Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Moi Tea Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

Questions

MAAGIZO:

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na shairi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

SEHEMU A: (FASIHI SIMULIZI)

  1.      
    1. Watu watatu walikuwa wakivuka mto. Mmoja alivuka pasi kukanyaga maji wala kuyaona.
      Wa pili aliyaona maji akayavuka bila kuyakanyaga. Wa watatu aliyaona akayakanyaga
      huku akiyavuka.
      1. Bainisha kipera cha makala hayo. (alama 1)
      2. Eleza umuhimu wa kipera ulichotaja(i) hapo juu. (alama 4)
    2. Fafanua muundo wa mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi. (alama 3)
    3. Fafanua sifa za mawaidha. (alama 12)

SEHEMU B: (TAMTHILIA) KIGOGO(PAULINA KEA)

  1.  …… kila mtu sagamoyo hafanyi kazi yakek – hata hao chatu! Kwa hivyo wataka niache raha zangu, nijishike kichwa nilie?
    1. Eleza muktadha wa dondooo hili. (alama 4)
    2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
    3. Kwa kutolea mifano mwafaka, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika tamthilia ya Kigogo. (alama 12)
  2. Mgala muue na haki umpe. Thibitisha ukweli wa methali hii ukimrejelea mhusika Husda. (alama 20)

SEHEMU C: (CHOZI LA HERI) Assumpta K. Matei

  1.    
    1. “Nyamaza wewe! Nyinyi ndio mlioturudhisha nyuma miaka yote hii …….”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4
      2. Fafanua baadhi ya malalamishi ya msemaji wa kauli hii. (alama 6)
    2. Fafanua dhuluma dhidi ya watoto katika Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 10)
  2. Fafanua nafasi ya vijana katika jamii kwa mujibu wa Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

SEHEMU D: (HADITHI FUPI)

  1. MAPENZI KIFAURONGO: Kenna Wasike
    “Hadi sasa mimi ni kama rubani aliyeharibikiwa na ndege angani.”
    Onyesha ukweli wa dondoo hili. (alama 20)
  2. Ndoto ya Mshaka: Ali Abdulla Ali
    Mwandishi wa hadithi hii anatupa taswira ya jamii iliyozongwa na masaibu yanayotamausha. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 20)

SEHEMU E: (SHAIRI)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  1. Weusi likosa nini?
    1. Sie watu weusi, lipataje weusi?
    2. Kila kitu kibaya, hupewa sifa mbyaya.
    3. Sifa hii ‘eusi’, yaleta wasiwasi.
    4. Rangi hii hakika, ni wapi ilitoka?
    5. Ibada za Weusi, harusi kuzitusi.
    6. Kama mtu mweusi, Lusifa ni mweusi
    7. Ibada ya Weupe, hupokewa peupe
    8. Adamu naye Hawa, weupe walipewa
    9. Yesu Mwana wa Mungu, alikuwa Mzungu
    10. Malaika wa Mungu daima ni Wazungu
    11. Mweusi ti hatendi, silaumiwe pindi
    12. Mweusi duniani, likosa kitu gani?
    13.  Mweusi jilaumu, measi yako damu.
    14. Mweusi umeiga, hata ya kutoiga
    15. Asojali mkuu, atavunjika guu
    16. Baa mejikatia, nani takulilia?
      MASWALI:
      1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu yako. (alama 2)
      2. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
      3. Toa mifano miwili ya matumizi ya mbinu ya inkisari katika shairi hili na uyaandike katika
      4. Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 2)
      5.  Ni nini dhamira ya mtungaji wa shairi hili? (alama 2)
      6. Kwa kutoa mifano matatu, eleza matumizi ya lugha mkato. (alama 6)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1.    
    1. Watu watatu walikuwa wakivuka mto. Mmoja alivuka pasi kukanyaga maji wala kuyaona.
      Wa pili aliyaona maji akayavuka bila kuyakanyaga. Wa watatu aliyaona akayakanyaga
      huku akiyavuka.
      1. Bainisha kipera cha makala hayo. (alama 1)
        • Mafumbo/chemsha bongo
      2. Eleza umuhimu wa kipera ulichotaja(i) hapo juu. (alama 4)
        • Hukuza uwezo na wepesi wa kufikiri
        • Hustawisha ubunifu
        • Hukuza maarifa ukabiliana na changamoto na kutumia marafiki kusuluhisha mambo
        • Huburudisha jamii
        • Hukuza uhusiano mwema.
    2. Fafanua muundo wa mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi. (alama 3)
      • Utangulizi – Anayetoa mawaidha huanza kwa kauli ya kuvuta makini ya hadhira.
        Mf: Sikiliza mwanangu na usikilize kwa makini …..
      • Mwili: Mawaidha huwasilishwa na kusisitizwa kwa kutumia kauli sisitizi pamoja na tamathali za usemi kama vile methali.
        Wasia, maonyo na maelekezo hutolewa kutegemea lengo.
      • Hitimisho: Mwasilishaji huonyesha msimamo wake kuhusiana na swala analousia, pia anaweza kuuliza msimamo wa hadhira yako.
    3. Fafanua sifa za mawaidha. (alama 12)
      • Mawaidha yaweza kutolewa katika miktadha rasmi na isiyokuwa rasmi. Miktadha rasmi ni kama vile katika harusi, kwenye mazishi nk. Miktadha isiyo rasmi ni kama vile mzazi anapotoa mawaidha kwa mwanawe.
      • Mawaidha hutolewa na watu waliopewa jukumu la kutoa mawaidha kama vile wazee na watu walio na vyeo na waliochukuliwa kuwa na ukima.
      • Mwenye kutoa mawaidha hulielewa jambo analousia kwa undani.
      • Mwenye kutoa mawaidha hutumia lugha inayoathiri hisia za wanaousiwa k.v. methali.
      • Maudhui katika mawaidha ni mapana.
      • Mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi huwa na muundo maalumu wenye sehemu tatu. Utangulizi, mwili na Hitimisho.
        (hoja 6 x 2 = 12)
  2. …… kila mtu sagamoyo hafanyi kazi yake – hata hao chatu! Kwa hivyo wataka niache raha zangu, nijishike kichwa nilie?
    1. Eleza muktadha wa dondooo hili. (alama 4)
      • Msemaji ni Majoka.
      • Alikuwa anamwambia chopi maneno haya.
      • Chopi alikuwa amemfahamisha kuwa ngurumo amenyongwa na chatu
      • Majoka alikuwa katika hoteli la kifahari la Majoka and Majoka Modern Resort akiwa na mkewe Husda.
    2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
      • ….. hao chatu! Nidaa.
      • ….. Nijishike kichwa nilie? Swali la balagha.
    3. Kwa kutolea mifano mwafaka, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika tamthilia ya Kigogo. (alama 12)
      1. NI shujaa na mkombozi:
        • Tunu amesawiriwa kama shujaa, mwanaharakati wa ukombozi wa jamii yake. Anashirikiana na wengine kuimbia jamii kutokana na uongozi dhalimu na majuka. Anawashauri vijana Mangweni kuwacha pombe haramu kutokana na madhara yake.
      2. Mwanamke ni mtetezi wa haki.
        • Ashua na Tunu wako mstari wa mbele kutetea haki za watu. Ashua anamwambia Majoka hakufanya vyema kufunga soko. Tunu anamsuta vikali Majoka kwa sabbu ya mauaji katika kampuni ya Majoka and Majoka Company.
      3. Mwanamke ni mwenye utu
        • Tunu anamshauri siti kuwapeleka watoto wa Sudi kwao wakale na watunzwe na Bi. Hashima. Siti anafika kwa kina Tunu kumjulia hali baada ya Tunu kuvamiwa na kuumizwa na wahuni.
        • Husda anaonyesha utu kwa namna anayomshughulikia mumewe baada yake kuzirai.
      4. Mwanamke ni jasiri
        • Ashua anamkosoa majoka waziziz kwa kulifubga soko ambalo ni tegemeo la wanajamii wengi. Pia anamwambia wanafunzi katika majoka and majoka Acadeny hawafuzu na huishia buwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka
        • Tunu anamkashifu majoka kwa kuhusika na vifo vya vijana watano wa Kampuni yake. Pia anamwambia mwanawe (Ngao Junior) si mume ni gugume.
      5. Mwanamke ni mcha mungu
        • Siti anakiri kuwa wanamtegemea Mungu kuwaondolea dhika waliokua wakipitia.
        • Hashima anasema ni vyema wamwombe Mungu kabla ya Tunu Kuondoka.
      6. Mwanamke ni msomi
        • Ashua na TUnu Wakesoma hadi chuo kikuu ni kupata shahada.
          (hoja 6 x 2)
    4. Mgala muue na haki umpe. Thibitisha ukweli wa methali hii ukimrejelea mhusika Husda. (alama 20)
      • Maana ya methali hii ni kuwa mgala anapaswa kulaumiwa inapobidi lakini apewe sifa anapostahiki. Hutumiwa kutukumbusho kuwa inafaa kuwwalaumu watu kutokana na udhaifu wao lakini tuwasifu wanapostahili. Husda ni wa kulaumiwa kwa sababu zifuatazo.
      • Husda ni mdaku. Ashua anamwita mdaku na msambazaji wa kanda za umbeya kwenye vikao vya masengenyo.
      • Mwenye wivu anamwonea wivu Ashua kwa kupendora na majoka. Anahiari kupigana na Ashua ili amlinde mumewe asinyakuliwe. Pia anamwonea wivu Ashua kwa kuwa amesoma hadi chuo kikuu.
      • Msherati anamtazama chopi lwa macho ya uchu na kumtamani namna chopi alivyovaa na kutembea. Anafanya haya yote nyuma ya miwani mweusi.
      • Mwenye matusi anamwita Ashua hawara kwa kumdhania ni mpenzi wa Majoka wa pembe za chaki.
      • Mpenda makuu aliolewa na Majoka kwa sababu ya mali za Majoka ila hakumpenda majoka akizipenda mali zake.
      • Fisadi anahakikisha Asiya mkoi wake amepata kandarasi ya kuoka keki ya uhuru
      • Mvumilivu alivumilia kuishi katika ndoa yenye dhuluma Majoka alizoea kumpiga Husda. Anatisha kumchafua Husda pale ofisini aatajileta fujo
      • Mwenye utu andhihirisho utu kwa jinsi anavyomshuglukikia mumewe akipozirai. Anamwambia chopi ampigie daktari wa Majoka simu. Pia anaandamana na mumewe hadi hospitalini na namwachi peke yake.
      • Mwajibikaji anawajibika kumtunza mumewe akiwa hospitalini.
        (hoja 10 x 2)
  3.       
    1. “Nyamaza wewe! Nyinyi ndio mlioturudhisha nyuma miaka yote hii …….”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4
        • Msemaji ni mmoja wa waliokuwa wakiandamana barabarani kupinga kutawazwa kwa ‘Musumbi”. Kaizari alikuwa akimsimulia dkt Ridhaa hali ilivyokuwa katika nchi ya wahafidaima baaada ya uchaguzi.
        • Mnenewa alikuwa wa walioashirika na vurugu za baada ya uchaguzi kwenye msitu wa mamba.. Msemaji alisema maneno haya huku akitoa dukuduku lake kwa gadhabu
      2. Fafanua baadhi ya malalamishi ya msemaji wa kauli hii. (alama 6)
        • Analalamikia mafunzo ya chuo kikuu ambayo ni kufunzwa ‘kukariri nadharia’ bila kupewa stadi za kuwawezesha kujitegemea.
        • Ukosefu wa kazi, hata ikiwa mtu ana digrii tatu bado hupati kazi.
        • Ukosefu wa njuga za ujasiria mali ili aweze kujiajiri.
        • Unyakuzi wa mashamba na waliotoka mbali ilhali viongozi wanawashauri kurudi maeneogatuzi na kufanya kazi mashambani.
        • Kuwafanyia viongozi kampeni baada ya wao kuhadaiwa kuwa watapata kazi. Pindi viongozi wapatapo nyadhifa za viongozi hawaonekani tena.
        • Ufisadi katika huduma ya hazina kwa vijana ambapo hazina imeandamwa na madonda ndugu ya ukabila na unasaba. (hoja 6 x 1)
    2. Fafanua dhuluma dhidi ya watoto katika Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 10)
      • Watoto wanadhulumiwa kimapenzi mfano mzee Maya anamdhulumu sana kimapenzi igwawa yeye ni baba wa kambo hali inayosababisha Sanna kupata mimba.
      • Watoto wa kaisari Limo na mwanaheri wanabakwa na vijana wenzao licha ya umri wao mdogo.
      • Dick anatumikizwa katika biashara za kuuza
  4. Fafanua nafasi ya vijana katika jamii kwa mujibu wa Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)
    • Nafasi ya vijana imeshughulikiwa pia katika kazi hii. Kuna maswala mbalimbali yanayoendelezwa au kuwakumba vijana. Mifano kutoka riwayani:
    • Elimu inayotolewa kwa vijana haiwawezeshi kuwa katika nafasi ya kuzalisha mali katika maisha yao. Hata wale waliosoma hadi vyuo vikuu na kupata shahada za ukapera, uzamili na uzamifu hawajapata nafasi ya kujipatia kazi; ila wao huwa katika nafasi ya kukariri nadharia walizofunzwa bila kujitegemea maishani mwao. Hii ina maana kwamba stadi zinazotolewa katika vyuo vikuu haziwapi wanafunzi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika uzalishaji wa mali na raslimali.
    • Swala lingine kuwahusu vijana ni kuwa hawako katika nafasi ya kujiajiri kutokana na ukweli kwamba hawana mataji wa kuanzisha biashara ambazo zinaweza kuzalisha nafasi za kazi kwao na kwa jamii kwa jumla. Hali hii inayafanya maisha ya vijana kuwa magumu ziaidi.
    • Viongozi wanawahimiza vijana kurudi mashambani katika maeneo gatuzi yao, ili wakazalishe mali huko. Tatizo ni kwamba baadhi ya vijana hawana mashamba ya kuzalisha mali kutokana na mashamba haya kuuziwa watu wengine na aila zao. Hii ndiyo sababu inayowafanya vijana kushindwa watarudi mashambani wanakohimizwa warudi wakafanye nini!
    • Vijana wana jukumu la kuelemishana kuhusu nafasi ya kila mmoja wao katika kuuboresha uongozi uliopo sasa kwa kuzalisha nafasi za kazi. Vijana hawa wanapasa kutumia vipawa vyao kwa njia endelevu, ili kusaidia katika kuzalisha nafasi za kazi badala ya kungojea serikali iwatafutie kazi. Hii ina maana kwamba, vijana hawapasi kungoja wafanyiwe kila kitu na serikali.
    • Vijana wana jukumu la kutambua kwamba wanatumiwa na viongozi kwa minajili ya kutimizwa matakwa yao ya kisiasa. Mwangeka anawashukuru vijana kwa kutambua kwamba wanatumiwa na viongozi wenye tama kuzua vita na mauaji yasiyokuwa na sababu maaalum.
    • Vijana wanakumbwa na hali ya mtafaruku wa kihisia kutokana na umri wao mdogo unaoufanya damu yao kuchemka. Baadhi yao huingilia swala la mapenzi kwa pupa na kuishia kuambulia ujauzito. Umri wa ujana wa Zohali unamfanya kuingilia maswala ya mapenzi ambapo hatimaye anaambulia ujauzito usiotarajiwa.
    • Viajana ni watu wanotafuta njia za kuyamaliza alu kuyapunguza matatizo yanayowakumba kwa nljia moja au nyingine. Chaurembo anafanya kazi katika shamba la majanichai kama njia ya kumpunguzia mzigo mfadhili wake kwa jina Bwana Tenga. Kidogo anachopata kutokana na kazi hii anakitumia kununulia sare za shule na adaftari.
    • Vijana ni watu wanaofuata utamaduni wa jamii zao. Tuama na wasichana wengine wanashiriki katika itikadi za tohara za jamii yao. Wanaamini kwamba msichana hawezi akaolewa kama hajapshwa tohara. Hata hivyo, wengi wao wanaaga dunia kutokana na tohara hii.
    • Vijana hukumbwa na mabadiliko mengi wanapoendelea na kukua. Baadhi ya mabadiliko hayo huwa ni ya kimwili na kimaumbile. Sare za awali za Pete zinapoanza kukata mwili kutokana na iukuaji wake ananunuliwa nyingine na mamake. Hii ina maana kwamba ukuaji wa maumbile ya msichana huyu umeanza kufanya kazi.
    • Vijana wana uhuru wa kujichaguliwa wake aul waume watakaowaoa. Nyanyake Pete anataka mjukuu huyu wake ajichagulie mume wa kumuoa baada ya kutimiza maazimio yake ya elimu. Hata hivyo, wajomba wake na mamake wanamshurutisha kuolewa na Fungo ambaye ni mzee mwenye wake kadhaa, jambo ambalo hapendezwi nalo. Hatimaye anatoroka kutoka kwa mumewe mzee huyu.
    • Vijana wanalaghaiwa kwa urahisi na watu wenye pashau ya kujitajirisha kwa kuahidiwa kazi nzuri kule ughaibuni ambazo kwa hakika hazipo. Vijana wanauzwa ng’ambo kupitia mtandao mpana wa Bi. Kangara bila ufahamu wao watakumbana na kazi duni kuliko za nchi yao. Baadhi yao wanateswa na waajiri wao. Inakuwa ni bora kama wangeishi nchini mwao kuliko kwenda huko ng’ambo ambako wanakumbana na maisha magumu zaidi kuliko yale yaliyoko nchine mwao.
      (hoja 10 x 2)
  5. MAPENZI KIFAURONGO: Kenna Wasike
    • “Hadi sasa mimi ni kama rubani aliyeharibikiwa na ndege angani.”
    • Onyesha ukweli wa dondoo hili. (alama 20)
    • Dennis alitokea katika familia ya kimaskini hangemudu mavazi mazuri kama ya wenzake chuoni au vifaa meme vya kisasa kama vile ipad, tarakilishi n.k.
    • Dennis hakusomea shule za kifahari kama wenzake chuoni.
    • Somo la Dakatari Mabonga linamvunja moyo Dennis na anahisi hapo hapamweki kwa vila namna anavyoendesha somo hilo anawaitia fadhaa. (uk 14)
    • Dennis anapomwomba mhadhiri atumie lugha nyepesi, darasa nzima linamcheka huku mwalimu akimkejeli kuwa ipapo alinuia kuwachekesha hajui kuchekesha.
    • Dennis kinyume na wenzake hana pa kukimbilia mambo yanapoharibika chuoni – wengine wataajiriwa na jamaa zao huku wengine wakiwa na wachumba wanaofanya kazi za kifahari serikalini na watawafadhili na kuwaondoshea kero la elimu ya juu.
    • Chuoni Dennis anaishi maisha duni. Malazi yake yamechanikachanika. Hana chakula na analazimika kupika uji mweupe na kuunywa kama chamcha.
    • Dennis anatafuta kazi sana baada ya kufuzu kama mtangazaji wa redio-kazi kwake inakuwa ni kuitafuta kazi yenyewe.
    • Dennis anakosa nafasi ya ajira kwenye shirika la kuchapisha magazeti. Kazi hiyo anapewa Shakila kwa sababu mamake ni mkurugenzi wa kamppuni hiyo – hapa anafanyiwa ubaguzi moja kwa moja.
    • Baada ya Penina kutambua Dennis hakufanikiwa kupata kazi, hataki hata amwite mpenzi. Hampikii kwa sababu alipotoka asubuhi hakuchangia chochote.
    • Penina anamfukuza Dennis pale kwao nyumbani na anamweleza asija akamwambia mtu kuwa waliwahi kuwa wapenzi.
      (Hoja 10 x 2 = 20)
  6. Ndoto ya Mshaka: Ali Abdulla Ali
    Mwandishi wa hadithi hii anatupa taswira ya jamii iliyozongwa na masaibu yanayotamausha. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 20)
    • Mashaka hakupata malezi mema – alikosa lishe bora. Chakula kilikuwa ni tikitimaji na matango.
    • Mashaka katika umri mdogo aliwapoteza wazazi na kulelewa na Bi. Kidege.
    • Mamake mlezi (bI. Kidege) anakabiliwa na maradhi ya miguu hivyo anashindwa kuzumbua riziki yao.
    • Mashaka anashiriki katika ajira katika umri mdogo ili wapate rizsiki yeye na mamake mlezi (uk 72)
    • Punde Mashaka anapokamilisha masomo ya chumba cha nane, mamake mlezi anaaga dunia na kumwacha katika ukiwa.
    • Ndoa ya Mashaka haikuwa ndoa ya kutajika – ilikuwa ni ndoa ya kulazimishiwa licha ya umaskini wake.
    • Mashaka anabaguliwa na Mzee Lubeya na mkewe ambao ni wakwe zake kwa umaskini wake. Wanalazimika kuhamia Yemeni kukimbia aibu.
    • Mashaka na mkewe Waridi kuishi kimaskini katika chumba kibovu. Anaeleza kuwa shida ziliwatamiria kila upande. (uk 74)
    • Mashaka na Waridi Kuwazaa watoto wengi ambao wanashindwa kuwapa malezi mema. Watoto wa kike kulala chini kwenye chumba kimoja na mamao ilhali wale wa kiume waliombewa jikoni kwa Chakupewa walikolala kama nyau. (uk 75)
    • Mazingira ya pale kwa kina Mashaka ni mabovu. Harufu ya choo kinachokumbatia chumba chao kuhamia chumbani mwao. Kuna mfereji wa maji chafu unaotema maji yake kwenye Mto Msimbazi (uk 74)
    • Mashaka na familia yake hawana choo – wanakwenda haja zote kwenye karatasi za plastiki na kuzitupa ovyo.
    • Viongozi kusaliti raia wanyonge – waakati wa mafuriko huwatangazia wahame mabondeni lakini hawawapi makao bora. (uk 75) – hawasemi waende wapi.
    • Mashahara wa mkia wa mbuzi aliopewa Mashaka kazini haungemruhusu kununua vifaa vya nyumbani. Aidha nafasi ya chumba chao haingetosha.
    • Waridi na watoto wanamtoroka Mashaka bila kuaga. Aliwahi kudokeza kuhusu kutoroka kwake katika wimbo ambao Mashaka hakuuelewa wakati huo (uk 77)
      (Hoja 10 x 2 = 20)
  7. (SHAIRI)
    MASWALI:
    1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu yako. (alama 2)
      • Shairi hili ni la tathmina kwa kuwa beti zake ni za mstari mmoja mmoja ambao una maana kamili. Ni la bahari ya manthawi kwa sababu mistari yenyewe imagawanywa katika vipande viwiliviwili.
    2. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
      • Shairi hili lina beti kumi na sita za mshroro mmoja mmoja. Kila mshororo una ukwapi na utao, yaani, vipande viwiliviwili.
      • Mishororo ni ya urefu wa mizani saba bsaba , jumla, kumi na nne. Beti za shairi hizi zina vina viwili kila mmoja, yaani, cha ukwapi na cha utao, ambavyo vinafanana lakini vinabadilika kutoka ubeti hadi mwingine. Kwa mfano, vina vya ubeti wa kwanza ni ‘si’ bali vya ubeti wa pili ni ‘ya’
      • Umbo kwa jumla ni:
        -7si, -7si. Ubeti wa kwnza
        -7ya, -7ya. Ubeti wa pili
    3. Toa mifano miwili ya matumizi ya mbinu ya inkisari katika shairi hili na uyaandike katika lugha ya kawaida. (alama 4)
      • Mifano ya matumizi ya inkisari katika shairi ni:
        Neno badala ya
        Lipataje tulipataje; tuliupataje
        Naye na yeye
        Silaumiewe asilaumiwe
        Likosa alikosa
        Jilaumu ujilaumu
        Measi umeasi
        Asojali asiyejali
        Mejitakia umejitakia
        Takulilia atakayekulilia
    4. Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 2)
      • Maudhui ya shairi hili ni malalamiko. Mweusi analalamika juu ya rangi nyeusi aliyopewa na hasa jinsi inavyohusishwa na jambo lolote baya kiasi cha rangi nyeusi kuleta wasiwasi.
      • Analalamika kuwa ibada za watu weusi hutukanwa kwa raha huku za weupe (wazungu) zikikubaliwa hadharani.
      • Manung’uniko yanasema Mweusi (Mwafrika) amefananishwa na Lusifa (Shetani) huku Adamau na Hawa, malaika wa Mungu na Yesu Mwana wa Mungu wamelinganishwa na Weupe.
      • Kuna sikitiko ya kuwa Mwafrika atendapo jambo hulaumiwa wakati huo.
      • Hatimaye ni shutuma dhidi ya Mwafrika huyo huyo ya kuwa ajilaumu yeye mwenyewe kwa kuiasi damu yake (asili yake); kuiga ovyo na kutojali ya mkuu.
    5. Ni nini dhamira ya mtungaji wa shairi hili? (alama 2)
      • Dhamira ya mtungaji wa shairi hili ni kuuupinga ubaguzi dhidi ya Wafrika kwa kuwapndelea
      • Wazungu. Tena ni kuwashauri watu weusi (Wafrika) wasiikane asili yao na mambo yao kwa kuiga yale ya watu weupe (Wazungu) kwani wanajiletea balaa wao wenyewe.
    6. Kwa kutoa mifano matatu, eleza matumizi ya lugha mkato. (alama 6)
      • Mifano ya matumizi ya lugha ya mkato ni: Ubeti wan ne, ‘Rangi hii hakika ni wapi ilitoka’ badala ya ‘Kwa hakika, rangi hii ilitoka wapi?’
      • Ubeti wa kumi na moja, utao, ‘silaumiwe pindi’ badala ya ‘pindi asilaumiiwe’. Ubeti wa kumi na tatu, utao, ‘measi yako damu’ badala ya ‘umeaiasi damu yako’ Ubeti wa kumi na sita, utao nani takulilia? Badala ya ‘ni nani atakayekulilia?’
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Moi Tea Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?