Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Wewe ni gavana wa kaunti yako. Andika tawasifu utakayotoa katika sherehe ya kuapishwa kwako.
 2. Ugonjwa wa korona umeleta hasara nyingi kuliko faida nchini Kenya. Jadili.
 3. Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
 4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya;
  ……………..nilisimama nikaangalia nyuma, machozi yakanitoka njia mbilimbili nilipokumbuka wosia wa wazazi na walimu.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA

 1. SWALI LA KWANZA
  • Hii ni insha ya kiuaminifu.
  • Haya ni maandishi ya mtu binafsi kuhusu sifa zake maishani (mambo mazuri ya kutujengea sifa)

   Mambo ya Kuzingatiwa
   1. Mada – Ieleze anayetajwa katika tawasifu hiyo.
   2. Nafsi – Nafsi ya kwanza izingatiwe.
   3. Ijikite katika ujumbe kuhusu mtu binafsi yaani,
    • Mwaka na mahali pa kuzaliwa.
    • Aila/familia yake.
    • Hali yake ya ndoa.
    • Kiwango chake cha elimu – chuo kikuu, shule ya upili, ya msingi na ya chekechea.
    • Vyeti na tuzo zote alizopata zitajwe.
    • Matendo yake mema na mafanikio yatajwe ili aonekane kama kielelezo katika jamii.
    • Aonyeshe tajriba yake katika kazi mbalimbali.
    • Ni vyema aangazie juhudi zake maishani k.m amekuwa akijihusisha na shughuli zipi na amefaulu vipi, mipango yake kwa kaunti (Ruwaza yake)
    • Ataje vipaji vyake mbalimbali;
     Tashbihi; Kazi hii ipangwe kiaya na mawazo yafululize
 2. SWALI LA PILI
  • Ni swali la mjadala.
  • Mtahiniwa akubaliane na kauli kwa kutoa hoja nyingi za hasara na chache za faida
  • Au mtahiniwa apinge kwa kutoa hoja nyingi za faida na chache za hasara.
  • Atakayetoa hoja za faida pekee au za hasara pekee atakuwa amejibu swali nusu na asipate kiwango cha C.

   Hasara
  • Vifo
  • Shule kufungwa
  • Kupoteza kazi
  • Kafyuu
  • Kusitishwa kwa usafiri.
  • Visa vya wanafunzi kupachikwa mimba kuongezeka.
  • Gharama ya maisha kupanda.
  • Kadiria hoja zingine.

   Faida
  • Wazazi kuwa na wanao kwa muda mwingi.
  • Usafi kuzingatiwa na kuzuia ndwele k.v. kipindupindu.
  • Biashara kuimarika – ya viyeyuzi, barakoa n.k.
  • Masomo kuendelea kupitia mitandao.
  • Kadiria hoja zingine.
 3. SWALI LA TATU
  1. Mti mkubwa huweka vitu vingi hasa ndege wanaojenga viota, kutaga na kuangua mayai yao pale. Ikiwa mti huo utaanguka makinda huumia kwa sababu wametegemea usalama wa mti huo.
  2. Mtu anayetegemea mtu mwingine kukidhi mahitaji yake hupata shida iwapo kifo au mtu huyo ataondolewa.
  3. Mtahiniwa athibitishe matumizi ya methali kwa kutoa kisa mwafaka.
  4. Mtahiniwa azingatie sehemu mbili za methali iwapo sivyo asipite Zaidi ya alama 10.
 4. SWALI LA NNE
  1. Mtahiniwa aandike kisa kinachomhusisha yeye akitenda makosa.
  2. Pawe na wasia/maonyo kutoka kwa wazazi na walimu.
  3. Akaidi wosia.
  4. Ajipate matatani na kujuta.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest