Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Eagle II Joint 2021 Mock Exams

Share via Whatsapp

Maagizo

 1. Jibu maswali yote
 2. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali
 3. Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki
 4. Karatasi hii ina kurasa 9 zilizopigwa chapa
 5. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali

Upeo

Alama

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 


MASWALI

 1. UFAHAMU: (Alama 15)

  Soma kifungu kifuataco kisha ujibu maswali.

  Nchi nyingi duniani zimetia sahihi mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto. Haki hizi ni pamoja na uhai, lishe bora inayotosha na makazi bora yaliyo salama. Hali kadhalika, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu inastahili kutokewa bure, iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi. Isitoshe, mtoto hastahili kupigwa, kudunishwa, wala kubaguliwa kwa namna yoyote ile; iwe kitabaka, kirangi, kijinsia au vinginevyo. Mtoto hapaswi kufanya kazi za kitumwa, nzito na za kushurutiswha. Vile vile, mtoto ana haki ya kutunzwa na kulindwa dhidi ya hali yoyote inayoweza kumhatarisha. Fauka ya haya, mtoto anastahili kushirikiswa katika kufanya maamuzi yanayoweza kumwathiri maishani. Pia, mtoto ana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum na habari kuhusu masuala mbalimbali. Pamoja na hayo, mtoto anastahili kupendwa na kuheshimiwa kimawazo na kihisia.

  Haki za watoto zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, serikali na wazazi wakiwa katika mstari wa mbele. Hii ndiyo sababu serikali za mataifa mengi zimeshiriksha haki hizi katika katiba na sheria za nchi huska. Yeyote anayezikiuka anapaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Walakini, haki hizi bado zinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. Kuna watoto ambao hawajawahi hata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wengi wa hawa wamejipata wakiselekea kwenye mitaa na hata majaa ya mji na vijiji ambako hulazimika kupitisha usiku hata katika majira ya kipupwe na masika! Wengine hawapati chakula; licha ya kuwa wanatakiwa kupata chakula chenye lishe bora. Kwao kutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi; kwani hata awamu moja ni adimu kupata! La kusikitisha ni kwamba wale wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaoongozwa katika kupalilia ukiukaji wazo. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kushinikizwa kufanya kazi za sulubu kipunda, na kunyanyaswa kijinsia, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Baadhi ya wanaohusika na vitendo hivi hasi huwa wazazi au jamaa wa karibu kama vile wajomba, shangazi au wahudumu wa nyumbani.

  Madhila yanayowapata watoto hayatokei tu katika mazingira ya nyumbani. Mateso huvuka mipaka na kufikia ngazi ya kimataifa. Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Linalokata maini ni kwamba baadhi ya viongozi katika mataifa haya hawafanyi lolote kuwanusuru. Lao huwa kuwatazama watoto wanaotakiwa kuwalinda wakigeuzwa kuwa mababe wa kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi ambayo huwa nanga kwao kubeba, licha ya bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani.

  Mojawapo ya mambo ambayo viongozi nchini humu walilenga shabaha kuyafikia baada ya kujinyakulia uhuru ni elimu kwa wote. Hata hivyo, hii imekuwa kama ndoto isiyotabirika katika baadhi ya janibu. Ni kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelezwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ingali kubwa. Jukwaa la vijiji nchini humu na hata katika mataifa mengine ya ulimwengu wa tatu limesheheni idadi kubwa ya watoto wasioenda shuleni. Kichocheo kikuu cha hali hii ni kwamba wazazi na walezi wamejipata katika lindi la ufukara uliokithiri. Hata wanapojitahidi kujinyanyua na kujikuna wajipatapo kuyakidhi mahitaji ya kielimu ya wanao, wao hujipata wakitapatapa katika kinamasi hicho hicho cha ulitima. Matokeo ni kwamba watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakia kwenye kiza cha ujinga. Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.

  Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima tuungane mikono na kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu utekelezaji wa haki za watoto. Twapaswa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati.

  Maswali

  1. Huku ukitoa mifano mine, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili. (alama 4)
  2. Eleza naman hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
  3. Kwa kurejelea aya ya nne, onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto. (alama 3)
  4. “Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu. (alama 2)
  5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 3)
   1. vigogo…………………………………………………..
   2. huwa nanga kwao………………………………………
   3. kujikuna wajipatapo…………………………………….
 2. UFUPISHO: (Alama 15)

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

  Wataalamu mbalimbali wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu Ziwa Victoria. Juhudi hizi za uchunguzi zimekuwa zikionyesha kwamba ziwa hili ambalo ndilo la pili kwa ukubwa miongoni mwa maziwa yenye maji matamu duniani linaangamia taratibu. Inakisiwa kuwa kukauka kwa ziwa hili kutahatirisha maisha ya watu zaidi ya milioni 30 ambao hulitegemea kwa chakula na mapato. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Masuala ya Bahari na Uvuvi nchini ulionyeshwa kuwa Ziwa Victora linaangamia kwa kiasi cha mita tatu kila mwaka. Hivi sasa baadhi ya fuo zilizokuwa kwenye ziawa hili upande wa Kenya zimekauka. Mandhari ya fuo hizi nayo yameanza kutwaa sura mpya. Badala ya kupata madau na wavuvi wakiendesha shughuli zao katika maeneo haya, huenda isiwe ajabu kupata watoto wakicheza kandanda.

  Rasilimali za samaki ziwani humu zinaendelea kudidimia huku wavuvi wakitupwa kwenye biwi la umaskini. Walisema wasemo kwamba akosaye la mama hata la mbwa huamwa. Wavuvi wamebuni mikakati ya kukabiliana na hali hii ambayo inatishia kukiangamiza kizazi chao. Wengi wao wameaumua kufanya biashara maarufu kwa jina, ‘bodaboda,’ wengine wameingilia kilimo baada ya kushindwa kujikimu kimaisha kutokana na uvuvi. Wavuvi wanaoendelea kuvua samaki katika ziwa hili wamejipata katika hali ngumu ya kiuchumi. Hali hii imewalazimisha baadhi yao kuanza kuvua samaki katika maji ya mataifa jirani; jambo ambalo limewachongea, wengi wakatiwa mbaroni huku wengine wakinyanyaswa na maafisa wa usalama wa mataifa hayo jirani.

  Sekta ya uchukuzi na mawasiliano nayo imeathirika si haba. Shughuli za uchukuzi katika ziwa hili zimetingwa na gugu-maji ambalo limetapakaa kote ziwani. Mbali na gugu-maji hili, shughuli za kilimo cha kunyunyuzia maji zimetanzwa. Kadhalika, kupungua kwa viwango vya maji humu ziwani ni changamoto nyingine ambayo inawashughulisha wanaharakati wa mazingira. Inahofiwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanalipoteza ziwa hili hatua kwa hatua. Hakika, wanasayansi wa masuala ya bahari wameonya kuwa ziwa hili litakauka katika kipindi cha karne moja ijayo!

  Ni dhahiri kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ina jukumu la kulitunza ziwa hili kwa jino na ukucha. Serikali za nchi husika, hususan Kenya, Uganda na Tanzania zinapaswa kutekeleza sheria zinazodhibiti shughuli za uvuvi katika ziwa hili. Mathalan, kuna haja ya kuvua kwa misimu ili kukinga dhidi ya kuangamai kwa rasilimali za samaki. Wavuvi nao hawana budi kushauriwa kuhusu umuhimu wa kufuata kanuni za uvuvi zilizowekwa na kutahadharishwa kuhusu madhara ya kuendesha uvuvi kiholela. Sheria kuhusu aina za nyavu za kuvulia pia inapaswa kutekelezwa kwa ziwa hili, pamoja na kwenye mito iliyo katika ujirani wa ziwa lenyewe. Hatua hii itasaidia kukomesha kusombwa kwa udongo na mbolea kutoka mashambani hadi ziwani. Hali kadhalika, muungano huu unapaswa kuweka sheria za kusimamia matumizi ya maji. Hili litawadhibiti raia wenye mazoea ya kubadhiri maji.

  Isitoshe, serikali za mataifa ya Afrika Mashariki hazina budi kuchunguza viwanda vinavyotupa taka ndani ya ziwa hili. Mbali na kuchafua maji, viwanda hivi vinaangamiza mimea na wanyama wa majini. Uchunguzi huo unapaswa pia kuhusisha mito inayomimina maji katika ziwa hili. Viwanda vyote vinavyotumia maji ya mito kama vile: Nzoia, Yala, Sondu-Miriu, Awach, Kuja na Kagera vinastahili kuchunguzwa pia.

  Juhudi za kufikia ustawi wa kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki zinapaswa kutilia maanani uhifadhi wa Ziwa Viktoria. Kukauka kwa ziwa hili ni sawa na kukauka kwa maazimio na ndoto zote za serikali za nchi husika za kuboresha hali ya maisha ya raia wake. Wakati ni sasa.

  1. Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 70 – 75. (alama 9, 1 ya mtiririko)
   Matayarisho:
   …………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
   Nakala safi:/Jibu
   ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2. Huku ukitumia maneno 50 – 55, eleza masuala muhimu ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (alama 6, 1 ya mtiririko)
   Matayarisho:
   …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..…………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
   Nakala safi:
   ……………………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………...………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
   MATUMIZI YA LUGHA -ALAMA 40
   1. Andika maneno yenye miundo ifuatayo: ( alama 3)
    1. Kipasuo sighuna cha kaakaa laini, irabu ya nyuma kati, kipasuo ghuna cha masine, irabu ya mbele juu
    2. Nazali ghuna ya kaakaa gumu, irabu ya kati chini, nazali ghuna ya ufizi, irabu ya mbele juu
    3. Irabu ya chini kati, irabu ya mbele juu, kipasuo ghuna cha midomo, irabu ya nyuma juu.
   2. Bainisha silabi zinazowekwa shadda katika maneno yafuatayo. ( alama 2)
    1. Mdahalo________________________________________
    2. nyuma ________________________________________
    3. Nta__________________________________________
    4. Wakilisha_____________________________________
   3. Andika sentensi ifuatayo katika umoja. ( alama 1 )
    Kucha za binadamu na kwato za ngamia ni muhimu.
   4. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. ( alama 2)
    Ngoma hizo zao zimeibwa na Rukia.
   5. Tunga sentensi yenye nomino dhahania na kivumishi cha pekee cha dhana ya umilikaji. (al. 2) 
   6. Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.
    1. Atawahudumia wagonjwa watano. Atawahudumia wengine wawili.
     (Unganisha kuonyesha mfuatano wa vitendo ). (alama 1)
    2. Shairi hilo lilikaririwa vizuri na wengi wakafurahi.
     (Badilisha vitenzi vilivyopigiwa mstari kuwa nomino). ( alama 1)
    3. Walimu walipewa chanjo. Wanafunzi hawakupewa.
     (Unganisha iwe sentensi moja kwa kutumia kiunganishi cha kinyume). (alama 1)
    4. Nilifika mapema. Sikuwapata wenzangu. (alama 1)
     (Badilisha iwe sentensi moja ya masharti)
   7. Tunga sentensi ukitumia kihisishi cha kutaka kusikilizwa (alama 1)
   8. Tunga sentensi kuonyesha kihusishi cha ‘a’ unganifu chenye dhana ya umilikaji . (alama 1)
   9. Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo: ( alama 1)
    Yule mwenyekiti amejiponza mwenyewe
   10. Akifisha sentensi ifuatayo: ( alama 2)
    Mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue mtoto aliuliza nani babu.
   11. Andika maneno yenye mofimu zifuatazo: ( alama 2)
    1. Kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja, mzizi, kiishio
    2. Nafsi ya pili umoja, mzizi, kiishio
   12. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: ( alama 3 )
    KN(V+N+V)+KT(TS+T+E)
   13. Eleza matumizi ya ‘i’ kwenye sentensi ifuatayo (alama 2)
    Mitihani i tayari na itafanywa kesho kutwa.
   14. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kukanusha. (alama 1 )
    Mfungwa huyo aliachiliwa huru na kurejea nyumbani.
   15. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali ya mazoea. ( alama 2 )
    Hamisi alisoma riwaya.
   16. Tunga sentensi ukitumia kitenzi ulichopewa na kauli iliyo mabanoni. ( alama 1 )
    Suka (tendata)
   17. Tambua aina za virai vilivyopigwa mistari. (alama 2)
    Wale wote walifurahia msimamo huo wa mahakama jana jioni
   18. Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo ( alama 3)
    Wafula alimkatia nyasi nyingi ng’ombe wake jana asubuhi.
   19. Naam ni kwa kukiri ni kwa kukataa jambo na…………………….ni kwa kujuta. (alama 1)
   20. Juu ni kwa chini ni kwa furaha na………………..ni kwa kali. (alama 1)
   21. Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Ingawa alitia bidi masomoni alifeli mtihani huo
   22. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno: andika. Alama 2

ISIMUJAMII: ALAMA 10
Wewe ni mshukiwa katika kesi ya wizi wa mabavu. Andika sifa kumi za lugha utakayotumia mahakamani unapojitetea.MWONGOZO

 1.                              
  1.                                  
   1. Watoto wananyimwa haki licha ya katiba kulazimu haki hizi zitimizwe.
   2. Mojawapo wa haki hizi ni makazi ilhali watoto wanala mitaani
   3. Watoto hawapati chakula ilhali wanatakiwa ilhali wanatakiwa kupata lishe .
   4. Wanaotakiwa kuzilinda haki za watotot ndio wanaozikiuka.
   5. Wazazi na jamaa wa karibu wanashiriki katika unyanyasaji wa watoto.
  2.                      
   1. Watoto hutekwa na kutumikiswa vitani
   2. Watoto hugeuzwa kuwa mababe wa kuwa na kuuana
   3. Huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili.
   4. Hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi hubeba bunduki nzito (Huwa nanga kwao)
  3.                            
   1. Serikali ilikuwa na shabaha ya elimu kwa wote
   2. Kubuni sera ya elimu bila malipo
   3. Utekelezaji wa sera hii unaendelea
   4. Kunao wanaopigania kuwepo na elimu bila malipo ila ya matatizo yaliyopo/wanangangania kuwepo kwa elimu bila malipo wanaonekana kana kwamba wanaota mchana.
  4.                            
   1. Asilimia ya watoto na watu wazima wasiojua kusoma bado ni kubwa.
   2. Kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wasioenda shuleni.
   3. Wazazi wanaojitahidi kujinyanyua/kujkuna wajipatapo kuyakidhi mahitaji ya kielomu ya wanao wanashindwa/kujipata katika kinamasi hicho hicho cha ulitima
   4. Watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibaki katika kiza cha ujinga.
  5.                        
   1. Vigogo – walio katika mstari wa mbele/wapigaruaji haki za watoto mabingwa wakerekujua/watetezi/wenye mamlaka/viongozi/matamalaki/wapenda kuendeleza elimu ya watoto.
   2. Huwa nanga kwa – mazito kwao, mzigo kwao
   3. Kujikuna wajipatapo – kujitahidi kulingana na uwezo wao/kujaribu kujinyanyua kwa uwezo wao.
 2.                                
  1. Nakala safi:
   1. Wataalamu wamekuwa wakitafiti kuhusu ziwa viktori a.
   2. Linaangamia taratibu/kwa kiasi cha mita tatu kila mwaka
   3. Kukauka kwalo kunahatisha maisha ya wengi
   4. Fuo za upande wa Kenya zimekauka/zimechukua sura mpya.
   5. Rasilmali za samaki zimedidimia na kuleta umaskini
   6. Waruri wanakaribiana na hali hiyo/mikakati
   7. Wengi wanafanya biashara ya bodaboda au kilimo
   8. Baadhi yao wanavua samaki katika mataifa jirani
   9. Wengi wananyanyaswa na maafisa wa mataifa hayo
   10. Uchukuzi na mawasiliano umetingwa na gugu maji
   11. Kilimo cha kunyinyizia maji kimetanzwa
   12. Wanasayansi wameonya kuwa ziwa utakauka katika karne moja iyayo
  2. Nakala Safi
   1. Jumuiya ya Afrika Mashariki itunze ziwa hili.
   2. Serikali zitekele sheria za umri
   3. Waruri washauriane na kutahasharishwa na kuhusu kuwa kicholela
   4. Kilimo kando kando mvua/kando ya ziwa na mito jirani kikomeshwe.
   5. Kuwekwe sheria za maji
   6. Kuchunguza viwanda vinavyopotupa toka ziwani
   7. Uchunguzi uhusisho mito inayomimina maji ziwani.
   8. Kuwepo juhudi za kuhifadhi ziwa.

a). MATUMIZI YA LUGHA -ALAMA 40

 1. Andika maneno yenye muundo ifuatayo: alama 3
  1. Kipasuo sighuna cha kaakaa laini, irabu ya nyuma kati, kipasuo ghuna cha masine, irabu ya mbele juu kodi
  2. Nazali ghuna ya kaakaa gumu, irabu ya chini kati, nazali ghuna ya ufizi, irabu ya mbele juu nyani
  3. Irabu ya chini kati, irabu ya mbele juu, kipasuo ghuna cha midomo, irabu ya nyuma juu. aibu
 2. Bainisha silabi zinazowekwa shadda katika maneno yafuatayo. alama 2
  1. mdhahalo
  2. nyuma
  3. Nta
  4. Wakilisha
 3. Andika sentensi ifuatayo katika umoja. alama 1
  Kucha za binadamu na kwato za ngamia ni muhimu.
  Ukucha wa binadamu na ukwato wa ngamia ni muhimu
 4. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. Alama 2
  Ngoma hizo zao zimeibwa na Rukia.
  Vigoma hivyo vyao vimeibwa na Rukia
 5. Tunga sentensi yenye nomino ya fikra na kivumishi cha pekee cha dhana ya umilikaji.
  Urafiki wenye faida unafaa/ Usomaji wenye faida unahitajika (alama 2)
 6. Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.
  1. Atawahudumia wanafunzi watano. Atawahudumia wengine wawili
   (Unganisha kuonyesha mfuatano). Alama 1
   Atawahudumia wanafunzi watano kisha wengine wawili/na kuwahudumia wengine wawili
  2. Shairi hilo lilikaririwa vizuri na wengi wakafurahi.
   (badilisha vitenzi vilivyopigiwa mstari kuwa nomino). alama 1
   Kukaririwa kwa shairi hilo vizuri kuliwaletea wengi furaha
   Ukariri wa shairi hilo vizuri uliwaletea wengi furaha
  3. Wazee walipewa marupurupu. Vijana hawakupewa.
   (unganisha iwe sentensi moja kwa kutumia kiunganishi cha kinyume). Alama 1
   Walimu walipewa chanjo lakini/ingawa/ilhali/ijapokuwa/ ijapo wanafunzi hawakupewa.
  4. Nilifika mapema. Sikuwapata wenzangu. (alama 1
   (badilisha iwe sentensi moja ya masharti
   Ningefika mapema ningewapata wenzangu/Ningalifika mapema ningaliwapata wenzangu.
   Nikifika mapema nitawapata wenzangu.
 7. Tunga sentensi ukitumia kihisishi cha kutaka kusikilizwa. Alama 1
  Jamani! mnisikilize/Pulika! Maisha haya siyapendi/Aisee!/hebu!
 8. Tunga sentensi kuonyesha kihusishi cha ‘a’ unganifu chenye dhana ya umilikaji . (alama 1)
  Kiatu cha mtoto kimepotea./ Shamba la wanyama lilimilikiwa na Mtiki
 9. Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo: alama 1
  Yule mwenyekiti amejiponza mwenyewe
    V          N                 T                V
 10. Akifisha sentensi ifuatayo: alama 2
  Mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue mtoto aliuliza nani babu.
  Mzee alimwambia mwanawe, “Njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue.” Mtoto aliuliza. “Nani babu?” au
  “Njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue.”Mzee alimwambia mwanawe. “Nani babu?” mtoto aliuliza. au
  Mzee alimwambia mwanawe aende aliko ili ampeleke kwa babu yake angalau amjue na mtoto akauliza babu alikuwa nani.
 11. Andika maneno yenye mofimu zifuatazo: alama 2
  1. Kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja, mzizi, kiishio
   sili, sinywi, siji
  2. Nafsi ya pili umoja, mzizi, kiishio
   Ucheze /usome, ule
 12. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: alama 3
  KN(V+N+V)+KT(TS+T+E)
  1. Yule mtoto mrembo alikuwa akipika jikoni.
  2. Eleza matumizi ya ‘i’ kwenye sentensi ifuatayo (alama 2)
   Mitihani i tayari na itafanywa kesho kutwa.
   • kitenzi kishirikishi kipungufu
   • kiambishi ngeli
 13. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kukanusha. Alama 1
  Mfungwa huyo aliachiliwa huru na kurejea nyumbani.
  Mfungwa huyo hakuachiliwa huru wala kurejea nyumbani/na hakurejea nyumbani
 14. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali ya mazoea. Alama 2
  Hamisi alisoma riwaya.
  Hamisi alikuwa akisoma riwaya/alikuwa anasoma riwaya
 15. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kuzingatia kauli zilizo mabanoni. alama 1
  Shangazi alisokota mkeka.
 16. Tambua aina za virai vilivyopigwa mistari. (alama 2)
  Wale wote walifurahia msimamo huo wa mahakama jana jioni.
  RN RT RH RE ½ X 4=2
 17. Naam ni kwa kukiri la hasha ni kwa kukataa jambo na Mungu wangu/ Ole wangu ni kwa kujuta. Alama 1
 18. Juu ni kwa chini , huzuni ni kwa furaha na tamu/butu ni kwa kali. Alama 1
 19. Bainisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
  Ingawa alitia bidi masomoni alifeli mtihani huo
  • Ingawa alitia bidii masomoni- kishazi tegemezi
  • Alifeli mtihani huo –Kishazi huru
 20. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno: andika. Alama 2
  Maria aliwaandikia wageni meza kisha akaenda kuwaandikia watoto barua

ISIMUJAMII: ALAMA 10
Wewe ni mshukiwa katika kesi ya wizi wa mabavu. Andika sifa kumi za lugha utakayotumia mahakamani unapojitetea.

 1. Matumizi ya msamiati maalum wa kisheria kama vile kukata rufaa, korti, faini.
 2. kuzingatia urasmi wakati wowote kwa kuwa kortini ni sehemu rasmi.
 3. Kunukuu vifungu vya sheria ili kuondoa shaka.
 4. Lugha ya unyenyekevu ili hakimu apate huruma na kutoa hukumu hafifu.
 5. Urudiaji ili kuweka wazo wazi au kusisitiza wazo hilo.
 6. Kanuni za kisarufi huzingatiwa kwa kiasi kikubwa ili kukinga dhidi ya kupotosha maana.
 7. Kauli fupi fupi wakati wa kujibu maswali ya wakili au jaji. Kuchanganya msimbo/ndimi ili kurahisha mawasiliano.
 8. Lugha ya ushawishi ili kutoa utetezi ili kupata kuachiliwa.
 9. Toni ya huzuni na unyenyekevu ili hakimu apate kunionea huruma.
  Kubali hoja nyingine zinazoakisi sajili hii 10 x1=10
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Eagle II Joint 2021 Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest