Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

 MAAGIZO:

 • Karatasi Hii Ina Sehemu Nne.
 • Ni Sharti Mtahiniwa Ashughulikie Sehemu Zote.
 • Maswali Yote Yajibiwa Kwa Lugha Ya Kiswahili.
 1. UFAHAMU
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
  Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamehangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwaua maelfu ya watu na kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu.

  Hata hivyo magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya Ukimwi. Neno “UKIMWI” lilitoholewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha Ukosefu wa Kinga Mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kichaka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile ‘umeme’ na pia ‘ugonjwa wa vijana’. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo, linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wasioweza kujimudu.

  Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufika mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini . Hivi sasa, inasemekana kuwa takriban watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imethibitishwa kwamba takriban wafu milioni mbili u nusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa.

  Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao.

  Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia. Tuwe na matumaini kwamba siku moja tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira huvuta heri.
  Maswali
  1. Fafanua maana ya vifungu vifuatavyo
   1. Kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. (Alama 1)
   2. Kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. (Alama 1)
  2. Eleza aina ya magonjwa yafuatayo:-
   1. Homa ya matumbo (Alama 1)
   2. Kifua Kikuu (Alama 1)
  3. Kwa nini ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina ya kimajazi? (Alama1) 
  4. Eleza madhara yoyote matatu ya UKIMWI kulingana na taarifa (Alama3)
  5. Ni harakati zipi zinazoendelezwa kukumbana na janga hili? (Alama2)
  6. Eleza mienendo inayopaswa kuendelezwa kuondoa kukata tamaa (Alama3) 
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.
   1. Takriban ……………………………………………………………………………………… (Alama 1) 
   2. Hima ya kuishi ……………………………………………………………………………… (Alama 1)
 2. MUHTASARI (Alama 15)

  Tunapinga na kulaani vikali visa vya ugaidi vinavyoendelea kutetemesha usalama wa wananchi.Hivi ni vitendo vya kinyama vinavovyotekelezwa na watu waliokosa ubinadamu na utu kabisa.Inakera mno kwa vitendo vya kigaidi .Inagadhabisha kuona Wakenya wasio na makosa wakiteswa na kuuwawa kinyama bila huruma na watu wasio na utu. Hatuogopi wala hatuna fedheha kuamba magaidi hawa wameelaaniwa na siku zao zimehesabiwa hapa duniani, damu ya mwananchi asiye na makosa katu watailipia. Napinga vikali pale magaidi hawa wanapohusisha vitendo hivi kuwa vita vya kidini, vita hivi si vya kidini kwani hakuna dini yoyote iliyo na imani ya kumwua kinyama binadamu asiye na makosa.

  Kando na tishio la ugaidi, Wakenya pia wanakabiliwa na hatari za ujambazi, mauji, unajisi, ubakaji na maovu mengine. Katika juhudi za kudumisha usalama, polisi wana jukumu la kutumia kila mbinu kuhakikisha kuwa haki ya kikatiba ya Wakenya kuhusu kulindwa kwa maisha na mali yao. Lakini cha kusikitisha ni kuwa, mbinu ambazo polisi wamekuwa wakitumia hasa ile ya kufanya misako inayoishia kuwanasa mamia ya raia wasio na habari kinachoendelea, inawaongezea Wakenya mateso. Hali hii inawaacha kwenye hatari ya kunaswa na majambazi ama polisi.

  Matumizi ya mbinu hii ya misako imeishia kunasa raia wengi wasio na makosa.Wanaponaswa, hurundikwa kwenye seli usiku mzima ama siku kadha na hata kama wanaaachiliwa huwa tayari wameteseka. Huu ni ukiukaji wa haki za raia. Kadhalika, mbinu hii yanaonekana kama hila ya polisi kutaka kuonyesha wanafanya kazi lakini sio mwafaka kwani wanapokuwa wakiwanasa raia mijini na mitaani, magaidi na majambazi wanaendelea na shughuli zao.

  Badala ya kusaka wakora kwa kubahatisha kwenye umati, polisi wanapaswa kubuni njia ambazo zitawapa mwelekeo mwafaka zaidi kuhusu wahalifu ili waweze kuwafuatilia. Ushirikiano baina yao na majasusi uwepo. Hii itawezesha polisi kupata habari muhimu kuhusu vitisho vya uhalifu. Maafisa wa usalama pia wanaweza kupata habari muhimu kutoka kwa raia.
  MASWALI
  1. Ni nini maoni wa mwandishi kuhusu suala la ugaidi. (alama 7, 1 utiririko) (maneno 60-70)
   Matayarisho:
   Nakala safi
  2. Kwa kutumia maneno yasiyozidi 50 fupisha aya mbili za mwisho. (alama 6, 1 utiririko)
   Matayarisho:
   Nakala safi
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40) 
  1. Kipashio kikubwa zaidi katika ujenzi wa lugha kinaitwaje? (alama 1)
  2. Andika sauti mbili ambazo ni vikwamizo vya mdomo na meno. (alama 2)
  3. Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Nitawafundisha usemi wa taarifa kesho,” mwalimu alituambia.
  4. Tunga sentensi moja ukitumia kielezi cha nomino. (alama 2)
  5. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. (alama 4)
   Wanafunzi wenye bidii masomoni hufuzu mtihani.
  6. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: (alama 3)
   Baba alipashwa habari kwa rununu.
  7. Tambua muundo wa virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo: (alama 2)
   1. Mikakati iliyobuniwa na serikali itaimarisha usalama nchini.
   2. Mara nyingine msimu wa masika umewadia.
  8. Andika upya sentensi zifuatazo kwa kuzingatia kauli zilizomo mabanoni. (alama 2)
   Watoto wenyewe wamekunywa maziwa yao yote. (tendwa)
  9. Pombe haramu inawafisha Wakenya wengi. (Badilisha kitenzi kiwe nomino)
  10. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha matumizi yafuatayo ya ndivyo. (alama 2) 
   1. Jinsi
   2. Kirejeshi cha kuthibitisha.
  11. Eleza maana tatu zinazoibuliwa na vitate vilivyotumika katika sentensi hii. (alama 3) Bosi wetu ana pozi nyingi lakini ni bozi sana.
  12. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.
   Uso wa kijana yule ulichujuka alipoanguka. (alama 2)
  13. Eleza matumizi mawili ya viakifishi vifuatavyo: (alama 4)
   1. Herufi nzito (H) / zilizokolezwa.
   2. Mstari
  14. Bainisha mofimu za: (alama 3)
   Nitakujia
  15. Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati mwafaka. (alama 1)
   Gari limeibwa.
   Gari ni langu.
  16. Ainisha vihusishi katika sentensi hizi: (alama 2) 
   1. Mwanafunzi huyu ni mwerevu sana kuliko wenzake wote.
   2. Tangu apate mamlaka amepuuza wadogo wake.
  17. Unda kitenzi kutokana na neno“Zawadi” (alama 1)
  18. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
   Ingawa amefunga bao hajacheza kwa muda.
 4. ISIMU JAMII (Alama 10)
  Maafisa 3 wakana kusaidia mshukiwa wa mauwaji ya watoto kutoroka kituoni."
  Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya kumsaidia mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi…”
  1. Huku ukitoa sababu mbili, tambua sajili hii. ( alama 3) 
  2. Fafanua sifa zozote saba za sajili hii. (alama 7) 


MARKING SCHEME

 1. UFAHAMU
  1.    
   1. Kuvuruga/ kuharibu hali ya maisha ya watu. (alama 1)
   2. Kuwaua watu (alama 1)
  2.   
   1. Ugonjwa uletwao na kula chakula kichafu.Dalili zake ni kuendesha,kuumwa na tumbo na homa kali. (alama 1)
   2. Tibii, ugonjwa wa kukohoa damu (alama 1)
  3. Kutokana na kasi yake ya kuua watu (alama 1)
  4.   
   • Huambukizwa sana kwa watu walio na miaka kati yawalio na nguvu za kutunza jamii/ watasalia wakongwe na watoto wasioweza kujimudu.
   • Umesababisha vifo vingi
   • Hospitali na zahanati zimeshindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa.(hoja 3 x 1 = 3)
  5.   
   • Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa
   • Makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa
   • Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani
   • Wanasayansi na madaktari wanatafuta tiba (Hoja 4 x ½ = 2)
  6.  
   • Tuwe na matumaini kwamba siku moja tiba itapatikana
   • Tujikinge kutokana na maradhi haya
   • Tuwe na subira kwani subira huvuta heri (hoja 3 x 1 = 3)
  7.  
   1. Utaratibu wa utendaji au utekelezaji (alama 1)
   2. Wema /baraka/ fanaka/ ustawi (alama 1)
    Maelezo ya kutuza
    • Makosa ya tahajia – Ondoa nusu 6 yaani ½ x 6 ili kuwa jumla ya alama 3
    • Makosa ya sarufi – Usiondoe zaidi ya nusu ya tuzo kwa kila swali.
 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  1. Ni nini maoni ya mwandishi kuhusu suala la ugaidi? (alama 7, 1 utiririko)
   • Tunapinga na kulaani visa vya ugaidi.
   • Ugaidi ni kitendo cha kinyama kinachotekelezwa na watu waliokosa ubinadamu.
   • Ugaidi hauna uhusiano na dini yoyote.
   • Polisi wanazembea katika kuzuia matendo ya kigaidi.
   • Polisi wabuni njia mbadala ya kukabiliana na ugaidi badala ya kunasa raia wasio na hatia. 
   • Wakenya wasio na makosa huteswa na kuuawa kinyama.
   • Magaidi watalipia matendo yao.
   • Wakenya wana haki ya kulindwa kikatiba.
    Hoja zozote 7×1=7, alama 1 ya utiririko.
  2. Kwa kutumia maneno yasiyozidi 50, fupisha aya mbili za mwisho. (alama 6, 1 utiririko)
   • Raia wasio na hatia hunaswa.
   • Hurundikwa kwenye seli na kuachiliwa huru kama wameteseka.
   • Huu ni ukiukaji wa haki za binadamu.
   • Hii ni hila ya polisi kujionyesha kuwa wanafanya kazi.
   • Magaidi huendeleza shughuli zao.
   • Polisi wanapaswa kubuni njia zitakazowapa mwelekeo mwafaka kuhusu wahalifu.
   • Ushirikiano baina yao na majasusi uwepo.
   • Maafisa wa usalama kupata habari muhimu kutoka kwa raia.
    Hoja zozote 6×1=1, alama 1 ya utiririko.
    Ondoa ½ alama kwa kila kosa la sarufi hadi makosa sita kila litokeapo mara ya kwanza.
    Ondoa ½ alama kwa kila kosa la hijai hadi makosa sita kila litokeapo mara ya kwanza.
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Kipashio kikubwa zaidi katika ujenzi wa lugha kinaitwaje? (alama 1)
   • Sentensi
  2. Andika sauti mbili ambazo ni vikwamizo vya mdomo wa meno. (alama 2)
   • /f/ na /v/
  3. Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Nitawafundisha usemi wa taarifa kesho,” mwalimu alituambia.
   • Mwalimu alituambia kuwa angetufundisha usemi wa taarifa siku ambayo ingefuata (keshoye)
  4. Tunga sentensi moja ukitumia kielezi cha nomino. (alama 2)
   swaPP22022LMQ2d
  5. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. (alama 4)
   Wanafunzi wenye bidii masomoni hufuzu mtihani.
   • Kitondo/ambiwa – baba
   • Kipozi/yamba tenda – habari
  6. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: (alama 3)
   Baba alipashwa habari kwa rununu.
  7. Tambua muundo wa virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo: (alama 2)
   1. Mikakati iliyobuniwa na serikali itaimarisha usalama nchini
    • Nomino na kishazi tegemezi
   2. Mara nyingine msimu wa masika umewadia
    • Kwelezi la idadi
  8. Andika upya sentensi zifuatazo kwa kuzingatia kauli zilizomo mabanoni. (alama 2) 
   Watoto wenyewe wamekunywa maziwa yao yote. (tendwa)
   • Maziwa yote ya watoto yamenyweka nao wenyewe
  9. Pombe haramu inawafisha Wakenya wengi. (Badilisha kitenzi kiwe nomino)
   • Pombe haramu imesababisha vifo vya wakenya wengi
  10. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha matumizi yafuatayo ya ndivyo. (alama 2)
   1. Jinsi
    • Hivi ndivyo aandikavyo
   2. Kirejeshi cha kuthibitisha.
    • Hivi ndivyo vilivyorumbiwa jana
  11. Eleza maana tatu zinazoibuliwa na vitate vilivyotumika katika sentensi hii. (alama 3)
   Bosi wetu ana pozi nyingi lakini ni bozi sana.
   • Bosi – mkubwa wa ofisi/ikawa Fulani/mwajiri /tarjiri
   • Pozi – maringo (mtwazo), madaha, matuko, gogi, majivuno, goto
   • Bozi – mpubmavu bahau, fala, bwege, zebe, bakunja, mjinga
  12. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.
   Uso wa kijana Yule ulichujuka alipoanguka. (alama 2)
   • Juso la jana lile lilichujuka lilipoanguka
   • Jijusa la jijana lile lilichunyika
  13. Eleza matumizi mawili ya viakifishi vifuatavyo: (alama 4)
   1. Herufi nzito (H) / zilizokolewa.
    • Kuonysha wanwani, mada k.m utangulizi, sura ya pili, vishozi
    • Kusisitiza kitulia mazo km wakihishi vya nafasi ni mimi , wewe
    • Madekezo k.m kwa mfano
   2. Mstari
    • Kutilia neno au fungu la maneno msisitizo
    • Kuonyesho anwani ya vitabu na majin aya majarida, magazeti km gazeti la taifa leo, riwaya ya kidagaa kimemzoea
  14. Bainisha mofimu za: (alama 3)
   Nitakujia
   • Ni – nafsi
   • Ta – wakati
   • Ku – nafsi/mtendewa/yambiwa
  15. Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati mwafaka. (alama 1)
   Gari limeibwa.
   Gari ni langu.
   • Gari lililoibwa ni langu
  16. Ainisha vihusishi katika sentensi hizi: (alama 2) 
   1. Mwanafunzi huyu ni mwerevu sana kuliko wenzake wote.
    • Kuliko – ulinganisho
   2. Tangu apate mamlaka amepuuza wadogo wake.
    • Tangu – uhusiano wa wakati
  17. Unda kitenzi kutokana na neno “Zawadi” (alama 1)
   • Zawadi, zawidia, zawidika, zawidiano n.k
  18. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
   Ingawa amefunga bao hajacheza kwa muda.
   • Ingawa amefunga bao – kishazi tegemezi
   • Hajacheza kwa muda – kishazi huru
 4. ISIMU JAMII
  “ Maafisa 3 wakana kusaidia mshukiwa wa mauwaji ya watoto kutoroka kituoni.
  Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya kumsaidia mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi…”
  1. Huku ukitoa sababu mbili, tambua sajili hii. ( alama 3)
   • Sajili ya magazetini/ matangazo
   • Sababu
    • kuwepo kwa anwani/mada yenye mvuto
    • matumizi ya usemi wa taarifa/ lugha ya kuripoti ( sajili 1, sifa 2x1)
  2. Fafanua sifa zozote nyingine saba za sajili hii. (alama 7) 
   1. mara nyingi vichwa vya habari havizingatii sarufi – ili kuokoa nafasi katika gazeti/muda
   2. baadhi ya jumbe ya mambo ya kweli – ili kuvutia wasomaji/ wanunuzi/wasikilizaji/mtazamaji 
   3. mada/ anwani huwa fupi sana na ya kuvutia- ili kuvutia wateja/ wasomaji wa gazeti/wasikilizaji 
   4. lugha inayotumika hutegemea taarifa inayotolewa- kila taaluma ina msamiati wake.
   5. ujumbe huandikwa/husomwa katika aya fupifupi/ kwa muhtasari- ili kuokoa nafasi katika magazeti/muda
   6. lugha yenye kauli/ sentensi ndefundefu- ili kufafanua hoja kikamilifu.
   7. matumizi ya tarakimu badala ya maneno- ili kuokoa nafasi/kusomeka haraka viii) lugha ya kuvutia – “mwalimu aonja asali”
   8. matumizi mengi ya chuku- “ paka amla ndovu”
   9. matumizi ya sitiari/jazanda- ili kutasfidi lugha
   10. matumizi ya lugha rahisi- ili kupasha ujumbe kwa watu wa matabaka yote.
   11. lugha ya maelezo – ili kupasha ujumbe kwa njia nyepese na kueleweka rahisi. (zozote 7x1) 
   12. matumizi ya tasfida – ili kuficha ukali
   13. lugha ya picha / michoro – ili ujumbe ueleweke

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?