Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 1


MAAGIZO:

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobaki.
 • Kila insha isipungue Maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa.
 • Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
 1. Wewe ni Kiranja Mkuu Shuleni Juhudi. Umetembelewa na waandishi wa habari kutoka ‘Redio Nipashe’ na ‘KTV’. Wangependa kujua changamoto zilizowakumba wanafunzi wa shule za upili nchini baada ya janga la Korona. Andika mahojiano yenu.
 2. “ Uvumbuzi wa rununu umeleta madhara mengi kuliko manufaa kwa vijana.” Jadili.
 3. Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.
 4. Andika Insha itakayoishia kwa maneno haya … Nilikuwa nimepanda shari nikavuna laana. Nilijuta kwa nini sikumtunza marehemu nyanya yangu.

 MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Hii ni insha ya mtindo/kiuamilifu
  Mtahiniwa azingatie mtindo/sura ya mahojiano (kitamthilia)
  Kuwe na upande wa maswali – waandishi wa habari
  wa majibu – Kiranja Mkuu
  • Izingatie yafuatayo:
   1. Kichwa:
    1. Kionyeshe kuwa ni mahojiano.
    2. Wahusika – Kiranja Mkuu shule ya Juhudi na Waandishi wa habari.
    3. Kiini – changamoto zinazowakumba wanafunzi katika shule za upili.
    4. Mahali pa mahojiano – kwa mfano , Shuleni.
   2. Utangulizi:
    1. Maelezo mafupi kuhusu mahali (mandhari)
    2. Maelezo kuhusu wahusika : mtahiniwa ni Kiranja Mkuu, kisha awatambulishe waandishi wa habari (anaweza kuwapa majina au atumie tarakimu kama vile M.H.1, M.H.2, n.k. Kuwe na makaribisho, salamu na kujitambulisha).
   3. Mwili – Hoja ziibuliwe kwa njia ya mahojiano k.m. KIRANJA MKUU:……MWANDISHI 1:………
    Changamoto ni kama zifuatazo:
    1. Dawa za kulevya / mihadarati
    2. Unywaji / uraibu wa pombe au vileo
    3. Kuwapoteza jamaa wa karibu / kuachwa mayatima
    4. Shinikizo la marika
    5. Wazazi kupoteza kazi
    6. Mimba za mapema
    7. Ndoa za mapema
    8. Dhiki za kisaikolojia k.v
    9. Ukosefu wa karo
   4. Tamati – Mtahiniwa aonyeshe kuwa ametamatisha mahojiano kwa kuonyesha wahusika (Kiranja Mkuu na Waandishi wa habari wakiagana)

  • KUTAHINI
   • Asiyezingatia mtindo/sura wa mahojiano atozwe maki nne sura (-4s)
   • Asipowahusisha wahusika wasiopungua watatu atozwe alama (-2S)

 2. Uvumbuzi wa rununu umeleta madhara mengi kuliko faida / manufaa
  • Mtahiniwa ajadili madhara yanayoletwa na uvumbuzi wa rununu.
  • Swali linalenga madhara yanayosababishwa na rununu.
  • Mwisho atoe maoni yake / awe na msimamo kuhusu swala hili.
   Au
  • Mtahiniwa ajadili madhara na faida za rununu, kisha atoe msimamo wake.

   MADHARA
  • Uwezekano wa kukuza matendo mabaya mf. Udanganyifu
  • Athari za kiafya mf. Kuathiri ubongo, masikio n.k.
  • Athari za maadili / upotovu kwa watoto
  • Wizi wa mitihani-uvivu kwa wanafunzi
  • Uwezekano wa kuvamiwa na wakora ili waibe simu n.k.
  • Kufungwa jela kutokana na arafa za vitisho na matusi.
  • Uraibu unaosababisha uzembe
  • Uhalifu kama vile utapeli wa kiteknolojia.
  • Uraibu wa mikopo ya kiteknolojia

   FAIDA:
  • Kurahisisha mawasiliano
  • Kuharakisha mawasiliano
  • Kurahisisha maingiliano ya jamii
  • Kuwa msingi wa uchumi – biashara/kuweka akiba/mikopo
  • Ubadilishanaji wa pesa (M-pesa n.k)
  • Kujifunza kupitia mtandao
  • Burudani mf. Nyimbo, michezo n.k

 3. Maana ya Methali:
  Ikiwa umekwisha jitayarisha kufanya jambo, basi bora ulikabili / ulifanye na ulimalize.
  • Mtahiniwa aandike kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali.
  • Aonyeshe mtu aliyeanza jambo licha ya vikwazo / matatizo, alijibidiisha kulikamilisha.

 4. Mwanafunzi atunge kisa kinachoonyesha sehemu hizi tatu:
  1. Kisa kionyeshe maovu/ kupuuza nyanya yake
  2. Aonyeshe mabaya yaliyompata baada ya mapuuza.
  3. Aonyeshe mhusika akijuta(majuto) yanayotokana na mapuuza.
   • Sehemu zote tatu zishughulikiwe.
   • Akikosa kuonyesha sehemu zote tatu amepungukiwa kimaudhui.
   • Insha ikadiriwe kulingana na viwango hivi.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest