Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Pavement Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki: yaani; Riwaya, Ushairi na Fasihi simulizi
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

LAZIMA : SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Ngomezi ni nini? (alama 1)
  2. Taja mifano minne ya ngomezi za kisasa (alama 4)
  3. Eleza hasara tano za miviga (alama 5)
  4. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
   Lulu, mwanangu tulia,
   Wewe mtoto lala, mvua imekuja
   Si uongo hata na miti huichangamkia mvua,
   Hakuna haja ya kuelezwa,
   Lulu mwana tulia,
   wewe mtoto lala, mvua imekuja.
   1. Tambua kipera hiki (alama 2)
   2. Taja sifa nne za kipera hiki (alama 4)
   3. Eleza majukumu manne ya kipera hiki (alama 4)

SEHEMU B: CHOZI LA HERI (ASSUMPTA MATEI)

 1. “Sasa huu ni mji mpya kwake.Ametengana nao kwa muda sasa …”
  1. Eleza muktadhawadondoohili (alama4)
  2. Ni masaibu yapi yaliyomkumba mrejelewa alipofika tu mjini? (alama5)
  3. Fafanua sifa za mhusika anayerejelewa (alama5)
  4. Eleza umuhimu wa mrejelewa (al 6)
 2. Tathmini jinsi mwandishi wa riwaya ya Chozi La Heri alivyo faulu katika matumizi ya Taswira na majazi (alama20)

SEHEMU C: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo
Jibuswali la 4 au la 5

 1. “Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao yakufungiwa soko.”
  1. Weka maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua tamathali moja ya usemi katika dondoo hili. (alama 1)
  3. Majeraha yanayouguzwa na wanasagamoyo ni chungu nzima. Kwa kudondoa hoja kumi na tano dhibithisha ukweli wa kauli hii. (alama 15)
   Au
 2. “... kwa mamapima ni raha na maraha. Twasherehekea uhuru.”
  Onyesha kinaya cha maneno yaliyopigiwa mstari ukirejelea hoja ishirini kutoka katika tamthilia ya
  Kigogo. (alama 20)

SEHEMU YA D: TUMBO LISILOSHIBA na hadithi nyingine)

 1. Jadili swala la mikosi maishani ukirejelea hadithi zifuatazo
  1. Nizikeni Papa Hapa (alama 6)
  2. Ndoto ya Mashaka (alama 14)

   Shibeinatumaliza : Salma Omar Hamad
 2. “Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
  3. Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)

SEHEMU YA E – USHAIRI

 1. Soma shairihilikishaujibumaswali.

  Nilikuomba chakula, nawe kweli kaninyima
  Sikuwa hata na hela, kakimbila kwenye dhima
  Megunduwa ewe Shilla, hunijalingi daima.

  Sisahau kisogoni, mnobe ulipokuwa
  Makabadhili nombeni, na ni kwa wema litowa
  Na liba si za mwilini, samani za mtakawa.

  Shilla ya shule sifutu, lo kufanyia hisani
  Dafutari na madutu, sare pia likupeni
  Lini sumbua kuntu, na mie kavumileni

  Kozi na nilikupeni, kulipaka rochuoni
  Ulinisapakamani, mnobeni kabakini
  Asante punda yani, ni matekewa jamani

  Bada ya kazi mwanangu, siku ‘tupa abadani.
  Nilisaka msenangu, lodi rafiki moyoni
  Ka ‘pakazi wanguwangu, hela nyingi kushikeni

  Babayo alifariki, ukiwa bado kiini
  Kiacha bila rafiki, hapohapo pa nyumbani
  Nami amiyo kacheki, na nikakuchukueni

  Waringa kama tausi, wewe Shilla ni kinyonga
  Daraja usilitusi, lo kuvushaengaenga
  Unapofika ofisini, kumbuka kutojitenga

  Maswali
  1. Lipe shairi hili anwani inayofaa. (alama 1)
  2. Bainisha hisani tatu alizofanyiwa nafsi nenewa. (alama 3)
  3. Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
  4. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari. (alama 3)
  5. Taja na ueleze mbinu tatu alizotumia malenga ilikutosheleza mahitaji yake ya kiarudhi.(alama3)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
  7. Fafanua sura ya shairi hili. (alama 3)
  8. Ainisha shairi hili ukizingatia vigezo vifuatavyo: (alama 3)
   1. Mishororo
   2. Migao/ vipande
   3. Vina
  9. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 2)
   1. Dhima
   2. Sifutu
    AU
 2. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
  1. Mkata ni mkatika, harithi hatorithiwa
   Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
   Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
   Mrithi nini wanangu?
  2. Sina ngo’ombe sina mbuzi,sina konde sina buwa
   Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
   Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachiwa
   Mrithi nini wanangu?
  3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa
   Sina chembe ya majazi, mno ni kukamuliwa
   Nakwa’cheni upagazi, mgumu kwenu ku’tuwa
   Mrithi nini wanangu?
  4. Sina sikuacha jina, mkata hatasifiwa
   Hata nifanye la mana, mno ni kulaumiwa
   Poleni wanangu sana, sina kwenu cha kutowa
   Mrithi nini wanangu?
  5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa
   Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
   Sina wanangu mi sana, la kwacha na kuraduwa
   Mrithi nini wanangu?
  6. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa
   Nyuma yangu ila dhiki, na mbele imekaliwa
   N’na wana na mikiki, hadi n’tapofukiwa
   Mrithi nini wanangu?
  7. Sinai la kesho kwenu,wenyewe kuiongowa
   Muwane kwa nyingi,mbinu mwende pasi kupuwa
   Leo siyo, keshoyenu,kama mutajikamuwa
   Mrithi nini wanangu?
   (Kina cha maisha A.S.Mohammed)
   MASWALI
   1. Eleza hali ya mzungumzaji katika shairi hili ( alama 4)
   2. Eleza dhamira kuu ya mshairi kulitunga shairi hili (alama 2)
   3. Ni nani anayezungumziwa na nafsi neni katika shairi hili? (alama 2)
   4. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
   5. Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika shairi hili (alama 3)
   6. Tambua bahari ya shairi hili ukizingatia. (alama4)
    1. Mizani
    2. Vina
   7. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya tutumbi. (alama 3)


MARKING SCHEME

SEHEMU A : FASIHI

 1.  
  1. NGOMEZI ni sanaa ya ngoma
   Ni aina ya fasihi ambayo hutumia milio ya ngoma badala ya mdoma
  2. Ngomezi za kisasa
   • Kengele za milangoni
   • Milio kwenye ambulensi
   • Toni katika rununu
   • Kamsa kwenye magari ya polisi
   • Honi za gari
   • Ving’ora(vya usalama) NK 4x1
  3. Eleza hasara tano za miviga (alama 5)
   • Baadhi ya miviga huhatarisha Maisha ya wanajamii km kurithi mke wa mtu aliyeaga,kutiwa, unyagoni
   • Baadhi ya miviga hukinza malengo ya kitaifa km ukeketaji wa Watoto wa kike ni ukiukaji wa haki za binadamu
   • Hujaza watu hofu km miviga inayohitaji kafara ya binadamu au sherehe za kufukuza mapepo huhofisha
   • Baadhi ya miviga huhusisha ushirikina km mazishi katika jamii nyingine..Hili huweza kusababisha uhasama katika baadhi ya koo
   • Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa au mali.Hili huiacha familia katika hali duni kiuchumi km sherehe za kuomboleza katika baadhi ya jamii 5x1
  4.  
   1. Kipera- Bembea/Bembezi/Bembelezi 1x2
   2. Sifa za Bembea
    • Huimbwa taratibu kwa sauti na mahadhi ya chini
    • Huwa fupi
    • Huimbwa na wazazi au walezi wa watoto kuwaliwaza ili watoto wanyamaze au walale
    • Hutofaitiana kutoka jamii moja hadi nyingine kulingana na thamani za jamii hiyo
    • Hurudiwarudiwa maneno au kibwagizo
    • Hutumia lugha shawishi na wakati mwingine ahadi hutolewa
   3. Majukumu ya Bembea
    • Hutumbuiza na kuongoa watoto
    • Hutumiwa kama sifo kumsifu mtoto ambaye ni mtulivu
    • Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika
    • Husawiri mahusiano katika jamii
    • Hutakasa hisia ambazo mwimbaji huweza kuwa nazo
    • Humwelimisha mtoto katika umri mchanga (alama 4x1)

SEHEMU B : CHOZI LA HERI

 1.  
  1. Haya ni maneno ya mwandishi yakimrejelea Umu(Umulkheri)Umu alikuwa amefika tu asubuhi kwa gari moshi katika jiji la Karaha .Alikuwa ametoka kwao Mlima wa Simba baada ya wanuna wake. kutoroshwa na Sauna kijakazi wao.
  2. Masaibu yaliyomkumba Umu alipofika tu jijini (alama 5)
   • Alitafunwa na njaa
   • Alihisi baridi kali
   • Woga mkuu ulimsumbua maana hakulijua jiji vizuri
   • Hakujua iwapo angepata msaada na jinsi angeanza Maisha yake upya
   • Alihisi upweke mwingi maana hakujua yeyote 5x1
  3. SIFA ZA UMU 9al5)
   • Mwajibikaji -alienda kuripoti kutoroshwa kwa wanuna wake katika kituo cha polisi
   • Mwenye utu-alimpa kijana ombaomba shilingi 200
   • Msomi alitia bidii masomoni hadi akapata shahada ya uhandisi
   • Mwenye busara-hata anapogundua na kuhisi kuwa askari walimwuliza maswali ya kijinga(km walivaa mavazi gani ilihali walipotoroshwa hakuwaona) hakuonyesha kuudhika bali aliwajibu kwa unyenyekevu
   • Pia aliamua kutowaambia askari wale kuwa hakuwa na wazazi maana walidhihirisha ukatili mwingi.
   • Mwadilifu-baada ya taswira ya majanadume yakimtumia madanguroni kumpitia akilini aliamua angejidumishia heshima na uadilifu
   • Mcha Mungu-aliandamana na wazazi wake jumapili kwenda kanisani kwa ibada . Pia anawaombea wazazi wao malipo kutoka kwa Mungu kwa ajili ya wema wao
   • Mwenye Kumbukizi- kibao kilichoandikwa “Church Road “ kilimkumbushsha aliwahi kupitia hapo na kutoa msaada kwa ombaomba Fulani. Pia alikumbuka mamake akikataa kumpa shilingi mia ili ampe ombaomba
   • Mwenye Imani- alimwahidi Dick angewalea baada ya mama yao kutoweka
   • Mwenye mapenzi ya dhati – aliwapenda ndugu zake Dick na Mwaliko sana na alisikitika sana alipowakosa .Aliwapenda wazazi wake Mwangeka na Apondi
   • Mwenye shukrani- anawashukuru wazazi wake wa kupanga kwa kumlea na kumfadhili kwa kila hali.pia kwa kumchukyua Dick Anashukuru Mwangemi kwa kumlea Mwaliko
   • Mtani – anamkosoa mwangeka kuwa alikuwa amesahau kuna mhandisi mwingine katika familia yao(Engineer Umulkheri)
   • Mshauri 5x1
  4. UMUHIMU WA UMU (alama5)
   • Ni kielelezo cha Watoto wanaochukua usukani wa kuiongoza familia pindi tu wazazi wanapoondoka
   • Ni mfano wa Watoto ambao huwa wame wajibika anaulizia wanuna wake kwa majirani na hatimaye anapowakosa anapiga ripoti kwenye kituo cha polisi .
   • Ni kielelezo cha wasichana wanaokata auli kuwa waadilifu maishani.
   • Ni kielelezo cha watu wenye utu tofauti na Naomi anaahidi nduguze kuwa angewalea kwa mikono yake midogo, , ALIMFAA OMBAOMBA
   • Ametumiwa kufunza jamii kuwa na shukrani
   • Ni kielelezo cha vijana ambao wanawezakutumiwa kushauri na kuwaelekeza wengine- aliwashauri Sophie na Dick maishani.
   • Ni kielelezo cha watu ambao hawakati tamaa maishani
   • Ametumika kuwapa tumaini Watoto wanaopitia changamoto maishani kuwa hawatateseka milele km wanaotoka kwa familia zilizovunjika,mayatima kwenye vituo vya mayatima,,wanaorandaranda mitaani 5x1
 2. TASWIRA YA MAJAZI
  • Taswira ya watu wakingangania petruli kutoka kwa lori lililokuwa limeanguka barabarani
  • Msomaji pia anaweza kupata taswira ya mlipuko wa moto na watu kulia wakichomeka na kuangamia katika moto huo
  • Kuna taswira ya jinsi maombolezi na maziko ya Dede yalivyofanyika.km kuimba , kulia, kuzunguka nyumba na jeneza.
  • Msomaji pia anaweza kupata taswira ya Watoto wanaoigiza maombolezi ya Dedejeneza likiwa boksi na maiti ni mwanasesere
  • Taswira ya Ridhaa akitoa mshipi kiunoni na kumcharaza Mwangeka kwa hasira .
  • Taswira ya mwanafunzi aliyevaa sare(Lunga) mbele ya gwaride akitoa hotuba kwa walimu na waafunzi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira .
  • Picha ya makabiliano ya polisi na wakazi wa msitu wa mamba walioandamana wakipinga kuondolewa kwao huko.
  • Taswira ya Umu akiongea na askari wajeuri katika kituo cha ppolisi katikaumri wake mdogo
  • Taswira ya Umu akimsihi mamake ampe mia moja kisha anatoa pesa mfukoni mwa dangarizi yake na kumkabidhiombaomba na mazungumzo yao
  • Taswira ya kundi kubwa la vijana wa mtaani wakiwa mbele ya hoteli.Ni wachafu,macho mekundu,gundi mikononi nk
  • Taswira ya majonzi ya mama na wanawe wakiuzika mwili wa mtoto mdogo kichakani(mamake Kairu)
  • Taswira ya zohali akiwa ameangukia wazazi wake miguuni sebuleni na kuwaomba msamaha.
  • Picha ya nyumba ya bwana Tenge . Ndio sebule ,jiko na malazi…
  • Taswira ya mwalimu Dhahabu akisikiliza masikitiko ya UMU.anamhurumia Umu nusura amkumbatie.
  • Taswira ya Watoto watatu wanaoogelea na kucheza kidimbwini nao wazazi wao wameketi nje ya nyumba wakiwatazama(familia ya Apondi na Mwangeka)
  • Taswira ya Apondi akihutubia hadhira makini mno
  • Picha ya Lemi akipigwa na kuteketezwa na umati
  • Taswira ya jinsi Dick alimkimbilia Um una kwa sauti akimwita kwa jina.
  • Taswira ya Shamsikavaa koti kuukuu liloinama upande mmoja akiwa ameshikilia chupa mkononi
  • Picha ya wauguzi wawili wanaozunguka kwa wadi Selume na Meko.
  • Taswira ya Fungo,jitu nene lilotoa harufu mbaya
  • Taswira ya Sauna akifungua mlango uliobishwa na polisi

SEHEMU C :KIGOGO

 1.  
  1. Muktadha wa dondoo.
   • Msemaji: Ngurumo
   • Msemewa: Sudi
   • Mahali: Mangweni
   • Sababu: Ngurumo anaongea kuhusu vijana wengi waliokuwa wanashiriki ulevi mle kilabuni mwa Asiya.
  2. Tamathali moja ya usemi.
   • Jazanda - Majeraha.
  3. Majeraha yanayouguzwa na wanasagamoyo.
   • Wanyonge wanalipa kodi na ilhali soko halisafishwi.
   • Unyakuzi wa mali ya umma. Sudi anasema kwamba wamepokwa kiliicho chao.
   • Ubaguzi. Kandarasi kutolewa kwa vikaragosi. Asiya anapewa kandarasi ya kuoka keki kwa vile Boza ni kikaragosi cha Majoka.
   • Matumizi mabaya ya pesa za umma. Pesa kutumiwa kukichonga kinyago cha Ngao.
   • Mauaji. Jabali anauwawa.
   • Kupigwa. Ashua anapigwa gerezani. Tunu analemazwa.
   • Unyanyasaji wa kijinsia. Majoka kumdhalilisha mkewe mbele ya Ashua. Anasema mwanamke ni mwanamke.
   • Matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Polisi kuwatawanya waandamanaji.
   • Wafanyakazi katika kampuni ya Majoka kutokuwa na bima.
   • Soko kufungwa bila kuwazia hali ya maisha ya wanyonge.
   • Uharibifu wa mali ya umma. Vibanda vya wauzaji kubomolewa.
   • Uharibifu wa mazingira. Majitaka kuelekezwa wanakofanyia kazi akina Sudi.
   • Unyonyaji. Kupandishwa kwa bei ya bidhaa katika kioski cha kampuni.
   • Ukosefu wa ajira. Sudi na Ashua wanalazimika kufanya kazi za kujidhalilisha hali wamehitimu shahada.
   • Kuwapitishia wanyonge kwenye dhiki za kisaikolojia. Majoka anamsimanga Ashua anapokwenda kumwomba usaidizi.
   • Majoka kuwaangamiza wanafunzi kwenye academy yake. Wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana dawa.
   • Majoka kumwita Ashua ofisini ili amfumanishe na mkewe.
   • Kuwaangamiza wapinzani. Majoka kumfungia Ashua kwa kisingizio cha kuzua vurugu kwenye ofisi ya umma.
   • Serikali kuidhinisha uuzaji wa pombe haramu mamapima anasema amepewa kibali na serikari.
   • Kuwanyima wanyonge haki ya kuandamana. Wanatangaza kuwa maandamano ni haramu.
   • Ubaguzi. Vituo vya kurekebishia tabia kuwa na seli spesheli k.v. ya mke wa majoka na Ashua.
   • Viongozi kutowahakikishia raia huduma za kimsingi kama vile maji ilhali kwa viongozi kuna visima.
   • Kufungisha kituo cha runinga cha Mzalendo.
   • (Kuongeza walimu na wauguzi mshahara na kuongeza kodi zaidi.
   • Ufunguzi wa biasharaya ukataji miti ilhali mito inakauka na kuleta ukosefu wa maji.
   • Viongozi wanatishia kuwafurusha baadhi ya wanasagamoyo kwa kusambaza vijikaratasi.
 2. Kinaya cha maneno yaliyopigiwa mstari.
  • Uchafuzi wa mazingira - majitaka kuelekezwa wanakofanyia kazi wanyonge.
  • Kusherehekea mwezi mzima uhuru badala ya kufanya kazi.
  • Kupujua thamani ya elimu na kutobuni nafasi za kazi. Vijana wanahitimu chuoni na kufanya kazi duni k.v kuchonga vinyago.
  • Wanyonge kufungiwa soko la Chapakazi.
  • Maandamano kukabiliwa kikatili - Polisi kuwatawanya kwa risasi.
  • Wafanyikazi katika kampuni ya Majoka hawana bima ya afya.
  • Kuendeleza ubaguzi - watu kupata uongozi kutokana na ukoo. Ngao Junior anatarajiwa kurithishwa uongozi na Majoka.
  • Mwanamke kutopewa nafasi ya uongozi. Majoka anapinga Tunu.
  • Unyanyasaji wa kijinsia - Majoka kumdharau mkewe kwa kumwita mwanamke.
  • Kuwaangamiza wapiganiaji haki. Jabali anauwawa.
  • Majoka kuvipagaza vizazi vya kesho deni kutoka kwa wafadhili. Anatumia msaada huo kuchonga sanamu.
  • Kuwatelekeza vijana kwenye matumizi mabaya ya vileo - Shuleni vijana wanadungana dawa na kuwa makabeji.
  • Kuwapiga na kuwaumiza wapigania haki. k.v Tunu
  • Kuongeza mshahara na hapo hapo kuongeza kodi ya walimu na wauguzi.
  • Kupandishwa bei ya chakula katika kioski cha kampuni.
  • Wanasagamoyo kulipa kodi na hali soko halisafishwi.
  • Kuwarithisha mbinu hasi za uongozi k.v matumizi ya hongo Majoka anamgawia Kenga ardhi.
  • Uharibifu wa mazingira mfano ukataji miti.
  • Serikali kutoa kibali cha kuuza pombe haramu kwa Asiya.
  • Baadhi ya raia wanalazimika kula uroda ili wapewe kandarasi ya kuoka keki k.v. Asiya.
  • Baadhi ya wanasagamoyo wanatishiwa wahame kwa kutupiwa vijikaratasi.

SEHEMU D: TUMBO LISILOSHIBA

 1.  
  1. MIKOSI MSISHANI -NIZIKENI PAPA HAPA
   • Otii alivunjika mguu wake akichezea timu ya Bandari FC
   • Licha ya sifa kemkem alizoletea taifa lake alitelekezwa na maofisawasimamizi wa timu hizi
   • Otii alipopata nafuu alikosa kazi bora ya kufanya akarejelea kazi yake duni katika Halmashauri ya bandari
   • iliyokuwa na malipo duni
   • Mkosi wa kukutana na mpenzi mnafiki na kuambukizwa UKIMWI naye- Rehema Wanjiru
   • Marafiki wake walitayarisha mazishi yake akiwa hai huku akiwasikia
   • Hata baada ya kifo mkosi wa ajali ulimwaandama – Mtito Andei
   • Otii aliugua maradhi yasiyo na tiba. Madaktari walimkaaa hospitalini wakasema arejeshwe nyumbani.
  2. NDOTO YA MASHAKA
   • Mamake Mashaka alifariki tu baada ya kumzaa
   • Babake Mashaka naye alifariki muda mfupi tu baada ya mkewe kufa . Mashaka akawa yatima
   • Mamake mlezi naye Biti Kidebe daima alikuwa na maumivu ya mguu hivyo ilibidi waleane .
   • Mashaka alikulia mazingira magumu ya kufanya kazi za kijungu meko km kufua, kufyeka nk
   • Licha ya bidii yao knna wakati walikosa ikamlazimu Kidebe atumie akiba ndogo aliyokuwa nayo
   • Baada yakufiwa na wazazi,anaambulia mlezi maskini .walilima vishamba vya kupewa
   • Mkosi wa kufiwa na mama mlezi -kidebe-baada ya kumaliza 8
   • Mashaka alifungishwa ndoa ya mkeka na mzee Rubeya-hakuwa tayari
   • Mkosi wa kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa ajili ya umaskini -wantorokea Yemeni kuondokea aibu ati.
   • Walipooana Mashaka anasema ni kama ndoa yao iliingia nuksi moja kwa moja. Wanaendelea kuishi katika
    chumba kile kile kimoja pamoja Watoto wao kwani hawangeweza kuhamia chumba kingine (fedha)
   • Familia ya Masaka ilishi katika mtaa usiokuwa na mpangilio. Chumba chao kilikuwa karibu na choo cha jirani kilijaza uvundo kwao.Udhia ulizidi maradufu wakati wa mvua
   • Mkosi wa paa lao kuvuja nyakati za mvua.
   • Mkosi wa kupata pacha mara 3 wakaishia kuwa na Watoto wengi (7) . hawatoshelezi malazi hivyo anaombea wavulana mahali jikoni kwa jirani
   • Msahara alopewa na kampuni ya ZWS ulikuwa mdogo sana. Haungemwezesha kununua samani na hata angenunua hangepata pa kuweka
   • Mkewe Waridi alimtoroka,akaenda na Watoto wote bila taarifa
   • Ni mkosi kwamba mambo ya Mashka yanatengenea ndotoni tu.Anapoamka anajipata katika mashaka yale yale na Maisha yale duni tu. 14x1
 2. DONDOO
  1.  
   • Maneno haya yanasemwa na Mbura
   • alikuwa anazungumza na Sasa
   • walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa na mzee Mambo
   • walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ 4 x 1 = 4
  2. Sifa za Mbura
   • ni mzalendo - anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo
   • mwenye tamaa - anajaza sahani kwa chakula na kukila chote
   • mwenye utu - anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao
   • ni fisadi - amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali
   • mzembe - baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini
   • mletezi wa haki 
    • mvumilivu
    • mpyoro
    • msema kweli zozote 6 x 1 = 6
  3. Jinsi viongozi walivyo wabadhirifu
   • hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya umma
   • sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu
   • viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi - magari ya serikali
   • raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii
   • DJ na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katika kama hizi
   • viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kuzitolea jasho kamwe
   • upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu wa raslimali za umma
   • Mbura ana Sasa wanaendeleza ubadhirifu pale wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee Mambo
   • kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta tofauti za umma
   • vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi
    zozote 10 x 1 = 10

SEHEMU E: Ushairi

 1. Majibu ya maswali
  1. Anwani – Shilla / hisani (alama 1)
  2. Hisani tatu
   1. Kumpa au kumtafutia nguo/ mavazi
   2. Kumlipia karo, sare ya shule, daftari nk
   3. Kulipa karo ya chuoni hadi akabaki maskini
   4. Alimtafutia kazi – alilipa kumtafutia kazi
   5. Alimsaidia wakati alikosa yeyote wa kumfaa baba alipofariki (za kwanza 3 x 1 = 3)
  3. Nafsineni– Ami wa Shilla (alama 1)
  4. Lugha nathari. -
   • Malenga / nafsineni/ ami anamkumbusha Shilla na kumhimiza kuwa asisahau umaskini aliokuwa nao hapo zamani/ na jinsi alivyosaidiwa na malenga/ kwa nguo (mavazi) na samani mbalimbali liyomfaa. (3 x 1 = 3)
  5. Uhuru wa mshairi
   1. Inksari – kaninyima, kakimbilia, megunduwa, sisahau, litowa, lokufanyia, likupeni, linusumbua, siku’tupa, bada, ka’pa, lokuvusha
   2. Mazda/ mazida – hunijalingi, nilikupeni, nikabakini
   3. Udodoshaji – asante punda
   4. Tabdila – dafutari
   5. Utohozi – kozi (za kwanza 3 x 1 = 3)
  6. Toni – uchungu/ masikitiko (alama 1)
  7. Sura ya shairi
   1. Beti - Shairi lina beti 7
   2. Mishororo - Kila ubeti una mishororo mitatu
   3. Migao - Kila mshororo una migao/ vipande miwili
   4. Mizani - Kila mgao una mizani -8 -8 = 16
   5. Vina – kila ubeti una vina vyake. Kwa mfano, ubeti 1 ni – la – ma. Wa pili ni – ni – wa.
   6. Mshororo wa mwisho. Mshororo wa mwisho wa kila ubeti ni tofauti: ubeti wa kwa ni “Megunduwa ewe Shilla, hunijalingi daima.” Wa pili “Na libasi za mwilini, samani za mtakawa.”nk (zozote 3 x 1 = 3)
  8. Ainisha
   1. Mishororo – tathilitha
   2. Migao – mathnawi
   3. Vina – ukara (3 x 1 = 3)
  9. Maana ya maneno (2 x 1 = 2)
   1. Dhima – usaidizi
   2. Sifutu -sikusahau
 2. Ushari 2
  1. Hali yamzungumzaji. (alama 4)
   • maisha yenye umaskini mkubwa.
   • maisha yasiyo kuwa na matumaini.
   • maisha yaliyo kosa thamani.
   • maisha yenye kusikitisha.
  2. Dhamira kuu ya mshairi (alama 2)
   • kuwahimiza wanawe maishani ili kuhakikisha maisha mema ya baadaye kwa vile hali ya sasa ni ya kimaskini.
  3. mzungumziwa – watoto (alama 1)
   nafsi neni – mzazi (alama 1)
  4. toni ya shairi (alama 2)
   • masikitiko
   • kutamauka/kukosa matumaini
   • ya kuhuzunisha
  5. mbinu tatu za lugha zilizotumika. (alama 3)
   • sitiari – mkatanimkatika
   • Balagha – mrithininiwanangu?
   • takriri – sina
  6. Bahari ya shairi ukizingatia. (alama 4)
   1. mizani – msuko
   2. vina - ukara
  7. Ubeti wa mwisho – lugha ya nathari. (alama 3)
   • mshairi ana matumaini kwamba wanawe wataimarisha maisha yao ya baadaye .Anawashauri wafanye bidii, wakabiliane na matatizo bila hofu.

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Pavement Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest