Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021

Share via Whatsapp

MASWALI

UFAHAMU (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
Sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo imezidi kukua na kutia fora sana nchini na katika bara la Afrika kwa jumla katika siku za hivi karibuni. Sanaa hii imebadilika sana kadri ya mpito wa wakati. Kinyume na hapo awali ambapo mashindano ya urembo yalihusisha uzuri wa sura pekee, katika enzi za leo ,wawaniaji mataji mbalimbali huhitajika kudhihirisha kuwa wana maarifa na hekima ambapo hulazimika hata kueleza jinsi wanavyoweza kutumia taji fulani kuifaa jamii pana iwapo wataibuka washindi.
Vilevile, wanamitindo wamekubali mitindo yenye asili ya kiafrika na inayoendeleza tamaduni za Afrika, badala ya kuiga mitindo ya kimagharibi. Kwa sasa, Kenya na Afrika kwa jumla inajivunia mwigizaji aliyeshinda tuzo maarufu ‘Oscar’, Bi.Lupita Nyong’o, na mwanamitindo wa kutajika Bi.Ajuma. Ufanisi huu haungeweza kufikiwa iwapo Afrika ingeendelea kupapia na kuiga mitindo ya kimagharibi.
Hali kadhalika,maonyesho mengi ya urembo na mitindo yanasheheni mitindo inayosawiri uzuri wa kuegemea utamaduni wa kiafrika, kama vile, matumizi ya khanga,vikoi na leso katika utengenezaji wa mavazi mbalimbali. Siku hizi tamasha za kusherehekea urembo na mitindo huandaliwa katika shule za upili, vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi humu nchini kama mbinu ya kukuza vipaji vya wanafunzi.
Katika kongamano Ia Kimataifa Ia kuadhimisha miaka 50 ya maendeleo ya Kiswahili nchini Kenya lililoandaliwa na chama cha Kiswahili cha Taifa, CHAKITA, katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki, CUEA, kulibainika kuwepo haja ya mashindano ya sanaa ya urembo na mitindo kutangaza sura kamili ya Kiafrika.
Tamasha hizo za urembo na mitindo zinasheheni vipengele vingi vya fasihi simulizi. Itakumbukwa kuwa stadi ya fasihi simulizi husheheni sifa mahsusi ambazo hujidhihirisha kupitia tanzu na vipera vyake anuwai. Fasihi simulizi hubadilika kulingana na mpito wa wakati, maendeleo na mabadiliko ya jamii katika nyanja za kisiasa kijamii na kiuchumi. Katika ulimwengu wa sasa, kuna mambo mbalimbali yanayoshirikisha wanajamii ambayo yanasheheni vipengele vya fasihi simulizi. Tamasha za urembo ni miongoni mwa shughuli zinazowakilisha fasihi simulizi ya jadi pamoja na kusawiri hali halisi ya ulimwengu wa sasa.
Baadhi ya sifa katika sanaa ya maonyesho ya mitindo na urembo zinazosawiri sifa za fasihi simulizi ni kama utendaji,hadhira,wahusika na ubunifu. Wanamitindo mbalimbali hupita jukwaani kwa maringo na miondoko mbalimbali ili kuonyesha mitindo anuai ya mavazi,nywele na urembo. Utendaji ni miongoni mwa sifa muhimu za fasihi simulizi ambapo mtambaji hutumia utendaji ili kuteka hadhira yake na kuwasilisha ujumbe anaokusudia kwa hadhira Iengwa.
Tamasha za urembo haziwezi zikafanikishwa bila ya hadhira ambayo ni kiungo muhimu katika mashindano haya. Hadhira hufanikisha tamasha hizi kwa kulipishwa ada ya kiingilio , hadhira hufanya tamasha hizi kufana kwa kushangilia wanamitindo mbalimbali na kuhakiki mitindo na wahusika. Hadhira ni muhimu kwani huwezesha kuchagua washindi na hata kuboresha mitindo kutokana na maoni ya uhakiki wao kwa wasanii. Hili ni sawa na lilivyo katika fasihi simulizi, ambamo hadhira ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuifanikisha.
Wahusika ndio wanaoonyesha mitindo mbalimbali ya mavazi au urembo.Bali na kwamba urembo wa wahusika hawa huwa ni kigezo muhimu cha kuamua ufanisi wao katika mashindano hayo,ukakamavu wao na ustadi wa miondoko huchangia pakubwa kuboresha tamasha hizi na kuzifanya kuwa za kufana. Bila shaka, fasihi simulizi haiwezi kukami1ika bila kuwepo kwa wahusika ambao ni kiungo muhimu katika utanzu huu.Sharti msanii abuni mitindo mipya na mahsusi ili kuwapiku washindani wake. Mitindo hii huweza kubuniwa na kuundwa kwa matawi, maua, karatasi na kadhalika almuradi ivutie na kuwasilisha ujumbe unaokusudiwa kwa hadhira lengwa. Ili kufanikisha hili, mwanamitindo hana budi kuwa na ubunifu wa kiwango cha juu. Aidha, fasihi simulizi huhitaji umbuji katika uwasilishaji wake. Kwa mfano, itahitaji ubunifu wa hali ya juu kusimulia kisa kimoja kwa kutumia mbinu tofauti ili kukifanya kana kwamba kinasimuliwa kwa mara ya kwanza kila wakati mtambaji anaposimulia. Vilevile jinsi fasihi simulizi inavyoweza kuhifadhiwa kwa sasa kupitia kanda za video na filamu, tamasha za mitindo zinazohusisha utendaji hai huweza kuhifadhiwa katika video na filamu.Hivyo basi,hadhira inaweza kurejelea ili kutazama mashindano hayo. Maleba huhusishwa kupitia mitindo mbalimbali ya mavazi na nywele. Fasihi simulizi vilevile hufanya vivyo hivyo. Hata hivyo tofauti kuu inayojitokeza kati ya fasihi simulizi ya jadi na tamasha za mitindo na urembo ni kwamba,kinyume na fasihi simulizi ambayo ni mali ya jamii, mitindo ya mavazi au nywele ni mali ya mtu binafsi aliyeibuni, na mwenyewe huwa ana haki miliki kisheria.

Maswali

  1. Eleza tofauti iliyoko kati ya uhakiki wa wanamtindo wa awali na wa sasa. (alama 2)
  2. ‘Uafrika unatukuzwa katika maonyesho ya urembo na mitindo’ Thibitisha. (alama 2)
  3. Linganisha fasihi simulizi na sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo . (alama 6)
  4. Linganua fasihi simuilizi na sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo (alama 3)
  5. Eleza maana ya msamiati ufuatao ulivyotumiwa katika taarifa . (alama 2)
    1. Kutia fora
    2. Kuwapiku

UFUPISHO (alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Waatalamu wa maswala ya kielimu wanadai kuwa huenda nchi hii ikalaumiwa kwa kuendeleza mfumo wa elimu unaozingatia maslahi ya wakwasi na kuwapuuza wachochole. Mfumo huu wa elimu umezua mfumo mwingine wa kijamii ambapo watoto wa wenye hadhi wanapata elimu bora kuliko watoto wa maskini. Pengo baina ya haya matabaka linazidi kupanuka kama ardhi na mbingu.
Watoto kutoka jamii hohehahe wanasomea katika shule za umma zisizo na lolote wala chochote na watoto wa mabwenyenye wanasomea katika shule za kibinafsi zilizo na vifaa mufti na mazingira faafu. Mfumo wa jinsi hii ni wa kuitia jamii kitanzi kwa sababu ya unazusha matabaka yanayohasimiana.
Katika dunia ambamo asilimia sitini ya watu inaishi katika hali ambayo ni ya mapato yaliyo chini ya dola moja kila siku, watoto wengi huenda shuleni bila kula chochote na hushinda hivyo kutwa nzima wasiambue chochote darasani. Walimu wao nao hawana ilhamu au kariha ya kufanya kazi kwa sababu mazingira ya kikazi ni mabovu na huenda shuleni shingo upande kama wakulima bila pembejeo. Madarasa yao ni mabanda na wengine husomea chini ya miti ambayo inaweza kukatwa wakati wowote na wachoma makaa wanaozana na mazingira. Unapowatazama watoto hawa, kile kinachoitwa sare ya shule kinakirihisha na kuyaudhi macho. Ni matambara yaliyosheheni viraka vya kila aina katika mseto wa ufakiri. Hawa ni wenzetu eti!
Tatizo hili limekuwa nyeti hasa kutokana na utandawazi na mfumo wa soko huru ambao unaruhusu shule za kibinafsi kuendeshwa kama mashirika ya kibiashara. Karo inayolipwa katika shule hizi ni ya kibiashara, majengo na vifaa vinavyotumiwa ni vya kibiashara, walimu ni wa kibiashara, ilimuradi, kila jambo lalenga maslahi ya kibiashara ya walala hoi. Hapa ndipo chimbuko Ia makabila mawili maarufu nchini, yaani, matajiri walamba- vidole waishio Afueni na maskini walala-hoi,wanaostakimu Madongo-Kuinama.
Uchunguzi umethibitisha kwamba zaidi ya asilimia sitini ya wanafunzi wanaojiunga na shule za kitaifa hutoka katika shule za kibinafsi zinazomilikiwa na matajiri. Mbinu ya Wizara ya Elirnu ya kugawa nafasi kwa njia ya haki katika shule za upili za kitaifa, haijafua dafu kwa sababu matajiri wajanja huwasajili watoto wao waliosoma katika shule za kifahari kufanyia mtihani katika shule zisizokuwa na ushindani mkubwa zilizomo mashambani. Kwa kufanya hivyo, watoto wa maskini huwa wamefungiwa njia kotekote na kuporwa haki yao. Ama kwa kweli mwenye nguvu mpishe kwani dau Ia mnyonge haliendi joshi.
Wanafunzi katika shule za kibinafsi hufunzwa katika makundi madogo madogo ambayo humwezesha mwalimu kushughulikia mahitaji ya kibinafsi ya kila mtoto. Wazazi wao pia huwaajiri walimu wakati wa mapumziko ili kugongomeza au kushadidia mada arnbazo hawakuzielewa vizuri shuleni. Upeo wa lugha wa watoto hawa hauwezi kulinganishwa na wa wenzao wanaosoma katika shule za umma zilizo mashambani kwa sababu shule zao zina maktaba za kisasa, vifaa vya kisasa na vitumeme na hufunzwa kwa teknolojia za kileo zinazowezesha mawasiliano. Watoto hawa huandaliwa ziara za kielimu ili kupanua uelewa wao wa mambo, vile vile hualikiwa watu wanaosifika katika jamii ili kuwahutubia shuleni mwao kuhusu mada mbali mbali. Wawasilishaji hawa huwa ni kielelezo tosha kwa watoto hawa. Mzazi aliyesoma hujua umuhimu wa elimu na hivyo basi huandaa mikakati mahsusi ili kumfaulisha mwanawe kinyume na wazazi wakata.
Ni bayana kuwa iwapo hivi ndivyo mambo yalivyo basi hata vyuo vikuu vitakuwa himaya ya watoto wa matajiri huku watoto wa kimaskini wakisubiri kuajiriwa nao kama walinzi na matopasi. Sera za elimu nchini haziwezi kufanikiwa pale ambapo rasilmali muhimu zinatengewa watu wachache katika jamii. Watoto wa waunda sera hizi husomea katika shule ambazo hufuata mifumo ya kimataifa ambayo haina mkuruba na yetu hafifu. Katika majukwaa ya kisiasa utawasikia wakisifu mfumo ambao watoto wao wanaukwepa kama ukoma. Imekuja kudhihirika kuwa wale wanaosemekana kuwa viongozi wa kesho ni wale ambao sasa hivi wanasomea katika hizo akademia na kufuata mifumo ya kigeni au akademia zinazofuata mfumo wetu katika mazingira teule. Swali ni hili, kesho ya mtoto wa kimaskini ni ipi? Inahitajika mikakati ya kimakusudi kulitanzua swala hili kabla ya milipuko ya kijamii kama vile, ujambazi,uuaji, ubakaji, uraibu wa mihadarati, na kadhalika. Ipo lazima ya kujenga shule vielelezo katika kila wilaya ambazo zitafadhiliwa na serikali kwa kupewa mahitaji yote muhimu na lazima ya küanzishwe mpango wa lishe bora katika shule zote ili kukidhi matilaba ya watoto wote. Usajili wa wanafunzi katika shule za kitaifa na katika vyuo vikuu ni sharti uvalishwe vazi la utu na uzalendo bila ubaguzi. Shule za umma ziwe na madarasa na walimu wa kutosha ili kuondoa matatizo yaliyoibuka kutokana na kuanzishwa kwa mpango wa elimu ya bure katika shule za msingi. Sera kuhusu shule za chekechea lazima izinduliwe kitaifa ili kusawazisha msingi wa kila mtoto kielimu. Walimu wa shule hizi za malezi lazima wawe na maandalizi sawa yatakayowawezesha kusawazisha viwango kitaalamu. Mtaala wetu ulenge kuzalika kwa binadamu ambaye atajinufaisha yeye binafsi na taifa kwa jumla.

Maswali

  1. Mambo yapi muhimu yanajitokeza katika aya ya tatu hadi ya saba? ( maneno 90-95) (alama 8, 1 utiririko)
    Matayarisho
    ……………………………………………………………………………………………..…………………..
    Jibu
    ……………………………………………………………………………………………..……………………………….
  2. Ni mapendekezo yapi yanayotolewa katika aya ya mwisho ( maneno 55- 65) ( alama 7, 1 ya utiririko)
    Matayarisho………………………………………………………………………………………………………..
  3. Jibu……………………………………………………………………………………………..…………

MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)

  1. Tambua viwakifishi vinavyoafiki maelezo haya (alama 2)
    1. Hutumiwa kutenga msemaji na maneno au kauli yake.
    2. Hutenga maelekezo au maagizo na kauli ya mhusika katika tamthlia.
  2. Andika sifa mbili za sauti /r/. (alama 1)
  3. Bainisha silabi zinazowekewa shadda katika maneno yafuatayo : (alama 1)
    1. mwanariadha ……………………………………………………………………………………….
    2. mbunge ………………………………………………………………………………………………
  4. Andika neno lenye muundo ufuatao : (alama 1)
    kiambishi cha nafsi ya kwanza umoja, wakati ujao,kiambishi ngeli,kauli ya kutendea,kauli ya kutenda
  5. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo. (alama 4)
    1. Mwana mwadilifu huwaletea wazaziwe fahari.
      Badilisha neno lilopigiwa mstari kuwa nomino.
    2. Nyota wengi waliipamba anga usiku huo.
      Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.
    3. Makokha ni mkakamavu.Onyango ni mkakamavu pia.
      Unganisha iwe sentensi moja yenye kihusishi cha kulinganisha.
    4. ‘Kibali, nionyeshe ulipoandika zoezi hilo.’Mwalimu alisema.
      Tumia kiwakilishi nafsi badala ya nomino pekee.
  6. Andika sentensi ukitumia nomino hizi kuonyesha upatanisho ufaao wa kisarufi. (alama 2)
    1. Upwa
    2. wapwa
  7. Unganisha sentensi hizi kuunda moja ya masharti. (alama 1)
    Mvua kubwa itanyesha kwa fujo.Mvua itasitisha shughuli.
  8. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. (alama 2)
    Rubani alilikwepa wingu lile,chombo kikapaa angani.
  9. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
    nomino, kishazi tegemezi, kielezi cha wakati, kitenzi, nomino, kivumishi
  10. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (alama 1)
    Wanafunzi wote watajiunga katika kidato cha kwanza.
  11. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kuanza kwa neno:Baraka (alama 1)
    Askari wamekuja kwa ajili ya Baraka.
  12. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. (alama 2)
    Mbuzi wake amekata kamba akaingia shambani na kula mahindi.
  13. Unganisha kuunda sentensi changamano. (alama 2)
    Hashima alisoma kwa bidii. Hashima aliupasi mtihani.
  14. Tumia kiwakilishi kisisitizi badala ya neno lililopigiwa mstari. (alama 1)
    Mwanafunzi aliyetuzwa kwa matokeo mema masomoni ndiye amekifungia kikoa cha shule yake bao.
  15. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Watahiniwa wote walikuwa wanyenyekevu mno baada ya mtihani huo.
  16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)
    Huyu wangu alikuwa amehitimu ila hakuwasilisha maombi.
  17. Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. (alama 2)
    Selume alimsimulia Ridhaa kisa chake.
  18. Akifisha. (alama 2)
    samahani akasema jumba sikutazamia kuwa ningefika nikiwa nimechelewa
  19. Kanusha. (alama 1)
    Mwanafunzi, utakihitaji cheti hicho.
  20. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno : kina (alama 2)
    Rubani ni kwa ndege,………………..ni kwa meli na ……………..ni kwa matwana (alama 1)
  21. Bainisha kiima na shamirisho katika sentensi hii. (alama 3)
    Lanina aliapishwa na Tembo kuwa kigogo wa Ungazebo.
  22. Tunga sentensi mbili zitakazodhihirisha matumizi ya -ji-. (alama 2)

ISIMUJAMII (alama 10)

Umepewa fursa kuhutubia warsha inayojumuisha maafisa wa usalama kutoka katika vikosi mbalimbali kuhusu jukumu lao katika kudumisha usalama,amani na maridhiano nchini.

  1. Taja sajili ambayo utatumia kisha ueleze sababu ya jibu lako. (alama 2)
  2. Andika huku ukifafanua vipengele vinane vya kimtindo utakavyotumia kufanikisha mazungumzo yako.(alama 8)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

UFAHAMU (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
Sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo imezidi kukua na kutia fora sana nchini na katika bara la Afrika kwa jumla katika siku za hivi karibuni. Sanaa hii imebadilika sana kadri ya mpito wa wakati. Kinyume na hapo awali ambapo mashindano ya urembo yalihusisha uzuri wa sura pekee, katika enzi za leo ,wawaniaji mataji mbalimbali huhitajika kudhihirisha kuwa wana maarifa na hekima ambapo hulazimika hata kueleza jinsi wanavyoweza kutumia taji fulani kuifaa jamii pana iwapo wataibuka washindi.
Vilevile, wanamitindo wamekubali mitindo yenye asili ya kiafrika na inayoendeleza tamaduni za Afrika, badala ya kuiga mitindo ya kimagharibi. Kwa sasa, Kenya na Afrika kwa jumla inajivunia mwigizaji aliyeshinda tuzo maarufu ‘Oscar’, Bi.Lupita Nyong’o, na mwanamitindo wa kutajika Bi.Ajuma. Ufanisi huu haungeweza kufikiwa iwapo Afrika ingeendelea kupapia na kuiga mitindo ya kimagharibi.
Hali kadhalika,maonyesho mengi ya urembo na mitindo yanasheheni mitindo inayosawiri uzuri wa kuegemea utamaduni wa kiafrika, kama vile, matumizi ya khanga,vikoi na leso katika utengenezaji wa mavazi mbalimbali. Siku hizi tamasha za kusherehekea urembo na mitindo huandaliwa katika shule za upili, vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi humu nchini kama mbinu ya kukuza vipaji vya wanafunzi.
Katika kongamano Ia Kimataifa Ia kuadhimisha miaka 50 ya maendeleo ya Kiswahili nchini Kenya lililoandaliwa na chama cha Kiswahili cha Taifa, CHAKITA, katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki, CUEA, kulibainika kuwepo haja ya mashindano ya sanaa ya urembo na mitindo kutangazai sura kamili ya Kiafrika.
Tamasha hizo za urembo na mitindo zinasheheni vipengele vingi vya fasihi simulizi. Itakumbukwa kuwa stadi ya fasihi simulizi husheheni sifa mahsusi ambazo hujidhihirisha kupitia tanzu na vipera vyake anuwai. Fasihi simulizi hubadilika kulingana na mpito wa wakati, maendeleo na mabadiliko ya jamii katika nyanja za kisiasa kijamii na kiuchumi. Katika ulimwengu wa sasa, kuna mambo mbalimbali yanayoshirikisha wanajamii ambayo yanasheheni vipengele vya fasihi simulizi. Tamasha za urembo ni miongoni mwa shughuli zinazowakilisha fasihi simulizi ya jadi pamoja na kusawiri hali halisi ya ulimwengu wa sasa.
Baadhi ya sifa katika sanaa ya maonyesho ya mitindo na urembo zinazosawiri sifa za fasihi simulizi ni kama utendaji,hadhira,wahusika na ubunifu. Wanamitindo mbalimbali hupita jukwaani kwa maringo na miondoko mbalimbali ili kuonyesha mitindo anuai ya mavazi,nywele na urembo. Utendaji ni miongoni mwa sifa muhimu za fasihi simulizi ambapo mtambaji hutumia utendaji ili kuteka hadhira yake na kuwasilisha ujumbe anaokusudia kwa hadhira Iengwa.
Tamasha za urembo haziwezi zikafanikishwa bila ya hadhira ambayo ni kiungo muhimu katika mashindano haya. Hadhira hufanikisha tamasha hizi kwa kulipishwa ada ya kiingilio , hadhira hufanya tamasha hizi kufana kwa kushangilia wanamitindo mbalimbali na kuhakiki mitindo na wahusika. Hadhira ni muhimu kwani huwezesha kuchagua washindi na hata kuboresha mitindo kutokana na maoni ya uhakiki wao kwa wasanii. Hili ni sawa na lilivyo katika fasihi simulizi, ambamo hadhira ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuifanikisha.
Wahusika ndio wanaoonyesha mitindo mbalimbali ya mavazi au urembo.Bali na kwamba urembo wa wahusika hawa huwa ni kigezo muhimu cha kuamua ufanisi wao katika mashindano hayo,ukakamavu wao na ustadi wa miondoko huchangia pakubwa kuboresha tamasha hizi na kuzifanya kuwa za kufana. Bila shaka, fasihi simulizi haiwezi kukami1ika bila kuwepo kwa wahusika ambao ni kiungo muhimu katika utanzu huu.Sharti msanii abuni mitindo mipya na mahsusi ili
kuwapiku washindani wake. Mitindo hii huweza kubuniwa na kuundwa kwa matawi, maua, karatasi na kadhalika almuradi ivutie na kuwasilisha ujumbe unaokusudiwa kwa hadhira lengwa. Ili kufanikisha hili, mwanamitindo hana budi kuwa na ubunifu wa kiwango cha juu. Aidha, fasihi simulizi huhitaji umbuji katika uwasilishaji wake. Kwa mfano, itahitaji ubunifu wa hali ya juu kusimulia kisa kimoja kwa kutumia mbinu tofauti ili kukifanya kana kwamba kinasimuliwa kwa mara ya kwanza kila wakati mtambaji anaposimulia.

Vilevile jinsi fasihi simulizi inavyoweza kuhifadhiwa kwa sasa kupitia kanda za video na filamu, tamasha za mitindo zinazohusisha utendaji hai huweza kuhifadhiwa katika video na filamu.Hivyo basi,hadhira inaweza kurejelea ili kutazama mashindano hayo. Maleba huhusishwa kupitia mitindo mbalimbali ya mavazi na nywele. Fasihi simulizi vilevile hufanya vivyo hivyo. Hata hivyo tofauti kuu inayojitokeza kati ya fasihi simulizi ya jadi na tamasha za mitindo na urembo ni kwamba,kinyume na fasihi simulizi ambayo ni mali ya jamii, mitindo ya mavazi au nywele ni mali ya mtu binafsi aliyeibuni, na mwenyewe huwa ana haki miliki kisheria.

Maswali na majibu

  1. Eleza tofauti iliyoko kati ya uhakiki wa wanamtindo wa awali na wa sasa. (alama 2)
    Uhakiki wa awali ulihusu urembo wa sura pekee ilhali
    Wa sasa unahusu urembo wa sura pamoja na marifa au hekima ya mhusika
  2. ‘Uafrika unatukuzwa katika maonyesho ya urembo na mitindo’ Thibitisha. (alama 2)
    Maonyesho mengi ya urembo na mitindo yanasheheni mitindo inayosawiri utamaduni wa kiafrika kama vile matumizi ya khanga,vikoi na leso katika utengenezaji wa mavazi mbalimbali .
  3. Linganisha fasihi simulizi na sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo . (alama 6)
    1. Utendaji : Wanamitindo hupita jukwaani kwa maringo na miondoko mbalimbali ili kuvutia hadhira .Sawa na mtambaji katika fasihi simulizi ambaye hutumia utendaji ili kuteka hadhira yake .
    2. Hadhira : Tamasha za uremboo hufanikishwa kwa kuwepo na hadhira sawa na fasihi simulizi
    3. Wahusika : Hawa ndio wanaonyesha mitindo mbalimbali ya mavazi na urembo hawa ni kiungo muhimu katika kipera cha fasihi simuluzi
    4. Ubunifu: Mwanamitindo sharti abuni mitindo mipya na mahususi ili kuwapiku washindani wake.Mtambaji sharti awe mbunifu anaposimulia kisa kimoja kwa kutumia mbinu tofauti ilikukifanya kivutiwe nyakati zote
    5. Uhifadhi: Huhifadhiwa kupitia kanda za video na filamu kwa minajili ya kuirejelea
    6. Maleba:Huhusishwa kupitia mitindo mbalimbali ya mavazi na nywele katika sanaa zote mbili.
  4. Linganua fasihi simuilizi na sanaa ya maonyesho ya urembo na mitindo (alama 3)
  5. Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali sanaa ya urembo na mitindo ni mali ya mtu binafsi
  6. Hakuna mtu anayeweza kudai haki ya umiliki wa fasihi simulizi lakini mwasisi wa sanaa ya urembo na mitindo ana haki ya umiliki.
  7. Hadhira ya sanaa ya urembo na mitindo hulipishwa ada ya kiingilio ilhali hadhira ya fasihi
    simulizi hailipishwi chochote.
  8. Eleza maana ya msamiati ufuatao ulivyotumiwa katika taarifa . (alama 2)
  9. kutia fora -kufanikiwa/kunawiri/kuwa bora
  10. kuwapiku-kuwashinda

UFUPISHO (alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Waatalamu wa maswala ya kielimu wanadai kuwa huenda nchi hii ikalaumiwa kwa kuendeleza mfumo wa elimu unaozingatia maslahi ya wakwasi na kuwapuuza wachochole. Mfumo huu wa elimu umezua mfumo mwingine wa kijamii ambapo watoto wa wenye hadhi wanapata elimu bora kuliko watoto wa maskini. Pengo baina ya haya matabaka linazidi kupanuka kama ardhi na mbingu.
Watoto kutoka jamii hohehahe wanasomea katika shule za umma zisizo na lolote wala chochote na watoto wa mabwenyenye wanasomea katika shule za kibinafsi zilizo na vifaa mufti na mazingira faafu. Mfumo wa jinsi hii ni wa kuitia jami kitanzi kwa sababu ya unazusha matabaka yanayohasimiana.
Katika dunia ambamo asilimia sitini ya watu inaishi katika hali ambayo ni ya mapato yaliyo chini ya dola moja kila siku, watoto wengi huenda shuleni bila kula chochote na hushinda hivyo kutwa nzima wasiambue chochote darasani. Walimu wao nao hawana ilhamu au kariha ya kufanya kazi kwa sababu mazingira ya kikazi ni mabovu na huenda shuleni shingo upande kama wakulima bila pembejeo. Madarasa yao ni mabanda na wengine husomea chini ya miti ambayo inaweza kukatwa wakati wowote na wachorna makaa wanaozozana na mazingira. Unapowatazama watoto hawa, kile kinachoitwa sare ya shule kinakirihisha na kuyaudhi macho. Ni matambara yaliyosheheni viraka vya kila aina katika mseto wa ufakiri. Hawa ni wenzetu eti!
Tatizo hili limekuwa nyeti hasa kutokana na utandawazi na mfumo wa soko huru ambao unaruhusu shule za kibinafsi kuendeshwa kama mashirika ya kibiashara. Karo inayolipwa katika shule hizi ni ya kibiashara, majengo na vifaa vinavyotumiwa ni vya kibiashara, walimu ni wa kibiashara, ilimuradi, kila jambo lalenga maslahi ya kibiashara ya walala hoi. Hapa ndipo chimbuko Ia makabila mawili maarufu nchini, yaani, matajiri walamba- vidole waishio Afueni na maskini walala-hoi,wanaostakimu Madongo-Kuinama.
Uchunguzi umethibitisha kwamba zaidi ya asilimia sitini ya wanafunzi wanaojiunga na shule za kitaifa hutoka katika shule za kibinafsi zinazomilikiwa na matajiri. Mbinu ya Wizara ya Elirnu ya kugawa nafasi kwa njia ya haki katika shule za upili za kitaifa, haijafua dafu kwa sababu matajiri wajanja huwasajili watoto wao waliosoma katika shule za kifahari kufanyia mtihani katika shule zisizokuwa na ushindani mkubwa zilizomo mashambani. Kwa kufanya hivyo, watoto wa maskini huwa wamefungiwa njia kotekote na kuporwa haki yao. Ama kwa kweli mwenye nguvu mpishe kwani dau Ia mnyonge haliendi joshi.
Wanafunzi katika shule za kibinafsi hufunzwa katika makundi madogo madogo ambayo humwezesha mwalimu kushughulikia mahitaji ya kibinafsi ya kila mtoto. Wazazi wao pia huwaajiri walimu wakati wa mapumziko ili kugongomeza au kushadidia mada arnbazo hawakuzielewa vizuri shuleni. Upeo wa lugha wa watoto hawa hauwezi kulinganishwa na wa wenzao wanaosoma katika shule za umma zilizo mashambani kwa sababu shule zao zina maktaba za kisasa, vifaa vya kisasa na vitumeme na hufunzwa kwa teknolojia za kileo zinazowezesha mawasiliano. Watoto hawa huandaliwa ziara za kielirnu ili kupanua uelewa wao wa mambo, vile vile hualikiwa watu wanaosifika katika jamii ili kuwahutubia shuleni mwao kuhusu mada mbali mbali. Wawasilishaji hawa huwa ni kielelezo tosha kwa watoto hawa. Mzazi aliyesoma hujua umuhimu wa elimu na hivyo basi huandaa mikakati mahsusi ili kurnfaulisha mwanawe kinyume na wazazi wakata.
Ni bayana kuwa iwapo hivi ndivyo mambo yalivyo basi hata vyuo vikuu vitakuwa himaya ya watoto wa matajiri huku watoto wa kimaskini wakisubiri kuajiriwa nao kama walinzi na matopasi. Sera za elimu nchini haziwezi kufanikiwa pale ambapo rasilmali muhirnu zinatengewa watu wachache katika jamii. Watoto wa waunda sera hizi husomea katika shule ambazo hufuata mifumo ya kirnataifa ambayo haina mkuruba na yetu hafifu. Katika majukwaa ya kisiasa utawasikia wakisifu mfumo ambao watoto wao wanaukwepa kama ukoma. Imekuja kudhihirika kuwa wale wanaosemekana kuwa viongozi wa kesho ni wale arnbao sasa hivi wanasomea katika hizo akadernia na kufuata mifumo ya kigeni au akademia zinazofuata mfumo wetu katika mazingira teule. Swali ni hili, kesho ya mtoto wa kimaskini ni ipi?
Inahitajika mikakati ya kimakusudi kulitanzua swala hili kabla ya milipuko ya kijamii kama vile, ujarnbazi,uuaji, ubakaji, uraibu wa mihadarati, na kadhalika. Ipo lazima ya kujenga shule vielelezo katika kila wilaya ambazo zitafadhiliwa na serikali kwa kupewa mahitaji yote muhimu na lazima ya küanzishwe mpango wa lishe bora katika shule zote ili kukidhi matilaba ya watoto wote. Usajili wa wanafunzi katika shule za kitaifa na katika vyuo vikuu ni sharti uvalishwe vazi la utu na uzalendo bila ubaguzi. Shule za umma ziwe na madarasa na walirnu wa kutosha ili kuondoa matatizo yaliyoibuka kutokana na kuanzishwa kwa mpango wa elirnu ya bure katika shule za msingi. Sera kuhusu shule za chekechea lazirna izinduliwe kitaifa ili kusawazisha msingi wa kila mtoto kielimu. Walimu wa shule hizi za malezi lazirna wawe na rnaandalizi sawa yatakayowawezesha kusawazisha viwango kitaalamu. Mitaala wetu ulenge kuzalika kwa binadamu ambaye atajinufaisha yeye binafsi na taifa kwa jumla.

Maswali

  1. Mambo yapi muhimu yanajitokeza katika aya ya tatu hadi ya saba? ( maneno 90-95) (alama 8, 1 utiririko)
    1. Watoto wa maskini hushinda njaa shuleni.
    2. Walimu wao hawana ari ya kufunza wala vifaa vya kutosha .
    3. Madarasa huwa mabanda au chini ya miti.
    4. Hili limesababishwa na utandawazi na mfumo wa soko huru unaoruhusu shule za kibinafsi kuendeshwa kama mashirika ya kibiashara ambayo hulenga maslahi ya matajiri.
    5. Zina mazingira na vifaa vya kisasa vya kutosha.
    6. Mzazi aliyesoma huandaa mikakati kumfaulisha mwanawe kinyume na wazazi wakata.
    7. Asilimia kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili hutoka katika shule za kibinafsi.
    8. Juhudi za Wizara ya Elimu kugawa nafasi katika shule za upili hazijafua dafu.
    9. Nafasi zote katika shule za upili, za kitaifa na vyuo huchukuliwa na watoto matajiri .
    10. Sera za elimu haziwezi kufanikiwa rasilmali zikitengewa wachache.
    11. Watoto wa waunda sera husomea katika shule za kifahari zinazofuata mifumo ya kigeni.
    12. Wengine wanasoma katika akademia zinazofuata mfumo wetu hafifu katika mazingira tofauti.
    13. Nafasi ya mtoto maskini inazidi kudidimia.
  2. Ni mapendekezo yapi yanayotolewa katika aya ya mwisho ( maneno 55- 65) ( alama 7, 1 ya utiririko)
    1. Mikakati ya kimakusudi inahitajika kabla ya balaa kuzuka.
    2. Ujenzi wa shule vielelezo wahitaji ufanyike katika kila wilaya .
    3. Shule za umma ziwe na mpango wa lishe bora.
    4. Utu na uzalendo uelekeze usajili wa wanafunzi katika taasisi zote za elimu .
    5. Shule za umma ziwe na walimu na madarasa ya kutosha.
    6. Sera kuhusu shule za chekechea izinduliwe kusawazisha msingi wa kila mtoto.
    7. Walimu wazo wawe na maandalizi yatakayowawezesha viwango kitaalamu
    8. Mtaala wetu ulenge kuzalika binadamu atakayejinufaisha yeye na taifa kwa jumla

MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)

  1. Tambua viwakifishi vinaafiki maelezo haya (alama 2)
    1. Hutumiwa kutenga msemaji na maneno au kauli yake.
      nukta pacha/koloni alama 1
    2. Hutoa maelekezo na maagizo katika tamthilia.
      parandesi/mabano alama 1
  2. Andika sifa mbili za sauti /r/. (alama 1)
    1. kimadende
    2. cha ufizi
    3. ghuna alama ½ kwa kila moja ya majibu yoyote mawili
  3. Bainisha silabi zinazowekewa shadda katika maneno yafuatayo : (alama 1)
    1. mwanariadha -a-/mwanari-a-dha/mwanariadha
    2. mbunge -bu-/m-bu-nge/mbunge
  4. Andika neno lenye muundo ufuatao : (alama 1)
    kiambishi cha nafsi ya kwanza umoja, wakati ujao,kiambishi ngeli,kauli ya kutendea,kauli ya kutenda nitakikalia/nitakuchezea/nitayapalilia
  5.  Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo. (alama 4)
    1. Mwana mwadilifu huwaletea wazaziwe fahari.
      Badilisha neno lilopigiwa mstari kuwa nomino.
      Uadilifu wa mwana huwaletea wazaziwe fahari.
      Mwadilifu huwaletea wazaziwe fahari.
    2. Nyota wengi waliipamba anga usiku huo.
      Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.
      Thurea ya nyota iliipamba anga usiku huo.
    3. Makokha ni mkakamavu.Onyango ni mkakamavu pia.
      Unganisha iwe sentensi moja yenye kihusishi cha kulinganisha.
      Makokha ni mkakamavu kama/sawa na/zaidi ya/kuliko/ Onyango.
    4. ‘Kibali, nionyeshe ulipoandika zoezi hilo.’Mwalimu alisema.
      Tumia kiwakilishi nafsi badala ya nomino pekee.
      ‘Wewe,nionyeshe ulipoandika zoezi hilo.’Mwalimu alisema.
  6. Andika sentensi ukitumia nomino hizi kuonyesha upatanisho ufaao wa kisarufi. (alama 2)
    1. upwa (U-U) : Upwa wake Mwangemi ulimsalimisha mbele ya ami yake.
      upwa (U-ZI) : Upwa wa Ziwa Viktoria hauzuriki kwa kujaa maji yanayofurika.
    2. wapwa (A(yu) -WA) : Wapwa wake Juma walimnunulia gari.
  7. Unganisha sentensi hizi kuunda moja ya masharti. (alama 1)
    Mvua kubwa itanyesha kwa fujo.Mvua itasitisha shughuli.
    Mvua kubwa ikinyesha kwa fujo itasitisha shughuli.
  8. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. (alama 2)
    Rubani alilikwepa wingu lile,chombo kikapaa angani.
    Marubani waliyakwepa mawingu yale vyombo vikapaa angani.
  9. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
    nomino,kishazi tegemezi,kielezi cha wakati,kitenzi,nomino,kivumishi
    Mwanafunzi anayejizatiti masomoni leo atafaulu maishani mwake.
    Ua lililochanuka asubuhi limempendeza Mwalimu Mkuu.
  10. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (alama 1)
    Wanafunzi wote watajiunga katika kidato cha kwanza.
    Wanafunzi wote walikuwa wamejiunga katika kidato cha kwanza.
  11. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kuanza kwa neno:Baraka (alama 1)
    Askari wamekuja kwa ajili ya Baraka.
    Baraka amejiwa na askari.
  12. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. (alama 2)
    Mbuzi wake amekata kamba akaingia shambani na kula mahindi.
    Kibuzi chake kimekata kikamba kikaingia kijishambani na kikala vihindi
    Kijibuzi chake kimekata kikamba kikaingia kijishambani na kikala vijihindi
  13. Unganisha kuunda sentensi changamano. (alama 2)
    Hashima alisoma kwa bidii. Hashima aliupasi mtihani.
    Hashima aliposoma kwa bidii aliupasi mtihani.
  14. Tumia kivumishi kisisitizi cha neno lililopigiwa mstari. (alama 1)
    Mwanafunzi aliyetuzwa kwa matokeo mema masomoni ndiye amekifungia kikoa cha shule yake bao.
    Mwanafunzi yuyu huyu/yuyo huyo/yule yule aliyetuzwa kwa matokeo mema masomoni ndiye amekifungia kikoa cha shule yake bao.
    Mwanafunzi aliyetuzwa kwa matokeo mema masomoni ndiye yuyu huyu/yuyo huyo/yule yule amekifungia kikoa cha shule yake bao.
  15. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Watahiniwa wote walikuwa wanyenyekevu mno baada ya mtihani huo.
    kirai nomino – watahiniwa wote
    kirai kivumishi -- wote walikuwa
    kirai kitenzi – wanyenyekevu mno baada ya
    kirai kielezi – mno baada ya
    kirai kihusishi – baada ya mtihani huo (vyovyote viwili 2 x 1 = 2)
  16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)
    Huyu wangu alikuwa amehitimu ila hakuwasilisha maombi.
    S-KN((W+V +S)+KT(T)+ U+KT(T+E)
  17. Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. (alama 2)
    Selume alimsimulia Ridhaa kisa chake.
    kisa cha Selume
    kisa cha Ridhaa (zozote mbili 2 x 1=2)
    kisa cha Mtu mwingine
  18. Ridhaa asikilize
    kwa niaba ya Ridhaa
  19. Akifisha. (alama 2)
    samahani akasema jumba sikutazamia kuwa ningefika nikiwa nimechelewa
    ‘ Samahani ,’ akasema Jumba , ‘ Sikutazamia kuwa ningefika nikiwa nimechelewa .’ vitahini 8 x ¼ =2
    Samahani akasema, ‘ Jumba , sikutazamia kuwa ningefika nikiwa nimechelewa .’ vitahini 6x ½ =2
  20. Kanusha. (alama 1)
    Mwanafunzi, utakihitaji cheti hicho.
    Mwanafunzi, hutahitaji cheti hicho.
  21. Weka shadda kubainisha maana mbili za neno : kina (alama 2)
    ‘kina – urefu wa kwenda chini katika shimo au kwenye mkusanyiko wa maji mengi kama bwawani au baharini.
    ‘kina – pigo la sauti za namna moja zinazotokea kila baada ya mizani kadhaa katika mishororo katika ushairi.
    ‘kina- kwa undani :soma kwa kina- soma kwa makini.
    ki’na – hali ya kumiliki katika ngeli ya KI-VI
    ki’na – wingi wa nomino zinazotaja uhusiano wa wanajamii ambazo hazichukui viambishi vya hali. Kwa mfano :mama, baba, shangazi,dada na kadhalika matumizi ni kama :kina mama,kina shangazi
  22. Rubani ni kwa ndege, nahodha ni kwa meli na dereva ni kwa matwana (alama 1)
  23. Bainisha kiima na shamirisho katika sentensi hii. (alama 3)
    Lanina aliapishwa na Tembo kwa bibilia nyeupe kuwa kigogo wa Ungazebo.
    1. kiima –Tembo
    2. shamirisho kipozi-Lanina
    3. shamirisho ala- bibilia nyeupe 3 x 1= 3
  24. Tunga sentensi mbili zitakazodhihirisha matumizi ya -ji-. (alama 2)
    -ji- -ukubwa kwa mfano, Jibwa lake halili likashiba.
    -ji- - inayorejelea mtendaji kwa mfano, Tonny ana-ji-ikaza kikondoo.
    -ji- - kuunda nomino kutokana na kitenzi, kwa mfano, imba - mwimba-ji
    Mwimbaji maarufu amewasili shuleni mwetu

ISIMUJAMII (alama 10)
Umepewa fursa kuhutubia warsha inayojumuisha maafisa wa usalama kutoka katika vikosi mbalimbali kuhusu jukumu lao katika kudumisha usalama,amani na maridhiano nchini.

  1. Taja sajili ambayo utatumia kisha ueleze sababu ya jibu lako.
    Sajili ya kitaaluma/Mazungumzo rasmi alama 1
    Hotuba kwa wataalamu,maafisa wa usalama. alama 1
  2. Andika huku ukifafanua vipengele vinane vya kimtindo utakavyotumia kufanikisha mazungumzo yako.
    1. Nitatumia msamiati maalum
    2. Nitatumia sentensi fupifupi/ndefu ndefu ili kutoa maelezo
    3. Nitatumia lugha rasmi ya Kiswahili
    4. Nitatumia lugha sanifu
    5. Nitatumia lugha ya heshima, mabibi na mabwana
    6. Nitatumia lugha shawishi
    7. Nitatumia lugha ya ushauri
    8. Nitatumia lugha ya tasfida kuficha makali ya msamiati
    9. Nitachanganya na hau kuhamisha msimbo
    10. Nitatumia msamiati wa kutoholewa/maneno ya kukopwa kuakisi maendeleo ya kiteknolojia na zana za kivita.
    11. Nitataja na kunukuu takwimu kwa kutoa ushahidi.
    12. Nitatumia ishara
    13. Nitatumia lugha ya kuwapa matumaini.
    14. Nitatumia takriri ili kusisitiza mambo muhimu.
    15. Nitatumia kiimbo kuhalisi hisia tofauti tofauti
      Tanbihi:
      Ama mwanafunzi atoe ufafanuzi wa kina au mfano ili atuzwe alama 1 kwa kila hoja.
      Jumla hoja 8 x 1 = 8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest