Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021

Share via Whatsapp

MASWALI
SEHEMU A: TAMTHILIA.
P. KEA: KIGOGO.

 1. Lazima.
  1. “La, koma! La, koma. Siwezi mimi, siwezi mimi. Sitaki kuwa gurudumu la akiba….hujayaacha hayo.?”
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Bainisha vipengele vinne vya kimtindo katika dondoo hili. (alama.4)
   3. Fafanua sifa mbili za nafsinenewa katika dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza umuhimu wa mandhari husika kwenye dondoo hili katika kuijenga tamthilia ya Kigogo. (alama.8)

SEHEMU B: RIWAYA
A.MATEI: CHOZI LA HERI.

jibu swali la 2 au la 3.

 1.        
  1. “Basi…..muda haukupita kabla ya kusikia mlio wa bunduki, mitutu yake ilitema risasi jinsi bafe atemavyo mate. Vilio vya kite vilihanikiza hewani, vita vikaanza.”
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama.4)
   2. Bainisha aina mbili za taswira katika dondoo hili. (alama.2)
   3. Eleza vipengele viwili vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
  2. Vita vinavyorejelewa katika dondoo hili viliwaathiri wahafidhina kwa njia hasi. Fafanua. (alama 12)
 2.        
  1. “Nashangaa kinachompa kijana kama huyu, na wengine waliofariki jana, ambao wamesomea shahada za uzamili, kujihusisha na unywaji wa pombe haramu!
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Fafanua umuhimu wa msemaji katika dondoo hili. (alama 4)
   3. Kando na maudhui ya elimu eleza maudhui mengine mawili katika dondoo hili. (alama 2)
  2. Eleza jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu zifuatazo katika kuijenga riwaya hii.
   1. Hadithi ndani ya hadithi. (alama 5)
   2. Mbinu rejeshi (alama 5)

SEHEMU C: HADITHI FUPI.
Jibu swali la 4 au 5
.
A. chokocho na D. Kayanda (wah): Tumbolisiloshiba na Hadithi Nyingine.
Alifa chokocho : “Masharti ya Kisasa”

 1.      
  1. “Pom poom! pom poom! pom poom…Honi ya muuza samaki hiyo. Alibonyeza mpira wa honi ili kuashiria kwamba sasa yumo njiani juu ya baiskeli yake, anapita akitembeza samaki.
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika dondoo hili. (alama.3)
   3. Bainisha aina tatu za taswira katika dondoo hili. (alama 3)
  2. ”….mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana. “Thibitsha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi ya Masharti ya kisasa. (alama 10)
 2.      
  1. Onyesha jinsi ufisadi unavyoshughulikiwa katika hadithi, “Shibe inatumaliza.” (alama 10)
   Ali Abudulla Ali: “Ndoto ya Mashaka”
  2. “….Kumbe hii yote ilikuwa ndoto – ndoto yangu. Ndoto ya mashaka yangu.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kumrejelea mhusika husika katika hadithi hii. (alama 10)
 1. SEHEMU YA D: USHAIRI.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Said A. Mohamed: Mbele ya Safari.

Ilipoanza safari, ilianza kwa dhiki
Tulishikana kwa ari, kwenda safari ya haki
Tukawa ni majabari, nyoyo zisitaharuki
Tukajizatiti

Njaa ikawa thabiti, na kiu kutamalaki
Nasi tulitia dhati, tusijali kuhiliki
Ingawa mbele mauti, dhila na mingi mikiki
Tulijizatiti.

Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki
Shangwe kwetu na fahari, utumwa hatuutaki
Kuwa mbele ya safari, juhudi iliyobaki
Tulijizatiti

Ile ilikuwa ndoto, Mwisho wake mafataki
Nguvu zimechomwa moto, sahala ‘mekuwa dhiki
Wagombania kipato, utashi haukatiki
Na kutabakari.

Msafara ukasita, kwenye mlima wa haki
Kijasho kinatuita, Mlima haupandiki
Basi sote ‘kajipeta, kukikwea kima hiki
Twataka hazina.

Tukiwa migongo wazi, tukainama kwa shaki
Tukawa’chia ukwezi, kialeni wadiriki
Wakapanda bila kazi, kuteremsha miliki
Wakaitapia

Wakafikia makazi, ya pumbao na ashiki
Huko wakajibarizi, kwenye raha lakilaki
wakaisahau ngazi, ya umma uliomiliki
Mbele ya safari.

Na hazina yetu sote, kuishusha hawataki
Wamo wanatema mate, kwa umati halaiki
Imezima nia yote, kiza hakitakasiki
Mbele ya safari.

 1. Eleza safari inayorejelewa katika shairi hili. (alama 2)
 2. Onyesha kinaya cha safari inayozungumziwa. (alama 3)
 3. Taja na ueleze bahari tatu za shairi hili ukizingatia: (alama.2)
  1. Mizani
  2. Vina
 4. Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama.4)
 5. Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa sita.(alama 2)
 6. Bainisha aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. alama 2)
 7. Fafanua aina mbili za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 2)
 8. Kando na kinaya, bainisha vipengele vingine viwili vya kimtindo katika shairi hili. (alama 2)
 9. Eleza toni ya shairi hili (alama.1)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI.

 1. Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali.
  Ewe mpwa wangu,
  Kwetu hakuna mwoga, usiwe kama msichana
  Uoga ukikufika, huenda ni wa akina mamayo.
  Fahali tulichinja ili uwe mwanamume
  Iwapo utatingiza kichwa
  Uhamie kwa wasiokatwa
  Waume wa mbari yetu
  Si waoga wa kisu
  Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo.
  Simama jicho liwe juu
  Ngariba alilala jikoni
  Visu ametia makali
  Kabiliana na kisu kikali
  wengi wasema ni kikali
  Mbuzi utampata
  Na hata shamba la mahindi
  Usiende kwa wasiotahiri.
 1. Huu ni wimbo wa aina gani? Fafanua. (alama.2)
 2. Eleza shughuli mbili za kiuchumi zinazodokezwa na wimbo huu. (alama 2)
 3. Eleza aina mbili za taswira katika utungo huu. (alama 2)
 4. Kando na taswira, bainisha vipengele vingine viwili vya kimtindo katika wimbo huu. (alama.2)
 5. Onyesha jinsi taasubi ya kiume inavyojitokeza katika wimbo huu. (alama 4)
 6. Fafanua umuhimu wa aina hii ya wimbo katika jamii. (alama 8)


MWONGOZO WA KISWAHILI

 1. LAZIMA.
  1.        
   1.      
    1. Msemaji – Majoka akiiga jinsi alivyosema Ashua hapo awali.
    2. Msemewa – Ashua
    3. Mahali – katika ofisi/ofisini mwa Majoka
    4. Sababu- Ni baada ya watoto wa Ashua kulala njaa. Ashua anaamua kwenda kumuomba msaada Majoka. (4x1=4)
   2. Takriri/Uradidi- La, Kama! Siwezi mimi
    1. Nidaa – Koma!
    2. Mdokezo – akiba ….hujayaacha hayo
    3. Maswali balagha – hujayaacha hayo?
     4x1=4
   3.        
    1. Mwenye bidii – Anafanya kazi kwa bidii ndipo aweze kukidhi mahitaji ya familia yake.
    2. Ni Msomi – amesoma na kuhitimu chuo kikuu. Ana shahada ya ualimu.
    3. Ni mwanamapinduzi – anashirikiana na Sudi, Tunu na Siti kuikomboa Sagamoyo.
    4. Ni mlezi mwema – anafanya bidii kuwatafutia wanawe chakula
     2x2=4
  2.        
   1. Mandhari husika – Ni katika afisi ya Majoka (Onyesho la pili.)
   2. Kujenga tabia za wahusika kama Majoka kuwa mwenye tama ya kimapenzi kwa Ashua.
   3. Kuangazia uozo wa maadili katika jamii. Majoka ni kiongozi, ana mke Husda, anajua vyema kuwa Ashua ana mme lakini anamtamani kimapenzi.
   4. Kuonyesha suala la uwajibikaji katika ndoa. Ashua anachukua hatua ya kuwatafutia wanawe chakula kwa Majoka baada ya kulala njaa.
   5. Kuonyesha changamoto mbalimbali katika ndoa. Umaskini, ukosefu wa uaminifu.
   6. Kuchimuza matukio ya awali. Awali Ashua alikataa pete ya Majoka ya uchumba. (Uk.23).
   7. Kuonyesha ukosefu na uwajibikaji wa viongozi. soko linakosa kusafishwa ilhali wachuuzi wanalipa kodi.
   8. Kuonyesha suala la ukiukaji wa haki. Wachuuzi wanafungiwa soko ambalo ni tegemeo kwa mahitaji ya jamaa zao. Chakula, kuvaa n.k.
   9. Kuonyehsa suala la uchafuzi wa mazingira. Majoka anasema takataka za soko hilo zitaharibu sifa nzuri ya jimbo lao.
   10. Suala la ukosefu wa kazi kutokana na mfumo duni wa elimu linaangaziwa. Ashua amesoma hadi chuo kikuu na kuhitimu kama mwalimu, lakini anaishia kuwa mchuuzi wa maembe sokoni.
   11. Kuonyesha athari mbaya za matumizi ya dawa za kulevya. Wanafunzi katika shule wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka na kushindwa kufuzu. (uk.26)
   12. Kuonyesha migogoro inayosababishwa na ukosefu wa uamninifu katika ndoa. Husda anashuku kukosekana kwa Majoka nyumbani kwake kunatokana na Ashua. 8x1=8 (zozote 8)
 2.              
  1. RIWAYA
   1.          
    1. Msemaji – Kaizari
    2. Msemewa – Ridhaa
    3. Mahali – katika kambi/Mabanda yaliyosongamana ndani mwa msitu wa mamba.
    4. Sababu- Ni baada ya kutangazwa kwa kiongozi mpya – mwanamke, mwekevu mambo yakaharibika. 4 x 1= 4
   2.        
    1. Taswira usikivu – kusikia mlio wa bunduki
    2. Taswira uoni- tema risasi, bafe atemavyo mate 2 x 1=2
   3.      
    1. Tashhisi – bunduki, mitutu yake ilitema risasi
    2. Tashbihi- …ilitema risasi jinsi bafe atemavyo mate 2x1=2
  2.        
   1. Vifo/Mauti- Ridhaa anapoteza familia yake, mkewe Terry, wanawe wawili, mkaza mwanawe na mjukuu wake Becky
   2. Uharibifu wa mali- Ridhaa anapoteza jumba lake la kifahari kwa kuteketezwa na moto.
   3. Hasara kwa wafanyi biashara – Maduka yao yaliporwa na wezi waliobeba walichoweza kabla ya kukutana na mkono mrefu wa utawala.
   4. Kutiwa nguvuni – waliohusika katika uporaji mwishowe walikutana na mkono mrefu wa utawala.
   5. Huzuni- Baada ya Ridhaa kupoteza familia pamoja na jumba lake, machozi yalimfurika machoni, yakayaziba na kuulemaza uwezo wake wa kuona.
   6. Watu kutoroka makwao – kuna wale ambao waliona ku moto, wakaamua kuacha makazi yao na kukimbia. (uk.20)
   7. Kulemazwa kwa usafiri – vijana barobaro waliyazingira magari barabarani na kuyawasha moto.
   8. Majerushi – subira alikatwa kwa sime akazirai kwa uchungu (uk 25)
   9. Kubakwa – Lime na mwanaheri wanatendewa unyama na mabarobaro watano. (uk.25)
   10. Kusambaratishwa kwa jamaa/familia- Selume aliondoka katika ndoa yake sababu alihitilafiana na wakwe zake kwa kumuunga Mwekevu mkono.
   11. Utegemezi- katika kambi kaizari na wenzake, mfano aliyekuwa waziri wa Fedha wanang’a ng’ania chakula – uji hasa (uk.15), kujengewa nyumba (uk.31) kutoka kwa mashirika mbalimbali
   12. Magonjwa –katika msitu wa mamba, Ridhaa alipata ugonjwa wa shinikizo la damu baada ya kupoteza jamaa na mali yake. (uk.36)
   13. Uhasama kati ya makabila – Kaizari anahimizwa na jirani yake kuhama kwa sababu ya tofauti za kitabaka, kijinsia na kikabila . (uk.26)
    12x1=12 (zozote 12)
 3.      
  1.        
   1.        
    1. Msemaji – Selume
    2. Msemewa –Meko
    3. Mahali _ kituo cha afya cha mwanzo mpya.
    4. kiini – Ni baada ya kifo cha mmoja wa wagonjwa hospitalini hali inayomfanya Meko kutaka kujua iwapo ni yule aliyeletwa usiku.
     4 x 1=4
   2.      
    1. Msemaji ni Selume.
    2. Amejenga tabia za wahusika kwa mfano utu wa Ridhaa. Anaazisha kituo cha Afya na kuajiri Selume na Kaizari.
    3. Anaoyonyesha changamoto katika hospitali za umma. Anashangaa kama alivyovumilia kufanya kazi bila glavu.
    4. Anajemga maudhui ya ufisadi. Dawa zilizotengewa hospitali ziliuzwa na wasimamizi.
    5. Anaendeleza ploti. Kupitia sadfa. Kituo kinakamilika wakati ambapo Selume anajiuzulu, anapata kazi na mkondo wa matukio kubadilika.
    6. Anaonyesha mgogoro unaosababishwa na siasa. Anatenga na jamaa yake kwa sababu ya kumuunga mwekevu mkono. 4x4=4
   3.      
    1. Vifo/Mauti – wengine waliofariki jana
    2. Ulevi – Unywaji wa pombe haramu. 2x2=2
  2.      
   1. Hadithi ndani ya hadithi.
    1. Usimulizi wa Kairu (Uk.91-93) Unaonyesha dhiki za wakimbizi. Mnuna wa Kairu anafia njiani, kuna msongamano kambini.
    2. Usimulizi wa Mwanaheri (uk93-98) ndio unaonyesha hatima ya familia ya Kaizari; wanarudishwa nyumbani na Mwanaheri na Lime kurudia maisha ya kawaida..
    3. Usimulizi wa Zohali (uk98=-101) kuonyesha matatizo ya vijana. Zahali anashindwa kujidhibiti na kuambulia ujauzito akiwa shuleni.
    4. Usimulizi wa chandachema (uk.101-108) Unaendeleza maudhui ya malezi. Analelewa na nyanya baada ya baba yake, Fumba, kumtelekezea huko.
    5. Usimulizi wa Pete (uk.146-153) Unaonyesha ukiukaji wa haki za watoto. Mama Pete anaridhia wazo la kumwachisha Pete masomo. Anoazwa kwa Mzee Fungo bila hiari.
    6. Hadithi ya Sally kumsaliti Billy inayosimuliwa kama kifani cha Naomi kumsaliti Lunga. (uk.81)
     5x1=5. (zozote 5)
   2. Mbinu Rejeshi.
    1. Ridhaa anakumbuka kupepesa kwa jicho lake la kulia, anguko aliloanguka sebuleni, milio ya bundi iliyomtia kiwewe. (uk.1)
    2. Ridhaa anakumbuka mazungumzo kati yake na Terry mkewe akimuuliza “since when has man ever changed his destiny?” (uk.2)
    3. Ridhaa anakumbuka jinsi mwanawe Mwangeka alivyozaliwa katika chumba chake ambacho kwa sasa kimeteketea. (uk.4)
    4. Ridhaa anakumbuka mjadala kati yake na mwanawe Tila kuhusu mafanikio ya baada ya uhuru.
    5. Mwandishi kupitia mbinu rejeshi anatueleza jinsi Ridhaa alivyojipata katika msitu wa Heri.
    6. Ridhaa anakumbuka jinsi wanafunzi wenzake walivyomtenga shuleni na kumuita “Mfuata Mvua” (uk.10)
    7. Tetei, mwanaharakati anakumbuka jinsi wanaume walivyotumikishwa katika enzi za kiistimari. (uk.17)
    8. Mja aliyevaa shati lililoandikwa Hitman mgongoni anakumba jinsi kila baada ya miaka mitano viongozi huwatumia katika kampeni zao na kushiriki katika njama ya viongozi za kuiba kura. (uk.22)
    9. Kupitia kisengere nyuma, mwandishi anatueleza jinsi Mwangeka alivyokutana na Lily Nyamvula mkewe wa kwanza- katika chuo kikuu.
    10. Mwangeka anakumbuka jinsi babake alivyomchapa baada ya kumpata yeye na wenzake wakiigiza mazishi ya nduguye Dedan Kimathi. (uk.60)
     5x1= 5 (zozote 5)
 4. HADITHI FUPI.
  1.      
   1.      
    1. Msemaji – msimulizi
    2. Msemewa – Akimrejelea Dadi
    3. Mahali – Njiani akitemebeza samaki.
    4. Ni baada ya miaka tisa katika ndoa. Ndoa ambayo Dadi ana hisi kuwa mkewe ndiye aliyevunja masharti kwa kumwendea kinyume.
     4x1=4
   2.      
    1. Tanakali ya sauti – pom poom! pom poom!
    2. Mdokezo – pom poom….Honi.
    3. Takriri – pom poom! pom poom, samaki
     3x1=3
   3.      
    1. Taswira hisi – pom, poom! pom poom….Honi ya muuza samaki huyo.
    2. Taswira mwendo – anapita akitembeza samaki.
    3. Taswira usikivu- Honi ya muuza samaki huyo.
     3x1=3
  2.      
   1. Dadi ndiye mchuma riziki – yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kulisha jamaa yake. Pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya na mapambo.
   2. Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.
   3. Kidawa hakubali kuwa mwanaume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu.
   4. Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui
   5. Dadi anaosha nyumba, kufagia na hata kupiga nguo pasi.
   6. Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na athari za usasa.
   7. Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya hivyo anaumia sana.
   8. Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula
   9. Kila mara Dadi alitarijiwa kuwa baada ya kula anageviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha.
   10. Dadi anapoamua kuzua mpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu, anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaanguka na kuumia. 10x10=10 (zozote 10)
 5.      
  1.        
   1. Mzee mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa.
   2. Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala ya taifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kuperurusha sherehe nyumbani kwake.
   3. Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. Dj na wenzake wanaliwa pesa za serikali kusimamia sherehe.
   4. DJ anaipunja serikali kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka la dawa.
   5. Dj anaifilsi serikali kwa kupokea huduma za maji umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
   6. Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa Mbura wanahudhuria sherehe zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
   7. Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula kuwaleta jamaa wake shereheni na mapambo.
   8. Vyakula katika sherehe vinanunuliwa kwa pesa za umma. Pesa hizi zingetumika kuendeleza asasi za kijamii.
   9. Viongozi wa serikali kama vile Sasa na Mbura wanaamua kujipakulia chakula kupita kiasi.
   10. DJ kupewa kazi ya mipango na mipangilio katika sherehe ilhali kuna mawaziri wawili wanaolipwa mshahara kwa kazi hiyo. (10x1=10)
    (zozote 10)
  2.        
   1. Mamake mashaka alifariki tu baada ya kumzaa.
   2. Babake Mashaka naye alifariki muda mfupi tu baada ya mkewe Kufa. Mashaka akawa yatima
   3. Mamake mlezi naye Biti Kidebe daima alikuwa na maumivu ya mguu hivyo ilibidi waleane
   4. Mashaka alikulia katika mazingira magumu ya kufanya kazi ya kijungu jiko k.m kufyeka.
   5. Mashaka alifungishwa ndoa ya mkeka na mzee Rubeya.
   6. Mkosi wa kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa ajili ya umaskini – wanatorokea Yemeni kuondokea aibu ati.
   7. Mkewe (Waridi) alimtoroka, akaenda na watoto wote bila taarifa.
   8. Mkosi wa kupata pacha mara tatu wakaishia kuwa na watoto wengi. Hawatoshelezi malazi hivyo anaombea wavulana mahali jikoni kwa jirani.
   9. Mkosi wa paa lao kuvuja nyakati za mvua
   10. Mshahara aliopewa na kampuni ya ZWS ulikuwa mdogo sana.
    10x1=10
    (zozote 10)
 6. MWONGOZO WA USHAIRI.
  1. Ni safari ya kupigania uhuru/safari ya kutafuta haki/harakati za kujiendeleza kiuchumi. Anasema walishikana kwenye safari ya haki. Anataja kuteremsha miliki.
   1x2=2
   kutaja alama 1
   Kueleza alama 1
  2. Maelezo ya (maana ya) kinaya yawepo
   Kinyume cha matarajio
   1. Viongozi wachache waliofika kileleni walijawa na uchoyo, wakaamua kujinufaisha.
   2. Walijitengenezea makazi ya raha, wakajinyakulia vyeo wakakaa kufurihiki huku wakiwasahau waliowakweza mamlakani.
   3. Wakawa ndio pekee waliofaidi matunda ya uhuru ambayo yalikuwa yamepiganiwa na wote.
   4. Viongozi wamefika hadi kuwadharau raia waliowapa hivyo vyeo – wanawatemea mate.
   5. Raia kupigania uhuru na baadaye kutofaidika kwao.
    (3x1=3)
    (kueleza kinaya/kujitokeza kwa kinaya alama 1)
  3.      
   1. Msuko – Mshororo wa mwisho una mizani chache kuliko mingine/umefupishwa.
   2. Ukara- Vina vya kati/ndani vinabadilika. vya mwisho/nje vinatiririka.
    2x1=2
    Kutaja- 1 ½ , kueleza ½ = 1 )
  4. Wawakilishi/viongozi walijikuta katika hali nzuri sana za maisha ya tamaa ya kujinufaisha ikazidi. Walishiriki starehe za kila hali hii walisahau wananchi/raia waliowakweza katika nafasi hizo za uongozi, na ambao ndio waliokuwa na nyenzo za kuwafanya kufikia hali yao ya sasa. (alama 4)
  5.        
   1. Inkisari – tukawa’chia – kutosheleza idadi ya mizani
   2. kufinyanga sarufi – kialeni wadiriki – Wadiriki
    kileleni – kuleta urari wa vina.
   3. Tabdila – shaki – badala ya shake – kuleta urari wa vina.
   4. Msamiati kikale – kialeni – kileleni
    kulipa shairi mapigo ya kimuziki.
    2x1=2
    (kutaja – ½ maelezo ½ =1
  6.    
   1. Urudiaji wa silabi – Ki, ti, to, zo, vi, te
   2. Urudiaji wa maneno – safari - ubeti 1,3, 7, 8
    mbele ya safari – ubeti 7,8
    2x1=1
  7.      
   1. Taswira hisi –shangwe kwetu na fahari. ubeti 3
   2. Taswira ya mwendo – kwenda safari ya haki. Ubeti 1
   3. Taswira oni – Tukiwa migongo wazi, tukainama kwa shaki. Ubeti 6.
    wamo wanatema mate. ubeti 8
    2x1=2
  8.    
   1. Takriri/uradidi – safari, tulijizatiti, mbele ya safari.
   2. Tashhisi/uhuishi- kijasho kinatuita – ubeti 5.
    2x1=2
  9.      
   1. Toni ya masikitiko/kuhuzunisha/kuhurumia- safari ilianza kwa dhiki
    • jaa ikawa thabiti, na kiu kutamalaki.
    • Wamo wanatema mate, kwa umati halaiki.
     1x1=1
     (Kutaja ½ kueleza ½ =1)
 7. FASIHI SIMULIZI.
  1.        
   1. Nyiso/wimbo wa tohara. Anayeimbiwa anahimiza kukabiliana na ukali wa kisu kwa ujasiri. (2x1=2)
  2.      
   1. Ufugaji – akivumilia atapewa mbuzi
   2. Kilimo – Atapata shamba la mahindi (2x1=2)
  3.        
   1. Taswira uoni – simama jicho liwe juu.
   2. Taswira mwendo – uhamie kwa wasiokatwa. 2x1=2
  4.      
   1. Takriri/uradidi – kikali, kikali
    kisu, kisu
   2. Tashbihi – usiwe kama msichana 2x1=2
  5.        
   1. Mwimbaji anasema kuwa waoga ni wa akina mama anayeimbiwa.
   2. Wanaume wa mbari ya mwimbaji si waoga wa kisu.
   3. Anayeimbiwa anaarifiwa kuwa fahali alichinjwa ili awe mwanaume.
   4. Anahimizwa asiwe muoga kama msichana.
    4x1=4.
  6.      
   1. Kuwaandaa vijana kwa uchungu watakaouhisi kupitia kijembe
   2. kuhimiza ujasiri na kukejeli uoga.
   3. kusifu wahusika kwa ujasiri wa kukabili kisu na kuingia katika utu uzima.
   4. Kuelekeza vijana kwenye matarajio mapya ya jamii.
   5. Kukuza umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuwaleta wanajamii pamoja.
   6. Kuonyesha vijana wamevuka kutoka utotoni hadi utu uzima.
   7. Kuburudisha waliohudhuria shughuli ya jando au unyago.
   8. kufunza majukumu katika utu uzima.
    8x1=8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Butere Mock Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest