Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika insha mbili.
  2. Insha ya kwanza in ya LAZIMA.
  3. Andika insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizosalia.
  4. Kila insha isipungue maneno 400.
  5. Kila insha iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. (LAZIMA)
    Andika tahariri kwa gazeti la Alwodo ukieleza sababu za watoto wengi nchini Kenya kuingilia ajira za mapema na kuacha masomo ya sekondari. (al.20)
  2. Matumizi ya tarakilishi katika shule za misingi na za upili yana uzuri na ubaya wake. Jadili. (al.20)
  3. Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ‘Cha mwenzako kikinyolewa chako kitiie maji’ (al.20)
  4. Adika insha itakayomalizia kwa: Nilijitazama na kujidharau kwa nini sikuwafahamisha walimu jambo hilo mapema. (al.20)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

Swali la kwanza
Tahariri kwa gazeti la Alwodo

  1. Sura
    • Iwe na kichwa cha gazeti
    • Iwe na terehe
    • I we na utangulizi.
    • I we na mwili/maelezo kiaya
    • Inaweza kutoa maoni au msimamo wa mhariri
  2. maudhui
    • Umaskini unafanya wengi kukosa mahitaji ya kimsingi
    • Uyatima – Kufiwa na mzazi na kuwachwa bila wa kutegemewa.
    • Mazingira magumu shuleni kama vile adhabu kali ambayo husababisha wao kuwacha masomokujiunga na ajira.
    • Shirikizo la rika kuwashawishi wajiunge na ajira za mapema.
    • Matumizi ya dawa za kulevya ambazo huchochea mahitaji ya kununua dawa hizi na kuwafanya wanafunzi watafute ajira za mapema.
    • Kushawishiwa na waajiri kwa sababu ajira ya watoto ni nafuu ikilinganishwa nay a watu wazima.
    • Ufisadi – waajiri wa watoto kutochukuliwa hatua na waliopewa jukumu.
    • Changamoto za shule kuwa mbali na kuwavunja watoto moyo wa kuendelea na masomo.
    • Wazazi wenye uwezo mdogo wa kifedha hutumia wato wao kufanya kazi.
    • Watoto kutolalamika kutokana na unyonge wao
    • Hufanya waajiri kuwapendelea
    • Kadiria hoja za mtahiniwa.

SWALI LA PILI

  1. Hii ni insha ya mjadala.
  2. Mtahiniwa ajadili pande zote mbili kasha aonyeshe msimamo wake.
  3. Mtahiniwa akiegemea upande mmoja allama zisizidi kumi.
  4. Atakayekosa kutoa msimamo alama za sura ziondolewe(-45)

Uzuri/Manufaa

  1. Tarakilishi imerahisisha utafti miongoni mwa wanafunzi.
  2. Baadhi zinaweza kuhifadhi umeme.
  3. Baadhi zinaweza kutumiwa mahali popote
  4. Zinapunguza gharama ya kununua vitabu vya kiada.
  5. Wafunzi wanaweza kutumia wakati wowote bilauwepo wa mwalimu.
  6. Huhifadhi ujumbe mpana.
  7. Inawapa wanafunzi ujuzi wa kutumia teknologia kwa mawanda.

Hasara

  1. Ina gharama ya juu kununua na kutunza .
  2. Inapotosha kimaadili kwani baadhi watatazama mambo mengine ya kupotosha.
  3. Baadhi ya wafunzi na wqalimu hawajui kutumia tarakilishi.
  4. Inahitaji nguvu za umeme na kuna baadhi ya sehemu ambazo hazina nuvu za umeme
  5. Inadhuni kiafya kwa kuathiri macho na hata mgongo kukaa kwa muda mrefu
  6. Ni vigumu kwa wale walio na kasoro ya kuona.
  7. TANBIHI
    Atakayezingatia hasara /uzuri atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Asipite kiwango cha C +
    (09-10)

Swali la tatu (mwongozo)
Hii ni insha ya methali ambapo kisa lazima kithibitishe ukweli wa methali
Maana
Anayecheka wenginewalio na tatizo lolote utafika wakati wake na atapatwa na tatizo sawia.

Matumizi

  1. Hutumika kutahadharisha wale wanaocheka wenzao wanapokuwa na janga, kwani wakati wao utafika.
  2. Kisa kionyeshe hali ambapo mtu alisherehekea wakati wenzake walikuwa na shida nae kapatwa na shida hio hio.
    Tathmini haya;

Kisa kinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:

  1. Mtu asherehekea mwenzake akifiwa na baadaye pia afiwe.
  2. Mwanafunzi amcheke.
  3. Tajiri amcheke maskini kisha mali yakeipotee baadaye awe maskini.
  4. Mtu mzima amudhihaki mgonjwa naye apatwe na ugonjwa baadaye.

Tanbihi

  1. Lazima kisa kitoe pande mbili za methali.
    1. Kucheka kilema
    2. Kilema kumpata
      Atakayezingatia upande mmoja tu amepungukiwa maudhui asipite lama (C wastani)
  2. Atakayetunga kisa lakini kisidhihirishe ukweli wa methali anupunguvu wa kimtindo aadhibiwe kimutindo
  3. Atakayekosa kutunga kisa yaani atumie mifano tu achukuliwe kama aliyepotokwa kimaudhui na awekwe katika kiwa cha D 03/20.
  4. Si lazima mtahiniwa aeleze maana ya methali.

Swali la nne

  1. Hii ni insha ya mdokezo ambapo mtahiniwa lazima aanze kwa mdokezo aliopewa.
  2. Kisa cha mtahiniwa sharti kikamilike kwa huu mdokezo.

Jibu

  1. Yawezekana uwe ni mkasa wa moto shuleni.
  2. Au uvamizi uliofanyika.
  3. Au wizi ulifanyika wa mtihani au chochote kile kisha anajutia kwa sababu alifahamu jambo hilo.
  4. Kutekwa nyara (miongoni mwa mambo mengine)

Tanbihi

  1. Insha zote lazima zitimize urefu uliokusudiwa. Upungufu wowote utashughulikiwa kulingana na mwongozo wa kudumu.
  2. Insha zote (2, 3 na 4) lazima ziwe na vichwa . Mtahiniwa akiacha achukuliwe kuwa amepungukiwa kimtindo.
  3. Mtahiniwa lazima asome kwa makini mtungo wa mtahiniwa akizingatia mada na matumizi ya miongozo miwili yaani, wa maswali na viwango ili kuweka insha ya mwanafunzi katika kiwango chake.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest