Kiswahili Paper 3 Questions - Eagle II Joint 2021 Mock Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

 1. Karatasi hii ina sehemu tano: A, B, C, D na E
 2. Jibu maswali manne pekee
 3. kila swali lina alama 20
 4. Swali la kwanza ni la lazima
 5. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja

Kwa matumizi ya mtahini pekee.

Swali

1

2

3

4

5

6

7

8

Upeo

               

Alama

               

Jumla

               

UPEO

80

ALAMA ZA MTAHINIWA

 


MASWALI

SEHEMU YA A: KIGOGO (alama 20)

 1. Swali la lazima
  “ lisilowezekana ni kukama ndume…….hujafa hujaumbika”
  1. Eleza muktadha wa dondoo (al 4)
  2. Taja na ueleze mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili (al 2)
  3. Fafanua umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. (al 4)
  4. Jadili mbinu zozote kumi walizozitumia Wanasagamoyo kujikomboa kutoka uongozi dhalimu katika jimbo la Sagamoyo. (al 10)
   SEHEMU YA B: RIWAYA YA CHOZI LA HERI (ALAMA 20)
   (Jibu swali la 2 au 3)
 2. “Haidhuru kuwa huenda wimbo huu unawaghasi waliolala. Atakalo mwimbaji huyu ni kuzitakasa hisia zake”
  1. Fafanua kwa hoja kumi na mbili sababu zinazomfanya mhusika anayerejelewa kutaka kuzitakasa hisia zake (al 12)
  2. Kwa kurejelea riwaya nzima ya Chozi la Heri, onyesha matumizi ya kinaya (al 8)
 3. “Hata hivyo maneno yake yalitupa matumaini. Uso wa kila mmoja wetu ulitwaa mng’ao na utulivu…”
  1. Onyesha jinsi mbalimbali zinazodhihirisha kwamba warejelewa walipewa matumaini kwenye mandhari ya dondoo hili. (al 10)
  2. “Kikulacho ki nguoni mwako” Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea wahusika mbalimbali kwenye riwaya ya Chozi la Heri. (al 10)
   SEHEMU YA C: HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
   (ALAMA 20)
   (Jibu swali la 4 au 5)
 4.                            
  1. MAME BAKARI – Mohammed Khalef Chassany
   “ Ubahimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake.” Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya Mame Bakari (al 10)
  2. MASHARTI YA KISASA – Alifa Chokocho
   “Hatimaye Dadi ilimbidi kuusikitikia ule uzuri ambao unapelekwa kwingine wala si kwake. Na tazama ile kanzu jinsi ilivyomfika magotini kidawa. Tazama anavyoiacha wazi ile miguu na miundi yake yenye kuvutia. Ndiyo, hata yeye Dadi , akifuatana na mkewe Kidawa, wakipitana njiani wanawake wanaovaa hivyo huwatumbulia macho. Kwa nini basi wanaume wengine wasimtumbulie macho mke wake yeye ? Na kidawa akimwona mumewe anawatumbulia macho wanawake hubwata kwa kimombo “ Stop your gaze! ” Na yeye humwuliza, ndiyo anasema nini ? Na kidawa hujibu , “ Acha kukodolea wanawake macho. Kwa nini wasiwe na uhuru wa kuvaa wanavyopenda ? Au huelewi wanawake wana uhuru ? “My dress my choice!” Lakini yeye hatimaye hujiuliza : Itakuwaje dunia iwapo watu wote (sio wanawake tu ) watavaa wanavyopenda?
   1. Jadili aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (al 4)
   2. Kando na taswira, tambua mbinu sita za kimtindo katika dondoo. (al 6)
 5. Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (Alama 20)
  1. Tumbo Lisiloshiba
  2. Mapenzi ya Kifaurongo
  3. Ndoto ya Mashaka
  4. Mtihani wa Maish
   SEHEMU YA D: USHAIRI
   Jibu swali la 6 au 7
 6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Maendeleo ya umma
  Sio vitu maghalani
  Kama tele vimesaki
  Lakini havishikiki
  Ama havikamatiki
  Ni kama jinga la moto
  Bei juu

  Maendeleo ya umma
  Sio vitu gulioni
  Kuviona madukani
  Kuvishika mikononi
  Na huku wavitamani
  Kama tamaa ya fisi
  Kuvipata ng’o

  Maendeleo ya umma
  Sio vitu shubakani
  Dhiki ni kwa mafakiri
  Nafuu kwa matajiri
  Ni wao tu washitiri
  Huo ni uistimari
  Lo! Warudia

  Maendeleo ya umma
  Ni vitu kumilikiwa
  Na wanyonge kupatiwa
  Kwa bei kuzingatiwa
  Bila ya kudhulumiwa
  Na hata kuhadaiwa
  Hiyo ni haki.

  Maendeleo ya umma
  Dola kudhibiti vitu
  Vijapo nchini mwetu
  Na kuwauzia watu
  Toka nguo na sapatu
  Pasibakishiwe na kitu
  Huo usawa.

  Mendeleo ya umma
  Watu kuwa na kauli
  Katika zao shughuli
  Vikaoni kujadili
  Na mwisho kuyakubali
  Maamuzi halali
  Udikteta la.

  Maendeleo ya umma
  Watu kuwa waungwana
  Vijakazi na watwana
  Nchini kuwa hakuna
  Wote kuheshimiana
  Wazee hata vijana.

  Maswali;

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (Ala 2)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (Ala 2)
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (Ala 2)
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya (ala 2)
  5. Eleza mambo ambayo mshairi anachukulia kuwa maendeleo halisi ya umma (ala 4 )
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano (Ala 2)
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (Ala 1)
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (Ala 1)
  9. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Ala 4)
   AU
 7. Soma shairi hili kisha uyajibu maswali;

  Jicho, tavumiliaje, kwa hayo unayo?
  Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo?
  Kwacho, lijalo nalije, nimechoka vumiliyo
  Naandika!

  Moyo, unao timbuko, maudhi tusikiayo
  Nayo, visa na mauko, wanyonge yawakutayo,
  Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
  Naandika!

  Hawa, wanatumuliya, dhiki wavumiliayo
  Hawa, mamiya, na mali wazalishayo
  Hawa, ndo wanaumiya, na mafia wakutayo
  Naandika!

  Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
  Hawa, huwapa unene, watukufu wenye nayo
  Hawa, bado ni wavune, kwa shida waitikayo
  Naandika!

  Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
  Bado, tofauti sana, kwa pato na mengineyo
  Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo.
  Naandika!

  Maswali

  1. Ni nini shabaha ya mwandishi aliyetunga shairi hili? (Ala 4)
  2. Eleza kwa kutoa sababu bahari kwa kuzingatia vina,kibwagizo ,idadi ya vipande na mishororo (Ala4)
  3. Je, mwandishi ametumia mbinu zipi ili kutimiza mahitaji ya kiarudhi? (Ala 2)
  4. Eleza mbinu za kimtindo alizotumia mshairi (Ala 4)
  5. Andika ubeti wa nne katika lugha nathari? (Ala 4)
  6. Tambua nafsi neni katika shairi hili ( Ala 2)
 8. SEHEMUYA E: FASIHI SIMULIZI
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
  Basi Kizito Matukio alipewa cheo kikubwa kutokana na uchapakazi wake. Shirika alilokuwa akifanya kazi likawa na matumaini makubwa. Kizito naye badala ya kuchapa kazi akawa anajigamba na kujitapa mitaani, “Ukubwa ninaujua miye. Mimi ndiye kizito hapa, Kizito mzito mimi , akaringa. Akawadharau akina Wanjiku, Amina na Shikuku. Akajitosa kwenye raha bila kujali na kuvaa suti nzito alizoagizia kwa fedha za shirika . Muda si muda shirika likaingia hasara. Mwishowe ametimuliwa kazi na wazito wenyewe. Ameondoka na mkoba mzito wa madeni na fedheha: nguo sasa anavaa za matambara mazito! Jamani uzito unakowapeleka wazito.
  1. Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (alam 4)
  2. Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu (ala2 )
  3. Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (ala 4)
  4. Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (ala 3)
  5. Eleza hasara nne za miviga (ala 4)
  6. Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa (ala 3)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Eagle II Joint 2021 Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest