        2. Mwenye msimamo thabiti – anashikilia msimamo wake wa Wahafidhina kutouziwa mahindi yaliyoharibika hata baada ya rai ya wakubwa.
        3. Mwenye utu – utu wake unamfanya kupinga Wahafidhina kuuziwa mahindi yaliyoharibika.
        4. Mwajibikaji – anawasomesha wanawe/anapinga uuzaji wa mahindi yaliyaharibika kwa Wahafidhina.
        5. Mwenye bidii – anajihusisha na ukulima alipokuwa katika msitu wa Mamba.
        6. Mwenye tamaa – tamaa ya kulima maekari inamfanya kukataa miti ili kujihusisha na kilimo.
        7. Msomi – alikuwa amesomea kilimo.
      3. Udhalimu/ukandamizaji/ukatili
        1. Ridhaa – familia yake inateketezwa na mzee Kedi isipokuwa Mwangeka/anabaguliwa akiwa shuleni/ majumba yake yanabomolewa bila kupewa fidia.
        2. Mwangeka – anampoteza mkewe Lily na mwanawe Becky katika mkasa wa moto baada ya wao kuteketezwa na mzee Kedi/anaadhibiwa kwa mshipi na babu Msubili/anakosa kupewa chakula na mamake kama adhabu.
        3. Kaizari – wanawe wanabakwa mbele yake na mabarobaro watano/mkewe anakatwa kwa sime/anaachwa na mkewe na baadaye kumpata akiwa amefariki/anaacha mali yake baada ya kuvamiwa na mabarobaro watano.
        4. Dick/Dickson – analazimishwa kulangua dawa za kulevya na Buda/ anatekwa nyara na Sauna/anatenganishwa na nduguze/ anakosa malezi ya wazazi baada ya Naomi kutoroka na Lunga kufa.
        5. Billy – anasalitiwa kimapenzi na mpenziwe Sally anapoliona jumba lake la kifahari kama kiota.
        6. Kiriri – mkewe Annette anamwacha na kuenda ughaibuni/ wanawe wanakosa kurejea katika nchi yao.
        7. Shamsi – shamba lao linanyakuliwa na Bwana Mabavu.
        8. Mwangemi – anaadhibiwa na babu Msubili kwa sababu ya kumtania/anakosa kupewa chakula na mamake kama adhabu.
        9. Mwaliko – anatekwa nyara na Sauna na kufungiwa ndani na Bi. Kangara.
        10. Kipanga – anakanwa na mtu aliyedhani kuwa ni babake.
          (wahusika kumi tofauti wa kiume waangaziwe) 10x1=10
  5. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe. Kwa hoja ishirini thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20) MAJIBU
    1. Ridhaa mbali na kupoteza familia yake, nyumba yake inateketezwa kwa moto.
    2. Mkewe Kaizari anakatwa kwa sime na binti zake kubakwa. Wakati wa usafiri lori linaisha petroli.
    3. Wahafidhina kwa kutaka uongozi mpya ni ishara walitaka mabadiliko lakini mabadiliko yanakuja kwa maafa na ghasia.
    4. Dick anatekwa nyara baada ya baba yao kuaga na kuuzwa kwa Buda. Anahofia maisha yake na mwisho kukubali kulangua dawa za kulevya.
    5. Wafanyabiashara wanawafungia wateja ndani ya maduka yao kwa kuhofia kuibiwa. Hawa wanakufa kwa mkasa wa moto.
    6. Subira aliyekatwa kwa sime anawatekeleza wanawe kutokana na ugomvi baina yake na mama mkwe.
    7. Serikali ilikosa kuwajibikia mahitaji ya vijana kama vile kuwapa kazi. Kuna vijana wanaokaukiwa mate ya kufunga bahasha za kuomba kazi. Viongozi hurejea kila baada ya miaka mitano kuwapa ahadi hizi za ujanja.
    8. Katika kambi za wakimbizi, vitoto vinakufa vilipoenda haja kwenye reli, njaa na magonjwa. Uk.29
    9. Chandachema anatelekezwa na wazazi wake na kupata malezi duni kutoka kwa bibi(nyanya) yake.
    10. Pete baada ya kukanwa kuwa hafanani babake alienda kulelewa na bibi mzaa mama. Huku anapatwa na matatizo ya hedhi na kukosa mapenzi na ushauri. Anadhani ana bahati kumpata Nyangumi lakini mkewe halisi anaporudi anafukuzwa.
      Vita vilipochacha, viongozi walikituma kikosi cha askari cha Penda Usugu Ujute. Kikosi hiki kinatumia risasi na vitoza machozi kuwakabili waandamanaji.
    11. Kitoto chao Kairu kinakufa kutokana na njaa na ugonjwa wakati walipofukuzwa kwao.
    12. Lunga anaachwa na mkewe baada ya kufutwa kazi.
    13. Umu baada ya kubaki yatima, kijakazi Sauna anawateka nyara ndugu zake.
    14. Vita vinatokea kutokana na uchaguzi. Watu wanahamia Msitu wa Mamba kama wakimbizi. Huku wanakumbana na matatizo kama uhaba wa vyumba na chakula.
      Wakimbizi wanafanya Msitu wa Mamba kuwa makao yao. Wanafanya ukulima na kujenga lakini mwishoni wanaondolewa kwenye msitu huu. Hakuna aliyejua mahindi ya akina Lunga yalikwenda wapi. Uk.77
    15. Wakoloni wananyakua mashamba ya Waafrika na kuwafanya wenyeji hazina ya vibarua.
    16. Tila anaonyesha kuna uongozi mbaya umaskini, ufisadi, ukosefu wa gharama za matibabu ya kimsingi na ukosefu wa lishe bora.
    17. Kazi nyingi za serikali kupeanwa zabuni kwa kapuni za kigeni ambao wanajilimbikizia mali ya wahafidhina.
    18. Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja
    19. Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake
    20. Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake Satua
    21. Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watoto watatu akiwa chini ya miaka ishirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua kwanza 20x1
      (hoja ziangazie pande zote mbili za methali)

      SEHEMU D: USHAIRI
  6. Mfumo wa kibepari, mkwasi atononoke Naye aliye mkata, ufukara atuame
    Nao hao mabwanyenye, walopoka watwonjeshe Utagawiwa mwairo!
    Wizi eti wa kalamu, waziwazi serikali Wizara kila idara, si huduma zinauma Raslimali za umma, wachache wazifaidi
    Utapewa madhila!
    Lengo lao kutuzuga, akili kutuzuzua Kila kona tuwafate, makombo kututupia
    Keki nzima tulooka, makapi tu ndiyo yetu?
    Kila chako kitaporwa!
    Tunotaka ni ajira, kwao waliohitimu Iwafae iwakimu, si mtu kusujudia Siasa za peremende, zajenga umaskini
    Tumebaki fakiri!
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 2)
      Mfumo wa kibepari 2x1
    2. Taja mambo ambayo nafsineni analalamikia. (alama 4)
      1. Matajiri kutajirika/maskini kuzidi kuwa maskini
      2. Ufisadi serikalini
      3. Raslimali kufaidi wachache
      4. Ukosefu wa ajira
        4x1
    3. Tambua bahari za shairi hili. (alama 4)
      1. Sabilia-lina kiishio/halina kibwagwizo
      2. Masivina-halina urari wa vina kwenye beti zake.
      3. Msuko-kiishio kifupi kuliko mishororo mingine
      4. Mathnawi-lina vipande viwili (ukwapi na utao) isipokuwa mshororo wa mwisho.
      5. Tarbia – lina mishororo minne katika kila ubeti
        4x1
    4. Tambua arudhi zilizotumika kwenye shairi hili. (alama 4)
      1. Lina mishororo minne kwa kila ubeti
      2. Lina vipande viwili kwa kila mshororo isipokuwa kiishio chake
      3. Mshororo wa mwisho ni mfupi kwa kila ubeti
      4. Lina beti nne kwa jumla
      5. Lina mizani kumi na sita kwa kila mishororo isipokuwa mshororo wa mwisho una mizani nane.
        4x1
    5. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)
      Mshairi anasema kuwa mfumo wa kibepari unawatajirisha matajiri na maskini kuendelea kumaskinika. Matajiri wanapaswa kuwagawia maskini utajiri/mali yao. Anasema utapewa bure/hakuna.
      4x1
    6. Tambua mbinu mbili za kimtindo kwenye shairi hili. (alama 2)
      Swali balagha-makapi tu ndiyo yetu? Jazanda-keki kuwakilisha raslimali/mapato
      2x1
  7. Soma shairi hili kisha uyajibu maswali yafuatayo:
    Ni sumu, sumu hatari Unahatarisha watoto Kwa ndoto zako leweshi Za kupanda ngazi
    Ndoto motomoto ambazo Zimejenga ukuta
    Baina ya watoto Na maneno laini Ya ulimi wa wazazi
    Ni sumu, sumu hasiri Unahasiri watoto
    Kwa pupa yako hangaishi Ya kuwa tajiri mtajika Pupa pumbazi ambayo Imezaa jangwa bahili Badala ya chemichemi
    Ya mazungumzo na maadili Baina ya watoto na mzazi
    Ni sumu, sumu legezi Unalegeza watoto
    Kwa mazoea yako tenganishi
    Ya daima kunywa ‘moja baridi’
    Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu Hadi saa nane usiku
    Huku yakijenga kutofahamiana Baina ya watoto na mzazi
    Ni sumu, sumu jeuri Unajeruhi watoto kwa pesa, Kwa mapenzi yako hatari
    Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
    Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi
    MASWALI :
    1. Andika mifano miwili ya mistari mishata katika shairi hili. (alama 2)
      1. Ndoto moto moto ambazo
      2. kwa pupa yako hangaishi
      3. pupa pumbazi ambayo
      4. badala ya chemichemi Kwanza 2x1
    2. Fafanua maudhui yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
      Ulevi – ya daima kunywa moja bairidi Ubinafsi – kuhasiri watoto ili kuwa Tajiri. Tamaa – tamaa ya utajiri
      Malezi - wazazi kuwapa watoto pesa
      Mapuuza / kutowajibika – wazazi kutowajibikia malezi (4 x 1 = 4)
    3. Fafanua umuhimu wa urudiaji katika shairi hili. (alama 4)
      Kusisitiza – Urudiaji wa maneno
      Kujenga taswira – mfano baina ya mtoto na mzazi – sentensi (2 x 2 = 4)
    4. Bainisha nafsi neni na nafsi nenewa katika shairi hili. (alama 2)
      Nafsi neni – mtetezi wa haki za watoto. Nafsi nenewa – wazazi/walezi
    5. Yanayozungumziwa yanajenga ukuta kwa njia gani. (alama 4)
      Hapana mazungumzo ys ushauri bina ya watoto na wazazi.
      Kulewa kila siku na kukaa kilabuni hadi usiku wa manane hujenga ukuta kwa kuwa wazazi hawapati wakati/muda wa kuwahsughulikia watoto wao. (2 x 2 = 4)
      Zozote mbili
    6. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari. (alama 4)
      Ni hatari inayotelekeza watoto kwa uzoefu wako wa kujiweka mbali na watoto wako. Kila wakati unashinda ulevini hadi usiku wa manane huku unayoyafanya yanajenga kutoelewana/kutoafikiana kati ya watoto na wazazi/walezi.
      SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
  8. Tambua vipera vifuatavyo: (alama 3)
    1. Wewe ni mweusi sana hadi ukibeba mtoto, analala akidhani ni usiku. (vichekesho)
    2. “Kwa nini mnabaguana? Mimi sikuwafundisha kubaguana…” (mawaidha)
    3. …hadi leo jamii hiyo inasadiki kuwa Luanda Magere alikuwa jagina wa kuenziwa. (mighani)
      1. Tegua vitendawili vifuatavyo: (alama 5)
        1. Popoo mbili zavuka mto. (macho)
        2. Pango lenye mawe meupe na mkeka mwekundu. (meno na ulimi)
        3. Naingia ndani ya nyama natoka bila kushiba. (sindano)
        4. Amenifukuza kote kwa blanketi lake jeusi. (giza)
        5. Aliwa yuala, ala aliwa (papa)
      2. Eleza umuhimu wa nyimbo katika utambaji wa ngano. (alama 6)
        1. Husaidia kuondoa ukinaifu/uchovu kutokana na urefu wa hadithi.
        2. Kusisimua hadhira kwa njia ya burudani.
        3. Kuteka makini ya hadhira.
        4. Kuweka mipaka baina ya matukio kwenye hadithi.
        5. Kushirikisha hadhira katika utambaji.
        6. Kuwasilisha mafunzo katika wimbo.
        7. Kurefusha hadithi.
        8. Kusisitiza ujumbe ikiwa unarudiwarudiwa.
        9. Kueleza sifa za wahusika. Zozote 6x1
      3. Ukusanyaji data katika fasihi simulizi huwa na changamoto zipi? (alama 6)
        1. Ukosefu wa utafiti wa kutosha.
        2. Uchache wa wataalamu wa kuitafiti na kuiendeleza.
        3. Ukuaji wa kazi za kimaandishi na hivyo kuondoa haja ya utambaji.
        4. Maendeleo ya kiteknolojia na sayansi yanayotoa njia za kisasa za kujiburudisha.
        5. Baadhi ya watu kuhusisha fasihi simulizi na ukale na hivyo kutoona haja ya kutafiti.
        6. Watu wengi kuhamia mjini na hivyo kufanya urithishaji wake kutowezekana.
        7. Mtaala wa elimu kupuuza lugha za kiasili ambazo huhifadhi na kurithisha fasihi simulizi.
        8. Kwa kuwa inahifadhiwa akilini, anayeihifadhi anaweza kuibadilisha, kutoweka au kufa.
          Zozote 6x1
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest