Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 1

Share via Whatsapp
MAAGIZO;
 • Jibu maswali yote.

SEHEMU A

 1. UFAHAMU  (alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

  Athari za muda mrefu za pombe hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini vya pombe hadi madhara makubwa katika hali ya matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu.

  Viwango vya juu  vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho, ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa na matumizi ya  kila mara ya pombe. Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili. Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.

  Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na kutumia kinywaji kimoja hadi viwili kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swali lenye utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta za dawa, wadau wa sekta ya pombe pia wamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na haipendekezwi kwa ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba.

  Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha. Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwa tahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi ya wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.

  Madhara mabaya ya matumizi ya pombe kwa muda mrefu kupita kiasi ni sawa na yale yanaoonekana katika vitulizi-hipnoti vingine (mbali na sumu kwa viungo ambayo hutatiza zaidi katika pombe). Athari za kujiondoa katika pombe na utegemezi hukaribia sana kufanana. Pombe cha kiwango wastani ina athari chanya na hasi kwa afya. Athari hasi ni pamoja na ongezeko la hatari ya magonjwa ya ini, saratani ya orofarinji, kansa ya umio na magonjwa wa kongosho. Kinyume na hayo, unywaji wastani wa pombe unaweza kuwa na athari  za faida kwa gastritis na kolelithiasi.  Matumizi sugu na mabaya ya pombe huwa na athari kubwa kwa afya mwili na akili. Unywaji sugu wa pombe kupita kiasi au utegemezi pombe, unaweza kusababisha uharibufu mpana wa viungo mbalimbali vya neva za ubongo, mfumo wa neva ugonjwa wa mishipa ya moyo, maradhi ya ini, na neoplamsi isiyopona.

  Matatizo ya akili ambayo huhusishwa na ulevi ni pamoja na mfadhailo mkubwa, disthimia, mania, hipomania, tatizo la hofu, tatizo la wasiwasi wa kijumla, tatizo la tabia za mtu, skizofrenia, kujinyoga, upungufu wa mfumo wa utendekazi mwilini (kwa mfano kazi za kumbukumbu, hisia, kazi za uamuzi, uwezo wa kuona, mwendo na uwiano) na uharibufu wa ubongo, utegemezi wa pombe ni huhusishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi cha iskemi, kansa ya mfumo wa upumuaji, mbali pia na saratani ya mfumo wa mlo, ini, kifua na ovari.

  Unywaji kupita kiasi huhusishwa na ugonjwa wa ini, kama vile sairosi. Tafiti zimelenga wanaume na wanawake, vikundi vya umri mbalimbali na watu wa makundi mengi ya kijamii. Machapisho kwa sasa yanafikia jumla ya mamia huku tafiti zikiweza kuonyesha uwiano uliopo kati ya matumizi wastani ya pombe na afya ambayo labda yanaweza kuwa yalitokana na athari za manufaa ya maingiliano ya kijamii ambayo mara nyingi huambatana na matumizi ya pombe. Baadhi ya njia mahususi ambapo pombe huweza kuathiri afya mishipa ya moyo zimetafitiwa.
  Maswali
  1. Yape makala haya mada faafu. (alama 1)
  2. Eleza madhara yanayotokana na uharibifu wa mfumo mkuu wa neva za pembeni   (alama 2)
  3. Eleza faida za matumizi ya pombe kwa mujibu wa kufungu.         (alama 3)
  4. Mwandishi anapendekeza vipi kwa matumizi ya pombe ya kiwango cha wastani?            (alama 3)
  5. Matumizi sugu yana malipo yapi kulingana na madaktari. (alama 3)
  6. Tafiti zilizofanywa zililenga jinsia ya kiume pekee. Thibitisha. (alama 1)
  7. Eleza maana ya misamiati hii kulingana na taarifa (alama 2)
   1. wadau
   2. aliyebaleghe

SEHEMU B

 1. UFUPISHO  (alama15)                         
  Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yafuatayo

  Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri kuzungumuza na kuwasikiliza wengine wakizumgumuza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumuzo.

  Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumuza kama vile michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumuzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidika katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile alivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka an amefiwa, haya yote  ni ujuzi . Wakati  mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambaye amepatikana na mambo kama hayo hana budi kufahamu zaidi.

  Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayp, karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.

  Inabidi mwanafunzi  asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu taaluma fulani  anayojifunza. Inafaa asome juu ya michezo, mambo, ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.
  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65  (alama 10, 1 ya utiririko)
  2. Kwa kuzingatisha habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho (Maneno 30) (alama 5 , 1 ya utiririko)

SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA NA SARUFI (alama 40)

 1. Andika sauti yenye sifa zifuatazo
  1. Sauti mwambatano ya midomo (alama 2)
  2. Andika neno  lenye muundo ufuatao (alama 2)
   Konsonanti + konsonanti + nusu irabu + konsonanti + irabu
 2. Bainisha vishazi katika sentensi (alama 2)
  Mwanafunzi huyo angelisoma sana, angelifaulu katika mtihani.
 3. Tunga sentensi yenye muundo huu: (alama 2)
  Nomino ya wingi, kivumishi kiradidi, kitenzi kishirikishi kikamilifu, chagizo cha Mahali
 4. Tunga sentensi ukitumia neno  ‘zawadi’ kama kitenzi  (alama 2)
 5. Andika upya katika wakati ujao hali ya mazoea (alama 2)
 6. Taja vigezo viwili vya kuanisha viambishi (alama 2)
 7. Changanua sentensi hii kwa kielelezo cha mstari
  Gazeti hilo litasomwa na mwanafunzi (alama 2)
 8. Ainisha viambishi (alama 2)
  Wasoila
 9. Tunga sentensi yenye vijenzi hivi (alama 1)
  KN(RH+ S)+KT(t+V)
 10. Eleza matumizi ya ‘A’ anganifu katika sentensi (Alama 3)
  1. Mlango wa chuma umenunuliwa.
  2. Msumeno wa kukatia ubao ni huu.
  3. Mwimbaji wa kwanza  yu  jukwaani sasa.
 11. Andika katika udogo
  Kiti hiki cha mwanamke huyu kimevunjika (alama 2)
 12. Eleza matumizi ya koloni na koma katika sentensi (alama 1)
  Nyanya alinunua vitu hivi: pilipili, parachichi, pipi na papai.
 13. Geuza katika hali ya wingi
  Seremala aliunda kasha kwa ubao na kumpa mtume (alama 2)
 14. Taja dhana  za kimaana mbili zilizo katika sentensi (alama 1)
  Ningekuwa na hela ningenunua shamba.
 15. Tunga sentensi venye kishazi tegemezi ambacho ni; (alama 2)
  1. Kielezi cha namna
  2. Kielelezi cha Mahali
 16. Ainisha sentensi hii kwa kuzingatia dhamira (alama 1)
  Komesha mchezo huu kuanzia leo!
 17. Onyesha kwa kutoa mifano miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U-_Zi (alama 2)
 18. Ainisha yambwa katika sentensi hii
  Yaya alitumia kijiko kumpatia mtoto huyo mdogo chakula kitamu (alamu 3)
 19. Andika kitenzi katika kauli ulizopewa kisha ukitungie sentensi (alama 2)
  1. Kauli tendata
  2. Kauli tendama
 20. Eleza maana mbili katika utungo huu (alama 2)
  Fundi alimkatia Makaa utepe huo.

SEHEMU D: ISIMU JAMII(alama 10)
Soma makala haya kisha ujibu maswali;

Rafiki yako amezongwa na mambo magumu na anafikiria suluhu ni kujiua umepewa jukumu la kumshauri.

 1. Utatumia Lugha ya sajili gani? (Alama 2)
 2. Fafanua sifa nane za kimtindo utakazomatumia ili kufanikisha mazungumuzo yako (alama 8)

MARKING SCHEME

SEHEMU A

 1. UFAHAMU(alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

  Athari za muda mrefu za pombe hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini vya pombe hadi madhara makubwa katika hali ya matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu.

  Viwango vya juu  vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho, ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa na matumizi ya  kila mara ya pombe. Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili. Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe

  Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na kutumia kinywaji kimoja hadi viwili kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swali lenye utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta za dawa, wadau wa sekta ya pombe pia wamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na haipendekezwi kwa ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba.

  Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha. Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwa tahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi ya wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.

  Madhara mabaya ya matumizi ya pombe kwa muda mrefu kupita kiasi ni sawa na yale yanaoonekana katika vitulizi-hipnoti vingine (mbali na sumu kwa viungo ambayo hutatiza zaidi katika pombe). Athari za kujiondoa katika pombe na utegemezi hukaribia sana kufanana. Pombe cha kiwango wastani ina athari chanya na hasi kwa afya. Athari hasi ni pamoja na ongezeko la hatari ya magonjwa ya ini, saratani ya orofarinji, kansa ya umio na magonjwa wa kongosho. Kinyume na hayo, unywaji wastani wa pombe unaweza kuwa na athari  za faida kwa gastritis na kolelithiasi.  Matumizi sugu na mabaya ya pombe huwa na athari kubwa kwa afya mwili na akili. Unywaji sugu wa pombe kupita kiasi au utegemezi pombe, unaweza kusababisha uharibufu mpana wa viungo mbalimbali vya neva za ubongo, mfumo wa neva ugonjwa wa mishipa ya moyo, maradhi ya ini, na neoplamsi isiyopona.

  Matatizo ya akili ambayo huhusishwa na ulevi ni pamoja na mfadhailo mkubwa, disthimia, mania, hipomania, tatizo la hofu, tatizo la wasiwasi wa kijumla, tatizo la tabia za mtu, skizofrenia, kujinyoga, upungufu wa mfumo wa utendekazi mwilini (kwa mfano kazi za kumbukumbu, hisia, kazi za uamuzi, uwezo wa kuona, mwendo na uwiano) na uharibufu wa ubongo, utegemezi wa pombe ni huhusishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi cha iskemi, kansa ya mfumo wa upumuaji, mbali pia na saratani ya mfumo wa mlo, ini, kifua na ovari.

  Unywaji kupita kiasi huhusishwa na ugonjwa wa ini, kama vile sairosi. Tafiti zimelenga wanaume na wanawake, vikundi vya umri mbalimbali na watu wa makundi mengi ya kijamii. Machapisho kwa sasa yanafikia jumla ya mamia huku tafiti zikiweza kuonyesha uwiano uliopo kati ya matumizi wastani ya pombe na afya ambayo labda yanaweza kuwa yalitokana na athari za manufaa ya maingiliano ya kijamii ambayo mara nyingi huambatana na matumizi ya pombe. Baadhi ya njia mahususi ambapo pombe huweza kuathiri afya mishipa ya moyo zimetafitiwa.
  Maswali
  1. Yape makala haya mada faafu. (alama 1)
   • Athari za pombe.
   • Madhara ya  unywaji wa pombe
   • Matumizi ya pombe na athari-yoyote mmojawapo
  2. Eleza madhara yanayotokana na uharibifu wa mfumo mkuu wa neva za pembeni   (alama 2)
   • Husababisha matumizi ya kila mara ya pombe.
   • Huathiri ubongo wa vijana waliobaleghe.
  3. Eleza faida za matumizi ya pombe kwa mujibu wa kufungu.         (alama 3)_
   • Ina uwezo wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo.
   • Dawa ya burudani
   • Inaminika kulinda mishipa ya damu .
  4. Mwandishi anapendekeza vipi kwa matumizi ya pombe ya kiwango cha wastani?            (alama 3)
   • Huongeza athari ya kupatwa na majeraha , vurugu, uharibifu wa mimba, saratani, ugonjwa wa kongosho na presha
   • Huchochea  matumizi ya kiwango kikubwa haswa kwa vijana.
   • Pombe ni sumu katika viungo vya mwili.
  5. Matumizi sugu yana malipo yapi kulingana na madaktari. (alama 3)
   • Matumizi sugu huathiri afya ya akili
   • Husababisha uharibifu wa neva za ubongo 
   • Maradhi y aini
   • Huzua ugonjwa wa akili unaozua mahangaiko makubwa
   • Kansa ya upumuaji
  6. Tafiti zilizofanywa zililenga jinsia ya kiume pekee. Thibitisha. (alama 1)
   • Tafiti zinaonyesha jinsia zote na umri huathirika na ugonjwa wa pombe.
  7. Eleza maana ya misamiati hii kulingana na taarifa (alama 2)
   1. wadau – waraibu, watumizi, wanywaji wa pombe, wanaunga mkono
   2. aliyebaleghe – mkubwa wa kimo, mzima ,aliyekomaa 

SEHEMU B

 1. UFUPISHO(alama15)                         
  Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yafuatayo

  Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri kuzungumuza na kuwasikiliza wengine wakizumgumuza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumuzo.

  Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumuza kama vile michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumuzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidika katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile alivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka an amefiwa, haya yote  ni ujuzi . Wakati  mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambaye amepatikana na mambo kama hayo hana budi kufahamu zaidi.

  Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayp, karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.

  Inabidi mwanafunzi  asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu taaluma fulani  anayojifunza. Inafaa asome juu ya michezo, mambo, ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.
  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65  (alama 10, 1 ya utiririko)
   Matayarisho
   • Kia jambo tufanyalio katika lugha hustawisha ufahamu wake.
   • Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma
   • Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.
   • Lugha iliyoandikwa ni ya aina ya mazungumzo
   • Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.
   • Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.
   • Husaidia kufahamu yaliyoandikwa .
   • Hali ya mwanafunzi kujionea sinema ni ujuzi.
   • Matatizo na shida ambazo wanafunzi hupitia pia ni ujuzi.
  2. Kwa kuzingatisha habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho (Maneno 30) (alama 5 , 1 ya utiririko)
   Matayarisho
   • Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni
   • Lugha zote hazina ustawi mwingi
   • Lugha zingine hazina vitabu vingi ama zina vitabu vingi.
   • Mwanafunzi anayesoma anafaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisoma.

SEHEMU C:MATUMIZI YA LUGHA NA SARUFI(alama 40)

 1. Andika sauti yenye sifa zifuatazo
  1. Sauti mwambatano ya midomo (alama 2)
   • pw-bweka
   • pw-pwani
   • mbw-umbwa
  2. Andika neno  lenye muundo ufuatao (alama 2)
   Konsonanti+konsonanti+nusu irabu +konsonanti+irabu
   • Mpyaro
   • Mkweli
   • Mkwezi
   • Mswada
   • Mswaki 
   • mpwake
 2. Bainisha vishazi katika sentensi (alama 2)
  Mwanafunzi huyo angelisoma sana, angelifaulu katika mtihani.
  • Mwanafunzi huyo angelisoma-kishazi tegemezi
  • Angelifaulu katika mtihani.-kishazi tegemezi
 3. Tunga sentensi yenye muundo huu: (alama 2)
  Nomino ya wingi, kivumishi kiradidi, kitenzi kishirikishi kikamilifu, chagizo cha mahal.
  • Maji yaya haya  yangali mtoni.
 4. Tunga sentensi ukitumia neno  ‘zawadi’ kama kitenzi  (alama 2)
  • Mwalimu mkuu alimzawidi wanafunzi waliofaulu.
 5. Andika upya katika wakati ujao hali ya mazoea (alama 2)
  • Wachezaji hodari watakuwa wanafanya mazoezi uwanjani.
 6. Taja vigezo viwili vya kuanisha viambishi (alama 2)
  • Nafasi-viambishi  awali na tamati
  • Uamilifu/dhamira /jukumu/dhana-kama viambishi vya nasfi, wakati  ,urejeshi, mtendwa, kauli
 7. Changanua sentensi hii kwa kielelezo cha mstari
  Gazeti hilo litasomwa na mwanafunzi (alama 2)
  • S-KN(N+V)+KT(T+H+N).
 8. Ainisha viambishi (alama 2)
  Wasoila
  • Wa-nafsi/wigi/ngeli
  • Si-uakanusho
  • o-kirejeshi
  • l-mzizi
  • i-yambwa
  • a-kiishio kauli ya kutenda
 9. Tunga sentensi yenye vijenzi hivi (alama 1)
  KN(RH+ S)+KT(t+V)
  • Miongoni mwa waliofika ni hawa.
 10. Eleza matumizi ya ‘A’ anganifu katika sentensi (Alama 3)
  1. Mlango wa chuma umenunuliwa.
   • aina
  2. Msumeno wa kukatia ubao ni huu.
   • kazi
  3. Mwimbaji wa kwanza  yu  jukwaani sasa.
   • Nafasi katika orodha
 11. Andika katika udogo
  Kiti hiki cha mwanamke huyu kimevunjika (alama 2)
  • Kijikiti hiki cha kinajike hiki kimevunjika
 12. Eleza matumizi ya koloni na koma katika sentensi (alama 1)
  Nyanya alinunua vitu hivi: pilipili, parachichi, pipi na papai.
  • Kuonyesha orodha inayofuata
  • kuorodhesha
 13. Geuza katika hali ya wingi
  Seremala aliunda kasha kwa ubao na kumpa mtume (ala1a 2)
  • Maseremala waliunda makasha kwa kutumia mbao na kuwapa mitume.
 14. Taja dhana  za kimaana mbili zilizo katika sentensi (alama 1)
  Ningekuwa na hela ningenunua shamba.
  • Kuonyesha uwezekano
  • Kuonyesha majuto
  • Kuonyesha masharti/hali ya kutegemeana
  • Kuonyesha matumaini
  • Kuonyesha wakati uliopita
 15. Tunga sentensi venye kishazi tegemezi ambacho ni; (alama 2)
  1. Kielezi cha namna
   • Amepika chakula alivyoelekezwa.
  2. Kielelezi cha Mahali
   • Mahali aliposimama pamesafishwa.
 16. Ainisha sentensi hii kwa kuzingatia dhamira (alama 1)
  Komesha mchezo huu kuanzia leo!
  • Sentensi agizi/a amri
 17. Onyesha kwa kutoa mifano miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U-_Zi (alama 2)
  • U-NY-unyayo-nyayo
  • U-ND-ulimi-ndimi
  • W-NY-wayo-nyayo
 18. Ainisha yambwa katika sentensi hii
  Yaya alitumia kijiko kumpatia mtoto huyo mdogo chakula kitamu (alama 3)
  • Yambwa tendwa-chakula kitamu
  • Yambwa tendewa-mtoto huyo mdogo
  • Yambwa ala-kijiko
 19. Andika kitenzi katika kauli ulizopewa kisha ukitungie sentensi (alama 2)
  1. Kauli tendata
   • Nata,kamata, pakata
  2. Kauli tendama
   • Kwama, ungama
 20. Eleza maana mbili katika utungo huu (alama 2)
  Fundi alimkatia Makaa utepe huo.
  • Fundi alikata utepe akampa Makaa
  • Alikata utepe kwa niaba ya Makaa.
  • Alimkata Makaa kwa utepe .
  • Likta kwa sababu

SEHEMU D:ISIMU JAMII(alama 10)
Soma makala haya kisha ujibu maswali;

Rafiki yako amezongwa na mambo magumu na anafikiria suluhu ni kujiua umepewa jukumu la kumshauri.
 1. Utatumia Lugha ya sajili gani? (Alama 2)
  • Sajili ya ushauri nasaha/ya ushauri
 2. Fafanua sifa nane za kimtindo utakazomatumia ili kufanikisha mazungumuzo yako (alama 8)
  • Matumizi ya maswali ya balagha-ukijitoa uhai utanufaikaje?
  • Lugha ya ushawishi-maisha ni matamu
  • Kuchanganya msimbo/ndimi-ucommit suicide kwa nini?
  • Matumizi ya tasfida-kujitia kitanzi
  • Matumizi ya chuku-utaenda kwa shetani straight
  • Matumizi ya viziada lugha ili kusisitiza hoja’
  • Lugha ya ucheshi kama vile-mtu akihang anajiendea haja kubwa
  • Matumizi ya lugha yenye mdokezo-watu wataachwa na…
  • Matumizi yenye toni kali ya kuonya kamavile -nitakushtaki kwa polisi
  • Matumizi ya lugha dadisi -mbaona unataka kujitoa uhai
  • Matumiziya nyimbo-kumrai asijiue
  • Matumizi ya maombi-kumshawishi abadili nia
  • Matumizi ya kauli fupi-chagua Maisha.
  • Matumizi ya lugha nyepesi-hamna haja ya kujiua 
   hoja zozote 8*1=8 

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 1.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?