MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ina alama 20
- Kila insha lazima iandikwe ;kwa lugha ya Kiswahili
- Insha zote sharti ziandikwe katika kijitabu cha majibu ulichopewa

MASWALI
- Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Elimu imeanzisha mfumo mpya wa elimu almaarufu CBC . Mwandikie barua mhariri wa gazeti la Taifa Leo ukitoa maoni yako kuhusu changamoto zinazotokana na mfumo huu.
- Magonjwa ya kuambukizana yanaleta hasara kubwa katika nchi na jamii kwa jumla. Fafanua.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
Mwana hutazama kisogo cha nina. - Anza kwa kifungu kifuatacho. Ni kweli mama ana haki ya kusamehewa , kwani hakuna binadamu hata mmoja aliyekamilika…

Mwongozo wa kusahihisha karatasi ya kwanza
Swali 1
Changamoto za CBC
- Walimu wengi wangali wanatatizika jinsi ya kuendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi.
- Mtaala wa CBC unawahitaji wanafunzi watumie asilimia kubwa ya muda uliotengewa somo wakijifunza kwa vitendo wakiwa pamoja hivyo muda mwingi hupotezwa
- Changamoto nyingine ni ile ya kutathmini kazi ya kila mwanafunzi katika kila kipindi. Wanafunzi wanashindwa kutekeleza hilo kwani muda ulioratibiwa kwa somo unaonekana mfupi kuliko mafunzo yanayohitajika kukamilishwa.
- Masomo kama vile muziki, sanaa ya uchoraji, somo la kilimo na mkengine ambayo yanatoa changamoto Nyingi kwa walimu kwani hawajazoea kuyafunza.
- Aidha mbinu zinazo pendekezwa kutumiwa na walimu ni ng`eni na walumu hawana uzoefu wa kutosha.
- Mtaala huu ni ghali mno na unaegemea sana vifaa halisi vya kufunzia.
- Baaadhi ya wazazi hawajasoma. Hawana uwezo wa kuwasaidia wanao.
- Wazazi wanaona kama usumbufu kuambiwa wagharamie vifaa vya kufundishia kila mara.
- Kazi Nyingi ya mtaala huu imeachiwa wazazi.
- Shule za mjini ambako hakuna shamba limekabiliwa na changamoto ya ufunzaji wa somo la kilimo.
- Masomo ni mengi zaidi takribani kumi na tatu kwa mwanafunzi wa gredi ya nne.
- Kuna mzigo mkubwa sana kwa watoto hawa.
- Itakuwa vigumu sana kukadiria viwango vya kufunzu kutoka darasa moja hadi lingine.
- Katika kuanzisha mtaala huu raia hawakutayarishwa kupitia vikao vya umma.
- Wazazi wengi ;hawana vifaa ;kama simu zenye uwezo wa kuchukua picha katika baaadhi ya vipindi ili kuvipeperusha mtandaoni.
- Uchache ;au u haba wa vitabu katika masomo mbalimbali.
- Idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa ni changamoto kwa walimu wanaoutekeleza mtaala huu
- Kuna uhaba wa madarasa yenye mazingira au vifaa vinavyofaaa kufunzia mtaala huu.
Swali 2.
- Vifo
- Kupoteza kazi
- Uchumi kuharibika
- Kuwapoteza watu wenye uwezo wakuzalisha uchumi wa jamii na inchi kwa jumla.
- Kupelejkea kutumia fedha Nyingi katika shughuli za matibabu.
- Watu huingia katika madeni.
- Inasababisha msongo wa mawazo na mfadhaiko wa mawazo.
- Huhatarisha maisha ya watu wengine katika jamii, hasa watoto na walio na magonjwa sugu kama kansa.
- Husababisha uwoga.
- Husababisha unyanyapaa.
- Walio wagonjwa huwa na mkabala hasi kujihusu na kuhusu maisha kwani huona kama watakufa.
- Hafanya watu kutengwa na jamii yao hata ile ya kimataifa.
- Inapunguza kinga mwilini na hivyo kumweka mgonjwa katika hatari ya kifo.
Swali 3
Mwanafunzi aandike kisa kitakacho onyesha kuwa katika maisha wale wadogo/wachanga huwafuata wakuu wao/walezi/waelekezi/vielelezo
Visa vinaweza kulenga:
- Mtoto atakayefuata mienendo ya wazazi wake
- Wafanyikazi wadogo watakaofuata mienendo ya wakuu wao.
- Mwanafunzi anayefuata mwalimu wake.
- Viongozi wa chini kama vile wabunge, watakaofuata Rais
Swali la nne
Kisa kilenga muktadha wa familia ilioachana kwa sababu fulani lakini wameafikia makubaliano ya kusameheana.
Tanbihi: insha ya 3 na 4 …kisa cha mwanafunzi ndicho maudhui hivyo mwalimu akitathmini kikamilifu.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates