Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - 2021 KCSE Eldoret Diocese Mock Exams

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO

 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani Tamthilia,Hadithi Fupi,Ushairi na Fasihi Simulizi.
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja

SEHEMU A: LAZIMA
Assumpta K. Matei: Chozi la heri

 1. “Hili lilimtia …………. uchungu, akajiona kama aliyedhalilishwa na mwanamke.”
  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
  2. Taja suala linalodokezwa katika dondoo hili (alama 1)
  3. Kwa kutumia hoja kumi na tano, eleza namna suala ulilolitaja hapo juu 1 (b) linalijitokeza (Alm 15)

SEHEMU YA B
Tamthilia Kigogo na Pauline Kea.
Jibu swali la 2 au 3

 1. Kwa kurejelea tamthlia ya 'Kigogo na Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa. (alama 20)
 2. “Mimi ni mtu wa vitendo, si vishindo,”
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Kwa kurejelea dondoo hili, eleza sifa mbili za msemaji. (alama 4)
  3. Thibitisha ukweli wa kauli ya msemaji. (alama 12)

SEHEMU YA C
HADITHI FUPI: TUMBO LISILISHIBA.
Jibu swali la 4 au 5

 1. Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo na shogake dada ana ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana. (al.20)
 2. Mame Bakari
  “Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Unaogopa nini?”
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (al.4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. (al.2)
  3. Eleza sifa za mrejelewa. (al.6)
  4. Eleza umuhimu wa msemaji. (al.4)
  5. Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. (al.1)
  6. Fafanua maudhui katika swali la (e) kwa kurejelea hadithi nzima. (al.3)

SEHEMU D ; USHAIRI A

 1.       MWANA
  1. Kwani mamangu u ng’ombe, au u punda wa dobi ?
   Nakuuliza usambe, nayavunja madhehebi
   Nalia chozi kikombe, uchungu wanisibabi
   Hebu nambie
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?
   MAMA
  2. Nang’ona mwana nang’ona, sitafute angamiyo
   Sinipe kuja sonona, kwa uchungu na kiliyo
   Babayo mkali sana, kubwa pigo la babayo
   Kwani kelele kunena, huyataki maishayo ?
   Hilo nakwambia.
   MWANA
  3. Sitasakamwa. Kauli, nikaumiza umiyo
   Nikabeba idhilali, nikautweza na moyo
   Siuvuwati ukweli, hazidisha gugumiyo
   Baba hafanyi halali, huachi vumiliyo
   Hebu nambie.
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?

   Nambie ipi sababu, ya pweke kwenda kondeni
   Nini yako matulubu, kulima hadi jioni ?
   Na jembe ukudhurubu, ukilitua guguni
   Yu wapi wako muhibu, Baba kwani simuoni?
   Hebu nambie.
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?

   Baba kwani simuoni, kuelekea shambani?
   Kutwa akaa nyumbani, na gumzo mitaani.
   Hajali hakudhamini, wala haoni huzuni.
   Mwisho wa haya ni nini ? ewe mama wa imani ?
   Hebu nambie.
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?

   Na kule kondeni kwako, ukate kuni kwa shoka
   Ufunge mzigo wako, utosini kujitwika
   Kwa haraka uje zako, chakula upate pika
   Ukichelewa vituko, baba anakutandika
   Hebu nambie.
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?

   Chakula kilicho ndani, ni jasho lako hakika
   Kiishapo u mbioni, wapiti kupokapoka
   Urudi nje mekoni, uanze kushughulika
   Ukikosa kisirani, moto nyumbani wawaka
   Hebu nambie.
   Kweli jaza ya kiumbe, ni madhila na mapigo ?
   MAMA
   Wanitonesha kidonda, cha miaka na miaka
   Usidhani nayapenda, madhila pia mashaka
   Nakerwa na yake inda, na sasa nimeshachoka
   Ninaanza kijipanga, kwa mapambano hakika
   Hilo nakwambia

   MASWALI
   1. Mtunzi wa shairi hili alikuwa na dhaimira gani katika kutunga shairi hili (al. 2)
   2. Shairi hili ni la aina gani. Toa ithibati (al. 2)
   3. Yataje mambo yoyote matano anayolalamikia mwana (al. 5)
   4. Eleza kanuni zilizotumika kasarifu ubeti wa tatu (al.5)
   5. Andika ubeti wa saba kwa lugha tutumbi (al. 4
   6. Eleza maana haya yaliyotumika katika shairi hili
    1. Jaza (al. 1)
    2. Muhibu (al. 1)

 2. SHAIRI B
  Soma shairi hili kisaha ujibu maswali
  1. Punda kalibebe gari, gari limebeba punda.
   Mwalimu ana pakari, muashi vyuma adunda
   Jaji gonga msumari, sonara osha vidonda
   Kinyume mbele.

  2. Saramala ahubiti, muhunzi tiba apenda
   Mganga anabiri, baharini anakwenda
   Hata fundi wa magari, anatomea vibanda
   Kinyume mbele

  3. Wakili anahiyari, biashara kuitenda
   Mtazame askari, akazakaza kitanda,
   Mkulima mashuhuri, jembe limemshinda
   Kinyume mbele

  4. Apakasa daktari, ukili anaupinda
   Seveya kawa jabari, mawe anafundafunda,
   Hazini wa utajiri, mali yote aiponda,
   Kinyume mbele

  5. Msemi huwa hasemi, wa inda hafanyi inda
   Fahali hawasimami, wanene walishakonda
   Walojitia utemi, maisha yamewavunda
   Kinyume mbele

  6. Kiwapi cha kukadiri, twavuna shinda kwa shinda
   Tele haitakadiri, huvia tulivyopanda
   Mipango nmehajiri, la kunyooka hupinda
   Kinyume mbele

   MASWALI
   1. Mtunzi aliuwa na malengo gani alipotunga shairi hili? (al. 3)
   2. Licha ya tarbia, eleza bahari nyingine zinazojitokeza katika shairi hili. (al. 4)
   3. Eleza namna mtunzi alivyotumia uhuru wake. (al. 5)
   4. Ni mbinu gani inayotawala shairi hili? (al. 2)
   5. Uandike ubeti wa nne katika lugha nathari (al. 4)
   6. Eleza toni ya shairi hili (al. 2)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

  Mimi ni morani
  Nguli aliyekamilika
  Nishatoka kumrarua simba dume
  Kwa hii mikono miwili
  Mimi ni shujaa asiyekanyanga kwa woga
  Wala kubabaika
  Simba mwenyewe ameungama
  Mkuki wangu ni shahidi.

  Mimi ni Jabali mtetemesha ardhi
  Azma yangu hairudi nyuma
  Nguvu zangu hazimithiliki
  Sina mzaha wala dhihaka
  Mimi ni jasiri
  Ngao ndio hii hapa mkononi ni Fumo nilirithi
  Kujikinga na kulinda hadhi yangu
  Yu wapi mwingine shujaa?

  Maswali.
  1.          
   1. Andika aina ya sifo hii. (alama 1)
   2. Toa sababu nne kuthibitisha jibu lako la (i) hapo juu. (alama 2)
   3. Tambua mbinu mbili la lugha zilizotumiwa katika utungo huu. (alama 2)
  2.    
   1. Eleza sifa saba za utungo huu. (alama 7)
   2. Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii nyingi. Fafanua kwa hoja nane sababu za hali hii. (alama 8)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1.        
  1. maelezo ya mwandishi
   • Anamrejelea Bwana Kimbaumbau
   • Ni baada ya Sauna kukataa kushiriki mapenzi naye
   • Wote wawili walikuwa Kazini
  2. Ubabedume/ Taasubi ya kiume
  3.                  
   • Jamaa za Kangata kupinga elimu ya mabinti zake
   • Kimbaumbau kumdhulumu Naomi anapokataa kujihusisha kimapenzi naye.
   • Mwimo Msubili kutotaka kukutana na mwanamke asubuhi kwa madai kuwa ni Mkosi.
   • Lime na Mwanaheri kunajisiwa na vijana wahuni.
   • Bwana Maya anamdhulumu mamake Sauna kwa mapigo na matusi aulizapo swali lolote lile.
   • Kuuzwa kwa Pete kwa Fungo ili wazazi wake wapate pesa za kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
   •  Pete anabakwa na mlevi anapolewa chakari
   • Mamake Zohari kuridhia kila asemalo mumewe na kushidwa kumtetea anapopata himila.
   • Mamake Mwangeke aliwahi kumwonya kulia kama msichana. Hii ni ishara kuwa jamii yamwona mwanamke kama mnyonge.
   • Mwanzi anakataa kukubali matokeo ya uchaguzi madhali anashindwa na mwanamke, Mwekevu.
   • Wahafidhina kuamini kwamba mtoto wa kiume ndiye pekee anayestahili kuwa mrithi wa mali ya babake.
   • Ushindi wa Mwekevu unaonekana kama kutoheshimiwa kwa mwanaume.
   • Mwekevu kusingiziwa wizi wa kura anapomshida Mwanzi.
   • Kutishwa, kutusiwa na hata kutengwa kwa Mwekevu anapojitosa katika siasa zilizoaminiwa kuwa ni za wanaume
   • Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto.
   • Mwanamke kuonekana kama mnyonge anayestahili kulia akabiliwapo na vizingiti au changamoto maishani. Mwanaume hafai kulia

 2. SEHEMU YA B KIGOGO
  • Tamaa ya kupata sanamu/ Majoka anataka Sudi amtengenezee sanam.
  • Tamaa ya kupata kodi. Majoka anawatoza kodi wafanyibiashara wa soko la Chapakazi kwa manufaa yao.
  • Tamaa ya shule zao kufuzwa na walimu waliofuzu vyuoni. Majoka anamrai Ashua afunze katika shule zake.
  • Tamaa ya kuungwa. Majoka anapata uungwaji mkono kupitia watu kama Ngurumo, Asiya na Boza – Anawapa hongo ili wamuunge mkono.
  • Tamaa ya kupewa sifa lufufu. Kwa mfano Majoka lazima atangazwe katika vyombo vya habari.
  • Tamaa ya kutafutia wanao wachumba. Majoka anamtaka Tunu aolewe na mwanawe Ngao Jur.
  • Tamaa ya mapenzi - Majoka ana tamaa ya kupendwa na Ashua.
  • Tamaa ya kujenga nyumba za kifahari. Majoka anatamani kujenga hoteli ya kifahari katika soko la Chapakazi.
  • Tamaa ya usalama - Majoka ana walinzi wengi.
  • Starehe na anasa. Majoka ana tamaa ya burudani. Anaenda kuogelea katika hoteli ya‘ Majoka and Majoka resort’
  • Tamaa ya viongozi kurithisha jamaa zao uongozi.
  • Tamaa ya uongozi. Majoka anawaua wapinzani wake. (10 ×2= 20)

 3.    
  1. Msemaji - Tunu
   • Wasemewa ni wanasagamoyo nje ya soko la Chapakazi. Tunu anawahutubia wanasagamoyo kwa vile
    soko limefungwa. (4×1 = 4)
  2. Jasiri - Anasema ni mtu wa vitendo.
   Mwanamapinduzi - Anaitisha mkutano wa kupinga kufungwa kwa soko la Chapakazi. (2×2 = 4)
  3.           
   • Anaitisha mkutano wa kutetea kufunguliwa kwa soko.
   • Alimkabili Majoka na kumwita muuaji.
   • Aliongoza maandamano ya kutaka soko lifunguliwe.
   • Akihutubia waandishi wa habari, Tunu anakashifu uongozi wa Majoka hadharani.
   • Anakataa mwito wa Majoka wa kumwoza mwanawe Ngao Jnr.
   • Kama viongozi wa chama cha wanafunzi anahapa kutetea haki za wanasagamoyo.
   • Anamkataza Majoka kujenga hoteli ya kifahari katika uwanja wa soko la Chapakazi.
   • Anamkabili Ngurumo maungweni kuwa ndiye aliyemvamia na kumuumiza. (6×2 = 12)

    HADITHI FUPI.
 4.               
  1. Mapenzi ya kifaurongo.
   • Dennis na wanafunzi wengine wanakaliwa na ugumu wa masomo katika chuo kikuu.
   • Umaskini matatiza masomo na mapenzi ya dennis machora.
   • Utabaka baina ya wanafunzi chuoni.
   • Ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu kwa Dennis na penina.
   • Mapuuza ya wahadhiri k.m Dkt. Mabonga.
   • Migogoro ya mapenzi rafiki wa kwanza wa penina wanatengana na pia tunamwona penina wakitengana na Dennis.
   • Kutamauka masomo chuoni yanakuwa unagumu kiasi kwamba wanafunzi wanaiali kufanya matatu na kukusanya kodi.
   • Njaa- Dennis alikuwa na unga wa kutengeneza uji kikombe kimoja bila sukari.Kuna mapenzi ya kiholela miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu, walitembea wakishikana mabega.
   • Shirikizo la rika – dennis alitamani kuvaa kama wenzake na vile vile kuwa na vifaa vya kieletroniki kama vya wenzake. ( zozote 10x1)

  2. SHOGAKE DADA ANA NDEVU.
   • Mapenzi miongoni mwa wanafunzi yanaathiri masomo yao.
   • Mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi k.m safia.
   • Kuna uavyaji wa mimba. K.m safia .
   • Mauti kifo cha safia.
   • Unafiki wa kidini k.m safia na kimwana.
   • Mapuuza ya wazazi yanapelekea watoto wao kupotoka kimaadili.
   • Kuna undanganyifu wa vijana kwa wazazi wao k.m safia kumdanganya mamake.
   • Kuna utovu wa maadili miongoni mwa vijana k.m mkadi alikuwa na vitendo viovu kushinda shetani.
   • Vijana wanapata changamoto katika maandalizi ya mtihani wa mwisho ndipo safia wanaungana kudurusu pamoja na kimwana.
   • Kutokuwepo kwa mawasiliano baina ya wazazi na watoto wao unawakosesha maelekezi mema.
    ( zozote 10x1)
 5. .              
  1.                  
   • Msemaji ni Babake sara.
   • Akimwambia sara.
   • Walikuwa hospitali katika chumba cha daktari.
   • Alikuwa ameenda kufanyiwa vya ujauzito na Belewa, alipowakuta wazaziwe ivv) wakisubiri katika chumba hicho. (4x1=4)
  2. Mbinu za lugha .
   • swali la balagha unanini?
   • takriri unaogopa. Zozote (2x1=2)
  3. Mrejelewa sara.
   • Mpenda masomo.
   • mwoga.
   • mwenye mapenzi ya dhati.
   • mwenye busara anamua kujiua sio suluhisho.
   • mwenye utu hakutaka kuavya mimba.
   • Msiri
   • Mvumilivu
   • Msamehevu.
   • mwenye madili
   • mwenye majuto. Zozote 6 x 1= 6)
  4. BABAKE SARA.
   • Kupitia kwake tunapata athari ya ukali kupita kiasi wa wazazi kwa wanao.
   • Nikielelezo cha wazazi ambao wako tayari kubadili msimamo wao mkali kwa watoto wao.
   • Anaonyesha umuhimu wa wazazi kushirikiana katika maelezi.
   • Anaonyesha umuhimu wa kuweka siri katika masuala tata ya familia.
   • Ni kielelezo cha wazazi wanaouenzi utamaduni wa jamii yake. (4x1=4)
  5. Malezi /mapenzi
   • Malezi – babake sora anakuwa mkali kwa sora.
   • Babake sora anabadilika na kumwonyesha mapenzi, anamsaidia.
   • Mapenzi – kuna mapenzi ya dhati kati ya sara na salina.
   • Salina anamsaidia sara anapokuwa mjamzito.
   • Salina aidha anamsaidia sara kuweka siri ya ujamzito na kufanyiwa vipimo na mipango ya kujifungua. (3x1=3.)

 6. USHAIRI A
  1. Kuonyesha madhila anayopitia mwanamke/mama mikononi mwa mwanamme. ( 1 x 2 = alm 2)
  2. Ngonjera – ni mazungumzo kati ya Mama na Mwana.(aina 1, idhibati 1 jumla alama 2)
  3.        
   • Kufanywa kufua nguo
   • Mama huenda shambani peke yake.
   • Baba hubaki nyumbani tu na kupiga gomzo mitaani.
   • Baba hamthamini mama.
   • Mama hukata kuni kondeni na kuzibeba kichwani.
   • Mama akichelewa kufika nyumbani akitoka kondeni huadhibiwa.
   • Mama ndiye hutafuta chakula (yoyote 5 x 1= alama 5)
  4. Ubeti una mishororo sita
   • Mshororo umegawika katika vipande viwili isipokuwa mshororo wa tano ambao umegawika katika kipande kimoja.
   • Kila mshororo una mizani kumi na sita isipokuwa mshororo wa sita ambao una mizani tano
   • Kibwagizo kimefupishwa
   • Mpangilio wa vina:
    li ----------------yo
    li ---------------yo
    li----------------yo
    li ---------------yo
    e
    mbe------------go
    (alama 1 kwa kila jibu sahihi, jumla alama 5)
  5. Umenifanya nihisi uchungu ambao nimekuwa nao kwa miaka mingi, usidhani kuwa nayapenda madhila na mashaka, nakerwa na hali yake ya kunidhibiti kufanya jambo na sasa nichoka, ninaanaza kwa hakika kujitayarisha kwa mapambano, hilo nakwambia. (alama 4)
  6.    
   1. Jaza – malipo kwa kutenda wema (alama 1)
   2. muhibu – mpenzi (alama 1)

 7. SHAIRI B
  1.                
   1. Kuwahimiza watu washikilie taalamu zao walizofuzu
   2. Kukashifu/ kushutumu/kukejeli ukosefu wa mwelekeo katika jinsi mambo yanavyoendeshwa.
   3. Kukuza msamiati wa wasomaji wake kuhusu watu wa kazi hizo.
    (malengo yoyote matatu 1 x 3 = alama 3)
  2.    
   1. Msuko – kibwagizo kimefupishwa
   2. Ukara – vina vya utao vinatiririka ilhali vya ukwapi vinabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. (bahari na maelezo yake alama 2 x 2 = alama 4)
  3. Inkisari
   1. Walojitia – waliojitia
   2. Kiwapi – kiko wapi
   3. Kalibebe - akalibebe
   4. Gonga – agonga
   5. Osha - aosha
   6. Kawa – kawa
   7. Tabdila
   8. Anahiyari - anahiari
   9. Yamewavunda – yamewavunja
   10. Kuboronga sarufi/ kufinyanga sarufi
   11. Muashi vyuma adunda – mwashi adunda vyuma
   12. Muhunzi tiba apenda – muhunzi apenda tiba
   13. Baharini anakwenda – anakwenda baharini nk.
   14. Utohozi
   15. Saveya - soroveya
   16. Lahaja
   17. Yamewavunda
   18. Anafundafunda
    (kutaja na kutoa mfano 1, aina tano za uhuru 1 x 5 = alama 5)
  4. Kinaya – matendo ya wahusika ni kinyume na matarajio yetu ya kazi wanazofaa kuzifanya, kwa mfano, muashi agonga vyuma ilhali jaji anagonga misumari.
   ( kutaja mbinu 1, maelezo 1 = alama 2
  5. Daktari anasuka/ anasokota kamba naye saveya amakuwa stadi wa kuvunjavunja mawe. Mtunzaji hazina au mali ya taje ndiye anayetumia vibaya, ni kinyume kimetiliwa mkazo. (alama 4)
  6. Masikitiko – anasikitika kuwa watu wanaopaswa kufanya mambo fulani hawafanyi wanavyostahili bali wanafanya kinyume na matarajio.
   Hakiki jibu la mtahiniwa) (kutaja 1, maelezo 1 = alama 2)
 8.               
  1. Aina ya sifo.
   1. Vivugo / majigambo
   2. Sababu nne kuthibitisha ni vivungo / maji gambo.
    • Mimi ni nguli aliyekamilka.
    • Nimeshatoka kumrarua simba dume.
    • Mimi ni shujaa asiyekanyaga kwa woga.
    • Mimi ni jabali mtetemesha ardhi.
    • Nguvu zangu hazimithiliki.
    • Yu wapi mwingine shujaa?
   3. Mbinu mbili za lugha.
    • Tashihisi - mkuki wangu ni shihidi.
    • Chuku - nguvu zangu hazimithiliki.
   4. Sifa za majigambo.
    • Hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe.
    • Anayejigamba hutumia mfanano, sitiari, ishara na urudiaji.
    • Anayejigamba hujitungia kivugo kufuatia tukio mahususi katika maisha yake m.f siku za jandoni, ndoa, vitani n.k
    • Huwa na matumizi ya chuku.
    • Hutolewa kwa nafsi ya kwanza kwa sababu anayejigamba ni mshairi mwenyewe.
    • Kwa kawaida majigambo hutungwa papo hapo.
    • Maudhui makuu katika majigambo ni ushujaa.
    • Wanaojigamba mara nyingi ni walumbi au washairi wanaoelewa kwa kina wanalolitongoa.
    • Majigambo hutungwa na kughanwa na wanaume.
    • Anayejigamba huweza kutaja usuli wake wa kinasaba. (za kwanza 7 x 1 = al 7
  2. Sababu za kufifia kwa vivugo.
   • Vivugo vilihifadhiwa akilini kwa sababu hii, anayehifadhi anaweza kuibadilisha au hata kufa na kutoweka nayo.
   • Kuna baadhi ya watu ambao wanaihusisha fasihi simulizi na ukale, hivyo kutoona haja ya kuitafitia wala kuirithisha vizazi vya sasa.
   • Mtaala wa elimu kupuuza lugha za kiasili ambazo ndizo zinazohifadhi na kurithisha fasihi simulizi ya majii mbalimbali.
   • Kuhamia mjini kwa wanajamii wengi na kutangamana na watu wa jamii tofauti kumefanya uhifadhi wa tamaduni za jamii na urithishaji wake kutowezekana.
   • Maendeleo ya kiteknolojia na kisayansi. Fasihi simulizi ilikuwa nyenzo ya kuburudisha baada ya kazi, lakini sasa teknolojia inatoa njia za kisasa za kujiburudisha k.v vipindi katika runinga.
   • Ukuaji wa kazi za kimaandishi, mtu anaweza kujisomea. Hili limefanya stadi ya kughana au utambaji kufifia.
   • Uchache wa wataalamu wa kuitafitia na kuiendeleza. Wasomi wengi hupuuza utafiti wa fasihi simulizi.
   • Ukosefu wa utafiti wa kutosha. Ingawa mengi yameandikwa kuhusu fasihi simulizi, kuna vipera ambavyo bado havijaandikwa. (kwanza 8 x 1 = al 8)

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - 2021 KCSE Eldoret Diocese Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest