Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Moi Tea Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha nyingine kutoka tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Watahiniwa lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

MASWALI

 1. Wewe ni mhariri wa gazeti la Msemakweli. Andika tahariri kuhusu athari za baa la njaa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo hili.
 2. Matumizi ya afyuni katika taasisi za masomo nchini ni suala muhali kutatuliwa. Jadili.
 3. Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali: Mtaka yote hukosa yote.
 4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno haya:
  Ilinichukua muda mrefu kusadiki niliyoyapata...

Mwongozo wa Kusahihisha

SWALI LA LAZIMA
Ni insha ya kiuamilifu.
Sura /mtindo wa tahariri uzingatiwe

 1. Kichwa- Kiandikwe kwa herufi kubwa
 2.  Jina la gazeti - Msemakweli litumiwe.
 3. Tarehe.
 4. Jina la mhariri
  Athari za baa la njaa
  1. Vifo vya mifugo.
  2. Shule kufungwa kutokaba na ukosefu wa chakula.
  3. Kuhama kwa jamii kutafuta chakula.
  4. Vifo vya binadamu/watu
  5. Maradhi mbalimbali kwa mfano utapiamlo.
  6. Pato kubwa la kitaifa linatumiwa kushughulikia njaa.
  7. Kudumaa kwa maendeleo ya wananchi na taifa.
  8. Wanasiasa na mataifa kujinufaisha wakitumia fursa hii.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUKABILIANA NA BAA LA NJAA

 1. Wakulima kuhimizwa kupanda mimea inayochukua muda mfupi kukomaa katika sehemu zinazopata mvua chache.
 2. Wakulima kupewa mbegu za kupanda bila malipo.
 3. Serikali kutangaza baa la njaa kama janga la taifa.
 4. Kubuniwa kwa wizara ya mipango maalum inayoshughulikia katizo hili miongoni mwa mengine.
 5. Misaada ya chakula kwa wahasiriwa kutoka kwa serikali na wahisani wengine.
 6. Serikali kuwahimiza wafugaji kuuza mifugo wao ili kuepuka ukosefu wa nyasi/lishe na maji.
 7. Serikali kununua mifugo kutoka kwa wakulima/wafugaji walioathiriwa na baa la njaa.
 8. Wakulima kupanda mimea inayoweza kuhimili ukame kama vile mihogo na mtama.
 9. Serikali kujenga mabwawa ya maji ili kukusanya maji wakati wa mvua ambapo wakulima wataweza kunyunyizia mimea tao maji wakati wa kiangazi.
 10. Serikali kutenga pesa ili kuwezesha shirika la nafaka nchini kununua na kuhifadhi mazao kutoka maeneo yanayojitosheleza kwa mvua.

SWALI LA PILI

KUUNGA MKONO

 1. Shinikizo la rika kuwasukuma vijana kutumia afyuni.
 2. Sheria hafifu inayowaruhusu wauzaji na watumizi kuendelea na shughuli zao.
 3. kuporomoka kwa maadili ya jamii na kushindwa kwa wazazi kuwathibiti watoto wao kwa kutowapa mawaidha.
 4. Ukosefu/ Uchache wa wataalamu wa kutoa nasaha na mwelekeo kwa wanafunzi shuleni.
 5. Vyombo vya habari vinachangia pakubwa katika kuwashawishi vinajana kutumia afyuni. Kama vile redio, runinga.
 6. Upungufu wa vielelezo/mifano katika jamii.
 7. Ufisadi -Wananaowauzia vijana mihadarati hutumia hongo kufanikisha maovu haya.

KUPINGA.

 1. Kutumia sheria kali zitakazowazuia watumiaji na wauzaji wa afyuni kuendeleza shughuli zao.
 2. Kuwashauri wazazi kuwa mstari wa mbele kuwazungumzia na kuwashauri watoto wao.
 3. Kuthibiti vyombo vya habari katika harakati za kupigana na matumizi ya afyuni.
 4. Kuwaajiri na kuongeza wataalamu wa ushauri shuleni na vijijini.
 5. Serikali kukabiliana na ufisadi katika vitengo vyote.
 6. Kuwashauri wanafunzi kujisimamia kimawazo na kuepuka shinikizo la rika.
 7. Vijana kupewa nasaha kuhusu athari za matumizi ya afyuni.

TANBIHI

 1. Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kuunga na moja/zaidi za kupinga.
 2. Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kupinga na moja /zaidi za kuunga.
 3. Mtahiniwa atoe msimamo wake.
 4. Anayekosa kushughulikia pande zote mbili asipitishe alama 10.
 5. Mtahiniwa anaweza kutoa hoja sawa pande almuradi atoe msimamo wake.
 6. Kadiria hoja zingine za mtahiniwa.

SWALI LA TATU.

 1. Kisa kinafaa kioane na methali
 2. Mwanafunzi aonyesha sehemu zote mbili za methali.
 3. Dhana ya mtaka yote ionekane vizuri.
 4. Dhana ya kukosa yote ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja.
  Maana : Anayetaka vitu vingi kwa tamaa hawi na mwisho mzuri.

SWALI LA NNE

 1. Mtahiniwa aweze kujenga kisa ambacho kinamhusisha yeye mwenyewe kama mhusika mkuu.
 2. Akimjenga mhusika mkuu mwingine atakuwa anepotoka na hivo basi atuzwe 03/20.
 3. Mtahiniwa asibadili wakati uliohusika katika swali .Akifanya hivyo atakuwa amepotoka.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Moi Tea Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?