Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 1

Share via Whatsapp
Maagizo
 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Kila insha lazima  iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 1. Lazima:
  Wewe ni mwakilishi wa vijana katika gatuzi lenu. Kumekuwa na tuhuma za vijana kutumia vibaya simu tamba katika jamii. Andika mahojiano yako na mwanahabari ukitetea namna simu tamba inavyowafaidi vijana.
 2. Fafanua umuhimu wa kudumisha amani nchini wakati wa kampeni na uchaguzi wa kisiasa.
 3. Andika insha inayooana na methali mchuma janga hula na wa kwao.
 4. Andika insha itakayoisha kwa maneno yafuatayo:
  ….nilipogutuka niliangaza macho huku na kule. Aah! Kumbe nilikuwa nikiota!


MARKING SCHEME

 1. Hii ni insha ya mahojiano. Ichukue mtindo wa tamthilia.
  kumb: mwanahabari ndiye anayehoji.
  Baadhi ya hoja ni kama vile:
  1. Kuleta  vijana pamoja duniani na hivyo kupunguza tuhuma zinazoelekea kuleta vurugu kutokana na vijana  kutofahamiana
  2. Usambazaji wa teknolojia inayorahisisha maisha ya vijana kote duniani kupitia kwa huduma zinazotolewa na simu.
  3. Kuendeleza biashara - kubadilishana bidhaa na pesa kupitia mtandao kama vile MPESA.
  4. Hurahisisha  huduma za benki. Vijana  wanaweza kufikia akaunti zao kupitia kwenye rununu.
  5. Huwa na vifaa kama vile vikokotoo vya kurahisisha kufanya hesabu.
  6. Ni chombo cha burudani - vijana hupata michezo mbalimbali.
  7. Huimarisha utafiti. Vijana  wanaweza kufanya utafiti kupitia kwenye rununu.
  8. Huweza kutumiwa kupigia picha, hivyo kuokoa pesa ambazo zingenunulia kamera au video.
  9. Vijana  wanaweza kuwasiliana na familia zao kutoka mbali, hivyo kuokoa muda na fedha ambazo wangetumia kusafiri.
  10. Vijana wnaweza kuhifadhi msahafu(Biblia au Korani) kwenye simu, hivyo kujikuza kiroho kila mara.
  11. Ni njia ya kupata habari kutoka kwenye mashirika ya usambazaji wa habari. Baadhi ya rununu zina redio na hata runinga. Vijana wanaweza kusikiliza na kutazama habari hata wakiwa safarini.
  12. Hufanikisha kuwanasa matapeli na magaidi wanaowadhuru vijana. Baadhi ya rununu huonyesha simuilipopigiwa hivyo kusaidia kudhibiti mitandao ya uhalifu.
 2. Hii ni insha ya ufafanuzi. Mwnafunzi asipinge swali.
  Hoja ni kama vile:
  1. kudumisha umoja na upendo wa wananchi
  2. kuwezesha wananchi kuendeleza biashara zao hivyo kujipatia mapato na kukuza uchumi wa taifa.
  3. kuwawezesha wanasiasa kuuza sera zao bila kutatizika
  4. kuhakikisha usalama wa wananchi
  5. kuendeleza uzalendo kwa kutii sheria na katiba
  6. kuwavutia wawekezaji wa kigeni
  7. kuzuia uharibifu wa mali
  8. kuwezesha masomo kuendelea shuleni
  9. kuwezesha usafirishaji na usambazaji wa bidhaa
 3. Mchuma janga hula na wa kwao
  1. Hii ni insha ya methali
  2. Chuma ni kufanya kazi na kupata faida/ tungua matunda kutoka mtini.
  3. Janga-balaa /baa / shida / hatari / taabu
  4. Ajitafutiaye shida huathirika na jamii / jamaa yake .
  5. Mtahiniwa asimulie kisa /visa vitakavyoafikiana na methali.
  6. Asipinge methali.
   Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza;
   • Mhusika kushiriki raha za kilimwengu, akaambukizwa magonjwa yasiyotibika,hatimaye anarejea nyumbani anakougua , mzigo wa kumtunza unakuwa kwa familia yake.
   • Mhusika aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni au shirika fulani, Anafutwa kazi labda kutokana na uzembe au utovu wa maadili ya kikazi,anarejea nyumbani kwa familia yake; kule hana chochote hivyo basi anaishia kutegemea jamma zake, huu unakuwa mzigo mkubwa kwa watu wake.
   • Mtoto ambaye anatokea kuwa mhalifu, anafikishwa kortini na kutozwa faini kubwa.Hii inakuwa gharama kwa familia yake kwa vile ndio wanaotakiwa kulipia.
   • Mwanafunzi ambaye anakosa kuwajibika masomoni shuleni , anafeli mtihani, maisha ya halafu yanakuwa  magumu kwa hivyo jamaa zake wanalazimika kuingilia kati ili kumuauni kwa mahitaji ya kila siku
   • na kadhalika
 4. Ni insha ya kubuni fikra
  • Azingatie sehemu zote kv utangulizi, mwili, hitimisho.
  • Mtahiniwa atunge kisa kinachomalizia kifungu kilichotolewa.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 1.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?