Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:    

 • Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Chagua swali lingine lolote moja kutoka maswali matatu yaliyosalia. 
 • Majibu yote yaandikwe kwa Kiswahili katika kijiabu cha majibu ulichopewa.
  Sehemu hii imehifadhiwa kwa matumizi ya mtahini pekee:
 1. Ulisoma tangazo katika gazeti la Taifa Leo kuhusu nafasi ya kazi ya Uuguzi. Umealikwa kwa mahojiano ya kazi hii baada ya kuomba nafasi. Andika tawasifu- kazi yako utakayowasilisha.
 2. Serikali ni ya kulaumiwa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini. Jadili.
 3. Andika kisa kitakachodhihirisha ukweli wa methali: Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani
 4. Andika Insha itakayoanza kwa maneno haya:
  Baada ya kusafiri mwendo wa kilomita mbili hivi, watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa na bunduki mikononi...


MARKING SCHEME

 1. Ulisoma tangazo katika gazeti la Mzalendo kuhusu nafasi ya kazi ya udaktari. Baada ya kuandika ombi la kazi hiyo, umealikwa kwa mahojiano. Andika tawasifu- kazi yako utakayowasilisha.
  Mtahiniwa azingatie mambo yafuatayo:
  1. Anwani : Iandikwe kwa herufi kubwa na ipigwe mstari. Aonyeshe ni tawasifu ya nani.
  2. Utangulizi: mtahiniwa aoneshe usuli wake, tarehe ya kuzaliwa, wazazi n.k.
  3. Mwili wa insha uonyeshe:
   • Maisha yake kuanzia utotoni
   • Maelezo ya kina kuhusu elimu yake
   • Ufanisi wake katika masomo- hasa unaolenga sayansi n.k
   • Mafanikio yake katika kazi mbali mbali alizofanya
   • Afafanue juu ya taaluma na tajriba yake
   • Aangazie pandashuka zake maishani
   • Aonyeshe uraibu wake na talanta (si lazima)
    *Maelezo yapangwe kiwakati kama yalivyofuatana
  4. Awe na warejelewa
   TANBIHI: Mtahiniwa aandika WASIFUKAZI
                   Akiandika kwa mtindo wa moja kwa moja atuzwe juu ya kumi.
   Muundo wa Tawasifukazi
   Wasifukazi huwa na anwani kuu yenye neno ‘WASIFUKAZI’ na vichwa vidogovidogo vyenye sehemu zifuataza
          Maelezo ya binafsi
   • Jina.
   • Anwani.
   • Umri.
   • Uraia.
   • Kitambulisho.
   • Simu.
   • Baruapepe.
    Elimu
   • Chuo kikuu.
   • Chuo.
   • Shule ya upili.
   • Shule ya msingi.
    Uzoefu wa kazi
   • Shirika/ kampuni na wakati wa kazi (anza na ile ya kwanza hadi ya sasa)
    Maelezo mengine kama;
   • Uraibu.
   • Shughuli katika jamii.
   • Mchango katika ujenzi wa taifa.
   • Shughuli nyinginezo.
    Warejelewa
   • Cheo wanachoshikilia.
   • Majina yao.
   • Anwani zao.
   • Simu na barua pepe.
   • Wasizidi watatu ila wasipungue wawili.
 2. Serikali ni ya kulaumiwa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini. Jadili.
  Kuunga
  • Uchache wa maafisa wa usalama nchini.
  • Ukosefu wa ajira nchini.
  • Uchochole uliokithiri miongoni mwa wanajamii.
  • Kutotekeleza sera kuhusu mpango wa uzazi ambapo kuongezeka kwa idadi ya watu kunasababisha kung’ang’aniwa kwa rasilimali kama mashamba na nyinginezo.
  • Kuwepo kwa silaha haramu mikononi mwa raia.
  • Wachache kuruhusiwa kumiliki bunduki bila kufanyiwa uchunguzi wa sawa.
  • Askari kuzembea kikazi au kukosa kutekeleza majukumu yao kama inavyotarajiwa.
  • Kutokuwa na sera faafu kuhusu usalama wa mwanainchi.
   Kupinga
  • Serikali inafanya msako wa kitaifa kuwasaka na kuwatambua magaidid wanaojificha miongoni mwa wananchi.
  • Serikali ina mpango wa kuwasajili upya wananchi.
  • Serikali imeanzisha mpango wa nyumba kumi.
  • Ukiwa na fadhaa huwasukuma watu kufanya maovu.
  • Kuwapo kwa misimamo mikali ya kidini ambayo baadhi yayo huhimiza mauaji. ⮚ Vijana kukosa maelekezo faafu kutoka kwa wazazi.
  • Kuvunjika kwa asasi za kijamii ambapo hapana uelekezi kwa wana.
  • Jukumu la ulezi wa wana limeachiwa familia husika badala ya jamii nzima kama ilivyokuwa awali.
  • azingira wanamokulia na kulelewa wanajamii (watoto wa mitaani)yanafunza uhalifu.
  • Kutokuwa na msimamao sawa kuhusu suala zima la usalama miongoni mwa viongozi.
   Tanbihi
  • Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kuunga mkono na moja au zaidi za kupinga.
  • Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kupinga na moja au zaidi za kuunga.
  • Mtahiniwa atoe msimamo wake.
  • Katika hali zote mtahiniwa asiwe na chini ya hoja nane.
  • Anayekosa kushughulikia pande zote mbili asipite alama 10.
  • Mtahiniwa anaweza kutota hoja sawa pande zote alimradi atoe msimamo.
  • Hakiki hoja zingine za mtahiniwa.
 3. Andika kisa kitakachodhihirisha ukweli wa methali: Mjinga akierevuka, mwerevu huwa mashakani
  Hii ni insha ya methali.
  Kisa kidhihirisha mambo yafuatayo
  • Mtu/ watu ambao wana tabia ya kuwadanganya wenzao au kuwatapeli watafikiwa na makuu pale wale wanaodanganywa wakierevuka na kuyatambua matendo yao
   AU
  • Viongozi wasiwafanyie maovu raia wawaongozao kwani wakiwatambua basi watakuwa mashakani kwani watavuliwa vyeo.
  • Mtahiniwa abuni kisa ambacho waliokuwa na mazoea ya kuwadanganya wenzao wanafikia hali ambapo hila zao hugunduliwa na hivyo waathirirwa kuchukua hatua fulani dhidi yake au yao. 
  • Mtahiniwa aweze kuonyesha:
   1. Hali ya mwanzo ya mhusika kutapeli au kuhadaa wenzake
   2. Wahadaiwa kutambua hadaa au utapeli au udanganyifu kisha wanavyochukua hatua mwafaka kuhusu janmbo hilo
    Tanbihi
    • Mtahiniwa akishughulikia upande momja pekee alama zisipite 10
    • Anwani si lazima. Maana yamethali si lazima.
 4. Andika Insha itakayoanza kwa maneno haya:
  Baada ya kusafiri mwendo wa kilomita mbili hivi, watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa na bunduki mikononi...
  Hii ni insha ya kiubunifu. Mtahiniwa abuni kisa ambacho chaangazia mamabo kama vile ∙ wizi
  • ugaidi
  • utekaji nyara
  • uharamia n.k
  • Mtahiniwa aonyeshe walichotendewa, walivyokabiliana na tukio hilo, walivyojinasua na hatima ya waathiri na waathiriwa.
  • Mtahini ahakiki ukomavu wa lugha ya mtahiriwa na hoja alizotoa.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?