Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Wewe kama msimamizi wa mifumo ya elimu umealikwa na mwandishi wa habari ili kuhojiwa  kuhusu changamoto zinazokumba mfumo mpya wa elimu ya umilisi. Andika mahojiano hayo.
 2. Serikali za majimbo zitawafaa wananchi wote. Fafanua.
 3. Mchagua nazi hupata koroma. Thibitisha ukweli wa methali hii.
 4. Anza insha kwa maneno haya;  Nilizinduka jimbi la kwanza na kujiandaa kwenda katika hafla…….


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.    
  1. Majina ya waliohojiwa na mhoji au vyeo vyao huandikwa upande wa kushoto wa karatasi.
  2. Koloni hutenga majina haya na maswali au majibu hufuata.
  3. Huanzia na maswali mepesi na kuelekea yale magumu. Mawazo yafuatane na kuwiiana.
  4. Maswali ni ya kuendeleza mahojiano na kumchochea mhojiwa kutoa habari inayotakikana.
  5. Maswali yampe mhojiwa nafasi ya kutoa maelezo kikamilifu.
  6. Hitimisho humpa mhojiwa nafasi ya kufikisha mawazo yake ukingoni. Yasihitimishwe kwa ghafla.
   Baadhi ya hoja
   Changamoto za mfumo wa umilisi (CBC)
   • Walimu wengi wangali wanatatizika jinsi ya kuendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi.
   • Mtaala wa CBC unawahitaji wanafunzi watumie asilimia kubwa ya muda uliotengewa somo wakijifunza kwa vitendo wakiwa pamoja hivyo muda mwingi hupotezwa
   • Changamoto nyingine ni ile ya kutathmini kazi ya kila mwanafunzi katika kila kipindi. Wakufunzi wanashindwa kutekeleza hilo kwani muda ulioratibiwa kwa somo unaonekana mfupi kuliko mafunzo yanayohitajika kukamilishwa.
   • Masomo kama vile muziki, sanaa ya uchoraji, somo la kilimo na mengine ambayo yanatoa changamoto nyingi kwa walimu kwani hawajazoea kuyafunza.
   • Aidha mbinu zinazopendekezwa kutumiwa na walimu ni ngeni na walimu hawana uzoefu wa kutosha.
   • Mtaala huu ni ghali mno na unaegemea sana vifaa halisi vya kufunzia. 
   • Baaadhi ya wazazi hawajasoma. Hawana uwezo wa kuwasaidia wanao.
   • Wazazi wanaona kama usumbufu kuambiwa wagharamie vifaa vya kufundishia kila mara.
   • Kazi nyingi ya mtaala huu imeachiwa wazazi.
   • Shule za mjini ambako hakuna shamba zimekabiliwa na changamoto ya ufunzaji wa somo la kilimo. 
   • Masomo ni mengi zaidi takribani kumi na matatu kwa mwanafunzi wa gredi ya nne. Kuna mzigo mkubwa sana kwa watoto hawa.
   • Itakuwa vigumu sana kukadiria viwango vya kufuzu kutoka darasa moja hadi jingine.
   • Katika kuanzisha mtaala huu raia hawakutayarishwa kupitia vikao vya umma.
   • Wazazi wengi hawana vifaa kama simu zenye uwezo wa kuchukua picha katika baaadhi ya vipindi ili kuvipeperusha mtandaoni.
   • Uchache au uhaba wa vitabu katika masomo mbalimbali.
   • Idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa ni changamoto kwa walimu wanaoutekeleza mtaala huu.
   • Kuna uhaba wa madarasa yenye mazingira au vifaa vinavyofaaa kufunzia mtaala huu. 
 2.      
  • Itawashirikisha wananchi wote katika maamuzi yanayowahusu
  • Raslimali za kifedha zitasambazwa katika majimbo yote bila ubaguzi wowote.
  • Itahimiza uwajibikaji wa viongozi na wafanyikazi wote.
  • Itatoa nafasi zaidi za ajira kwa wananchi wa jimbo mbalimbali na taifa zima  
  • Uimarishaji wa miundo misingi k.v. maji, barabara, nyumba, hospitali n.k.
  • Itasuluhisha tatizo la ukabila nchini
  • Itazua mashindano ya utendaji bora wa kazi baina ya viongozi wa majimbo mbalimbali
  • itaimarisha umoja wa wanajamii
 3.      
  • Koroma ni nazi iliyo karibu kupevuka yaani hali baina ya nazi na dafu. Maana yake: mtu anayependa kuziangalia- angalia nazi ili apate zuri sana huishia kuchagua ili ambayo ni  changa.
  • Haifai kupoteza wakati kwa kutahadhari sana kabla ya kutenda jambo.
  • Mtu asichukue muda mrefu kabla ya kulitenda jambo linalostahili kutendwa
   *Ni sharti maudhui yaoane na maana ya  methali.
 4.      
  • Yaliyomo kwenye mwili yaoane na maneno yaliyoanza insha.
  • Mada ikuzwe kikamilifu ili kuibua taharuki
  • Mbinu za uandishi kama vile methali , tashbihi n.k. zitumiwe kwa njia ifaayo.
  • Kisa kionyesha kuamka mapema ili kuhudhuria sherehe fulani.

USAHIHISHAJI

Karatasi hii imedhamiria kutahini uwezo wa mtahniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mwanafunzi, kwa mfano kutunga sentensi sahihi, zenye utiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawázo asilia. Ubunifu rnwingi na hati nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe na lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.

Mtahini lazima asome insha yote ili aweze kukadiria viwango rnbalimbali vilivyopendekezwa.

KIWANGO CHA D
01-05

 1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.
 2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahill kwa njia inayofaa.
 3. Lugha imevurugika, uakifishaji usiofaa na insha ina makosa ya kila aina ya kisarufi, kimaendelezo, mtindo mbovu u.k

VIWANGO TOFAUTI VYA D
D- (KIWANGO CHA CH1NI)
Maki 01-02
Insha haina inpangilio maalum na haiweleweki kwa vyovyote vile. Kama vile kunakili au kujitungia swali na kulijibu,..
D WASTANI
Maki O3

Utiririko wa mawazo haupo, na insha haieleweki. Makosa ni mengi
D+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 04-05
Ingawa insha hii ina lugha dhaifu ya Kiswahili na makosa mengi ya kila aina, unaweza kutambua kile ambacho anajaribu kuwasilisha.

KIWANGO CHA C
Maki 06-10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo.

 1. Mtahiniwa anaweza kuwasilisha mawazo yake lakini kwa kiwango kisichoeleweka kikamilifu.
 2. Hana uhakika wa matumizi ya lugha.’
 3. Mada huwa haikukuzwa au kuendelezwa kikamilifu.
 4. Mtahiniwa anaweza kupotoka hapa na pale
 5. Kujirudiarudia ni dhahiri.
 6. Mpangilio wake wa kazi ni hafifu na hauna mtiririko
 7. Hana matumizi mazuri ya lugha.
 8. Mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza ambayo huonekana dhahiri, kama vile “papa” badala ya    “baba”“chakura” badala ya” chakula”, “juki” badala ya “chuki”, “tata” badala ya “dada” u.k

C- ( KIWANGO CHA CHINI)
Maki 06-07
Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
Hana msarniati ufaao wala muundo wa sentensi.
Ana makosa mengi yamsamiati, hijai na matumizi mabaya ya sarufi.

C (WASTAN1) Maki 08

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwä njia hafifu.
 2. Hufanya makosa mengi ya sarufi.
 3. Hana ubunifu wa kutosha.
 4. Katika sentensi ndefu uakifishaji wake ni mbaya.
 5. Ana makosa kadha ya hijai na msamiati.

C+ ( KIWANGO CHA JUU)
Maki 09- 10

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri Iakini kwa njia isiyo na mvuto sana
 2. Dhana tofauti hazijitokezi
 3. Anatumia misemo, methali, tashbihi, tanakali za sauti n.k kwa njia isiyofaa.
 4. Utiririko wa mawazo bado haujitokezi wazi.
 5. Kuna makosa machache ya sarufi na hijai.

KIWANGAO CHA B

 1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anoiomyesha kijjimudu lugha vilivyo.
 2. Mtahiniwa hudhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
 3. Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
 4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti na ikaleta maana sawa.
 5. Mada huwa imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.

VIWANGO TOFAUTI VYA B 
B- (KIWANGO CHA CHIN1)
Maki 11 - 16

 1. Mtahiniwa huwasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti..
 2. Kuna mtiririko mzuri wa mawazo.
 3. Ana uwezo Wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
 4. Makosa machache yanaweza kutokea hapa na pale

B (WASTANI)
Maki 13

 1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
 2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo
 3. yanayodhihirika.
 4. Matumizi ya lugha ya mnato huweza kudhihirika.
 5. Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
 6. Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika.
 7. Makosa ni machache hapa na pale.

B+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 14- 15

 1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia 4yovutia kwa urahisi.
 2. Kuna makosa ya hapa na pale ambayo mtahiniwa hakudhamiria kuyafanya
 3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri.
 4. Sarufi yake ni nzuri•
 5. Uakifishaji wake ni mzuri.

KIWANGO CHA A
Maki 16-20

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa rnawazo yanayodbihirika na kutiririka.
 2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia iliyo bora na kwa urahisi.
 3. Uumbuji wake hudhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.

VIWANGO TOFAUTI VYA A
A- (Kiwango cha chini) - maki 16-17

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha 
 2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada
 3. Ana pamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi
 4. Anazingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi
 5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi
 6. Makosa ni machache yasiyokusudiwa

A WASTANI   - Maki 18

 1. Mawazo yanadhihirika wazi.
 2. Makosa ni machache mno.
 3. Hutumia lugha ya mnato.
 4. Hutumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia.
 5. Sarufi yake ni nzuri
 6. Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi
 7. Hujieleza kikamilifu

A+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 19-20

 1. Mtahiniwa huwasilisha ujumbe kuiingana na mada
 2. Hutiririsha mawazo yake vizuri zaidi
 3. Hujieleza kikamilifu bila shida.
 4. Hutoa hoja zilizokomaa.
 5. Msamiati wake ni wa hali ya  juu
 6. Makosa ya aina yoyote yasizidi matano
A A+
A
A -
 19-20
18
16-17
B B+
B
B-
14-15
13
11-12
C C+
C
C-
09-10
08
06-07
D D+
D
D-
04-05
03
01-02

JINSI YA KUTUZA INSHA MBALIMBALI

 1. Mtahiniwa asipozingatia sura ya insha aondolewe maki 4 (4sura) baada ya kutuzwa.
 2. Insha isiyotosheleza idadi ya maneno itaondolewa maki 2 baada ya kutuzwa (2u)
 3. Mitindo ya kuandika herufi tofauti tofauti  isiingile sana utahini.
 4. Hati ya mtahiniwa isitiliwe maanani mno.

SARUFI
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea.
Makosa ya sarufi hutokea katika:

 1. Kuakifisha vibaya: mifano, vikomo, vituo, alama ya kuulizia n.k
 2. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake
 3. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi vya nyakati.
 4. Kuacha au kuongeza neno katika sentensi kwa mfano, kwa
 5. Matumizi ya herufi kubwa.

Tazama : Matumizi ya herufi kubwa

 1. Mwanzo wa sentensi
 2. Majina ya pekee
 3. Majina ya mahali, miji, nchi 
 4. Siku za juma, miezi n.k
 5. Mashirika, masomo, vitabu n.k
 6. Makabila, lugha n.k
 7. Mungu 

MAKOSA YA HIJAI
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukiyaonyesha yanapotokea.
Makosa ya tahajia huwa katika:

 1. Kutengainisha neno kama vile ‘aliye kuwa’ 
 2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwasababu’
 3. Kukata silabi vibaya kama vile ‘nguv-u’
 4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno; kama ‘thahari’ badala ya ‘mahali’
 5. Kuacha herufi katika neno kama ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’
 6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno karna ‘piya’ badala ya ‘pia’.
 7. Kuacha alarna inayotarajiwa kuwepo katika herufi km. j badala ya j.
 8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno afikapo pambizo au mwishoau kuandika mahali si pake.
 9. Kukiandika kistari mahali pasipofaa k.m. -alikuwa
 10. Kuacha ritifa au kuiweka pasipofaa
 11. Kuandika maneno kwa kifupi. Mfano k.m nk. k.v 

MTINDO.
Mambo yatakayochunguzwa:

 1. Mpangilio wa kazi kiaya.
 2. Utiririko wa mawazo
 3. Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
 4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
 5. Unadlilifu Wa kazi
 6. Kuandika herufi vizuri km Jj, Pp, Uu, Ww.
 7. Sura ya insha 

MSAMIATI
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.

MAUDHUI NA MSAMIATI
Baada ya kusoma mtungo, utafikiria na kukadiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla.

ALAMA ZA KUSAHIHISHA
= hupigwa chini ya sehemu ambayo kosa la sarufi; limetokeza kwa mara ya kwanza
- hupigwa chini ya sehemu au neno ambako kosa Ia hijai limetokeza kwa mara ya kwanza
^ hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno
√ hutumiwa kuonyesha msamiati bora juu ya msamiati wenyewe
x hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa juu ya msamiati wenyewe

Maelezo mafupi kuhusu tuzo la mtahini yanahitajika. Kila ukurasa uwe na alama ya √chini katikati kuonyesha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo

Urefu utakadirwa ufatavyo;

Maneno 
Maneno 8 kurasa 1%
Maneno 7 kurasa 2
Maneno 6 kurasa 2 ¼ 
Maneno 5 kurasa 2 ¾ 
maneno 4 kurasa 3 ¾ 
maneno 3 kurasa 4 ½ 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?